UGANDA KUKIPIGA NA GHANA LEO

UGANDA KUKIPIGA NA GHANA LEO

Like
354
0
Tuesday, 17 January 2017
Slider

Kocha wa Ghana Avram Grant amesema anataka kufika mbali zaidi katika fainali za mwaka huu tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015 walipofungwa na Ivory Coast kwa njia ya penalti.

Mshambuliaji Asamoah Gyan na kiungo wa West Ham Andre Ayew walikuwa miongoni mwao miaka miwili iliyopita na uzoefu wao unatarajiwa kuwasaidia katika mchezo wa leo.

Wachezaji wa Uganda Murushid Juuko na Khalid Aucho wote hawatakuwepo katika mchezo huo.

Cranes wanaingia katika michuano hiyo tokea mwaka 1978 walipopoteza dhidi ya Ghana katika hatua ya fainali, lakini wakati huu wanaingia wakiwa ndio timu bora ya Afrika 2016.

Katika mchezo wa mwisho kwa timu hizi kukutana zilitoka suluhu ya 0-0 na hapa ilikuwa kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 nchini Urusi.

Ghana nao wanataka kushinda kombe hili ambalo hawajalipata tokea mwaka 1982.

Comments are closed.