Category: Slider

  • SERIKALI YATEKELEZA MAOMBI 5 YA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WILAYANI LONGIDO

    SERIKALI YATEKELEZA MAOMBI 5 YA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WILAYANI LONGIDO

    Baadhi ya mifugo wakiwa katika eneo la kunywa maji kablaya kuuzwa katika Soko la Kimkakati la Longido, Wilayani Longido ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

    Serikali kupitia, Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), imetekeleza maombi 5 ambayo yanawasaidia wafugaji hao  kuongeza thamani ya mifugo yao  kupitia Soko la Kimkakati la mifugo Longido lililojengwa na Program hiyo.
     
    Mwishoni mwa mwaka 2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira ,Kazi,  Vijana na Watu wenye Ulemavu ) Mhe.Jenista Mhagama, alikuwa na ziara ya kukagua  ujenzi wa soko hilo wilayani humo, ambapo  baada ya ukaguzi alikutana na wafanyabiashara ya mifugo, ambao  waliwasilisha maombi  5,  ambayo yangeweza kuongeza Thamani Biashara za Mifugo na kutatua  kero zote  za wafanyabiashara wa mifugo wilayani humo.
     
    “Serikali ya awamu ya tano imeamua kuwasikiliza watu wanyonge na ambao wanajituma kuchapa kazi, lakini pia lengo la Program ya MIVARF ni kuongeza kipato kwa  wananchi hasa waishio vijijini, kwa mantiki hiyo nilimuelekeza Mratibu wa Program Kutekeleza maombi yao haraka sana ili wafugaji hawa wapate tija ya ufugaji kupitia soko hili” alisema Mhagama
     
    Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Mifugo wilayani Longido, Saruni Laizer amesema maombi waliyowasilisha serikalini ili waweze kupata tija ya mifugo kupitia soko la Kimkakati la Mifugo Longido yamefanyiwa kazi na Program ya MIVARF ndani ya miezi mitatu tangu wayasilishe, ikiwa ni; Mizani ya kupima mifugo, Maji ya kunyweshea mifugo, machinjio, Josho, pamoja na  umeme.
     
    “Tulihitaji maji hapa ili mifugo isije ikafa wakati inasubiri kuuzwa kwa kukosa maji, lakini umeme hapa ni muhimu kwani biashara zetu zinafanyika usiku, tayari hadi jenereta imeletwa kwa ajili ya kuhakikisha biashara haikwami kwa dharura yoyote ile, lakini mizani itasaidia kutowauza mifugo kwa kuangalia kwa macho bali kwa uzito wao” alisema Laizer
     

     

  • RAISI WA PERU KUJIUZULU

    RAISI WA PERU KUJIUZULU

    Pedro Pablo Kuczynski

    Rais wa Peru Pedro Pablo Kuczynski amepata kuwasilisha barua yake ya kujihuzulu bungeni hapo jana. Hii ni kutokana na tuhuma za kununua kura zinazomkabili na serikali yake, Amefanya hivyo kutokana na mchakato uliopambana moto wa kutaka kumng’oa madarakani

  • KAMANDA MURILO ASEMA KUHUSU AFISA BALOZI WA SYRIA

    KAMANDA MURILO ASEMA KUHUSU AFISA BALOZI WA SYRIA

    Kamanda Jumanne Murilo

     

     

    Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Jumanne Murilo, amezungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake kuhusu kushambuliwa kwa nondo Afisa wa ubalozi wa Syria nchini H. Alfaori na kuibiwa Euro 93,000 sawa na Shilingi Milioni 251 za Kitanzania jana March 20.

    Hata hivyo kamanda mulilo amesema, kwasasa jeshi la polisi litaongea na ofisi nyingine za nje kabla ya kuajiri wawe wanaomba polisi iwasaidie jinsi kuwachunguza wale waliowapitisha wakitaka kuwaajiri.

  • BALCELONA YAIDHIBU  CHELSEA NA KUITOA NJEE YA MASHINDANO YA UEFA CHAMPIONI LIGI

    BALCELONA YAIDHIBU CHELSEA NA KUITOA NJEE YA MASHINDANO YA UEFA CHAMPIONI LIGI

     

    Baada ya Manchester United Jana kutupwa nje na Sevilla kutoka Hispain kwa kufungwa mabao 2-1, jana usiku ilikuwa ni zamu ya Chelsea Kutupwa Nje ya Mshindano ya Kombe la UEFA Championi Ligi na kufungwa Na Barcelona Mabao 3-0, magoli ya Barcelona yaliwekwa kimyani na Messi ambaye alifunga mabao 2, goli la kwanza alifunga dakika ya 2 na goli lake la pili alifunga kwenye dakika ya 63, na goli la tatu lilifungwa na Ousmane Dembele dakika ya 20.

