Tag: magufuli

  • Magufuli Ateua Wakuu wa Wilaya Wapya

    Magufuli Ateua Wakuu wa Wilaya Wapya

    Daniel Chongolo, Mkuu wa wilaya ya Kinondon akichukua nafasi ya Ally Hapi
    Lengay Ole Sabaya Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ameteuliwa leo
    Moses Machali Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara ameteuliwa.
    Jokate Mwegelo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.
    Patrobas Katambi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
    Jerry Muro Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

     

    Rais Magufuli amemteua Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Aidha, amemteua David Kafulila kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe
    Rais Magufuli amemteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na Patrobas Katambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
    Rais Magufuli amemteua Ndg. Moses Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na Ndg. Lengay Ole Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai
    Pia amemteua Daniel Chongolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akichukua nafasi ya Ally Hapi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa

  • Rais Magufuli ateuliwa mshindi wa tuzo ya Ukombozi Afrika

    Rais Magufuli ateuliwa mshindi wa tuzo ya Ukombozi Afrika

    Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameibuka mshindi wa tuzo ya Afrika katika masuala ya uchumi.

    Makamo mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya ukombozi Afrika, Mwebesa Rwebugia ameieleza BBC kwamba rais Magufuli ameibuka mshindi kutokana na mchango wake wa kiuchumi hasaa katika ukuaji wa miundo mbinu.

    Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Tanzania kupata tuzo hii, baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutuzwa pia kutokana na mchango wake wa kuleta uhuru katika nchi za Afrika.

    Mwebesa Rwebugia ameeleza kuwa, katika kuegemea kwenye muktadha wa uchumi, kamati iliangalia umaskini ambao unatajwa kuwa adui mkubwa anayefahamika, lakini pia maradhi na ujinga.

    Kwa mujibu wa kamati hiyo ya Tuzo ya Ukombozi wa Afrika, ukombozi katika kipengelee cha elimu huangazia elimu na ujinga kama sehemu ya ukombozi.

    Tanzania imetolewa mfano wa elimu ya bila malipo kutoka kutoka shule za msingi mpaka sekondari.

    Katika suala la umaskini, kamati imeangalizia hatua ya kuwajali watu wa kipato cha chini, ukitolewa mfano wa kusajiliwa kwa ‘machinga’ katika kuwatambua rasmi kwa shughuli zao, na pia kuondolewa kodi za mazao kwa wananchi.

    Lakini sio kila mtu amepokea vyema ushindi huu wa rais Magufuli kutokana na kwamba kiongozi huyo hajakamilisha hata miaka mitano tangu aingie madarakani.

    Wakosoaji wanasema amepunguza nafasi ya raia kujieleze kwa uhuru.

    Na serikali yake imekosolewa kwa hatua za kuvizima vyombo vya habari na kinachotajwa kama kuvikandamiza vyama vya upinzani.

    ‘Rais magufuli hakutazamwa kwa muda aliyoingia madarakani lakini tangu miaka 20 iliyopita. Tangu alipokuwa wizara ya ujenzi na mawasiliano na nyingine tofauti, mpaka kufikia hadi ya kuwa rais wa taifa. Je ni mambo gani aliyoyafanya?’ Amefafanua Rwebugia.

    Mnamo 2016 Magufuli alishinda tuzo ya Forbes Africa kwa kuwa mtu anayeheshimika zaidi – na aliteuliwa kwa kutambulika jitihada zake za “kushinikiza uchumi wa Tanzania”.

    Tuzo ya Ukombozi Afrika inatambuliwa barani Afrika na Kimataifa lengo lake ni kutambua mchango wa viongozi wa bara la Afrika , wapigania uhuru, wapatanishi wa amani na washiriki wengine wa Ukombozi wa Afrika.

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni mwishoni mwa mwaka jana aliwahi kuteuliwa mshindi na kamati inayoratibu Tuzo hiyo ya Ukombozi Afrika.

    Ushindi wake Museveni ulitangazwa baada ya kamati hiyo kuketi mwezi Oktoba, 2017 na kujiridhisha kupitia vigezo vilivyowekwa kuwa kiongozi huyo anakidhi vigezo vyote.

    Alitambuliwa miongoni mwa mengine kwa mchango wake mkubwa wa kipekee alioutoa katika kusimamia amani katika nchi zilizokumbwa na migogoro ya ndani Somalia, Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo na Burundi.

    Vigezo vinavyozingatiwa pia ili kuteuliwa mshindi ni pamoja na mchango wa kiongozi katika ukombozi wa taifa kutoka tawala dhalimu miaka ya nyuma.

    Viongozi wengine waliowahi kuishinda tuzo hiyo ni pamoja na Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Kenneth Kaunda wa Uganda ambao walitunukiwa tuzo hiyo mwaka 2014.

    Rais Magufuli sasa anatarajiwa kupokea medali na cheti katika tarehe rasmi itakayotangazwa na kamati baada ya maridhiano kati ya mgeni rasmi na watu wa itifaki.

  • Kauli ya JPM kwa Machinga Mbezi: Biashara Haifanywi Porini

    Kauli ya JPM kwa Machinga Mbezi: Biashara Haifanywi Porini

    RAIS Dkt. John Magufuli ametangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa eneo la Mbezi Jijini Dar es Salaam kuendelea kufanya biashara zao pembezoni mwa barabara huku akizitaka mamlaka husika zisiwanyanyase wafanyabiashara hao wanaotafuta kipato .
    Dkt. Magufuli ameeleza hayo jana Julai 16, 2018 wakati akiwa njiani kuelekea Ikulu akiwa anatokea Mkoa wa Pwani, Kibaha kuweka jiwe la msingi la Chuo cha Uongozi cha Julius Nyerere na kusema wafanyabiashara hawawezi kunyanyaswa katika kipindi chake ambacho atakuwa madarakani huku akiwataka wafanyabiashara hao nao pia kuacha tabia ya kuinyanyasa serikali.
    “Biashara haifanywi porini, biashara inafanywa mahali pa watu. Kama mnaviongozi wenu mkae nao na muambizane msisogee barabarani kufanya biashara zenu, kwasababu kwa amri hii niliyoitoa ikitokea watu wakafa kesho kwa kugongwa na gari watasema Magufuli aliamrisha watu wagongwe, maana nitakuwa nina deni kubwa la kulipa kwa Mwenyezi Mungu”, amesema Rais Magufuli.
    Pamoja na hayo, Magufuli ameendelea kwa kusema “sitaki nikalipe hiyo dhambi kwa hiyo nawaomba sana ndugu zangu wa Mbezi na TANROADS wameshanisikia.

    “Kuanzia leo wasiwanyanyase watu wa pembeni lakini na nyinyi msifanyie biashara barabarani maana TANROADS watawashika na Jeshi la Polisi litashughulika. Kama kuna wafanyabiashara wowote wameshikiliwa bidhaa zao warudishiwe”.
    Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ubungo na Mkurugenzi kutenga eneo kwaajili ya wafanyabiashara hao waliopo katika eneo la Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam ili kusudi wawe na eneo maalum la kufanyia kazi zao.
  • Rais Magufuli ateua Kamishna mpya wa Magereza

    Rais Magufuli ateua Kamishna mpya wa Magereza

    Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais leo July 13, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza.

    Uteuzi huu umeanza leo July 13, 2018.

    Kabla ya uteuzi huu Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga, DSM.

    Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike anachukua nafasi ya Dkt. Juma Alli Malewa ambaye amestaafu.

     

  • RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUAGANA NA MABALOZI WATATU WALIOMALIZA MUDA WAO HAPA NCHINI

    RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUAGANA NA MABALOZI WATATU WALIOMALIZA MUDA WAO HAPA NCHINI

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatambulisha Baadhi ya Viongozi (hawaonekani pichani ) kwa Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 

     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchumi kutoka Ubalozi wa Sweden True Schedvin

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi Balozi wa Norway anayemaliza muda wake hapa nchini Hanne-Marie Kaarstad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Norway anayemaliza muda wake hapa nchini Hanne-Marie Kaarstad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Malawi anayemaliza muda wake hapa nchini Hawa Olga Ndilowe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi Balozi wa Malawi anayemaliza muda wake hapa nchini Hawa Olga Ndilowe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  • RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA VIONGOZI WAKUU NA VIONGOZI WASTAAFU IKULU DAR ES SALAAM LEO

    RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA VIONGOZI WAKUU NA VIONGOZI WASTAAFU IKULU DAR ES SALAAM LEO

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiiongozi Balozi John Kijazi akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam ili kukutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wakuu na viongozi wastaafu ambao anakutana nao kwa mara ya kwanza wote kwa pamoja.
    Viongozi Wakuu wastaafu wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam tayari kukutana na kuzungumza na mwenyeji wao Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyewaalika.
    Viongozi Wakuu wastaafu wakimsikiliza Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza nao leo.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilali.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mtaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, John Samuel Malecela.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Spika Mstaafu, Pius Msekwa.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Spika Mstaafu, Anne Makinda.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Barnabas Samatta.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino Ramadhan.
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chande 
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
  • DKT. BASHIRU ALLY APITISHWA NA NEC KUWA KATIBU MKUU WA CCM

