Mwizi akutwa amelala kwenye Gari la Mwandishi wa Habari wa ITV katika harakati zakutaka kuiba Steve Nyerere amechambua zaidi ndani ya Joto la Asubuhi.
Author: E-FM CO LTD
-

Kocha mkuu Luc Eymael kurejea Tanzania Juni 06/07 kunoa kikosi chake.
Kocha mkuu wa Young Africans Luc Eymael amethibitisha kupokea tiketi ya ndege, kwa ajili ya safari ya kurejea Tanzania kuendelea na kazi ya kukinoa kikosi chake.

Eymael amethibitisha taarifa za kupokea tiketi ya safari, baada ya kueleza wazi namna uongozi wa Young Africans ulivyokua umekaa kimya kuhusu mpango wa kumrudisha nchini ili aendelee na kazi.
Kocha huyo amesema amepanga kuanza safari ya kuja nchini Juni 06 ama 07 na atakuwa sehemu ya benchi la ufundi kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya kikosi chake yanayoendelea jijini Dar es salaam.
“Nikiwasili moja kwa moja nitaanza kazi, ninafahamu kwa sasa msaidizi wangu Mkwasa anafanya kazi nzuri ya kuwanoa vijana, nitakapofika nitaongeza nguvu katika benchi la ufundi na mambo yatakuwa sawa kabla ya kucheza mchezo wetu dhidi ya Mwadui.” Alisema Eymael
Kikosi cha Young Africans kilianza kujiandaa na michezo ya ligi kuu Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho (ASFC), juma lililopita chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.
“Ni vizuri kusaini mkataba na La Liga lakini kama unataka kuwa klabu kubwa kwanza jaribu kumrudisha kocha wako haraka iwezekanavyo kama una muheshimu”
Young Africans watarejea dimbani Juni 13 kuendelea na michezo ya ligi kuu dhidi ya Mwadui FC kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, kisha watapambana na JKT Tanzania Juni 17 mjini Dodoma, Uwanja wa Jamuhuri.
-

Ugonjwa wa Virusi vya corona Kuvuruga utaratibu wa chanjo kwa watoto .
Mamilioni ya watoto wanaweza kupoteza maisha kutokana na maradhi yanayoweza kuzulika kwa sababu ya kukatizwa kwa programu za chanjo kutokana na virusi vya corona ambapo wataalam wametahadharisha.
Shirika la Afya duniani limeshauri nchi nyingi kusitisha chanjo ili kusaidia kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona ambapo takribani nchi 68 zimeathirika na baadhi zikisitisha kabisa kampeni za chanjo.
Lakini sasa makundi kadhaa ya wataalamu wanaona kuwa kutakuwa na madhara ya muda mrefu kutokana na hali hii Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia watoto (Unicef), Taasisi ya chanjo, Sabin na Shirika la Chanjo la Gavi pia yameonesha wasiwasi kuwa maelfu ya watoto watapoteza maisha kwa sababu zinazoweza kuzuilika.
Wahudumu wa afya wakielekeza nguvu yao kuhudumia matatizo mengine kama kupata vifaa vya chanjo hospitalini Lakini Polio, ambayo inaweza kusababisha kupooza au hata kifo, pia inarejea- wagonjwa wanne wapya wa polio wameripotiwa tangu mwezi Februari.
-

Vyuo vyapewa siku 3 kukamilisha mgao fedha za kujikimu kwa wanafunzi
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameagiza vyuo vyote nchini kuhakikisha hadi kufikia ijumaa Juni 5, mwaka huu viwe vimeshawalipa wanafunzi wote fedha zao za kujikimu na ambao hawatafanya hivyo watachukuliwa hatua.

