Tag: kombe la dunia 2018

  • Ujeruman Yaendeleza Record ya Bingwa Mtetezi Kutolewa Htaua ya Makundi

    Ujeruman Yaendeleza Record ya Bingwa Mtetezi Kutolewa Htaua ya Makundi

    Imekuwa kawaida kwa bingwa wa Kombe la Dunia kutolewa hatua ya makundi, lakini hakuna aliyetegemea hilo lingetokea kwa Ujerumani.

    Ujerumani haikuwahi kutolewa katika hatua ya makundi katika miaka 80 iliyopita.

    Korea Kusini wameilaza kwa mabao 2-0 na kuitupa nje katika Kombe la Dunia katika hatua ya makundi. Maana yake wameivua ubingwa.

    Kipigo hicho kimezua hofu kubwa kwa mashabiki wa timu hiyo ya taifa na huo ndiyo ukweli usiopingika.

     

    1998: France alikuwa bingwa

    2002: France alitoka hatua ya makundi

    2006: Italy alikuwa bingwa

    2010: Italy alitoka hatua ya makundi

    2010: Spain alikuwa bingwa

    2014: Spain alitoka hatua ya makundi

     

    Kwa nini Mabingwa wa kombe la Dunia hutolewa hatua ya Makundi tena kwa kufungwa na Timu dhaifu kabisa ??

  • Brazili Yaitandika Costa Rica Dakika zanyongeza

    Brazili Yaitandika Costa Rica Dakika zanyongeza

    Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kimesafisha makosa yake iliyoyaonyesha katika mchezo wa kwanza dhidi ya Switzerland kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Costa Rica leo.

    Mabao ya Brazil yamewekwa kimiani katika dakika za nyongeza kuelekea mchezo kumalizika kupitia kwa Philippe Countinho na Neymar Jr.

    Ushindi huo umemfanya Neymar ashindwe kuamini matokeo hayo baada ya kumwaga machozi ya furaha baada ya kufunga bao la pili.

    Katika kundi E Brazil imeongoza kwa kuwa na alama 4 ikifuatiwa na Serbia yenye 3 huku Uswizi ikiwa na 1 na Costa Rica wakiwa na 0.

    Matokeo hayo yamefuta kiu ya Wabrazil wengi ambao waliponda namna timu yao ilivyocheza mchezo wa kwanza dhidi ya Uswizi.

  • KOMBE LA DUNIA URUSI LEO NI ZAMU YA BRAZIL, MECHI ZINGINE KWA UJUMLA HIZI HAPA

    KOMBE LA DUNIA URUSI LEO NI ZAMU YA BRAZIL, MECHI ZINGINE KWA UJUMLA HIZI HAPA

    Michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi inaendelea tena Jumapili ya leo kwa jumla ya mechi tatu kupigwa.

    Brazil ambao wametwaa ubingwa wa mashindano hayo mara tano watakuwa wanacheza na Switzerland, wakati Ujerumani watakuwa wanakipiga na Mexico.

    Ratiba kamili ya mechi za leo hii hapa.

     

  • Urusi yaanza Vema Mashindano ya Kombe la Dunia baada ya Kuibebesha Zigo la Mabao Saudi Arabia

    Urusi yaanza Vema Mashindano ya Kombe la Dunia baada ya Kuibebesha Zigo la Mabao Saudi Arabia

    Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Luzhniki kwa wenyeji Urusi kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 5-0 dhidi ya Saudi Arabia katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia.

    Mechi hiyo ya aina yake imeshuhudiwa bao la kwanza likiwekwa kimiani mnamo dakika ya 12 na Ganzizky ambalo limeandika rekodi ya kuwa bao la kwanza katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa mwaka huu.

    Mabao mengine yametiwa kimiani na Cheryshev (43′ minutes, 90’+1), Dzyuba (71′ ) na Golovin (90’+4).

    Baada ya wenyeji kuanza vizuri, mechi zingine za kesho zitakuwa ni Iran itakayowakaribisha Morocco na vilevile Ureno itakuwa inacheza dhidi ya Spain.

