Category: Slider

  • Dk. Mukwege na Murad washinda Tuzo ya Nobel ya Amani

    Dk. Mukwege na Murad washinda Tuzo ya Nobel ya Amani

    Daktari raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Dennis Mukwege na mwanaharakati kutoka jamii ya Wayazidi, Nadia Murad, wameshinda Tuzo ya Nobel ya Amani, 2018 kwa jitihada zao za kupambana na unyanyasaji wa kingono.

    Tangazo la ushindi wa Dk. Mukwege na Murad wa Tuzo ya Nobel limetolewa na mwenyekiti wa kamati ya tuzo hiyo Berit Reiss-Andersen mjini Oslo muda mchache uliopita. Bi Reiss Andersen amesema wote wawili wamekuwa nembo ya mapambano dhidi ya janga la unyanyasaji wa kingono, ambalo limeenea kutoka mzozo mmoja hadi mwingine, kama vuguvugu la MeeToo lilivyodhihirisha.

    ”Washindi hawa wawili wametoa mchango mkubwa katika kuumulika na kuupinga uhalifu huo wa kivita. Dennis Mukwege ni mtu aliyejitolea maisha yake kuwasaidia wahanga hao. Nadia Murad ni shahidi anayesimulia unyanyasaji, uliofanywa dhidi yake na dhidi ya wengine.” Amesema Reiss-Andersen.

  • Raila asema lazima mabadiliko ya katiba Kenya yafanyike

    Raila asema lazima mabadiliko ya katiba Kenya yafanyike

     

    Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema kwamba mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo hayawezi kuepukika kwa namna yoyote ile na kwamba hata walio madarakani hawawezi kuzuia kura ya maoni kuhusu katiba, ili kusuluhisha matatizo yanayo ikabili nchi hiyo.

  • Afrika yaelekea kuzidiwa na watu

    Afrika yaelekea kuzidiwa na watu

    Idadi ya watu barani Afrika inakuwa kwa kasi ambapo kufikia mwaka 2050 itakuwa imeongezeka maradufu ya ilivyo sasa, huku 40% ya watu masikini kabisa duniani wakihofiwa kuja kuishi kwenye mataifa mawili tu ya bara hilo.

    Kwa sasa barani Afrika wanaishi watu bilioni 1.3. Miaka 32 ijayo, idadi hii itaongezeka mara mbili zaidi, na kama ukuwaji wa kiuchumi hautakwenda sambamba na ukuwaji huu wa idadi ya watu, basi kitakachotokea ni ongezeko la umasikini.

    Khofu hiyo imeufanya Wakfu wa mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates, kufanya utafiti wa namna ya kukabiliana na kitisho kijacho. Yaliyogunduliwa na utafiti huo uliopewa jina “Walindamlango 2018” ni kwamba ikifika mwaka 2050, asilimia 40 ya watu walio masikini sana duniani watakuwa wanaishi kwenye mataifa mawili tu: Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Hivi sasa, Nigeria inakaliwa na watu milioni 190, ambapo kwa wastani mwanamke mmoja huzaa watoto watano, na hilo lina matokeo yake, kwa mujibu wa Farouk Jega, mkurugenzi wa Wakfu wa Bill na Melinda Gates nchini Nigeria:

    “Tayari hali ni mbaya hapa Nigeria. Umasikini wa kutupwa unazalisha hali ya ukosefu wa usalama, machafuko, uhalifu. Lakini serikali ya Nigeria inajaribu kukabiliana na ongezeko hili la kupindukia la idadi ya watu. Waziri wa afya anapigia kampeni njia za kisasa za uzazi wa mpango. Lakini ni asilimia 10 ya wanawake wanaotumia njia hizo, ambayo ni idadi ndogo. Gharama pia ni kubwa, hasa kwa wanawake na familia za kimasikini,” anasema Jega.

    Kama ilivyo kwenye mataifa mengine mengi ya Afrika, jukumu la mwanamke nchini Nigeria ni lile lile la kuzaa, kulea watoto na kuhudumia nyumba. Serikali ya Nigeria inapambana kubadili mtazamo huu kwa kushirikiana na asasi za kijamii, viongozi wa kidini na kimila, anasema Faouk Jega, ambaye anaona kuwa kuna aina fulani ya mafanikio kwenye ushirikiano huu.

    Angalau sasa raia wako tayari kujadili faida na hasara za kuwa na watoto wengi na ile mila kwamba mwenye watoto wengi anakuwa amejijengea uhakika wa kuwa na watu wa kumuangalia afikiapo umri wa uzee. Hata hivyo, naye mkurugenzi huyo wa Wakfu wa Bill na Melinda Gates nchini Nigeria, anakiri kuwa: “Panahitajika juhudi kubwa zaidi kubadili imani na mitazamo ya watu.”

  • Tetemeko la ardhi Indonesia: Idadi ya waliofariki dunia yafika takriban watu 832

    Tetemeko la ardhi Indonesia: Idadi ya waliofariki dunia yafika takriban watu 832

    Takriban watu 832 wameuawa baada ya tetemeko kubwa la ardhi na tsunami kupiga kisiwa cha Indonesia cha Sulawezi, kwa mujibu wa shirika la majanga la kitaifa.

    Juhudi za kuwatafuta manusura zinaendelea na idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda pakubwa maeneo mengi ambayo kufikia sasa hayajafikiwa na waokoaji yakifikiwa.
    Shirika hilo liloongeza kuwa eneo lililoathiriwa lilikuwa kubwa kuliko iliyodhaniwa.
    Watu wengine waliripotiwa kukwama kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomka siku ya Ijumaa.

     

  • Ujerumani Yakana Tuhuma za Ubaguzi Dhidi ya Özil

    Ujerumani Yakana Tuhuma za Ubaguzi Dhidi ya Özil

    Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB), limekana kuhusika na tuhuma za ubaguzi dhidi ya mwanasoka, Mesut Özil (29) na kusema kuwa lilipaswa kuwajibika kuhakikisha mchezaji huyo habaguliwi. Özil ametangaza kutoichezea tena timu ya taifa ya Ujerumani kutokana na kukithiri kwa vitendo na maneno ya kibaguzi dhidi yake.

    Özil alishutumiwa na DFB kupitia vyombo vya habari vya Ujerumani baada ya picha akiwa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kusambaa katika vyombo mbalimbali vya habari. Mchezaji huyo wa Klabu ya Arsenal FC alishutumiwa zaidi baada ya Ujerumani kutolewa katika hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia.

    DFB limekiri kwamba huenda halikulishughulikia suala hilo ipasavyo, na kuongeza kuwa linasikitisha kuwa Mesut Ozil amehisi hakulindwa vya kutosha dhidi ya kauli za kibaguzi Ujerumani haikubaliani na mwenendo wa nchi ya Uturuki hasa baada jaribio la mapinduzi kukwama. Maelfu ya watu wanashikiliwa na Serikali huku wengine wakiachishwa kazi.

  • Waziri wa Nishati Ahukumiwa Jela Miaka Minne kwa Rushwa

    Waziri wa Nishati Ahukumiwa Jela Miaka Minne kwa Rushwa

    WAZIRI wa zamani wa Nishati wa Zimbabwe, Samuel Undenge, amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa ya rushwa

    Waziri huyo aliyefanya kazi kipindi ya Rais Robert Mugabe amekuwa kiongozi wa kwanza kuhukumiwa tangu kiongozi huyo aondolewe madarakani ambapo alituhumiwa kusaini mikataba na kuzilipa kampuni ambazo hazikuwahi kufanya kazi (kampuni hewa) ikiwemo Zimbabwe Power Company (ZPC) kiasi cha dola za Marekani 12,650, (sawa na Tsh. Milioni 28.6) mwaka 2016.

    Aidha, wakili wa Undenge amesema atakata rufaa juu ya hukumu hiyo kwa kuwa imekuwa ya kushtua mno

    Wakati huohuo, waziri wa zamani wa mambo ya nje, Walter Mzembi, anakabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya ofisi ya umma ambapo pia waziri wa zamaani wa fedha, Ignatius Chombo, akishitakiwa kwa makosa ya rushwa. Mawaziri wote hao wamekana mashitaka yao.

  • Rais Magufuli Ashuhudia Utiaji Saini Daraja la Salander

    Rais Magufuli Ashuhudia Utiaji Saini Daraja la Salander

    Rais John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Korea Lee Nak-yeon leo wanashuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa daraja jipya la Selander jijini Dar na njia zake.

    Hafla ya utiaji saini wa mkataba huo inafanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo serikali kupitia wakala wa barabara Tanzania (Tanroads) inatiliana saini na mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja hilo.

    Daraja la Salander litaunganisha eneo la Aga Khan katika barabara ya Barack Obama na eneo la Coco Beach Katika Makutano ya baabara za Kenyatta na Toure.

  • WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU MICHANGO YA SHULE

    WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU MICHANGO YA SHULE

    WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hakuna michango yoyote itakayokusanywa kutoka kwa wazazi kwa ajili ya shule kama haina kibali cha Mkurugenzi wa Halmashuri.

     

    “Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli alishapiga marufuku michango ya aina hii na akatangaza mpango wa elimumsingi bila malipo. Sasa hivi zinaletwa zaidi ya sh. bilioni 20 kila mwezi kwa ajii ya kuboresha elimu ya msingi katika kila wilaya.”

     

    Waziri Mkuu ametoa katazo hilo jana (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa wa Kahama, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

     

    Alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Kahama, Bw. Jumanne Kishimba ambaye alisema kuna michango inatozwa bila kibali chochote na kwamba kila kaya inatakiwa ilipe sh. 20,000. “Michango hii itolewe kwa kibali ina iangalie uwezo wa familia kiuchumi,” alisema.