    DKT. BASHIRU ALLY APITISHWA NA NEC KUWA KATIBU MKUU WA CCM

    Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally kwenye meza kuu mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwa meza kuu mara baada ya kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally wapili kutoka kulia kwenye meza kuu kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa NEC hawaonekani pichani, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally
    Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe mara baada ya kikao cha NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Dkt. Bashiru Ally amepitishwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.
    Dkt. Bashiru amepitishwa leo Mei 29, 2018 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama(NEC)

    Dkt. Bashiru ni Mwalimu Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia alikuwa Mwenyekiti wa Tume maalum ya kuchunguza mali za CCM iliyoundwa na Rais Magufuli

    PICHA NA IKULU

  • Rais Magufuli Atoa Wito kwa Majeshi Yote Nchini

    Rais Magufuli Atoa Wito kwa Majeshi Yote Nchini

    Rais Magufuli Atoa Wito kwa Majeshi Yote Nchini

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Mei, 2018 amezindua kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo katika kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani (831KJ) Jijini Dar es Salaam.

    Kituo hicho kina viwanda vya kushona nguo, kutengeneza maji, kukereza vyuma na pia kina chuo cha ufundi stadi (VETA), shule ya sekondari Jitegemee na kumbi mbili za mikutano (Muhuga Hall na Isamuhyo Hall). Uwekezaji wote umegharimu Shilingi Bilioni 5 na Milioni 793.

    Pamoja na kuzindua kituo hicho Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha ushonaji wa nguo kilichogharimu Shilingi Milioni 810 na ambacho kina uwezo wa kushona jozi 500 za sare za askari kwa siku na kuzalisha ajira za watu 350, na pia ametembelea kiwanda cha kutengeneza maji ambacho kimegharimu Shilingi Bilioni 1 na Milioni 600 na kina uwezo wa kuzalisha chupa 3,600 za maji kwa saa.

    Akizungumza katika mkutano uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Maafisa Wakuu na Askari wa JWTZ, Wakuu wa Majeshi wastaafu na Majenerali wastaafu, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza JWTZ kupitia Shirika lake la SUMAJKT kwa kuitikia vizuri wito wake wa kujenga viwanda na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa JWTZ katika jukumu hili la kujenga uchumi wa nchi kupitia viwanda na shughuli nyingine za uzalishaji mali.

    “Naomba nimpongeze Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuyo kwa jitihada alizozifanya kujenga miradi hii akiwa Mkuu wa JKT, nampongeza Mkuu wa JKT wa sasa na SUMAJKT kwa kazi nzuri mnayoifanya, kwa kweli leo nimefurahi sana kuona jeshi letu linajenga viwanda, huu ni mwelekeo mzuri, askari wetu sasa watashonewa nguo kutoka hapa hapa nchini kwetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

    Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa majeshi yote nchini kununua sare kutoka viwanda vya majeshi na kwa upande wa maji ametoa wito kwa Watanzania kunywa maji ya Uhuru Peak yanayotengenezwa na SUMAJKT zikiwemo ofisi za umma, na amebainisha kuwa uwekezaji huo utasaidia JWTZ kupata mapato kwa ajili ya kujiendesha na kupunguza ukubwa wa fedha za bajeti kutoka Serikalini.

    Aidha, Mhe. Rais Magufuli ametoa muda wa mwezi mmoja kwa taasisi za Serikali, taasisi binafsi na watu binafsi waliokopeshwa matrekta kupitia SUMAJKT na hawajarejesha Shilingi Bilioni 38 mpaka sasa, na taasisi za Serikali zinazodaiwa na SUMAJKT Shilingi Bilioni 3.4 kutokana na kutolipia huduma za ulinzi, kulipa madeni hayo vinginevyo vyombo vya dola viwakamate wadaiwa wote popote walipo.

    “Jen. Mabeyo nimekusikia juu ya madeni mnayodai, nataka ndani ya mwezi mmoja madeni haya yawe yamelipwa, najua mkipata fedha hizi mtaweza kujenga viwanda vingine ili tuendelee kuzalisha ajira kwa Watanzania na kujenga uchumi wetu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

    Mapema akitoa taarifa kwa Mhe. Rais Magufuli, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo ameishukuru Serikali kwa kuunga mkono jitihada za jeshi hilo kujenga viwanda na amemhakikishia kuwa JWTZ imedhamiria kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais ambapo kupitia mashirika yake ya Mzinga Corporation, Nyumbu Project na SUMAJKT imekamilisha viwanda vya kuchakata nafaka vya Mlale JKT na Mafunga JKT, Kiwanda cha kuchakata kahawa cha Itende JKT na inaendelea kujenga kiwanda cha mafuta ya kula cha Kigoma.