Waziri Ndalichako ametoa agizo hilo leo Juni 3, jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi magari manne kwa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambacho ni miongoni mwa vyuo vinne vitakavyonufaika na mkopo wa Benki ya Dunia kupitia mradi wao wa Kuleta Mapinduzi kwenye elimu ya ufundi Afrika Mashariki (EASTRIP).
Profesa Ndalichako amesema kuna baadhi ya vyuo mpaka leo bado havijawapatia wanafunzi fedha hizo za kujikimu licha ya kwamba Serikali imeshazitoa hivyo anatoa siku tatu kuanzia leo kuhakikisha wanazitoa ili wanafunzi waendelee na masomo bila kupata usumbufu wowote.
-

Maandamano yaendelea usiku kucha Marekani kufuatia kifo cha George Floyd
Kimataifa
Maandamano juu ya kifo cha raia mweusi wa Marekani George Floyd bado yanaendelea kwa usiku wa nane mfululizo.
Kifo cha Floyd kilichotokea Mei 25, mikononi mwa polisi huko Minneapolis kimesababisha maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali nchini huko.
Waandamanaji wameamua kukiuka hatua ya kusalia ndani iliyowekwa katika miji mbalimbali.
Katika eneo la Fort Worth, Texas, inasemekana kundi dogo la watu lilisalia nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa mbili usiku.
Waandamanaji katika mji wa New York pia nao walikiuka hatua ya kutoka nje iliyowekwa kuanzia saa mbili usiku.
Meya wa mji alisongeza mbele muda huo kwa usiku wa pili mfululizo baada ya waandamanaji kupora eneo la kibiashara la Manhattan Jumatatu.
-

Waafrika wenye rangi nyeusi huwa na wakati mgumu pale wanapohitaji tiba ya dawa
Waafrika wenye rangi nyeusi huwa na wakati mgumu pale wanapohitaji tiba ya dawa kwa sababu wanawakilisha asilimia mbili tu ya sampuli ya vina saba iliyotumika na utafiti wa kutengeneza dawa, lakini kampuni mpya ya Nigeria inataka kubadili mumo huo.
Uhaba wa tafiti kuhusu watu wa aina fulani unahatarisha kuenea kwa magonjwa duniani kote.
Kwa mujibu wa muasisi na mkurugenzi wa kampuni inayoangazia biolojia ya vina saba ‘ 54gene’ , Dkt. Ene-Obong, watu wenye rangi nyeusi wako na utofauti wa kimaumbile ofauti na watu wengine duniani , na kutengeneza taarifa zao za vina saba kuna uhitaji wa raslimali kubwa zaidi kupatikana.
Amefanya utafiti wa vinasaba katika maabara ya nchini Nigeria katika mji wa Lagos , ambapo timu yake ina mpango wa kufanyia utafiti vinasaba 4000 vya sampuli zitakazokusanywa kwa mwaka 2019, kwa malengo ya kuwafikia watu laki moja ifikapo miezi 12 ijayo.

Abasi Ene-Obong ameiongoza timu ya utafiti wa dawa ambazo zinaweza kutumika duniani kote Dkt. Ene-Obong anasema kuwa ufahamu wa jukumu la vina saba katika magonjwa litasaidia katika uhusiano wa tiba .
“Dawa hazitengenezwi hata kwa kuwafikiria kuwa kuna waafrika wapo, idadi ya waafrika haifanyiwi majaribio ya kitabibu kulingana na mahitaji yao , kile kilichopo ni dawa ambazo hazina uwezo wa kutibu kiufanisi ,” alisema.
Dawa mpya pia inachukua muda mrefu kufika Afrika – mara nyingine ni kati ya miaka 15 mpaka 20 , alisema Dkt. Ene-Obong.
Watengenezaji wakubwa wa dawa huwa wanaangalia soko la mataifa ya magharibi, na aina ya vina saba vinavyopatikana barani Afrika baada ya makampuni hayo kupoteza wagonjwa wao.
Dkt Ene-Obong anasema kwamba anadhamiria kutatua tatizo hili kwa kuongeza upatikanaji wa takwimu za vina saba kutoka Afrika ili kuhamasisha utafiti wa kisayansi kufanyika zaidi kwa kuwaangazia watu hao.
“Mpango huo utatoa mwanya wa upatikanaji wa matokea ambayo yatawafanya waafrika wapate tiba kulingana nao lakini pia tiba ya kila mmoja ipatikane,” alisema.
Kampuni yake ina mpango wa kufanyia utafiti magonjwa kama ya selimundu(sickle cell), ugonjwa ambao unawaathiri waafrika zaidi.
Licha ya kuwa Dkt. Ene-Obong anasema kuwa ’54gene’ itaweza kubainisha namna ambavyo jenetiki inafanya kazi katika magonjwa ya muda mrefu na yasioambukiza kama saratani ,shinikizo la damu, ugonjwa wa kupoteza kumbukukumbu na mengineyo.
Kwa sasa wameanza katika hospitali za Nigeria ili kukusanya sampuli za DNA.
“Hatutaingilia huduma ambayo wagonjwa wanapata, lakini kwa ruhusa yao tutawaomba kupata damu au tishu za mwilini kwa ajili ya utafiti, alisema Dkt. Ene-Obong .
Vilevile amesema kampuni haina nia ya kuhifadhi tu lakini kuboresha huduma ya afya katika jamii inazozifanyia kazi.
Kampuni hiyo ilipokea ufadhili wa dola milioni 4.5 kutoka kwa wafadhili wakati ilipozindua mradi huo mwezi januari.
Fedha nyingi zilitumika kuongeza maabara zilizopo mjini Lagos, kukodisha wafanyakazi na kutengeneza mfumo wa kusambaza umeme kwa sababu Nigeria inakabiliwa na tatizo kubwa la kukatika umeme.


