Tag: Padri wa Kanisa Katoliki

  • Padri mwimba Rap asimamishwa kazi

    Padri mwimba Rap asimamishwa kazi

    Padri wa Kanisa Katoliki aliyejizolea umaarufu nchini Kenya kwa
    kutoa ibada kwa mtindo wa ku-rap,Paul Ogalo maarufu kwa jina la
    ‘Sweet Paul’ amesimamishwa kazi.
    Padri Ogalo (45) amekuwa akitumia staili ya ku-rap kuwashawishi
    vijana nchini Kenya kwenda kusali ili wajiweke karibu na Mungu.
    Taarifa hiyo ya kusimamishwa kazi kwa Padri huyo imetolewa na
    Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Homa Bay, Philip Anyolo ambaye
    amemtaka padri huyo achague kati ya kuwa rapper au kuwa Padri.
    Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation la nchini Kenya limeeleza
    kuwa Padri Ogalo amesimamishwa kwa mwaka mmoja kutoongoza
    ibada au misa kwa kipindi cha mwaka mmoja ingawaje
    ameruhusiwa kushiriki ibada na shughuli nyingine za Kanisa.