Category: Slider

  • CANADA: ONGEZEKO LA JOTO LAUA WATU 130

    CANADA: ONGEZEKO LA JOTO LAUA WATU 130

    Watu zaidi ya 130 wamefariki nchini Canada kutokana na joto lisilo la kawaida kupiga ambalo limevunja rekodi ya kiwango cha joto.

    Polisi wa British Columbia wamepokea taarifa za vifo tangu Jumatatu, vifo vingi vikijumuisha wazee.

    Wanasema kiwango hicho cha joto kupiga katika eneo hilo kilisababisha vifo hivyo.

    Jumanne, kiwango cha joto nchini Canada kiliongezeka zaidi ikawa siku ya tatu mfululizo -ilikuwa nyuzi joto 49.5 huko Lytton, British Columbia.

    Kabla ya wiki hii , kiwango cha joto cha Canada hakikuwahi kuvuka nyuzi joto 45.

  • Wabunge Kenya watofautiana kuhusu matamshi ya ‘chuki’ ya Charles Kanyi ‘Jaguar’

    Wabunge Kenya watofautiana kuhusu matamshi ya ‘chuki’ ya Charles Kanyi ‘Jaguar’

    Matamshi ya mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles ‘Jaguar’ Kanyi kuhusu kuwatishia raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Kenya yaliwasilishwa mbele ya kikao cha bunge ili kujadiliwa.

    Hatua hiyo inajiri huku Mbunge huyo akizuiliwa katika kituo cha polisi usiku kucha ambapo anasubiri kuwasilishwa mahakamani siku ya Alhamisi.

    Kulingana na mtandao wa runinga ya Citizen nchini Kenya, licha ya wabunge wengi kushutumu jinsi ambavyo bwana Jaguar alitoa hoja yake , baadhi yao walikubaliana kwamba kuna swala tata kuhusiana na raia wa kigeni ambalo lilihitaji kuangaziwa.

    Kulingana na mtandao huo swala hilo liliwasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Uhusiano wa kigeni Katoo Ole Metito katika taarifa yake, akithibitisha kwamba raia wa kigeni hususan kutoka Jumuiya ya Afrika mashariki wana uhuru wa kufanya biashara nchini Kenya.

    ”Tunashutumu sana matamshi yoyote ya chuki yanayokiuka msimamo huu unaotuleta sisi pamoja kama taifa na kuthibitisha sera ya kuwakaribisha raia wote wa kigeni”, alisema mbunge huyo wa Kajiado kusini.

    Matamshi yake yaliungwa mkono na mbunge wa Suba Kaskazini John Mbadi ambaye aliwarai wabunge wenzake kutotoa matamshi mbele ya umma kwa lengo la kujitafutia umaarufu na badala yake kuchukua tahadhari.

    ”Kama bara, tunahitaji kukuza uwiano katika mipaka yetu ili kutafuta ajira; Wakenya wako huru kwenda Tanzania kufanya biashara iwapo biashara hiyo ni halali”, alisema Mbadi.

    Hatahivyo kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale, ambaye pia alishutumu matamshi hayo ya mbunge huyo wa Starehe alisema kwamba Kenya sio jaa la raia wa kigeni na bidhaa zao, kulingana na mtandao wa Citizen kenya.

    Kulingana na mbunge huyo wa Garissa mjini, Bunge pamoja na serikali zinafaa kuwalinda wananchi wa kawaida kutopoteza kazi kwa idadi kubwa ya raia wa kigeni waliomo nchini.

    Mbunge huyo alitaja mfano ambapo wataalam kutoka Kenya kama vile afisa wa kampuni ya Safaricom Sylvia Mulinge alinyimwa fursa ya kufanya kazi katika taifa jirani la Tanzania, akiongezea kuwa Kenya pia inafaa kutokubali maswala mengine.

    “Lazima ukweli usemwe; Unapoona biashara ya uchuuzi ikichukuliwa na raia wa taifa jingine tuna jukumu la kuwalinda watu wetu. Hawa wabunge hawafai kusahau kwamba kuku wetu walichomwa Tanzania , ng’ombe wetu walipigwa mnada Tanzania”, alisema Duale.