Dkt. Ene-Obong aliacha kazi yake ya ushauri wa viongozi wa sekta ya dawa na kuanzisha kampuni yake ya 54gene, ambayo sasa imeweza kutengeza watafiti zaidi ya 30 ambao wamefanya kazi katika taasisi za tiba nchini Marekani na Uingereza.
Lengo letu ni kuhakikisha kuwa watu wanatibiwa kiwango kisichokua na utofauti na Marekani au Uingereza.
Jina la kampuni hiyo imetokana na majina ya nchi 54 za Afrika .
“Hatutakikuwa kampuni ya wanaijeria peke yake bali tuko na mazungumzo na nchi za Afrika mashariki, magharibi na kusini mwa Afrika”.
Ingawa alikuwa na hofu kuhusu miongozo iliyopo katika baadhi ya mataifa ya Afrika na kutokuepo na utayari.
“Tunafuatilia sheria muhimu za kuzifuata katika nchi husika ,kwa sababu baadhi ya nchi miongozo haiko wazi.Hivyo lazima kujiandaa kufuata sheria husika na kufuata utaratibu wa taifa husika.”
Kampuni hiyo itatunza taarifa iliyozipata kwa kufuata utaratibu.
Kuna baadhi ya serikali za Afrika kama Kenya na Uganda,mamlaka imependekeza kuwa wakusanye taarifa za vina saba ambazo zitasaidia kupambana na uhalifu
Lakini Dk Ene anasema kuwa kampuni yake haina nia ya kuzigawa taarifa wanazozitafuta ingawa kampuni hiyo iko radhi kutoa picha kubwa ya takwimu ili serikali kuweza kuelewa hali ya afya ya watu.
cc;BBCswahili
-

