Tag: wanawake

  • Tangazo lililowahimiza wanawake kuzaa na wachezaji wa nje Urusi lashutumiwa

    Tangazo lililowahimiza wanawake kuzaa na wachezaji wa nje Urusi lashutumiwa

     

    Maduka maarufu ya vyakula nchini Urusi yameomba msamaha baada ya
    kutangaza zawadi ya dola 47,000 na 'burger' (mkate maalum uliotiwa nyama)
    maishani kwa mwanamke yeyote ambaye angejamiiana na kuzaa mtoto na
    mchezaji wa kandanda kutoka nchi za nje katika Kombe la Dunia.
    "Mwanamke ambaye atafanikiwa kupata jeni za mchezaji bora zaidi ataisaidia
    Urusi kupata mafanikio miaka inayokuja," tangazo hilo lilisema.
    Tangazo hilo lilizua hisia tofauti nchini Urusi ambayo ndiyo inaandaa Kombe
    la Dunia hali iliyolazimu kampumi hiyo kulifuta tangazo hilo.
    Kwenye matangazo na vyombo vya habari, wanawake wa urusi wanatajwa
    kuwa wawindani wa ngono.
    Makala katika vyombo vya habari vya Urusi yanaandika kuhusu jinsi
    wanawawinda mashabiki wa kigeni na kuongea nao.
    Katika video moja ya YouTube mtangazaji mmoja wa kipindi anasema "maelfu
    ya wanyonyaji damu" wamefurika Moscow kwa matumaini ya kukutana na
    mashabiki wa kandanda wa kigeni.
    Wakati video moja iliibuka mitandaoni ikionyesha mashabiki kutoka Brazil
    wakiimba maneno machafu kwa lugha ya Kireno kwa mwanamke Mrusi na
    kuzua ghadhabu nchini Brazil lakini hakukuchukuliwa hatua zozote nchini
    Urusi.
    Mwanamke ambaye haifahamu lugha ya Kireno anaonekana akitabasamu
    akijaribu kuimba na mashabiki hao wa Brazil, bila kuelewa kile walichokuwa
    wakiimba kuhusu moja ya sehemu yake ya mwili.
    Ombi la mtandaoni nchini Urusi la kutaka wahusika kuchukuliwa hatua za
    kisheria limepata sahihi 2,500. Baadhi ya wale walihusika wametambuliwa
    kwenye vyombo vya habari nchini Brazil.