Tag: world cup

  • Hawa Hapa Wachezaji waliobeba Tuzo Kwenye Kombe la Dunia 2018

    Hawa Hapa Wachezaji waliobeba Tuzo Kwenye Kombe la Dunia 2018

    KIUNGO na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Croatia, Luka Modric ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na kupewa Mpira wa Dhahabu wakati timu yake ikipoteza mchezo wao wa fainali kwa kukubali kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Ufaransa huko Urusi.

     

    Modric ambaye amemaliza mashindano akiwa na mabao mawili, ameisaidia timu yake kutinga fainali ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufikia hatua hiyio kubwa ya kihistoria.

     

    Staa huyo wa Real Madrid ameonyesha kumvutia zaidi uchezaji wake, Rais wa Croatia, mwanamama Kolinda Grabar-Kitarovic wakati wa kukabidhiwa zawadi hiyo na Rais wa FIFA, Gianni Infantino na Rais wa Urusi, Vladimir Putin wakati hafla za kukabidhi ubingwa huo.

     

    Modric amewashukuru mashabiki wa Croatia na wachezaji wenzake kwa sapoti kubwa waliowapa hadi kufikia fainali licha ya kufungwa.

    Mbelgiji, Eden Hazard akiwa mchezaji Bora wa Pili na kutunukiwa mpira wa Silver, na Mfaransa, Antoine Griezmann akiibuka mchezaji Bora wa Tatu na kupewa mpira wa shaba.

     

    Kinda Mfaransa mwenye umri wa miaka 19, Kylian Mbappe ameibuka mchezaji Bora Mwenye Umri mdogo zaidi, akifunga mabao manne kwenye mashindano hayo.

    Kipa wa Ubelgiji, Thibaut Courtois amechukua Medani ya Dhahabu kwa kuwa kipa Bora wa mashindano akiisaidia timu yake kushika nafasi ya tatu huku akiruhusu mabao sita pekee kwenye mechi saba na clean sheets tatu.

    Nahodha wa Uingereza,  Harry Kane ameibuyka na kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora akiwa na jumla ya mabao sita, Griezmann manne, na kuwa wa pili akichukua kiatu cha Silver na Mbelgiji Romelu Lukaku, wa tatu akichukua kiatu cha shaba.

    Mbappe, Cristiano Ronaldo na Denis Cheryshev pia wana mabao manne kila mmoja lakini wameshindwa kwenye kipengele cha assists kwani wana assists chache. Grizemann.

    Fifa imeitangaza Timu ya Taifa ya Hispania ndiyo timu yenye nidhamu zaidi kwani imemaliza mashindano ikiwa na kadi mbili za njano pekee.

  • Angalia Ufaransa Walivyobeba Kombe la Dunia – Video

    Angalia Ufaransa Walivyobeba Kombe la Dunia – Video

    TIMU ya Taifa ya Ufaransa imefanikiwa kunyakua Ubingwa wa Dunia mwaka 2018 baada ya kuifunga Croatia kwa bao 4-2.

     

    Mabao ya Ufaransa yamewekwa kimiani na Mario Mandzukic aliyejifunga, Antoine Griezmann aliyefunga kwa njia ya penati pamoja, Paul Pobga pamoja na Kylian Mpabbe.

    Wakati huo mabao ya Croatia yamepachikwa kimiani na Ivan Perisic pamoja na Mario Mandzukic aliyesahihisha makosa yake kwa kuifungia timu yake bao la pili.

    Ubingwa huo kwa Ufaransa unakuwa wa pili baada ya kuutwaa pia katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1998 nchini kwao.

    Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps amekuwa miongoni mwa makocha watatu kutwaa ubingwa huo kama mchezaji na Kocha baada ya Mbrazil Mario Zagallo na Mjerumani Franz Beckenbauer.
    Vilevile Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kufunga mabao manne katika fainali hizo tangu Brazil iifunge Italia 4-1 mwaka 1970.

     

    Mario Mandzukic (bao la kujifunga) 18′,
    Ivan Perisic (bao la kusawadhisha) 28′
    Antoine Griezmann 38′
    Paul Pogba 59′
    Kylian Mbappe 69′.
    Mario Mandzukic ni mchezaji wa pili kwenye historia ya kombe la dunia kuifungia goli timu yake na kujifunga kwenye mchezo mmoja baada ya Ernie Brandts kufanya hivyo mwaka 1978 kwenye mchezo wa nchi yake (Uholanzi) dhidi ya Italia.
    Mbappe anaandika Historia baada ya kuibuka mchezaji Bora Chipukizi akiwa na umi mdogo lakini akifanya maajabu makubwa kwa kumaliza michuano hiyo akiwa na mabao 4 na Luka Modric (32) akiibuka mchezaji Bora wa mashindano hayo na kuondoka na kiatu cha dhahabu.
    Kylian Mbappe anakuwa mchezaji wa pili mdogo kufunga goli kwenye mchezo wa fainali ya kombe la dunia baada ya Pele kufunga goli kwenye fainali ya mwaka 1958 akiwa na miaka 17 na siku 249, Mbappe ana miaka 19 na siku 207.

  • NI VITA KOMBE LA DUNIA,  URENO VS URUGUAY HUKU SPAIN WAKIKIPIGA NA URUSI

    NI VITA KOMBE LA DUNIA, URENO VS URUGUAY HUKU SPAIN WAKIKIPIGA NA URUSI

    Baada ya kwenda sare ya bao 1-1 na Iran usiku wa jana, timu ya taifa ya Ureno sasa itakutana na Uruguay katika mchezo unaofuata ya 16 bora kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

    Mchezo huo ulimazika kwa sare hiyo huku nyota na nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo akikosa penati ambayo ingeweza kuiongezea alama timu yake.

    Uruguay anayoichezea nyota Luis Suarez sasa itakuwa inakipiga na Ureno baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Urusi.

    Wakati huo Spain iliyokwenda sare ya mabao 2-2 na Morocco itakuwa inakipiga dhidi ya Russia iliyopokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uruguay.

    Mechi hizo za mkondo wa hatua ya 16 bora zitaanza kuwaka moto Juni 30 kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).