Vijana wapewa siri ya ubunifu katika Biashara zao
Vijana nchini wametakiwa kuachana na biashara ambazo zimekuwa zikiwapotezea muda na badala yake wajikite katika ubunifu wa kazi wanazozifanya, ili kuweza kupata matokeo chanya yatakayobadilisha maisha yao.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, katika uzinduzi wa shughuli za kiubunifu Kitaifa zilizofanyika jijini Dodoma, zilizoandaliwa na Tanzania Innovation Explore Gala.
“Epukeni biashara zinazowapotezea muda, haiwezekani miaka mitano unafanya biashara isiyokupa faida, jitahidini katumia ubunifu wa kazi ambazo zitawafanya mfikie malengo yenu, maana kama utajibidiisha katika ubunifu ni lazima utayapata mafanikio,” ameongeza Beng’i.
Amesema wengi wa Vijana wamekuwa hawana mawazo mbadala katika kujikwamua na hali ngumu ya kiuchumi inayowakabili kwa kuendelea kung’ang’ania mfumo mmoja wa mbinu za kibiashara ambazo haziwaingizii faida na mwisho huitupia lawama Serikali au mashirika ya utoaji mikopo.
Beng’i ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo amebainisha kuwa uzoefu unaonesha baadhi ya watu wanaoendesha biashara kwa mikopo wamekuwa hawafikii malengo yao kutokana na faida kidogo wanayoipata huku wakitakiwa kufanya marejesho.
“Mtu huna mbinu za biashara zilizo na mashiko halafu unachukua mkopo ni wazi kuwa utaanguka tu, hivyo ni lazima kuweka mawazo mbadala ambayo kibiashara yanaweza kukupa faida kwa kuwa mbunifu katika bidhaa zako,” ameongeza Beng’i.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Idara kuu ya Vijana Jiji la Dodoma Mfungo Daniel Manyama, amesema ili kupata maendeleo yenye muonekano chanya maishani, Vijana hawana budi kutumia Elimu walizonazo kwa kuleta ubunifu na kujiajiri.
Amesema utafutaji na uzalishaji wa mipango thabiti ikiwemo suala la ushirikishwaji wa mawazo ya Vijana kwa watu sahihi, utaleta utatuzi wa changamoto na kupata mafanikio kwa kila kijana mpambanaji, aliye na kiu ya maendeleo.
“Elimu hii tuipatayo mashuleni inatakiwa itusaidie katika suala la ubunifu na kujiajiri maana kuwa na elimu halafu haitumiki katika kupata mbinu mpya za ubunifu inakua haina mantiki, sasa sisi kama eneo la uwezeshaji watu mbalimbali hasa vijana katika vikundi vyao tupo tayari kuunga mkono juhudi zenu,” amesema Manyama.
Awali akiongea katika uzinduzi huo mwakilishi wa makundi ya Vijana toka chuo cha Mipango Dodoma (IRDP), Gabriel Muhuwa amesema uwezo wa kubuni na kuwa na vipaji mbalimbali utasaidia kuinua uchumi wa wajasiriamali wadogo ambao wamekuwa na kiu ya kupata mafanikio.
Suala la kukuza mitaji inayotokana na ufanyaji wa biashara kwa wajasiriamali mbalimbali limekuwa likilalamikiwa katika maeneo mengi nchini kutokana na baadhi yao kukosa ubunifu, kuwa na uelewa mdogo wa mambo ya kibiashara, kutoitumia ipasavyo elimu waliyoipata katika ubunifu na kukosa maarifa mapya.
-

Japan yazindua kifaa maalum cha kuwatambua wanyanyasaji wa kingono
Kifaa kilicho na muhuri maalum wa kuwatambua wanyanyasaji wa kingono katika magari ya usafiri wa umma kimezinduliwa nchini Japan.
Kifaa hicho kinamfahamisha muathiriwa kuwa kuna mtu anampapasa na kuwawekea alama ya wino ambayo hauonekani.
Watu wanaweza kuwatambua wanyanayasaji wa kingono waliowekwa alama hiyo kwa kutumia taa nyeusi kuwabaini.

Wasafiri wakiwa ndani treni Shirika la kiteknolojia lililobuni kifaa hicho linasema kiitasaidia kukabiliana na uhalifu wa kingono.
Hata hivyo shirika moja lisilokuwa na kiserikali linanahofia kifaa hicho kinaweza kutumika vibaya na watu wenye chuki dhidi ya watu fulani.
Kampuni Japani linalofahamika kama hachihata linasema liliamua kutengeza muhuri huo ili kuwadhibiti watu wanaowanyanyasa kingono abiria katika vituo vya treni.
Kampuni hiyo ilitangaza wazo la kubuni muhuri huo mara ya kwanza mwezi wa tano baada ya video inayowaonesha wasichana wawili wa Japan wakimkimbiza mshukiwa wa unyanyasaji wa kingono katika kituo cha usafiri wa treni iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii kupata umaarufu.
Msemaji wa kapuni ya Shachihata aliandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa kifaa hicho”ni hatua moja kuelekea ulimwengu usiokuwa na uhalifu wa kingono”.

