Author: E-FM CO LTD

  • KUPIGA KELELE NI UCHAFUZI WA MAZINGIRA

    KUPIGA KELELE NI UCHAFUZI WA MAZINGIRA

    Katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na kelele serikali imewaelekeza  wamiliki wa maeneo ya burudani na starehe kuzingatia matumizi ya vipima kelele na vizuia sauti kama inavyoelekezwa kwenye masharti ya leseni zao. Hili ni kwa sababu ya kulinda afya za wananchi kutokana na athari za kelele na mitetemo.

    Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Seleman Jaffo wakati akiongea na vyombo vya habari Juni 29 kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na vitu hivyo.

    “Kila mwananchi ahakikishe shughuli anazofanya haisababishi kero ya kelele na mitetemo, Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani wahakikishe sauti zinazozalishwa katika shughuli zao hazizidi viwango vinavyokubalika kwa mujibu wa sheria. Hili tumeazimia wenye kumbi za starehe na burudani isiwe starehe ya kwako na watu wengine ikawa kero kwa watu wengine, Sauti zinazotoka zisidi viwango vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni”.- Amesema Jaffo

  • WATOTO WAELEKEZWE MATUMIZI SAHIHI YA BARAKOA

    WATOTO WAELEKEZWE MATUMIZI SAHIHI YA BARAKOA

    “Watoto waelekezwe kuhusu matumizi ya barakoa, wajue namna ya kuzivaa, waelekezwe na mahali pa kuzitupa” Dkt Ama.

    Dkt. Ama Kasangala, Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya Afya kutoka Wizara ya Afya

    Alikuwa anajibu maswali ya Dina Marious kuhusu madhaara ya Corona kwa watoto. Japo hawako kwenye hatari kubwa kama wazee, lakini mi muhimi walindwe.

    .

    Swebe alisema watoto kwa kutokuelezwa vizuri kuhusu Barakoa, wawapo shuleni wanaweza kuchangia, au kuokota na kuzivaa.

    .

    Hivyo wazazi wanasisitizwa kuwalinda watoto, lakini pia Wizara ya Afta kwa kushirikiana mamlaka nyingine na walimu wanahakikisha watoto wanaelezwa vyema na kulindwa.

    .

    #JikingeWakingeWengine #CoronaInazuilika

  • CANADA: ONGEZEKO LA JOTO LAUA WATU 130

    CANADA: ONGEZEKO LA JOTO LAUA WATU 130

    Watu zaidi ya 130 wamefariki nchini Canada kutokana na joto lisilo la kawaida kupiga ambalo limevunja rekodi ya kiwango cha joto.

    Polisi wa British Columbia wamepokea taarifa za vifo tangu Jumatatu, vifo vingi vikijumuisha wazee.

    Wanasema kiwango hicho cha joto kupiga katika eneo hilo kilisababisha vifo hivyo.

    Jumanne, kiwango cha joto nchini Canada kiliongezeka zaidi ikawa siku ya tatu mfululizo -ilikuwa nyuzi joto 49.5 huko Lytton, British Columbia.

    Kabla ya wiki hii , kiwango cha joto cha Canada hakikuwahi kuvuka nyuzi joto 45.

  • Hatma maombi ya kukamatwa Lissu Julai 14.

    Hatma maombi ya kukamatwa Lissu Julai 14.

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam, inatarajia kuanza kusikiliza maombi ya wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambao wanataka akamatwe ili wajitoe udhamini.

    Mahakama imetoa siku 7 kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani na maombi ya wadhamini, Ibrahim Ahmed na Robart Katula Julai 14, mwaka huu ambapo Wadhamini hao wamefungua maombi wakiiomba itoe hati ya kumkamata kwa kuwa wameshindwa kumpata na kumfikisha Mahakamani hapo.

    Maombi hayo namba 2/2020 yalipelekwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo upande wa Jumhuri uliomba kuongezwa muda wa kuwasilisha majibu ya kiapo kinzani.

    Hakimu Simba amesema Mahakama itasikiliza maombi hayo Julai 14, mwaka huu na kesi ya msingi itatajwa siku hiyo ikiwa Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni Wahariri Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

    Katika kesi ya msingi kwa pamoja washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002 ambapo hii ilitokea Januari 12 na 14, 2016 Dar es salaam, washtakiwa waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’

  • Rais Magufuli Atoa tamko la kutengewa eneo kwa Wafanyabiashara wadogo stendi mpya Dodoma.

    Rais Magufuli Atoa tamko la kutengewa eneo kwa Wafanyabiashara wadogo stendi mpya Dodoma.

    Rais Magufuli ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, kuhakikisha wafanyabiashara ndogondogo (Machinga), mama lishe pamoja na magari ya mizunguko mifupi jijini, (Daladala) kutengewa maeneo ya kufanya kazi katika stendi mpya ya kisasa Dodoma.

    Ametoa agizo hilo Jun 18 kwa njia ya simu, baada ya Mkurugenzi kuwatembelea wafanyabiashara katika stendi hiyo na kusikiliza kero zao.

    Ameongeza kuwa Mama lishe lazima wawepo, ikiwa stendi hiyo imejengwa kwaajiri ya watanzania wote wakiwepo maskin ambapo Hakuna sababu ya kuwa na stendi ya watanzania wote wa maisha yote,.

    Usafiri mwingine wa daladala na pikipiki Rais amesema Nilazima jiji litengeneze mazingira, watu wa daladala wawe wanaweza kufika pale, wa bodaboda waweze kufika pale, wa pikipiki waweze kufika pale, ili kusudi hata mvua ikiwa inanyesha mtu asianze kutembea na mizigo yake, wapo wengine wagonjwa.

    Aidha ametoa onyo kwa walinzi waliopewa kazi kwenye stendi hiyo kutoka Suma JKT kuacha kuwarusha watu vichura na kufanya kazi ya kuwalinda, kama wanavyofanya mikoa mingine ikiwa hapo sio jeshini wanapaswa kuwalinda .

    Kwa upande wake Mkurugenzi, Kunambi ameahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa ndani ya muda mfupi na kuwatafutia vijana mikopo kama ambavyo Rais ameagiza.

  • Fabrice Mugheni Atajwa kutua Young Africans awaaga Rayon Sports.

    Hatimaye kiungo anayehusishwa kujiunga na Young Africans, Fabrice Mugheni, amewaaga rasmi mashabiki wa timu yake ya Rayon Sports ya Rwanda kwa kuwaambia ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

    Fabrice raia wa DR Congo aliwahi kusema kuwa, aliombwa video zake na Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambaye pia anahusika na masuala ya usajili ndani ya Young Africans.

    Fabrice kupitia mtandao wake wa Instagram, aliwaaga rasmi mashabiki wa timu hiyo jambo ambalo linatafsiriwa kama huenda akawa alishamalizana na Young Africans kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.

    Young Africans wamekua wanahusishwa na mipango ya usajili wa baadhi ya wachezaji wa kimataifa, hii ni kwa ajili ya kujipanga vyema kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, endapo watapata fursa ya kuiwakilisha nchi kupitia michuano ya Kombe La Shirikisho.

  • Msamaha wa Rais Magufuli kwa zimamoto watoka na onyo kali.

    Msamaha wa Rais Magufuli kwa zimamoto watoka na onyo kali.

    Rais Magufuli amesema amemsamehe aliyekuwa Kamishna wa Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye baada ya kumuomba msamaha kwa zaidi ya mara tatu na viongozi wengine katika jeshi hilo ambao ilitakiwa awafukuze.

    Amesema kwa upande wa Andengenye, hawezi kumrudisha katika Jeshi hilo ila ataonekana katika kazi nyingine kwani mtu akiomba msamaha na kuonesha kutubu inabidi asamehewe

    Rais Magufuli ametangaza msamaha huo huku akitoa onyo kwa askari wa Jeshi la Zimamoto juu ya uchukuaji wa rushwa na kuingia mikataba isiyo na tija kuacha mara moja ambapo amewaambia kuwa fedha za bure katika kipindi chake ni mbaya zitawaharibia maisha yao.

    Amesemahayo leo Juni 11 2020, alipokuwa  anazindua jengo la makao makuu ya jeshi hilo mjini Dodoma huku akiwasifia kuwa jeshi hilo ni sawa na malaika wa duniani hivyo hawapaswi kufanya mambo mabaya kwa kuanzisha moto.

    Aidha Rais magufuli ameongeza kuwa Fedha za bure kwenye kipindi chake ni mbaya na zinaweza kuwaharibia maisha ambapo ametaka fedha za walipakodi zikawaletee mabadiliko

    Ikumbukwe kuwa mapema January 23 2020, Rais John magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola na Andengenye kutokana na kuingia mkataba mbovu uliolengwa kusaidia jeshi la hilo.

  • Waziri Philip Mpango aishukuru IMF kuisamehe Tanzania deni la Bilioni 33.

    Waziri Philip Mpango aishukuru IMF kuisamehe Tanzania deni la Bilioni 33.

    Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango ametoa shukurani kwa shirika la fedha duniani, (IMF) kwa kusamehe deni ambalo walikuwa wanaidai Tanzania la takriban Bilioni 33.

    Ametoa shukurani hiyo leo Juni 11, Bungeni jijini Dodoma alipokuwa anawasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21 na kusisitiza kuwa wanaendelea kuomba mashirika mengine yatoe msamaha wa madeni.

    Hii baada ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) jana, kutangaza limeisamehe Tanzania deni lenye thamani ya Dola Milioni 14.3 (takriban Tsh. Bilioni 33) ambalo lilipaswa kulipwa ndani ya miezi minne ijayo, kuanzia Juni 10, 2020 hadi Oktoba 13, 2020.

    IMF imechukua hatua hiyo kupitia mfuko wake wa ‘Catastrophe Containment and Relief Trust (CCRT)’ ili kuiwezesha Tanzania kukabiliana na athari za virusi vya Corona katika nyanja za kijamii na kiuchumi.

    Taasisi hiyo imesema kutegemeana na uwepo wa fedha katika mfuko huo, huenda ikaongeza msamaha wa deni lenye thamani ya Dola Milioni 11.4 (takriban Tsh. Bilioni 26.4) ambalo linatakiwa kulipwa kati ya Oktoba 14, 2020 na Aprili 13, 2022.

    IMF imeeleza kuwa janga hili limesababisha athari mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kupungua kwa watalii, changamoto za kibajeti na kupungua kwa makadirio ya ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) kutoka 6% hadi 4% katika mwaka huu wa fedha, na 2.8% katika mwaka wa fedha ujao ambapo hatua hii imekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tangu Rais wa Tanzania, Dkt Magufuli alipozitaka nchi zote za Afrika kuungana kuziomba taasisi za kifedha za kimataifa kutoa msamaha wa madeni.

  • Serikali kutoweka bei elekezi zao la Pamba

    Serikali kutoweka bei elekezi zao la Pamba

    Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2020/2021 utazinduliwa tarehe 15 Juni 2020, ambapo serikali imejiweka kando kutopanga bei elekezi katika zao hilo pamoja na mazao mengine badala yake bei za mazao zitatokana na soko.

    Ameyasema hayo, wakati akizungumza kwenye mkutano maalumu wa wadau wa tasnia ya Pamba uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Benki kuu Jijini Mwanza.

    Ameongeza kuwa kazi ya serikali ni kuhakikisha inasimamia uzalishaji bora wa mazao kadhalika kusimamia upatikanaji wa masoko ya mazao ili kuwa na bei nzuri yenye manufaa kwa wakulima ambapo Kutokana na usimamizi madhubuti wa serikali kupitia Wizara ya Kilimo, uzalishaji wa pamba umeongezeka kutoka tani 122,178 msimu wa ununuzi wa 2015/2016 hadi tani 348,910 msimu wa 2019/2020.