    ”Leo chini ya utawala uliopo Tanzania Wakenya hawawezi kufanya biashara, kwa nini bidhaa zetu haziingi Tanzania? Kwa sababu wametuwekea kodi ya juu”.

    Duale aliwataka wabunge kutolichukulia swala hilo na hisia, bali kuchukua tahadhari wanapochukua jukumu lao la kuwalinda raia wa kawaida.

    ”Kama bunge ni lazima tuamue na kuleta sheria zitakazolinda biashara zetu. Munaweza kumshutumu Jaguar, lakini leo ndiye mbunge maarufu zaidi katika eneo bunge lake”, aliongezea Duale.

    Nae mbunge wa Ugenya David Ochieng, kwa upande wake aliilaumu idadi kuu ya raia wa kigeni wanaofanya biashara nchini Kenya kwa kushindwa kwa serikali kuidhinisha sera yake.

    ”Katika uchumi wa leo , ni rahisi kununua bidhaa kutoka mataifa jirani kama vile Tanzania na Uganda na kuleta Kenya. Sio kwamba hatuna sheria, ni swala la utekelezwaji na ufisadi. Tunwaruhusu watu kuingia nchini na kuanza kuuza vitu barabarani. Huwezi kuwalaumu Watanzania kwa kufanya hivyo ni kwa sababu ya mfumo wetu ambao ni dhaifu”, alisema Ochieng’.

    ”Hatuwakagui watu wanaoingia nchini. Watanzania wanafanya kazi yao, ndio sababu wanaweza kujua kwamba Mulinge hakuhitimu kufanya kazi Tanzania.

    Hatahivyo Mbunge huyo alishutumu matamshi ya Jaguar , huku akilitaka bunge hilo kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wabunge wanaoharibu jina la taifa hilo katika ulingo wa kimataifa.

    Tayari ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kupitia ukurasa wake wa Twitter imesema mbunge huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kuchochea ghasia.

    Katika kanda ya video iliosambazwa pakubwa nchini Kenya na katika nchi jirani Tanzania, mbunge huyo alisema hawatokubali watu wa nje waje kuendesha biashara nchini humo.

  • Kiboko cha mbu wa malaria chapatikana

    Kiboko cha mbu wa malaria chapatikana

    Ukungu (fangasi) – ambao umeboreshwa kisayansi kutoa sumu ya buibui – unaweza kuua idadi kubwa ya mbu wanaoambukiza malaraia, utafiti mpya wa kisayansi umebaini.

    Majaribio ya ukungu huo, ambayo yamefanyika nchini Burkina Faso, Afrika Magharibi yameonesha kuwa idadi ya mbu iliteketezwa kwa 99% ndani ya siku 45.

    Watafiti wanasema si lengo lao kutokomeza mbu hao bali kusaidia kuzuia maambukizi ya malaria.

    Ugonjwa wa malaria, unaoambukizwa na mbu jike aina ya Anopheles wanyonyao damu huua zaidi ya watu 400,000 kwa mwaka.

    Duniani kote, wagonjwa milioni 219 wa malaria kila mwaka huripotiwa.

    Utafiti huo umefanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Maryland cha Marekani – na kituo cha utafiti cha IRSS cha Burkina Faso.

    Wataalamu hao kwanza walianza kwa kutambua kuvu ama ukungu aina ya Metarhizium pingshaense ambao kiasili kudhuru mbu waambukizao malaria.

    Hatua iliyofuatia ilikuwa ni kuuongezea nguvu ukungu huo.

    “Kuvu hiyo ni rahisi kuiongezea kitu kisayansi, hivyo ni rahisi kuifanyia uhandisi jeni,” amesema Profesa Raymond St Leger, kutoka Chuo Kikuu cha Maryland.

    Wanasayansi hao wakageukia sumu itokanayo na aina ya buibui wa funnel kutoka Australia.

    Vipimo vya maambara vikathibitisha ufanisi wa kiwango cha juu cha sumu hiyo katika kuteketeza mbu.

    Baada ya maabara, wataalamu hao wakatengeneza kijiji maalum kwa ajili ya utafiti nchini Burkina Faso.

    Kijiji hicho kilizungushiwa neti ili kuzuia ukungu ama mbu kutoka kwenye eneo la utafiti.

    Ukungu huo kisha ukachanganywa na mafuta ya ufuta na kumwagiwa kwenye mashuka meusi ya pamba.

    Mbu hao walidhurika punde tu walipotuwa kwenye mashuka hayo.

    Watafiti walianza kazi hiyo na mbu 1,500.

    Matokeo ya utafiti huo, yaliyochapishwa kwenye jarida la kisayansi yalionesha kuwa idadi ya mbu inaongezeka kama wakiachwa bila ya ukungu.

    Ila, baada ya ukungu wenye sumu kuingizwa kwenye kijiji hicho, walisalia mbu 13 tu baada ya siku 45.

    Aina mpya za kupambana na malaria zinahitajika kwa haraka duniani, kutokana na mbu hao kutengeneza usugu wa dawa.

    Shirika la Afya Duniani (WHO) tayari limeshaonya kuwa idadi ya wagonjwa itaendelea kuongezeka kwenye nchi 10 ambazi zimeathirika zaid na malaria barani Afrika.

     

    cc;BBCswahili

  • Afa kwenye Ndege kwa kumeza dawa za kulevya

    Afa kwenye Ndege kwa kumeza dawa za kulevya

    Mwanaume mmoja raia wa Japan, amepoteza maisha ndani ya Ndege akitokea Mexico City baada ya kumeza kete 246 za Cocaine.

    Ndege hiyo, iliyokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Narita nchini Japan ililazimika kutua kwa dharura katika jimbo la Sonora nchini Mexico mwanaume huyo alipoanza kupoteza fahamu.

    Mamlaka zimesema mtu huyo aliyejulikana kwa jini la Udo N, alipoteza maisha baada ya ubongo wake kujaa maji kutokana na matumizi ya madawa kupita kiasi.

    Kwa mujibu wa taarifa ya mwanasheria mkuu wa jimbo la Sonora, Kete zilizokua na urefu wa sentimita 2.5 na upana wa sentimita 1 zilikutwa tumboni na kwenye utumbo wakati wa uchunguzi.

    Abiria wengine 198 waliobaki waliendelea na safari baada ya kutua kwa dharura katika mji wa Hermosillo.

    Mamlaka za Mexico zimesema zitaendelea na uchunguzi.

     

  • Kafulila autaka mpango kazi wa kisheria kukamilika mapema

    Kafulila autaka mpango kazi wa kisheria kukamilika mapema

    Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, David Kafulila ameutaka mpango kazi wa kuratibu taasisi na mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kwa wananchi ukamailike haraka ili wananchi wapate huduma ya usaidizi wa kisheria kwa ufanisi.

    Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa msaada wa kisheria kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe.

    “Watu wengi wamepoteza haki zao kwa kutokujua sheria au kutokuwa na fedha za kumudu gharama za mawakili lakini serikali imetengeneza utaratibu wa kuratibu taasisi ambazo zinatoa msaada wa kisheria bila malipo ili wananchi wengi zaidi wasiojiweza waweze kupata msaada wa kisheria na wasikose haki zao,” amesema Kafulila.

    Amesema kuwa mpango kazi wa kuziratibu taasisi zinazotoa msaada wa kisheria uwe unapimika na hasa uwe na lengo la kutoa elimu kwa wananchi ili wajue kuwa hata kama hawana fedha za kugharimia mawakili wa kuwatetea ili wapate haki zao.

    Naye Msajili wa Mashirika na taasisi zinazotoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Felista Joseph amesema kuwa elimu kwa umma itapewa kipaumbele katika mpango kazi huo na ni jambo la msingi ili wananchi wafahamu uwepo wa taasisi hizo

    Kwa upande wake Mratibu wa shirika la Gender and Social Reform, Steward Shiwuga amesema shirika lake limekuwa likipata vikwazo katika kutoa msaada wa kisheria bila gharama yoyote na pia baadhi ya watendaji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwao.

    Msajili Msaidizi wa Taasisi za Msaada wa kisheria kwa Wilaya ya Ileje, Rodrick Sengela amesema kuwa hapo awali taasisi hizo zilijiendesha bila kuratibiwa pia baadhi ya watu wasio waaminifu walikuwa wakiwarubuni wananchi na kuwatoza fedha nyingi pale wanapohitaji msaada wa kisheria lakini kwa sasa wananchi wataelimisha mahali sahihi pa kupata msaada wa kisheria bila malipo

  • Berahino apatikana na hatia ya kuendesha gari akiwa mlevi

    Berahino apatikana na hatia ya kuendesha gari akiwa mlevi

    Mchezaji soka Saido Berahino amepatikana na hatia ya kuendesha gari huku akiwa amekunywa pombe.

    Mshambuliaji wa Stoke City alikuwa amezidisha takriban mara tatu ya kiwango cha kileo wakati wakati gari lake aina ya Range Rover liliposimamishwa katika eneo la West End jijini London majira ya saa tisa usiku tarehe 18 Februari.

    Mahakama ya Highbury Corner ilisikiliza kesi ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 25-ambaye alikamatwa dakika chache baada ya kuibiwa.

    Mahakimu walisema”hakuwa na uoga wa kifo wala wa kujeruhiwa vibaya ” kabla ya kumpiga faini ya £75,000 na kumzuwia kuendesha gari kwa kipindi cha miezi 30.

    mahakama iliambiwa kuwa “hapakuwa na mzozo ” juu ya wizi , ulionaswa na kamera za CCTV, lakini wakili wa Berahino Garry Green alidai kuwa muhimu katika kesi ilikuwa ni “ikiwa mteja ilikuwa ni muhimu kwa mteja kuendesha gari lake au la “.

    Jaji mkuu Mark Oxenham alisema kuwa rafiki wa kike wa Berahino alikuwa meendesha gari hilo kabla na “angeweza kuendelea na safari kutoka kwenye eneo la tukio “.

    Mahakama iliambiwa kuwa mchezaji huyo wa kimataoifa wa Burundi awali alipatikana na hatia ya kuendesha akiwa amelewa mnamo mwaka 2015 na ya kuwa mmiliki wa gari lililoendeshwa na mlevi being mwaka 2012.

    Katika usiku alipokamatwa, polisi waliitwa kutokana na ripoti ya uwezekano wa tukio la kudungwa kisu kwa watu saba nje ya mgahawa wa VQ Cafe, katika mtaa wa Great Russell.

    Berahino,ambaye ni mkaazi wa Old Penkridge Road, Staffordshire alikuwa anaendesha gari ya Range Rover wakati polisi walipolisimamisha katika eneo la Bedford Square.

    Aliulizwa kuhusu mapigano, lakini hakuwa ameona chochote, alisema mwendesha mashtaka Katie Weiss.

    Kamishna wa polisi Stephen Luu alisema kuwa dereva alionekana “muoga” na alikuwa ” alikuwa anapumua hewa yenye harufu ya pombe.

    Berahino alipatikana amekunywa mililita103 za pombe mililita 100 za hewa, iliambiwa mahakama . Kiwango kinachokubalika kisheria ni miligramu 35.

    Aliwaambia polisi kuwa aliibiwa, huku rafiki yake wa kike akisema anaamini rafiki yake wa zamani wa kiume alikuwa amepanga Berahino asha,mbuliwe, iliambiwa mahakama.

    Mahakama iliambiwa kiuwa Berahino kwa sasa hana kipato, kwasababu amesimamishwa kucheza na Stoke bila malipo na ana gharama za malipo ya £20,000 kila mwezi.

    Mzaliwa huyo wa Burundi aloiyejiunga na Stoke kutoka West Brom kwa mkataba wa awali wa £12m mwezi Januari January 2017, anatarajiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika linaloanza mwezi Juni.

    “Nilikuwa naogopa . nilikuwa tu ndio nimeshambuliwa na mpwa wangu alikuwepo pale na nilipaswa kuchukua hatua. ilinibidi niendeshe haraka kutoka eneo la tukio ,”alisema.