Wasafiri wakiingia ndani treni mjini Tokyo Lakini msemaji wa kitengo ckinachoshughulikia masuala ya ubakaji England na Wales ameiambia BBC huenda kifaa hicho kikatumiwa kibiasha na kufanya kuwa rasmi masuala ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono na kuwaeka hatarini wale wanaomiliki kifaa hicho.
“Japo waliobuni kifaa hicho wamekitengeza kwa nia njema nahofia pia kunawatu watakaotumia kujifaidi- kutokana na waathiriwa wa ubakaji’,” anasema Katie Russell.
Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni zaidi kufikiwa katika majaribio ya kukabiliana na visa vya upapasaji nchini humo, ikiwa ni miezi michache tu baada ya kuzinduliwa kwa programu inayojulikana kama Digi Police, inayolinda waathirika dhidi ya visa vya unyanyasaji katika maeneo yenye msongamano wa watu.
Kifaa hicho kinawafahamisha abiria wengine kwamba wako hatarini kwa kuonyesha ujumbe unaosema: “Kuna mtu anayepapasa watu hapa. Tafadhali nisaidie.” Kamera za kukabiliana na visa vya upapasaji ziliwekwa kwenye treni za jiji la Tokyo mwaka 2009 kusaidia kukabiliana na malalamiko ya unyanyasaji wa kingono.
Zaidi ya watu 6,000 walikamatwa kwa kushukiwa kutekeleza vitendo hivyo mwaka huohuo.
Harakati zinazoendeshwa na vuguvugu la #MeToo bado hazijafanikiwa nchini Japani ambayo inaorodheshwa kuwa nambari 110 katika nchini 149 kwenye suala la usawa wa kijinsia katika kipimo cha Kongamano la Kiuchumi Duniani.
cc:BBCswahili
-

Vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria: ‘Watu watatu’ wauawa katika shambulio la msafara wa magari ya kijeshi ya Uturuki
Shambulio la angani la serikali ya Syria uliolenga msafara wa kijeshi wa Uturuki uliokuwa ukielekea katika eneo linalotawaliwa na waasi kaskazini mwa Syria limesababisha vifo vya raia watatu, Uturuki imedai.
Watu wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio hilo katika mkoa wa Idlib siku ya Jumatatu kulingana na wizara ya ulinzi ya Uturuki.
Idlib ambayo ni mojawapo ya maeneo machache yasiodhibitiwa na serikali, ilitarajiwa kulindwa na kuwa eneo huru linalotenganisha majeshi pinzani lililoafikiwa na Uturuki inayowaunga mkono waasi mwaka uliopita.
Lakini mashambulizi ya serikali yamekuwa yakiongezeka tangu mwezi Aprili.
Mamia ya raia wameuawa kutokana na hilo na kuna hofu kwamba wengi watafariki iwapo hali itaendelea kuwa mbaya.
”Hii ndio hatari inayotukabili kwa sasa”, alisema Jan Egeland kutoka baraza la wakimbizi la Norway akizungumza na BBC.
Kwa miaka kadhaa sasa tumeonya kuhusu hatari inayoikabilia Idlib , ambapo hakuna mahala pa kutorokea kwa raia milioni 3.
Kuna wapiganaji wabaya mjini humo. Lakini shambulio la jumla katika eneo hilo pamoja na lile lililomkabala la kaskazini mwa Hama litamaanisha kwamba watoto milioni moja wataathiriwa na vita hivyo na hicho ndicho tunakiona kikifanyika
Uturuki inayounga mkono baadhi ya waasi na sio wote ina majeshi yake Idlib kama mojawapo ya makubaliano na Urusi mwaka uliopita.
Kulingana na Naji Mustafa , msemaji wa waasi wa National Liberation Front msafara huo ulikuwa ukielekea katika mojawapo ya vituo vyake vya uchunguzi na walinzi wakati shambulio hilo lilipotokea,
Mwandishi wa AFP ambaye aliuona msafara huo anasema ulishirikisha magari 50 ya kijeshi , matano kati yao yakiwa vifaru.
Lakini Syria imesema kuwasili kwa msafara huo katika eneo hilo ni kitendo cha uchokozi . Imesema kuwa silaha hizo hazitasitisha harakati za wanajeshi wa Syria kukabili kile ilichokitaja kuwa magaidi.
Kulingana na Shirika la haki za kibinadamu la Syrian Observatory for Human Rights (SOHR), lililo na makao yake nchini Uingereza , ndege ya kijeshi ya Urusi ilitekeleza mashambulio karibu na msafara huo tarehe 19 Agosti.
Uturuki imesema kuwa shambulio hilo linakiuka makubaliano ya mwaka uliopita huku kisa hicho kikizua hofu kuhusu makubiiano ya moja kwa moja kati ya mataifa hayo mawili.
Kwa nini shambulio hilo lifanyike?
Baada ya miaka minane ya vita , serikali ya Syria inajaribu kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na waasi.
Vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na Urusi , viliripotiwa kuingia eneo la kaskazini magharibi la Khan Sheikhoun siku ya Jumapili.
Eneo la Khan Sheikhoun ambalo lilishambuliwa na gesi aina ya sarin mwaka 2017 lipo katika barabara kuu inayounganisha Damascus na Aleppo na ni eneo muhimu la kimkakati kusini mwa mkoa huo.
Iwapo litakombolewa , itamaanisha kwamba utawala wa Syria umefanikiwa kulizunguka eneo linalodhibitiwa na waasi upande wa kusini ambalo linashirikisha kituo cha uchunguzi cha Uturuki katika mji wa Morek.
Bwana Mustafa alisema kwamba msafara huo ulikuwa unaelekea Morek.
cc;BBCswahili
-