     

    Akitoa mfano, Mbunge hiyo alisema kuna familia ina madebe matatu tu ya mahindi ukiitoza hiyo hela, manake wauze mahindi yao yote ndiyo walete ya michango ma hiyo wabaki na njaa kwa mwaka mzima. Ni vema michango hiyo izingatie kipato halisi cha kaya,” alisema,

     

    Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao juhudi mbalimbali ambazo Serikali imezichukua ili kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma za maji, umeme, elimu na afya.

     

    Alisema ameridhishwa na ujenzi wa viwanda unaoendelea kwenye mkoa wa Shinyanga na kukiri kuwa ameguswa kuona kuna uzalishaji mkubwa wa mafuta ya kula yanayotokana na mazao ya mbegu kama pamba na alizeti wakati kuna watu wanaagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

     

    “Nimetembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya pamba cha Kahama Oil Mills, na mwenye kiwanda ameniambia kuwa miaka yote huwa anafanya kazi kwa miezi mitatu tu lakini mwaka huu ana uhakika wa kufanya kazi kwa miezi tisa, kutokana na jinsi ambavyo wakulima wameitikia wito wa kufufua zao la pamba,” alisema.

     

    “Jana pia nilitembelea kiwanda cha JIELONG ambacho kiko kwenye Manispaa ya Shinyanga. Na kwenyewe nimeona uzalishaji mkubwa wa mafuta ya kula ambao sijapata kuona,” alisema Waziri Mkuu.

     

    Mapema,Waziri Mkuu alizindua kituo cha afya cha Mwendakulima ambacho kilianza kujengwa mwaka 2010 na kukamilika mwaka 2016 kwa ufadhili wa kampuni ya kuchimba madini ya ACACIA kupitia mpango wake wa Corporate Social Responsibility.

     

    Kampuni hiyo imejenga chumba cha wagonjwa wa nje (OPD), nyumba mbili za watumishi (2 in 1) ambazo zinakaliwa na watumishi wanne, wameweka vitanda na solar panel kwa gharama za dola za Marekani 710,000/- (kwa exchange rate ya kipindi hicho).

     

    (mwisho)

     

    IMETOLEWA NA:

    OFISI YA WAZIRI MKUU,

    JUMATATU, JULAI 16, 2018.

  • UFARANSA YAANZA VIZURI KOMBE LA DUNIA DHIDI YA AUSTRALIA

    UFARANSA YAANZA VIZURI KOMBE LA DUNIA DHIDI YA AUSTRALIA

    Ufaransa imefanikiwa kuibuka na ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Russia wa mabao 2-1 dhidi ya Australia.
    Mabao ya mchezo huo yametiwa kimiani na Antoine Griezmann katika dakika ya 58 kwa njia ya mkwaju wa penati na la pili likitiwa kimiani na Paul Pogba (80′).
    Bao pekee la Australia liliwekwa wavuni na Mile Jedinak mnamo dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati.
    Mechi hii imekuwa ya kwanza kushuhudiwa penati mbili ndani ya dakika 90 zikipigwa kwa pande zote.
    Ushindi huu wa Ufaransa unawapa alama tatu muhimu kwenye kundi C ambapo baadaye Peru na Denmark watakuwa wanacheza pia kutoka kundi hilo.
  • Walioshtakiwa ulaji rushwa Kenya kukaa rumande wiki moja

    Walioshtakiwa ulaji rushwa Kenya kukaa rumande wiki moja

    Watuhumiwa 24 walioshtakiwa kuhusiana na kashfa ya ufujaji wa pesa katika Shirika la Vijana wa huduma kwa Taifa (NYS) watakaa rumande kwa wiki moja.

    Jaji ameamuru wazuiliwe hadi Jumatano wiki ijayo ambapo uamuzi wa kuachiliwa kwa dahamana utatolewa.

    Miongoni mwa walioshtakiwa jana ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Jinsia Lilian Mbogo Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Richard Ndubai.

    Walikamatwa na wengine wakajisalimisha kwa polisi Jumatatu wiki hii na kisha kufikishwa kortini Milimani, Nairobi jana.

    Kikao cha kusikizwa kwa kesi dhidi yao kiliendelea hadi usiku wa manane.

    Upande wa mashtaka ulikuwa umepinga kuachiliwa kwao ukisema wanaweza kutoroka au kukosa kurejea mahakamani wakati wa kusikizwa kwa kesi dhidi yao.

  • Sikiliza Nyimbo mpya ya Ali Kiba “Mvumo wa Radi”

    Sikiliza Nyimbo mpya ya Ali Kiba “Mvumo wa Radi”

    Msanii Ali Kiba ameachia video ya wimbo mpya unaojulikana kwa jina la Mvumo wa Radi