    Kwa matokeo hayo Chelsea imeondoshwa kenye mashindano hayo kwa jumala ya mabaol 4-1, kutokana mchezo wa awali ulichezwa England timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

    Juzi Manchester United ilifungwa na Sevilla ya Hispain, na jana Chelsea ilifungwa na timu kutoka Hispain,

    JE KWA MATOKEO YA JUZI MANCHESTER DHIDI YA SEVILLA, NA JANA USIKU MATOKEO YA CHELSEA DHIDI YA BARCELONA

    KUNAUISHI TENA LIGI YA UINGEREZA NI BORA KULIKO YA HISPAIN ?

    https://youtu.be/GSPVaUUeA0U

  • MTI WAUA WATU 20 GHANA

    MTI WAUA WATU 20 GHANA

    Watu takriban 20 wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mti mkubwa kuwaangukia wakiogelea katika maporomoko ya maji eneo la Kintampo, Ghana.

    Maporomoko hayo ni maarufu sana kwa watalii.

    Watu hao walikuwa wakiogelea pale upepo mkubwa ulipoangusha mti na kusababisha mkasa huo, maafisa wa huduma za dharura wamesema.

    Msemaji wa taifa wa huduma za dharura Prince Billy Anaglate alisema kisa hicho kilitokea katika maporomoko ya Kintampo, katika jimbo la Brong-Ahafo.

    Kikosi cha pamoja na polisi na wahudumu za dharura kilifika eneo la mkasa kuwaokoa waliokwama chini ya mti huo.

    “Mti mkubwa ulianguka mvua kubwa iliyoandamana na upepo ilipokuwa inanyesha na kuwaangukia watu hao,” aliyeshuhudia aliambia Starr News ya Ghana.

    “WEngi walikuwa wanafunzi wa shule ya upili ya Wenchi Senior High. Wengine ni watalii. Tunajaribu kuwaokoa waliokwama chini ya mti huo kwa kuukata mti huo na matawi yake kwa msumeno.”

    Bw Anaglate aliambia AFP kwamba wanafunzi 18 walifariki papo hapo na wengine wawili wakafariki wakitibiwa hospitalini.

    ALisema watu 11 kwa sasa wanapokea matibabu, akiwemo mmoja wa maafisa wa shule hiyo aliyekuwa anasimamia ziara hiyo ya wanafunzi.

    Taarifa nyingine zinasema waliojeruhiwa ni zaidi ya 20.

    Wanatibiwa katika hospitali ya manispaa ya Kintampo.

    “Tunatuma salamu za rambirambi kwa familia za waliofariki na kuwaombea waliojeruhiwa,” waziri wa utalii wa Ghana Catherine Abelema Afeku alisema kupitia

  • KINA DADA WA ARSENAL WAILAZA TOTTENHAM 10-0

    KINA DADA WA ARSENAL WAILAZA TOTTENHAM 10-0

    Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Uingereza upande wa wawanawake Kina dada wa Arsenal waliwalaza wapinzani wao Tottenham 10-0 na kufika robo fainali Jumapili.

    Danielle van de Donk alifungia wenyeji hao mabao matatu, naye mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Beth Mead akafunga bao pia mechi yake ya kwanza kuchezea Arsenal.

    Chelsea, ambao walishindwa na Arsenal fainali mwaka jana, pia walipata ushindi mkubwa, kwa kulaza Doncaster 7-0.

    Bristol City walilaza Millwall 5-0.

    Liverpool, Notts County, Birmingham na Sunderland pia walishinda kwenye mechi hizo za raundi ya tano.

    Droo ya robofainali itafanyika baadaye Jumatatu.

  • UKWELI SAKATA LA SERIKALI KUUZIWA EKA MOJA KWA ZAIDI YA MILIONI MIA NANE

    UKWELI SAKATA LA SERIKALI KUUZIWA EKA MOJA KWA ZAIDI YA MILIONI MIA NANE

    Kampuni ya azimio estate iliyompa zawadi mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda inadaiwa kuhusika na wizi mkubwa wa pesa ya umma, baada ya kampuni hiyo kuingia mkataba na Shirika la taifa la hifadhi ya jamii (Nssf) wakuiuzia ardhi ekari 20,000 eneo la Dege Mbutu Kigamboni kwa makubaliano ya kila eka moja ni miloni ishirini na tano ( 25,000,000/=),  serikali ikalipa pesa yote.

    Serikali imekuja kupewa eka 3,000 tu hali inayotafsiriwa kuwa sasa imeuziwa eka moja kwa zaidi milioni mia nane (800,000,000/=).