    “Walikuwa na kisu na bunduki pia .”

    Alisema hakuwaarifu polisi mara moja juu ya wizi baada ya kuitwa .

    “Siku za nyuma nimekuwa katika vyombo vya habari na sikutaka lolote litangazwe kunihusu ,” alisema.

    “Ineharibu taaluma yangu nilikuwa naogopa hilo.

    “Hicho hi kitu ambacho sikukitaka kabisa.”

  • marufuku ya vipodozi vinavyobadili rangi ya mwili

    marufuku ya vipodozi vinavyobadili rangi ya mwili

    Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limepitisha azimio linalotoa wito wa kuwekwa kwa marufuku dhidi ya watengenezaji na waagizaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone.

    Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni, mafuta na urembo wenye kemikali ya hydroquinone inayobadilisha ngozi kuwa nyeupe.

    Hydroquinone ni kemikali inayopatikana katika aina mbali mbali za bidhaa mbali mbali za mwili ambayo kwa kawaida imetengenezwa kwa ajili ya kuifanya ngozi kuwa nyeupe.

    “Athari za vipodozi vyenye hydroquinone zinaonekanana zimesambaa katika jumuiya nzima ya Afrika mashariki ,” alisema Gideon Gatpan, mwanasheria kutoka Sudan Kusini.

    Chini ya kipengele 81(2) cha mkataba ulioanzishwa na Jumuiya ya Afrika Mashrariki ,unaotambua umuhimu wa nchi wanachama katika kuweka viwango, na vipimo, wabunge wamependekeza Baraza la Mawaziri liundwe kwa ajili ya kuchunguza aina za kemikali zilizopo ndani yabidhaa za urembo kama moja ya viwango vya lazima katika kanda ya Afrika Mashariki.

    “Baadhi ya bidhaa hizi huwa zina hadi 6% ya kemikali ya hydroquinone,”alisema mbunge kutoka Uganda Suzan Nakawuki.

    Jane Ndagire alitumia mafuta yanayochubua mwili kwenye uso wake kwa miaka kadhaa

    Kenya na Rwanda, sawa na Afrika Kusini , Ghana na Ivory Coast , zimekwishaweka hatua za sheria za udhibiti au marufuku ya uagizwaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone.

    Wataalamu wa masuala ya ngozi wanasema Kemikali ya hydroquinone inaweza kusababisha muwasho wa ngozi, mzio wa ngozi, kuchubuka kwa ngozi na kusababisha mabaka meusi na meupe na hata saratani ya ngozi.

    Namna hydroquinone inavyobadili ngozi:

    • Katika ngozi ya mwanadamu kuna chembechembe ambazo huitwa melanin.
    • Kemikali ya Hydroquinone inakwenda kuzuia utengenezaji wa melanin.
    • kwenye mwili wako hivyo ngozi kupoteza rangi yake ya asili na ulinzi kutokana na miale ya jua yenye madhara Kazi ya chembe chembe hizi ni kuipa Rangi ngozi yako na kuilinda kutokana ni miale ya jua yenye madhara.
    • Kemikali ya Hydroquinone inakwenda kuzuia utengenezaji wa melanin kwenye mwili wako hivyo ngozi kupoteza Rangi yake ya asili na ulinzi kutokana na miale ya jua yenye madhara.
  • Wanasayansi wagundua mti mrefu zaidi duniani

    Wanasayansi wagundua mti mrefu zaidi duniani

    Wanasayansi nchini Uingereza na Malaysia wanasema kuwa wamegundua mti mrefu zaidi duniani wenye urefu wa zaidi ya mita 100.

    Mti huo wa kitropiki aina ya meranti ulipatikana katika msitu wa Borneo na kundi moja kutoka chuo kikuu cha Nottingham mwaka uliopita.

    Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Oxford walifanya utafiti huo kwa kutumia kamera zisizokuwa na rubani kuthibitisha rekodi hio.

    Mti huo uliopatikana katika eneo la uhifadhi la Danum Valley huko Sabah umepewa jina Menara ambalo linamaanisha jumba refu.

