Miaka tisa tokea dunia ipate taarifa za kifo cha mfalme wa muziki wa
Pop duniani Marehemu Michael Jackson ambaye alifahamika
duniani kote kutokana na upekee aliokuwa nao katika uchezaji
pamoja na nyimbo zake ambazo zilipendwa na watu wengi
ulimwenguni.
Marehemu Michael Jackson alipendwa zaidi na watoto kutokana na
upendo na ukaribu aliokuwa nao kwa watoto wote ambapo hakujali
rangi na enzi za uhai wake Michael Jackson aliwahi pia kutembelea
Tanzania na kukutana na Rais wa awamu ya pili wa Tanzania
mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Marehemu Michael Jackson alifariki June 25,2009 akiwa nyumbani
kwake Holmby Hills, Los Angeles nchini Marekani ambapo alikutwa
chumbani kwake na mmoja wa madaktari wake Conrad
Murray akiwa hapumui na kukimbizwa hospitali ya Ronald
Reagan UCLA Medical Centre.
Marehemu Michael Jackson aliwahi kushinda tuzo ya Grammy
Awards katika wimbo bora wa RnB mwaka 1984, Grammy Award
wimbo bora wa mwaka 1986, MTV video music award 1995,Billboard
Music Award for spotlight 1989 na nyingine nyingi.
Marehemu Michael Jackson alitamba na ngoma kali ikiwemo
Thriller, Bill Jean, We are the World, The way you make me feel, Beat
It, You Rock My World, Earth song, Dirty Diana na nyingine nyingi
ambazo bado zinaheshimika duniani kote mpaka leo.
Category: Music
-

Nyota Ndogo alizwa na historia ya mama yake, Aomba msaada kwa Watanzania

Nyota Ndogo 
Nyota Ndogo Msanii wa muziki kutoka Kenya, Nyota Ndogo amewaomba wana Afrika Mashariki kumsaidia kutafuta ndugu wa mama yake mzazi ambao hadi leo hii hawajui walipo.
Nyota Ndogo amesema kuwa mama yake mzazi alifika nchini Kenya akitokea Zambia akiwa na miaka 14 akisafirishwa na rafiki na baba yake (Babu wa Nyota Ndogo) kwa lengo la kwenda kusoma.
Nyota Ndogo amesema kuwa mama yake hakufanikiwa kwenda shule kama alivyoahidiwa bali aliishia kuwa kijakazi wa nyumbani.
Baadaye Mama yake alipata bahati ya kuolewa na mwanaume kutoka Tanzania ambaye ndio baba yake mzazi, na kwa maelezo ya mama yake kwenye familia yao walizaliwa watoto 15 na mama yake alikuwa ndiye mtoto wa mwisho.
“Anatokea Zambia kisha baba anatokea Tanzania lakini sisi tumezaliwa pale makadara hospital. Mimi ni 001 damu kisha my mum alitoka kwao akiwa 14 years but kasahau kikwao. hatujui mtu hata mmoja wakutoka upande wa mama, anasema kwa wapo kumi na tano na yeye ndio alikua wa mwisho hajui kama babake yupo au hayupo anasema anatokea Tunduma.“ameandika Nyota Ndogo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Kwa upande mwingine Nyota Ndogo amesema kuwa kwa sasa anahitaji kufanya ziara nchini Tanzania maeneo ya Tunduma, ambapo amesema kuwa anachohitaji kutoka kwa watu wa Afrika Mashariki ni kumsaidia kutambua lugha anayozungumza mama yake ili apate wepesi wa kutafuta ndugu wa mama yake.
“Nataka kufanya tour ya kumtafutia familia yake alikuja vipi Kenya? Rafiki ya babake alikwenda kumchukua kwa wazazi wake nakusema anakuja kumsomesha badala yake akamgeuza kijakazi,” ameeleza Nyota Ndogo.
Baba mzazi wa Nyota Ndogo ni Mtanzania lakini kwa upande wa mama yake bado haijajulikana asili yake ingawaje wameishi Kenya kwa muda mrefu.
-

DOWNLOAD NYIMBO MPYA ZA ALBUM YA CHIN BEEZ
“My Baby” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 4. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Killer” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 2. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Nitulize” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 3. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“My Baby” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 4. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Check It” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 5. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Cynthia” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 6. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Ladha” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 7. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Msafiri” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 8. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Sqwizza” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 9. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Zungusha” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 10. Genre: Africa.
DOWNLOAD
“Mororo” from Ladha by Chin Bees. Released: 2018. Track 11. Genre: Africa.
DOWNLOAD
-

LADHANI LEO CHIN BEEZ ANA REVIEW ALBUM YAKE LIVE

CHIN BEEZ akiwa ndani ya kipindi cha Ladha 3600 
CHIN BEEZ kulia akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Ladha 3600, Jabiri Salehe kushoto wakionesha cover ya cd ya Album yake 
CHIN BEEZ akikamua CHIN BEEZ: unajua ukizungumzia swala la Albam, tukiziweka ndani hatuwatendei haki mashabiki wetu
CHIN BEEZ: Hii ni kama zawadi nimewapa mashabiki wangu
CHIN BEEZ: Hii albam ni bure kabisa una weza kudownload kupitia wanene
CHIN BEEZ: Na sisitiza usiuziwe hii Albam, ni bure ni zawadi kwamashabiki wangu
CHIN BEEZ: Sometie kila msanii ana stayle yake unajua ehe
CHIN BEEZ: Mimi sio mkorofi ila unajua mtu ukiwa na modi furani hivi ndio unaonekana hivyo
CHIN BEEZ: Sasa mimi nafikiria maisha, yale mambo ya zamani sinaga tena meen
CHIN BEEZ: Kwa Bongo hii ndio album ya kwanza ambayo haina korabo
CHIN BEEZ: Nimeimba mwenyewe Album nzima kwa sababu nyimbo nyingi nilikuwaga nazo
CHIN BEEZ: Toka niachane Mpenzi wangu, now Sina Perment love (Nipo Single)
CHIN BEEZ: Mimi sio mtu wa starehe, mimi ni mtu wa studio
CHIN BEEZ: Hii album ina nyimbo 11 na ni bure kabisa, unaweza kuipata youtube, au unaweza ukagoogle