    Bunge kupitia kamati yake imeiagiza takukuru kuchunguza wizi huu, ambapo kampuni hiyo imekiri udanganyifu huo na ikaamriwa
    kurudisha pesa na kusaini mkataba upya wa eka 3,000 zilizopo.

    Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Nssf, Prof Godius Kahyarara amekiri kuingia ubia na kampuni ya azimio lakini taarifa sahihi ni kwamba hawakuuziana kama inavyoelezwa
    bali wameingia ubia na mfanyabiashara huyo mohammed iqbal.

  • JPM AWANYIMA USINGIZI MAWAZIRI WAWILI

    JPM AWANYIMA USINGIZI MAWAZIRI WAWILI

    Rais John Magufuli amewataka watendaji wanaosimamia mradi wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam (Dart) kuhakikisha unaingiza faida kinyume na hapo hasara itakuwa kwao.

    Aidha, Rais Magufuli aliwataka mawaziri wanaosimamia mradi huo, George Simbachawene (Tamisemi) na Profesa Makame Mbarawa (Ujenzi) kumpatia taarifa inayoeleza kiasi cha fedha kilichoingia tangu mabasi hayo yaanze kufanya kazi.

  • UGANDA KUKIPIGA NA GHANA LEO

    UGANDA KUKIPIGA NA GHANA LEO

    Kocha wa Ghana Avram Grant amesema anataka kufika mbali zaidi katika fainali za mwaka huu tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015 walipofungwa na Ivory Coast kwa njia ya penalti.

    Mshambuliaji Asamoah Gyan na kiungo wa West Ham Andre Ayew walikuwa miongoni mwao miaka miwili iliyopita na uzoefu wao unatarajiwa kuwasaidia katika mchezo wa leo.

    Wachezaji wa Uganda Murushid Juuko na Khalid Aucho wote hawatakuwepo katika mchezo huo.

    Cranes wanaingia katika michuano hiyo tokea mwaka 1978 walipopoteza dhidi ya Ghana katika hatua ya fainali, lakini wakati huu wanaingia wakiwa ndio timu bora ya Afrika 2016.

    Katika mchezo wa mwisho kwa timu hizi kukutana zilitoka suluhu ya 0-0 na hapa ilikuwa kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 nchini Urusi.

    Ghana nao wanataka kushinda kombe hili ambalo hawajalipata tokea mwaka 1982.

  • HOLLANDE ASEMA ULAYA HAIHITAJI USHAURI WA TRUMP

    HOLLANDE ASEMA ULAYA HAIHITAJI USHAURI WA TRUMP

    Rais wa Ufaransa Francois Hollande amepuuzilia mbali hatua ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump kukosoa sera ya Ujerumani kuhusu wahamiaji barani Ulaya.

    Bw Hollande alisema hatua hiyo ya Bw Trump si ya busara.

    “[Ulaya] haihitaji ushauri kutoka nje, kuambiwa inafaa kufanya nini,” Bw Hollande alisema.

    Bw Trump alikuwa amesema Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alifanya “kosa kubwa” kwa kuwaruhusu wahamiaji kuingia nchini mwake kwa wingi.

    Bi Merkel kwa upande wake, akijibu tamko hilo la Trump, alisema bara Ulaya linafaa kuachwa lijifanyie maamuzi.

  • MTU WA MWISHO KUTEMBEA MWEZINI AFARIKI

    MTU WA MWISHO KUTEMBEA MWEZINI AFARIKI

    Mwana anga wa Marekani Gene Cernan, aliyekuwa binadamu wa mwisho kutembea kwenye Mwezi, amefariki dunia akiwa na miaka 82.

    Shirika la anga za juu la Marekani Nasa limesema limehuzunishwa sana kumpoteza mwana anga huyo mstaafu.

    _93621684_0cb24173-ee67-4f38-9c4d-8f8a5de9e989

    Cernan alikuwa mmoja wa watu watatu pekee waliowahi kwenda Mwezini mara tatu na ndiye binadamu aliyeukanyaga Mwezi mara ya mwisho kabisa, mwaka 1972.

    Maneno yake ya mwisho aliyoyasema kabla ya kuondoka kwenye Mwezi yalikuwa: “Tunaondoka jinsi tulivyokuja na, Mungu akitujalia, tutarejea na amani na matumaini kwa binadamu wote.”

    Alikuwa kamanda wa chombo cha anga za juu cha Apollo 17 wakati huo.

    Ni watu 12 pekee waliowahi kutembea kwenye Mwezi, na kati yao ni sita pekee ambao bado wako hai.