    Mkweaji miti kutoka eneo hilo, jami ambaye aliupima mti huo kwa kutumia kamba alisema alliogopa kuupanda mti huo

    ”Lakini kwa kweli picha kutoka juu ilikuwa nzuri mno. Sijui cha kusema isipokuwa tu ulikuwa uzoefu mzuri sana”, aliongezea.

    Daktari Doreen Boyd, kutoka chuo kikuu cha Nottingham, alisema kuwa ugunduzi huo ulikuwa muhimu kwa kuwa ni sayansi inayosema miti kama hii inapatikana , ni mirefu hali ya kwamba hatukuwahi kudhania na huenda kuna miti mirefu zaidi ambayo haijagunduliwa.

    ”Inatuambia kwamba tunahitaji kuilinda miti”, alisema.

    Daktari Alexander Shenkin , kutoka chuo kikuu cha Oxford , alisema baada ya kusikia ugunduzi huo walitembea kwa muda wa saa tatu hadi Menara.

    Alisema: Nimeona kile ambacho wanasema ni miti mingi , lakini nilipotembea hadi katika mti huu, kichwa changu kilizidi kuangalia juu unapokaribia kileleni.

    Sijawahi kuona mti mrefu kama huu.

  • Maandamano yakumba mpaka wa Kenya na Tanzania, kunani?

    Maandamano yakumba mpaka wa Kenya na Tanzania, kunani?

    Maandamano yamekumba mji wa mpakani wa Namanga uliopo kati ya kenya na Tanzania.

    Kulingana na maafisa wa polisi maandamano hayo yalizuka kufuatia kutekwa nyara kwa mfanyibishara mmoja wa Kenya ambaye waandamanji hao wanasema alipelkekwa nchini Tanzania.

    Mfanyikazi wa ofisi ya serikali katika mji huo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa waandamanaji hao waliojawa na ghadhabu walifunga barabara inayoelekea Tanzania na hivyobasi kukatiza uchukuzi kutoka na kuelekea nchini humo.

    Anasema hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi wakati maafisa wa polisi wa Tanzania walipowasili karibu na ukuta unaogawanya Kenya na Tanzania ambapo waandamanaji waliingiwa na mori na kuanza kukabiliana na maafisa hao ambapo walirusha vitoa machozi .

    Anasema kuwa Wakenya walitumia fursa ya upepo mkali uliokuwa ukielekea upande wa Tanzania ambapo waliokota na kurudisha vitoa machozi hivyo .

    Wakati hali hiyo iliposhindwa kudhibitika , anasema, maafisa wa polisi walipiga risasi hewani kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji hao kutoka Kenya.

    Kulingana na afisa huyo maafisa wa Polisi wa Kenya wamekuwa wakipiga doria katika eneo hilo huku wakiwaomba waandamanaji hao kuwa watulivu.

    Wakaazi waombwa kuwa watulivu

    Mfanyibiashara huyo anayejulikana kwa jina Moha alidaiwa kuchukuliwa kutoka eneo analofanya kazi na gari lenya sajili za Tanzania.

    ”Tangu alipochukuliwa usiku uliopita hajaonekana”, alisema mmoja wa wakaazi wa eneo hilo Odinga Nguduu.

    Akizungumzia kuhusu ufungaji wa barabara mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe alisema kuwa ni makosa kwa kundi lolote kusimamisha magari yanayovuka mpaka.

    ”Hiyo ni kinyume na sheria hivyobasi tutalazimika kutumia uwezo wa serikali kusitisha wazimu huu”, alisema.

    Mwaisumbe aliwashauri wakaazi wa namanga kuwa watulivu huku serikali ikichunguza swala hilo.

    ”Hakuna haja ya vurugu kwa kuwa sasa tunachunguza swala hili tujue ni akina nani waliotekeleza kitendo hicho kwa lengo la kuweza kuwachukulia hatua kali za kisheria”, aliongezea.

    Gazeti la The Citizen nchini Tanzania limeelezwa kwamba kamishna wa jimbo la Arusha Jonathan Shanni alizuru mji wa Namanga ili kuchunguza hali ilivyo.