Korea kaskazini yasusia mazungumzo ya amani na Korea kusini kuhusu mazoezi ya vita
Korea kaskazini imepinga mazungmzo ya ziada ya Korea kusini, na kusema uamuzi huo ni “makosa ya hatua za Korea kusini”.
Imetoa taarifa kufuatia hotuba ya rais wa Korea kusini Moon Jae-in hapo jana Alhamisi.
Wakati huo huo, mapema leo Ijumaa Korea kaskazini imefyetua makombora mawili baharini kutoka pwani ya mashariki, jeshi la Korea kusini limearifu.
Likiwa ni jaribio la sita la aina hiyo, na linafanyika chini ya mwezi mmoja.
Makombora hayo mawili “ambayo hayakutambuliwa ” yalifyetuliwa mwendo wa saa mbili asubuhi Alhamisi na kusafiri umbali wa kilomita 230 kufika ujuu wa 30km, Afisa wa vikosi jumla Korea kusini amesema.
Msururu wa majaribio hayo yanajiri baada ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Korea kaskazini Kim Jong-un kukubaliana katika mkutano mnamo Juni kuanza upya majadiliano ya jitihada za kusitisha matumizi ya silaha za nyuklia.
Korea kaskazini imekabiliwa na vikwazo vya kimataifa kwa kutengeneza silaha za nyuklia.
Korea kusini imesema nini?
Katika hotuba hiyo, ya kuadhimisha uhuru wa Korea dhidi ya utawala wa Japan, rais Moon aliapa kuiunganisha rasi ya Korea kufikia mwaka 2045.
Korea iligawanyika na kuwa mataifa mawili mwishoni mwa vita vya pili vya dunia.
Rais Moon amesema lengo la kufanikiwa kuacha matumizi ya silaha za nyuklia katika rasi ya Korea ni jambo muhimu zaidi wakati mazungumzo kati ya Kaskazini na Kusini yakionekana kukwama.
“Rasi mpya ya Korea, ambayo italeta amani na ustawi kwayo, na mashariki mwa Asia, pamoja na katika dunia nzima, inatusubiri,” alisema katika hotuba hiyo aliyoitoa kwenye televisheni.
Korea kaskazini imelipokea vipi?
Katika taarifa yake, Korea kaskazini imehoji maana ya mazungumzo wakati “hata katika wakati huu Korea Kusini inaendeleea kufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja na kuzungumzia suala la uchumi wa amani na utawala wa amani. Haina haki ya kufanya hivyo.”
Katika linaloonekana kuwa ni shambulio dhidi ya rais Moon, taarifa hiyo imeendelea kusema “Tunajiuliza pia iwapo yupo timamu katika fikra zake wakati anapotaja ‘mazungumzo’ baina ya Kaskazini na Kusini wakati anaendeleza taswira ya vita inayopanga kuangamiza vikosi vyetu katika siku 90.
“Ni mwanamume aliyekosa haya.”
Korea kaskazini imekasirishwa na mazoezi ya kijeshi baina ya Korea kusini na Marekani , ikieleza kuwa yanakiuka makubaliano yaliofikiwa baina ya rais Donald Trump na rais Moon.
Imewahi kuyataja mazoezi hayo kuwa “mazoezi ya vita”.
Katika barua ya hivi karibuni kwa Trump, kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un anaarifiwa kuwa alilalamika “kuhusu gharama kubwa na kichekesho” cha mazoezi hayo.
Mkwamo uliopo katika mazunguzo ya kuistisha matumizi ya silaha za nyuklia ni makosa ya uamuzi wa Korea kusini kufanya mazoezi ya kijeshi, msemaji wa utengamano kutoka Korea kaskazini amesema.
“Hatuna maneno ya ziada kuzungumza na maafisa wa Korea kusini,” afisa huyo amesema katika taarifa iliyopeperushwa kwenye televisheni ya taifa ya Korean Central News Agency.
cc;BBCswahili
-