  • Yajue Makundi ya Kombe La Dunia na Timu zake

    Yajue Makundi ya Kombe La Dunia na Timu zake

    Kombe la dunia linaanza siku tisa zijazo kuanzia leo. Afrika inawakilishwa 5 katika mashindano hayo yanayochezwa nchini Urusi na wachambuzi wanasema Afrika inayo nafasi zamu hii.

    Leo tunakuletea makundi ya timu hizi

    Kundi A

    Kundi hili lina mwenyeji wa mashindano nchi ya Urusi na Saudi Arabia, Misri na Uruguay. Ndani ya kundi hili Urusi ndio nchi pekee iliyo chini kisoka katika viwango vya FIFA ikishika nafasi ya 65 wakifuata Saudi Arabia, nafasi ya 63, Misri na Uruguay wakiongoza kundi hili wakishika nafasi ya 21 katika ubora duniani.

    Tathimini inaonyesha kuwa Urusi ina kazi ya ziada kupenya kundi hili kama nchi mwenyeji kitakwimu ingawa ubora wa FIFA si kigezo cha msingi katika maandalizi kimbinu na kiufundi kwa maana ya maandalizi.

    Mechi ya ufunguzi Urusi itakutana na Saudi Arabia na ndiyo mechi pekee ambayo wenyeji wana asilimia 50/50 kushinda ukiangalia ubora wa vikosi vya Uruguay ikiwa na akina Edinson Cavan na Luis Suarez, huku Mohamedi Salah akizidi kuonesha ubora wake na Liverpool.

    Kundi B

    Kundi hili ndilo alipo mfalme wa soka kwa sasa duniani Christiano Ronaldo na kikosi cha Ureno kitakachofungua mechi za makundi na Hispania. Hii inasadikiwa kuwa fainali ya mwisho kwa Ronaldo kutokana na umri wake.

    Hispania hawakuwa bora michuano ya mwaka 2014 nchini Brazil hali iliyowafanya kushindwa kuvuka hatua ya makundi hivyo inaleta changamoto kwa Ureno, Morocco na Iran. Morocco anahitajika kuwa makini zaidi ikiwa mara yake ya kwanza tangu fainali za mwaka 1998.

    Kundi D

    Kundi hili nalo lina mkali wa soka duniani  Lionel Messi na kikosi cha Argentina wakiwa na nchi za Croatia, Iceland na Nigeria, kwa mtazamo wa karibu unaweza kusema Argentina wakiongozwa na Messi wanaweza kupita kwa urahisi, lakini mambo hayatabiriki.

    Iceland katika fainali za Euro mwaka 2016 walimng’oa England licha ya udogo wao na hakuna asiyekumbuka maajabu ya Croatia 1998 nchini Ufaransa. Hili ni kundi gumu lisilo tabirika.

    Kama hiyo haitoshi Nigeria hivi karibuni alicheza mechi ya kirafiki na Argentina na ikaifunga Agentina nyumbani kwao 4-2 hivyo licha ya kupewa nafasi finyu kupenya, lakini anaweza kusonga mbele katika kundi hili pia.

    Kundi G

    Hapa kuna nchi za Ubelgiji, England, Panama na Tunisia, licha ya Ubelgiji kuwa bora kitakwimu, lakini England wanapewa nafasi kubwa kusonga mbele, kutokana na maandalizi yao  wakitengeneza kizazi kipya cha soka cha akina Harry Kane.

    Meneja wa England wa hivi sasa Gareth Southgate fainali za mwaka 1998 alikuwa mlinzi wa kati wa England wakiwaadhibu Tunisia hivyo atajipanga vyema kulinda ‘legacy’ yake na taifa hilo kwa ujumla.

    Kundi H

    Hapa kuna Senegal,  walioweza kufika hatua ya robo fainali mwaka 2002, Colombia, Japan na Poland iliyochini ya  Robert Lewandowski, ni kundi ambalo kila timu ina uwezo wa kuvuka hatua ya makundi endapo itakuwa na maandalizi mazuri.