  • Wasiochukua Vitambulisho Mtwara Watahadharishwa

    Wasiochukua Vitambulisho Mtwara Watahadharishwa

    Serikali wilaya ya Mtwara Mjini imewatahadharisha wafanyabiashara wilayani humo kwa kuwataka kila mmoja kutambua wajibu wake, ambapo hatua kali zitakuchuliwa kwa atakayekutwa hana Leseni wala Kitambulisho cha msamahama wa Kodi kama ilivyoelekezwa na Rais Dkt. Magufuli

    Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda katika kikao na Watendaji wa Kata na Mitaa wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, kikao kilicholenga kuwahamasisha watendaji hao kutoa elimu kwa wananchi kuwataka kuchangamkia Vitambulisho vya wajasiliamali vilivyotolewa na Rais.

    Amesema kuwa wajibu wa serikali ni kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabishara kuweza kuendesha shughuli zao kwa uhuru lakini pia wajibu wa wafanyabiashara hao ni kuhakikisha wanalipa Kodi kwa walio na vigezo.

    “Kila mtu anayefanya shughuli zake ajulikane hasa kama anafanya biashara/Mjasiriamali, kama ni mfanyabiashara mkubwa mtakua mnamfahamu, kama ni Mdogo mnamfahamu kwasababu jitihada za serikali ni kurasimusha wajasiliamali wadogo kwa kuwapa vitambulisho ili waweze kuingia kwenye mfumo wafahamike,Amesema DC Mmanda.

    Aidha, amesema Msimamo wa serikali ni kutambua shughuli zote zinazofanyika ukizingatia tayari ilishatolewa miongozo na viongozi wa kitaifa juu ya wajibu wa Wafanyabiashara ikiwemo kuwatambua wajasiliamali wadogo ambao wamepewa vitambulisho vya msamaha wa Kodi.

    Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Kasilda Mgeni amewataka watendaji hao wa Kata na Mitaa kuendelea kuwajibika katika nafasi zao hususani kuhamasisha wananchi wanao waongoza juu ya zoezi hilo la Vitambulisho.

    Hata hivyo, Serikali wilayani Mtwara imetoa msisitizo kwa Wajasiliamali hao kuitikia wito kwa kuchukua vitambulisho hivyo vilivyotolewa  na Rais ili kuondokana na usumbufu ambao unaweza kujitokjeza.

     

  • Rais Magufuli astopisha bomoa bomoa makazi holela

    Rais Magufuli astopisha bomoa bomoa makazi holela

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa serikali ya awamu ya tano ni Serikali inayojali wananchi wake hivyo kuanzia sasa amesitisha zoezi zima la kubomoa makazi ya watu yaliyojengwa bila kufuata mpango mji.

    Rais ameelekeza kuwa nyumba hizo zisibomolewe kwa kuwa hayakuwa makosa yao kujenga katika maeneo hayo na kuelekeza kuwa watu wote wasio na hati miliki za ardhi kufanyiwa urasimishaji wa makazi yao.

    ”Serikali ya awamu ya tano kuanzia sasa haitabomoa tena nyumba za wananchi waliojenga maeneo ya makazi yasiyo rasmi badala yake itarasimisha makazi holela” Amesema Rais Mgufuli.

    Hayo yamekaziwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, William Lukuvi alipokuwa wilayani Simanjiro mkoani Manyara akifanya ziara yake ya kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi kwa wakazi wa mji huo, ambapo amewataka wananchi wote wachangamkie fursa hiyo iliyotolewa na Rais.

    “Serikali ya awamu ya tano inajali sana wananchi wake kwakuwa zamani wananchi ambao hawakujenga kwa kufuata mipango miji wangebomolewa nyumba zao, lakini kwa sasa imeanzisha mpango kurasimisha makazi holela na kuwapatia hati wananchi wote waishio mijini ili waishi katika makazi rasmi”, amesema Lukuvi.

    Pamoja na hayo Lukuvi amewataka wananchi wote waishio mijini kuwa wazalendo kwa kurasimisha maeneo yao waweze kujipatia hati na ili walipe kodi ya pango la ardhi jambo ambalo litaiongezea Serikali mapato