    Ameongeza kuwa JWTZ inategemea kujenga kiwanda cha chumvi katika eneo la Msindo Kilwa Masoko, na kwamba ipo tayari kushirikiana na taasisi za ndani na nje ya nchi kujenga viwanda zikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF katika mradi mkubwa wa uzalishaji wa sukari wa Mkulazi, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambako wataanzisha kiwanda cha maji tiba (Intravenous Fluid).

    Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema mazungumzo na nchi ya Misri yamekwenda vizuri ambapo kwa ushirikiano na JWTZ wataanzisha kiwanda cha dawa, kujenga machinjio na kiwanda cha kuchakata nyama, wakati Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kujengwa kwa kiwanda cha maji ya Uhuru Peak kunafanya Tanzania iwe na jumla ya viwanda vya maji 67 vilivyojengwa kuanzia mwaka 2015 na ambavyo vimezalishaji ajira 6,000, vimelipa kodi Shilingi Bilioni 59.7 na vimefanikiwa kutosheleza mahitaji nchini.

     

    Gerson Msigwa

    Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

    Dar es Salaam

    17 Mei, 2018

  • Rais Magufuli Atoa Agizo  kwa wanaodaiwa na JWTZ

    Rais Magufuli Atoa Agizo kwa wanaodaiwa na JWTZ

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo Alhamisi Mei 17, 2018 amefungua kituo cha Uwekezaji cha Suma JKT kilichopo Mgulani.

    Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo mawaziri, pamoja na maafisa mbalimbali wa majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini.

    Katika hafla hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo ameeleza kuwa JWTZ linazidai sekta binafsi kiasi cha shilingi bilioni 40, huku taasisi za serikali zikidaiwa shilingi bilioni 3.4, jambo ambalo limekuwa likiwakwamisha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

    Ili kuliwezesha jeshi hilo kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo, JeneraliMabeyo amemuomba Rais Magufuli apokee orodha ya wote wanaodaiwa na jeshi hilo, ili aongeze msukumo katika ulipaji wake.

    Kutokana na ombi la Jenerali Mabeyo, Rais Magufuli ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wadaiwa wote, kuhakikisha kuwa wamerejesha madeni wanayodaiwa na kuagiza baada ya kuisha kwa kipindi hicho mamlaka zinazohusika na ukusanyaji wa madeni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua kali wadaiwa wote.

    “Niwaombe wote hawa wanaodaiwa madeni kwa kuchukua matreka, mimi niwape mwezi mmoja. Ndani ya mwezi mmoja wawe wamelipa. Baada ya mwezi mmoja vyombo vyote vya ulinzi na usalama vianze kuwasaka wote,” amasema Rais Magufuli.

  • JINSI RAIS MAGUFULI ALIVYOFANYA ZIARA YA GHAFLA BANDARINI DAR ES SALAAM KUKAGUA MATANKI YA MAFUTA YA KULA

    JINSI RAIS MAGUFULI ALIVYOFANYA ZIARA YA GHAFLA BANDARINI DAR ES SALAAM KUKAGUA MATANKI YA MAFUTA YA KULA

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Doto James, mwenye kofia ngumu ya njano ni Mkurugenzi wa kampuni ya uingizaji mafuta nchini TLS & VOT Bw. Claudio Ghirardi, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Olesante ole Gabriel anayefuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuchunguza mafuta ya Kula na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Joseph R. Buchweishaija.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018, Nyuma yake ni Mkurugenzi wa kampuni ya uingizaji mafuta nchini TLS & VOT Bw. Claudio Ghirardi,
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa pongezi kwa Bw. Ben Usage Asubisye baada ya kumpandisha cheo kuwa kamishna kamili kutoka Kaimu Kamishna wa Forodha na Bidhaa za Ndani katika Mamlaka ya Mapato (TRA) alipotembelea  eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018. Hapa akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Olesante ole Gabriel na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuchunguza mafuta ya Kula na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Joseph R. Buchweishaija.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akinunua mapapai na ndizi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akigawa mapapai na ndizi kwa wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akigawa mapapai na ndizi kwa wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akigawa mapapai na ndizi kwa wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018. Picha na IKULU
  • RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA KATIKA SEHEMU YA IRINGA-MIGORI-FUFU KM 189 ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI

    RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA KATIKA SEHEMU YA IRINGA-MIGORI-FUFU KM 189 ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI