BORIS JOHNSON AKUTANA NA MAAFISA WA TRUMP

BORIS JOHNSON AKUTANA NA MAAFISA WA TRUMP

Like
302
0
Monday, 09 January 2017
Slider

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson amekutana na washauri wakuu wa rais mteule wa Marekani Donald Trump mjini New York, Marekani.

Johnson alikuwa na shemejiye Trump, Jared Kuchner, na afisa mkuu wa mikakati wa Bw Trump Steve Bannon.

Huo ulikuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana kati ya maafisa wa Trump na waziri wa Uingereza.

Maafisa wanasema kwenye mkutano huo, sera ya Marekani kuhusu Syria, China na Urusi ilijadiliwa.

Jumatatu, Bw Johnson atakuwa mjini Washington D.C, kukutana na maafisa wakuu wa bunge.

Anatarajiwa kukutana na maafisa wakuu wa chama cha Republican katika Bunge la Congress akiwemo mwenyekiti wa kamati ya mashauri ya kigeni, Bob Corker na kiongozi wa Congress, Mitch McConnell.

Hata hivyo, hatakutana na Rex Tillerson, anayetarajiwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya Bw Trump.

Waziri Mkuu wa Uingereza Teresa May naye amesema kwamba amekuwa na mazungumzo ya kufana ya simu na Bw Trump.

Awali Rais huyo mteule wa Marekani alionekana kumuunga mkono Nigel Farage mwanasiasa wa chama cha uzalendo na anayepinga Muungano wa Ulaya, kama balozi wa Uingereza nchini Marekani.

Hii ilionekana kuwakera wakuu nchini Uingereza, licha ya taarifa kupinga hilo.

Comments are closed.