    Amezitaja Hatua zilizochukuliwa na serikali kuwa ni pamoja na kuhamisha makao makuu ya Bodi ya Pamba kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza ili kuwa karibu na maeneo yanayolima pamba na kuwahudumia wakulima kwa karibu zaidi ambapo Kutokana na hatua hiyo, ufanisi wa utendaji na huduma kwa wakulima umeongezeka.

    Aidha ameeleza kuwa zao la pamba ni mhimili wa uchumi wa wananchi wengi katika mikoa 17 na Wilaya 56 zinazozalisha zao hilo.

  • Man Utd na Real Madrid zagongana kwa Lautaro Martinez

    Man Utd na Real Madrid zagongana kwa Lautaro Martinez

    Manchester City wamejiandaa kuanza mapambano dhidi ya Chelsea kuhusu huduma za mlinzi wa pembeni wa Leicester City Ben Chilwell, 23, baada ya kuonyesha kiwango murua akiwa kwa mbweha hao.

    Napoli hawatapunguza bei ya beki wao raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 28, ambapo wanataka Pauni Milioni 100, haya yanakuja kipindi ambacho anahusishwa kujiunga na miamba kama Manchester United, Manchester City na Paris Saint Germain.

    Manchester United na Real Madrid wanamchunguza mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez 22, baada ya mazungumzo ya kujiunga na miamba ya Catalunya FC Barcelona kusimama kwa hivi sasa.

    Kiungo wa Bosnia-Herzegovina na Juventus Miralem Pjanic, 30, amekataa ofa za kujiunga na Chelsea na Paris Saint Germain kwani anahitaji kujiunga na Barcelona.

    Kiungo wa zamani wa Chelsea Michael Ballack ameukubali kwa asilimia 100 uamuzi wa klabu yake  kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 24, kwani anaamini ataiga mapema mazingira ya soka la EPL.

    Kiungo mshambuliaji wa Croatia na Fc Barcelona Ivan Rakitic, 32, anafikiria kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2021 ambako kandarasi yake inatamatika.

    Kiungo wa Paris St-Germain Ander Herrera, 30, amesema mshambuliaji wa Uruguay ambaye wanacheza pamoja Edinson Cavani, anatamani kucheza soka katika taifa la Hispania, Strika Cavani, 33, amekuwa akihusishwa kujiunga na Atletico Madrid.

    Beki wa Manchester United Brandon Williams, 19, anawindwa na mawakala wawili juu ya kumsaini mlinzi huyo kisha wakawa wanamtafuti timu, masoko, usimamizi na masuala kama hayo.

  • Ajali mbili za lori zatokea kwa mpigo na kusababisha vifo katika Daraja la Wami.

    Ajali mbili za lori zatokea kwa mpigo na kusababisha vifo katika Daraja la Wami.

    Daraja la Wami, ajali mbili tofauti zimetokea  kwa kufuatana mara baada ya malori hayo kufeli breki na kusababisha vifo ambapo Lori la kwanza limesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi wawili, huku lori la pili likiwa limesababisha vifo vya watu wawili mama pamoja na mtoto mdogo.

    Katika ajali ya Lori la kwanza lililokuwa linatokea Dar es salaam kuelekea Arusha limepoteza mtu mmoja ambae alikuwa dereva aliyeshindikana kuokolewa kufuatia kushindwa kufungua mkanda wa gari hivyo amezama katika mto wami wenye kina kirefu pamoja na lori hilo.

    Ajali hizo zimetokea June 5, 2020, ambapo wakati watu wakiwa wamejaa kushuhudia ajali hiyo ya lori, ghafla lori lingine pia likafeli breki na kusababisha vifo vya watu wawili ambao ni mama na mtoto waliokuwa kwenye eneo la tukio wakishangaa ajali ya kwanza ya lori.

    Lakini pia Lori hilo limezoa magari zaidi ya saba ambayo yote yameharibiwa vibaya.

    Aidha, jeshi la Uokaaji kwa kushirikiana na timu ya Askari polisi Wilayani bado wapo kwenye jitihada za kuhakiksha wanaokoa mwili wa dereva uliozama pamoja na lori mtoni.