Ni hatari kwa wanawake kufukiza sehemu zao za siri.
Madaktari wa magonjwa ya wanawake wameonya kuhusu hatari inayotokana na kutumia mvuke wa moto kwenye sehemu za siri, baada ya kutokea kuwa mwanamke mmoja alijiunguza sehemu zake za siri baada ya kutumia mvuke wa maji kufusha sehemu za siri.
Mwanamke huyo alikuwa na tatizo la kubadilika muundo wa maumbile ya sehemu zake za siri (prolapsed vagina) kitaalamu, na kuamini kuwa tiba hiyo itamfanya akwepe kufanyiwa upasuaji.
Kufusha kwa mvuke sehemu za siri, kitendo ambacho uhusisha kukaa kwenye chombo chenye maji ya moto chenye mchanganyiko wa maji na dawa, kimekuwa maarufu sana hivi sasa.
Tiba hiyo na tiba nyingine kwenye maeneo nyeti, imekuwa ikifanyika kwenye saluni na nyumba za Spa kwenye maeneo mbalimbali ya miji.
Nyumba za Spa zimekuwa zikitangaza kutoa huduma hiyo iitwayo ”v-steaming” ikidaiwa kuwa imekuwa maarufu miaka mingi barani Afrika na Asia. Wanasema tiba hiyo, ambayo wakati mwingine huitwa Yoni steaming hufanyika ”kuondoa uchafu” kwenye sehemu za siri.
Wataalamu hata hivyo, wanaasa kuwa ni hatari sana na hakuna uthibitisho wowote kisayansi kuwa ni tiba yenye kufanya kazi kiafya, ikiwemo kupunguza maumivu wakati wa hedhi au kusaidia kupata watoto.
Dokta Vanessa Mackay, msemaji wa shule ya wataalamu wa magonjwa ya wanawake, anasema ni ”imani” kuwa sehemu za siri zinahitaji usafi wa hali ya juu kiasi hicho au tiba ya namna hiyo.
Amesema inashauriwa kutumia sabuni zisizo na manukato kwenye eneo la nje la maungo hayo pekee.
”Sehemu za siri za mwanamke zina vijidudu vizuri, ambavyo husaidia kulinda maungo hayo,” alieleza katika taarifa yake.
Kuzifusha sehemu za siri kunaweza kuathiri vijidudu hivyo na kusababisha kuwashwa, na athari nyingine kama maumivu mithili ya kuwaka moto, pia ngozi laini pembezoni mwa sehemu za siri inaweza kuungua au kubabuka
Madaktari kadhaa wameeleza hadithi kuhusu mwanamke aliyepata madhara kutokana na kufusha sehemu zake.
Dokta Magali Robert, aliyeandika taarifa ya mwanamama huyo mwa miaka 60 wa huko Canada, alisema mwanamke huyo alijaribu kufukiza sehemu zake za siri kwa ushauri wa daktari wa tiba za kienyeji wa kichina.
Mwanamke huyo alikaa kwenye maji yaliyokuwa yamechemka kwa dakika 20 kwa siku mbili mfululizo kabla ya kujisalimisha kwa dharura baada ya kupata majeraha.
Alilazimika kuahirisha upasuaji ili kuuguza majeraha aliyoyapata.
Doka Robert anasema taarifa hizi za kupotosha huwafikia watu kwa wingi kwenye mitandao na taarifa kutoka kwa watu.
”Watu wanaotoa huduma kwa wanawake wanapaswa kufahamu tiba mbadala ili waweze kuepuka madhara.”Alieleza kwenye makala yake.
cc;BBCswahili





