Tag: singida united

  • SINGIDA WATOA TAMKO LAO JUU YA SUALA LA FEI TOTO KUSAINI YANGA

    SINGIDA WATOA TAMKO LAO JUU YA SUALA LA FEI TOTO KUSAINI YANGA

    Baada ya kiungo Feisal Abdallah ‘Fei Toto’ kutambulishwa na Yanga jioni ya jana kwa kusainishwa mkataba wa miaka miwili, Uongozi wa Singida United umeibuka na kueleza kuwa hatima yake itaamuliwa na TFF pamoja na Bodi ya Ligi.

    Mapema jana asubuhi ripoti kutoka Singida zilisema wamemalizana na Toto kwa kuingia naye mkataba wa miaka mitatu usio wa awali huku picha na video zikisambaa mitandaoni kuhusiana na usajili wake ndani ya Singida United.

    Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, amefunguka na kueleza kuwa hatima ya usajili wake utaamuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi kutokana na mamlaka kuwa kwao.

    Sanga ameeleza kuwa wao walikuwa wameshamalizana kwa kila kitu na Toto ambaye alikuwa na wakala wake pamoja na Mwanasheria wakati wa kusaini mkataba huku akiwa amechukua sehemu kubwa ya fedha.

    Kutokana na Yanga kumtambulisha jana jioni ikiwa ni saa kadhaa Singida wametoka kuweka wazi taarifa za kuwa mchezaji wao kwa miaka mitatu, Sanga amesema TFF itahusika na utatuzi wa suala hilo ambalo hata wao limewashangaza.

    “Sisi tunachoamini kuwa mchezaji huyu amesaini Singida United na ameshachukua sehemu kubwa ya fedha, taratibu zote za usajili wake zilifuatwa hivyo TFF na Bodi ya Ligi tunawaachia hatima ya utatuzi wa suala hili” alisema Sanga.

    Toto ametambulishwa jana na uongozi wa Yanga tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili baada ya kumalizana na JKU ya Zanzibar ambayo ipo kwenye mashindano ya KAGAME yanayoendelea hivi sasa Dar es Salaam.

  • Michuano ya Super Cup Kuendelea leo Singida United Vs Fc Leopard

    Michuano ya Super Cup Kuendelea leo Singida United Vs Fc Leopard

    Wachezaji wa FC Leopard wakipiga Jaramba
    Kikosi cha Singida United Kikipiga Jaramba

    Patashika Nguo Kuchanika nchini Kenya ambapo Michuano ya Super Cup Yanaendelea.

    Leo Wawakilishi wengine wa Tanzania, Singida United itatupa karata yake ya kuwania kuingia nusu fainal itakapo kukutana na FC Leopard, ya Kenya kwenya michuano hiyo.

    Jana tulishuhudia mnyama akitinga hatua ya Nusu fainal ya michuano hiyo baada ya kuwafunga timu ya Kariobang Sharks kwa penati 2-3.

    Ratiba inaonesha Simba watakutana na Wababe wa Yanga, Kakamega Homeboyz kesho, na mshindi wa leo kati ya Singida United dhidi ya FC Leopard atakutana na Gori Mahia.

    Na bingwa wa michuano hiyo atapata nafasi ya kwenda Uingereza kucheza na timu ya Evertoon inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza.