Category: Slider

  • RAIA WA CUBA KUANZA  KUINGIA MAREKANI KWA VIZA

    RAIA WA CUBA KUANZA KUINGIA MAREKANI KWA VIZA

    Marekani imesitisha sera ya muda mrefu ambayo ilikuwa inawapa raia wa Cuba hadhi maalumu ya kuingia na kuishi nchini Marekani bila ya visa.

    Serikali ya Cuba imekuwa ikilalamika kwamba, sera hiyo, ijulikanayo kama “wet foot, dry foot,” imewafanya maelfu ya raia wa Cuba kukimbia nchini humo kila mwaka.

    Rais Obama amesema hatua ya kuondolewa kwa sera hiyo, ni hatua muhimu katika kurudisha uhusiano na Cuba.

    Mahasimu hao wa muda mrefu wamerudisha uhusiano wa kidiplomasia mnamo mwaka 2015 baada ya karne ya uhasama.

  • MITANADAO YA UFARANSA ILIDUKULIWA MARA 24,000

    MITANADAO YA UFARANSA ILIDUKULIWA MARA 24,000

    Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, amesema mitandao ya idara za ulinzi za nchi zilishambuliwa mara 24,000 mwaka jana peke yake lakini udukuzi huo ulizimwa.

    Jean Yves-Le Drian, alisema udukuzi kama huo unaongezeka mara dufu kila mwaka.

    Alionya kuwa miundo mbinu ya taifa iko kwenye hatari, na kwamba kunaweza kufanywa jaribio la kuchafua uchaguzi wa mwaka huu.

    Bwana Le Drian amekuwa akisimamia mabadiliko makubwa katika mifumo ya mitandao ya Ufaransa, ambapo mkuu wa jeshi ataongoza operesheni mpya za komputa, Cybercom.

    Waziri huyo wa ulinzi alisema hayo alipozungumza na gazeti moja la Ufaransa, Le Journal du Dimanche, baada ya idara za usalama za Marekani, kusema kuwa Urusi ilijaribu kuingilia kati uchaguzi wa rais wa Marekani jambo ambalo Urusi inakanusha.

     

  • BORIS JOHNSON AKUTANA NA MAAFISA WA TRUMP

    BORIS JOHNSON AKUTANA NA MAAFISA WA TRUMP

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson amekutana na washauri wakuu wa rais mteule wa Marekani Donald Trump mjini New York, Marekani.

    Johnson alikuwa na shemejiye Trump, Jared Kuchner, na afisa mkuu wa mikakati wa Bw Trump Steve Bannon.

    Huo ulikuwa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana kati ya maafisa wa Trump na waziri wa Uingereza.

    Maafisa wanasema kwenye mkutano huo, sera ya Marekani kuhusu Syria, China na Urusi ilijadiliwa.

    Jumatatu, Bw Johnson atakuwa mjini Washington D.C, kukutana na maafisa wakuu wa bunge.

    Anatarajiwa kukutana na maafisa wakuu wa chama cha Republican katika Bunge la Congress akiwemo mwenyekiti wa kamati ya mashauri ya kigeni, Bob Corker na kiongozi wa Congress, Mitch McConnell.

    Hata hivyo, hatakutana na Rex Tillerson, anayetarajiwa kuwa waziri wa mambo ya nje chini ya Bw Trump.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Teresa May naye amesema kwamba amekuwa na mazungumzo ya kufana ya simu na Bw Trump.

    Awali Rais huyo mteule wa Marekani alionekana kumuunga mkono Nigel Farage mwanasiasa wa chama cha uzalendo na anayepinga Muungano wa Ulaya, kama balozi wa Uingereza nchini Marekani.

    Hii ilionekana kuwakera wakuu nchini Uingereza, licha ya taarifa kupinga hilo.

  • CRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA BALLON d’Or

    CRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA BALLON d’Or

    Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemshinda mpinzani wake Lionel Messi na kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or hii ikiwa ni kwa mara ya nne.

    Ronaldo mwenye miaka 31 sasa anahitaji tuzo moja tu kumfikia Messi ambaye mwaka jana alipata tuzo ya tano.

    Mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amemaliza katika nafasi ya tatu.

    Ronaldo aliisaidia Madrid kushinda ligi ya mabingwa ulaya msimu uliopita sambamba na kuisaidia nchi yake ya Ureno kushinda kombe la mataifa ya Ulaya 2016.

    Kwa sasa ameshinda Ballon d’Or 2008, 2013, 2014 na 2016 na tokea mwaka 2009 amekuwa akipokezana na Messi.

    ”sikuwahi kuwaza kama ningeshinda Ballon d’Or mara nne” nina furaha kubwa sana, najisikia fahari” alisema Ronaldo.

    ”Natumia nafasi hii kuwashukuru wachezaji wenzangu, timu yangu ya taifa, makocha na watru wote walionisaidia kupata tuzo hii.”

  • MPANGO WA UUZWAJI WA AC MILAN WASOGEZWA MBELE

    MPANGO WA UUZWAJI WA AC MILAN WASOGEZWA MBELE

    Mpango wa uuzwaji wa klabu ya Ac Milan wasogezawa mbele hadi mwakani mwezi wa tatu.
    Klabu hiyo ya nchini Italy inayomilikiwa na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Bwana Silvio Berlusconi ilitajwa kuuzwa kwa wawekezaji wa China mwezi huu wa kumi na mbili lakini mpango huo umesogezwa mbele hadi mwakani mwezi wa tatu,

  • MARTIN SAANYA NA SAMWELI MPENZU WAPIGWA CHINI

    MARTIN SAANYA NA SAMWELI MPENZU WAPIGWA CHINI

    Waamuzi waliochezesha mchezo namba 49 kati ya Yanga na Simba, Martin Saanya na Samweli Mpenzu wametolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, huku suala lao likipelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili ishughulikie tatizo lao kitaalam.

    Maamuzi hayo yamefanyika baada ya Kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya ligi, kuwaita na kuwahoji na kuangalia mkanda wa mchezo husika. Kamati imebaini mapungufu mengi ya kiutendaji yaliyofanywa na waamuzi hao, na hivyo kuitaka kamati ya waamuzi ishughulikie.

     

    Pia Mwamuzi Rajabu Mrope aliyechezesha mchezo namba 108 kati ya Mbeya City na Yanga naye ametolewa kwenye Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2016/2017 na kurudishwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili waweze kumpangia daraja lengine la uamuzi.

    Mrope alitiwa hatiani kwa kosa la kutojiamini mchezoni na kwenye uamuzi wake na kushindwa kuudhibiti mchezo.

    Miongoni mwa matatizo ya mwamuzi huyo ni kukubali goli, kisha kukataa na mwisho kukubali tena hali iliyoonyesha kutokujiamini na kusabisha mtafaruku mkubwa katika mchezo huo.

    Katika ligi ya Daraja la kwanza, Mwamuzi Thomas Mkombozi aliyechezesha mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kutokana na kushindwa kuudhibiti mchezo na kutoshirikiana na wasaidizi wake.

    Adhabu hiyo ametolewa baada ya Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi kuwaita waamuzi wa mchezo huo na kufanya mahojiano nao na kugundua Mkombozi alikuwa na maamuzi mengi bila umakini na hakushirikiana kiufundi na wasaidizi wake. Kutokua makini kulisababisha mchezo huo kumalizika kwa vurugu.

    Pia Klabu ya Coastal Union imepewa adhabu ya kucheza bila ya mashabiki kwa mechi mbili za nyumbani na mechi moja ya nyumbani kuchezwa uwanja wa ugenini kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kumshambulia Mwamuzi Thomas Mkombozi na kumsababishia majera ha maumivu makali.

    kuhusu Mwamuzi Ahmed Seif, Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya bodi ya Ligi, imemfungulia na kumtoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi kuu mwamuzi huyo aliechezesha mchezo namba 28 kati ya African Lyon na Mbao FC. hivyo, Mwamuzi Ahmed Seif atarudishwa kwenye kabati ya waamuzi ili apangiwe majukumu mengine.

  • BASHIR: NI RAHISI KUFANYA KAZI NA TRUMP

    BASHIR: NI RAHISI KUFANYA KAZI NA TRUMP

    Kiongozi wa Sudan Omar el Bashir amempongeza rais mteule wa Marekani Donald Trump akisema kuwa itakuwa rahisi kushirikiana naye, kulingana na gazeti la Emirati al Khaljee.

    ”Bw Trump anaangazia maslahi ya raia wa Marekani, ikilinganishwa na wale wanaozungumzia kuhusu demokrasia ,haki za kibinaadamu na uwazi”,alisema rais Bashir katika mahojiano na gazeti hilo.

    Aliongezea kwamba: Tunaweza kushirikina na watu wenye sura mbili lakini huyu hapa mtu mwenye uwazi wa anajua anacholenga.

    ”Nina hakika itakuwa rais kushirikiana na Trump ikilinganishwa na wengine kwa sababu ni mtu anayeangazia maswala moja kwa moja na mfanyibiashara ambaye anaangazia maslahi ya anaoshirikiana nao”,alisema Bashir.

    Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya ICC kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika eneo la Drafur amekana mashtaka hayo.

    Alichukua mamlaka mwaka 1989 kupitia mapinduzi na ameshutumiwa kwa kuwa na uongozi wa kiimla tangu wakati huo.

  • POLISI YAZUNGUMZIA ASKARI ALIYEJIUA BAHATI MBAYA

    POLISI YAZUNGUMZIA ASKARI ALIYEJIUA BAHATI MBAYA

    Kibaha. Jeshi la Polisi mkoani Pwani limezungumzia kifo cha askari wake PC Armand Furaha (33) aliyejipiga risasi kifuani bila kukusudia na kufariki dunia.
    Askari huyo alijipiga risasi hiyo usiku akiwa anaelekea kwenye lindo nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
    Tulio hilo lilitokea saa moja usiku eneo la Mailimoja sokoni usiku wa kuamkia jana, wakati askari huyo akiwa njiani kuelekea kwenye kituo cha lindo alichopangiwa.
    Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Blasius Chatanda amesema askari huyo alijipiga risasi bahati mbaya kwa bunduki aina ya SMG akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele katika gari alilokuwa anasafiria kwenda lindoni.
    Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa askari huyo alikuwa tayari ameweka risasi chemba kwenye bunduki hiyo aliyokuwa nayo na kwa bahati mbaya akiwa anashuka kwenye hilo gari ndipo risasi hiyo ikafyatuka na kumpiga kifuani eneo la kushoto na kufa wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tumbi. “Kabla ya tukio hilo, askari huyu aliwasili kazini jioni na kukuta amepangiwa kituo cha ulinzi kwa mkuu wa wilaya hivyo kama ilivyo ada alichukua zana za kazi ikiwemo bunduki hiyo na kuanza safari ya kuelekea lindoni kwake huko kwa DC, lakini bahati mbaya hakufika alifariki kwa kujipiga risasi bahati mbaya,” amesema Chatanda.
    Akizungumzia suala la askari kujipiga risasi Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema kila tukio hutokana na mazingira tofauti

  • TRUM KUTANGAZA BARAZA LA WAMAZIRI

    TRUM KUTANGAZA BARAZA LA WAMAZIRI

    Rais mteule wa Marekani Donald Trump anajiandaa kutangaza mawaziri zaidi watakaohudumia utawala wake.

    Ripoti zinasema kwamba Trump atamteua mshirika wake wa kibiashara wa zamani Steven Mnuchin kama waziri wa fedha.

    Wawili hao walikuwa wanamiliki Goldman Sachs, kampuni ambayo Trump aliikashifu wakati wa kampeni zake.

    Pia ameshiriki mazungumzo na Mitt Romney, ambaye anakisiwa kuwa mwaniaji wa wadhfa wa waziri wa mambo ya kigeni.

    Bwana Romney aliyewania urais kwa tiketi ya chama cha Republican mwaka 2012, kwa wakati mmoja alimwita Trump mtu muongo

  • SIMBA YAKATAA KUKIPIGA NA YANGA LIGI KUU

    SIMBA YAKATAA KUKIPIGA NA YANGA LIGI KUU

    Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba kwa sasa hawatacheza mechi yeyote ile dhidi ya Yanga endapo TFF itaendelea kupanga waamuzi wa hapa nyumbani.

    Mkuu wa mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema kuwa kama wao viongozi wameamua kufanya hivyo kwani waamuzi wa hapa nyumbani wamekuwa hawatendi haki kwa upande wao kwani mara nyingi hutoa maamuzi tofauti juu yao.

    “Angalia mechi yetu dhidi ya Yanga,Martine Saanya anakataa goli halali la Ibrahimu Hajibu baadae anakubali goli la mkono lililofungwa na Amisi Tambwe,mwamuzi anatoa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa nahodha wetu Jonasi Mkude pasipo kosa lolote inashangaza sana”alisema Manara.

    Amesema kuwa TFF kwa sasa inatakiwa kupanga waamuzi kutoka nje ya nchi katika mechi kubwa ya watani wa jadi ili kuondoa mzozo huo na wao watakuwa tayari kulipa gharama za waamuzi hao endapo TFF itashindwa kufanya hivyo.

    Tumeitisha mkutano wetu wa wanachama kwa ajili ya mabadiliko ya katiba, halafu tunasikia kuna mtu huyu anajiita Mohammed Kiganja (Katibu wa BMT) eti anasema kitakachoafikiwa siku hiyo wao hawakitambui wakati waziri mwenyewe amekubali.

    Tunashangaa huyu Kiganja ni nani hasa mpaka atuendeshe kiasi hiki, sisi tunasema, katika hili hakuna wa kutuzuia, tutafanya mabadiliko ya katiba kama wanachama wakikubali, hakuna wa kutuingia katika katiba yetu hata kama serikali ilihali hatuvunji katiba ya nchi.

    “Hivi kwa soka la sasa ni nani asiyependa mabadiliko, huyu Kiganja yeye amekuwa akijitokeza kwenye migogoro tu, kwa nini katika maendeleo hayupo, tumefuata sheria zote za kuitisha mkutano na tutaufanya bila ya kizuizi chochote kile,” alimaliza Manara.

  • MCHUNGAJI APULIZIA WAUMINI DOOM AFRIKA KUSINI AKIDAI NI TIBA

    MCHUNGAJI APULIZIA WAUMINI DOOM AFRIKA KUSINI AKIDAI NI TIBA

    Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amelaaniwa vikali.

    Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, pmchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.

    Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko.

    Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.

    Nchi hiyo imekuwa na wimbila visa ambapo wajumbe wa kanisawamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili kupata tiba.

    Katika picha zilizosambazwa kwenye kurasa za Facebook na Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mountzion General Assembly katika jimbo la Limpopo, anaeonekana akimpulizia dawa ya kuuwawadudu moja kwa moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya mwili mbele ya waumini wa kanisa lake.

    _92594055_982a15b3-9fe7-4edc-b400-9662df1d1e60

    ‘Nguvu za Mungu’

    Amemueleza mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa mmoja wa wanawake kwasababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa “yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu”.

    Pia alidai kuwa dawa hiyo ya Doom inaweza kuponesha saratani na virusi vya HIV vinavyosababisha.

    Kampuni inayotengeneza dawa ya Doom kwa nembo ya Tiger inasema kuwa inamsihi s mchungaji aliyejitangazia kuwa ”nabii” huko Limpopo – Lethebo Rabalogo kuacha kuwapuliza dawa ya wadudu kwenye nyuso za binadamu kama sehemu ya imani ya kuabudu:

    ”Tunaona tendo hili kuwa kutia hofu kubwa , na tungependa kubainisha wazi kwamba ni hatari kupulizia Doom ama dawa nyingine yoyote ile ya wadudu kwenye macho ya watu”.

    ”Doom ilitengenezwa kwa ajili ya kuwauwa wadudu wa aina fulani ambao wameonyeshwa kwenye kopo, na maelezo yaliyoandikwa bayana kwenye kopo la Doom yameonya juu hatari na yanapaswa kufuatwa.”

    ”Kampuni ya Tiger iko katika mchakato wa kuwasiliana na Nabii kumtaka aache kufanya tendo hilo,” imesema kampuni ya Tiger.