Tag: Mnangagwa

  • Emmerson Mnangagwa ashinda uchaguzi wa urais Zimbabwe

    Emmerson Mnangagwa ashinda uchaguzi wa urais Zimbabwe

    Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameshinda uchaguzi wa urais nchini Zimbabwe kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.

    Katika majimbo 10 yote yalioyotangazwa, Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 50.8 ya kura kwa asilimia 44.3 alizopata mgombea wa chama cha upinzani Nelson Chamise.

    Polisi waliwaondoa upinzani wakati wa kutangazwa matokeo baada ya kukataa kuyakubali matokeo hayo.

    Mwenyekiti wa chama cha MDC Alliance, Nelson Chamisa amesema kuhesabiwa kwa kura hakukufanyiwa uhakiki.

    Kwa ushindi wa asilimia 50 wa Mnangagwa umesababisha aepuke kwenda duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya Chamisa.

    Rais Mnangagwa amesema katika ukurasa wake wa Twitter kuwa huu ni mwamzo mpya.

    Bwana Chamisa amesisitiza kuwa ZANU-PF haikushinda uchaguzi huu, wanajaribu tuu kupitisha suala lisilo na ukweli, amesema pia watapambana na suala hilo.

    Uchaguzi huu ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe kung’atuliwa madarakani.

    Muungano wa Ulaya umekosoa kuchelewa kutangazwa kwa matokeo ya urais .

    Umesema kuwa ilibaini baadhi ya matatizo, ukiwemo upendeleo wa vyombo vya habari, vitisho kwa wapiga kura na kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi , ukiongeza kuwa ”mazingira ya uchaguzi hayakuboreshwa na hivyo kusababisha kuwepo kwa hali ya kiwango kikubwa cha ukosefu wa uaminifu “.

    Hii ni mara ya baada ya miaka 16 kwa serikali kuwaruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Muungano wa Ulaya na Marekani kuchunguza uchaguzi

    Kwa upande wa Muungano wa Afrika, mapema wiki hii umesema kuwa uchagauzi huo ulikuwa huru na wa haki , akiongezea kuwa unaadhimisha wakati muhimu wa mabadiliko ya kisiasa.

    Ripoti ya awali kutoka waangalizi wa SADC inasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa amani na ulifanyika kulingana na sheria.

  • Mnangagwa Asema Uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa

    Mnangagwa Asema Uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa

    Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesema uchaguzi utafanyika
    kama ilivyopangwa tarehe 30 mwezi Julai, ingawa kulitokea alichokiita jaribio
    la kukatiza uhai wake lililotokea siku ya Jumamosi.
    Katika hatua nyingine, msemaji wa Polisi, Charity Charamba amevitaka
    vyombo vya habari na Umma kujitokeza iwapo wana picha za video za tukio la
    mlipuko wakati huu ambapo uchunguzi unafanyika.
    Amwewaambia wanahabari mjini Harare kuwa zawadi nono itatolewa kwa
    taarifa itakayotolewa kusaidia kwenye uchunguzi wao.Idadi ya waliojeruhiwa
    sasa imefika 49 na Polisi na idara za usalama ziko katika uwanja wa White
    City eneo ambalo mlipuko ulitokea.
    Watu walijeruhiwa kutokana na mlipuko uliotokea kwenye mkutano wa
    hadhara mjini Bulawayo, tukio lililotokea karibu kabisa na Mnangagwa wakati
    akiondoka jukwaani. Maafisa wamesema masuala ya usalama yataangaliwa
    tena.
    mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa ni wa kwanza tangu aliyekuwa Rais wa
    nchi hiyo Robert Mugabe kuondolewa madarakani na kurithiwa na
    Mnangagwa.
    Mnangagwa alisema kuwa mlipuko ulitokea baada ya kitu ''kulipuka hatua
    chache na nilipokuwa-lakini muda wangu haujafika''. amesema kuwa ghasia
    hazina maana na ametoa wito wa kuwepo umoja.
    Kiongozi wa upinzani, Nelson Chamisa pia amekemea shambulio hilo,akisema
    kuwa machafuko ya kisiasa ''hayakubaliki''.
    Waliojeruhiwa kwenye shambulio hilo ni pamoja na makamu wa rais wawili,
    Mwenyekiti wa Chama cha Zanu-PF, wanahabari wa Televisheni ya taifa na
    maafisa wa usalama.
    Rais wa nchi hiyo alikuwa mjini Bulawayo, mji wa pili wa nchini humo na
    ngome ya upinzani, kwa ajili ya kufanya kampeni kwa ajili ya chama chake cha
    Zanu-PF wakelekea kwenye uchaguzi wa mwezi Julai.