Category: Slider

  • KANYE WEST ALAZWA HOSPITALI LOSS ANGELES

    KANYE WEST ALAZWA HOSPITALI LOSS ANGELES

    Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Kanye West amelazwa hospitalini mjini Los Angeles, vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti.

    Msemaji wa polisi ameambia BBC kwamba walipokea simu ya kutokea kwa mtafaruku Jumatatu adhuhuri, lakini hawakutaja jina la mwanamuziki huyo.

    Baadaye, mtafaruku huo ulidaiwa kuwa tukio la kimatibabu, na maafisa wa kutoa huduma ya dharura walifika eneo hilo.

    Msemaji wa maafisa wa huduma za dharura wa LA amesema mwanamume ambaye jina lake halikutajwa alipelekwa hospitalini “kufanyiwa uchunguzi zaidi”.

    “Mwendo wa saa 13:20 majira ya kanda ya pasifiki, idara ya huduma za dharura ya Los Angeles ilipokea ombi la dharura la huduma ya matibabu ambalo halikuelezwa kwa kina,” amsemaji huyo alisema.

    “Mwanamume mzima, ambaye hali yake ya afya ni thabiti, alipelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi zaidi.”

  • RAIA WA NIGERIA ALIYEKUTWA NA BANGI KUNYONGWA SINGAPORE

    RAIA WA NIGERIA ALIYEKUTWA NA BANGI KUNYONGWA SINGAPORE

    Singapore imekataa ombi la msamaha kutoka kwa raia mmoja wa Nigeria ambaye amepangiwa kunyongwa Ijumaa kwa kupatikana na bangi, shirika la haki za kibinadamu la Amnesty International limesema.

    Familia ya Chijoke Stephen Obioha ilifahamishwa kuhusu hatua hiyo Jumatano.

    Obioha alipatikana na kilo 2.6 za bangi Aprili 2007, kiasi kilichokuwa kimezidi kipimo cha gramu 500 ambacho mara moja humfanya mtu kuhukumiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya chini ya sheria za Singapore.

    Afisa wa Amnesty International Rafendi Djamin amesema shirika hilo limeshangazwa na hatua hiyo ya Singapore kumnyima mshtakiwa huyo msamaha.

    Hata hivyo, alisema shirika hilo bado lina matumaini kwamba Singapore haitatekeleza adhabu hiyo “katili na isiyoweza kubatilishwa dhidi ya mtu huyo aliyehukumiwa kifo kwa kosa ambalo halifai adhabu ya kifo.”

    “Hukumu ya kifo si suluhu. Haitaangamiza dawa zote za kulevya Singapore. Kwa kuwanyonga watu kwa makosa ya kuwa na dawa za kulevya, ambayo hayafikii kiwango cha makosa makubwa ya uhalifu, Singapore inakiuka sheria za kimataifa.

    “Mataifa mengi ulimwenguni yameacha adhabu hii ya kikatili, kinyama na ya kudunisha.”

  • MKWASA ALIA NA WACHEZAJI

    MKWASA ALIA NA WACHEZAJI

    Dar es Salaam. Siku moja baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa amesema ni vigumu kupima viwango vya wachezaji hasa wa Tanzania.

    Ligi hiyo imemaliza mzunguko wa kwanza huku baadhi ya wachezaji waliong’ara msimu uliopita wakishindwa kufanya hivyo msimu huu huku wachezaji wengine wakiibuka na kung’ara.

    Baadhi ya wachezaji waliong’ara raundi ya kwanza ni Shiza Kichuya, Omar Mponda, Simon Msuva wameng’ara raundi ya kwanza na kuzingia timu zao mabao muhimu huku wachezaji kama Nadir Haroub na Abdi Banda wakishindwa kufurukuta na kujikuta wakipoteza nafasi ya kucheza katika timu zao.

    Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo wa mwisho wa raundi ya kwanza ya Ligi Kuu kati ya Ruvu Shooting na Yanga Mkwasa alisema tatizo la wachezaji wengi wa Tanzania ni kutokudumu katika viwango vyao hali inayofanya hata kikosi cha timu ya taifa kubadilika mara kwa mara. “Nimeangalia mechi kadhaa za Ligi Kuu, tatizo tulilonalo ni lilelile, wachezaji wetu hawadumu katika viwango vyao.

    Unaweza kumwona anafanya vizuri lakini baada ya miezi miwili mitatu akapotea.

  • TRUMP KUWAREJESHA WAHAMIAJI KWAO

    TRUMP KUWAREJESHA WAHAMIAJI KWAO


    Donald Trump asema kati ya wahamiaji haramu milioni mbili ama tatu watasafirishwa kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa chi hiyo.
    Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani,CBS, Trump amesema wahamiaji wote wenye rikodi za uhalifu, ikiwemo makundi ya wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele chake .
    Hatma ya wahamiai haramu milioni nane na ushee waliosalia itafahamika mara tu mpaka utakapokuwa salama.
    Donald Trump ameongeza kuwa semhemu ya ukuta ambao aliahidi kujenga kwenye mpaka baina ya nchi yake na Mexico, unaweza kuwa ni uzio.

  • DONALD TRUMP AFANYA UTEUZI WA AWALI

    DONALD TRUMP AFANYA UTEUZI WA AWALI

    Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama mkuu wa wafanyakazi.

    Bwana Priebus ana uhusiano wa karibu na spika wa baraza la wawakilishi Paul Ryan. Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.

    Stephen Bannon, alikuwa ni mwenyekiti wa taasisi ya Breitbart News, ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia , naye ameteuliwa kwa nafasi ya mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi.

    Mkuu wa wafanyakazi ambaye anafanya kazi kama mruhusu na mtengeneza ajenda kwa rais, na kwamba ni mmoja wa chaguo muhimu la mapema kwa rais ajae.

    Katika taarifa yake, Trump alinukuliwa akiwazungumiza Priebus na Bannon ni viongozi wenye sifa za hali ya juu waliofanya kazi pamoja wakati wa kampeni zake za kuingia Ikulu ya Marekani.

  • NOTI ZA RUPEE 500 NA 1000 KUFUTWA INDIA

    NOTI ZA RUPEE 500 NA 1000 KUFUTWA INDIA

    Waziri mkuu wa India Narendra Modi ametangaza kuwa noti ya Rupee 500 na ile ya 1000 zitaondelewa katika mfumo wa fedha kwa siku moja.

    Hatua hiyo ya kushangaza ni mijawapo ya harakati za kukabiliana na Ufisadi pamoja na ukopeshaji wa fedha wa haramu alisema katika runinga.

    Benki zitafungwa siku ya jumatano huku huduma za mashine za kutoa pesa za ATM zkisitishwa.

    Noti mpya za rupee 500 na 2000 zitawekwa katika mfumo wa fedha ili kuchukua mahala pake noti hizo zilizoondolewa.

    Ulanguzi wa fedha na ufisadi ndio vikwazo vikuu katika kukabiliana na umasikini ,alisema Modi.watu wataweza kubadilisha fedha noti zao za zamani na mpya katika benki katika kipindi cha siku 50 na kwamba fedha hizo hazitatumika tena.

    Tangazo hilo liliwashinikiza raia kote nchini kuelekea katika mashine za ATM zinazotoa noti za rupee 100 katika hatua ya kutokosa fedha katika kipindi cha siku kadhaa zijazo.

  • SAMSUNG KWENYE TUHUMA ZA UFISADI WA KISIASA

    SAMSUNG KWENYE TUHUMA ZA UFISADI WA KISIASA

    Waendesha mashtaka nchini Korea kusini wamevamia ofisi za kampuni ya kielektoniki ya Samsung kama sehemu ya uchunguzi wa sakata ya kisiasa inayomuhusu rais Park Geun-hye.

    Waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba Samsung ilimpatia pesa mtoto wa kike wa Choi Soon-sil, ambaye ni rafiki wa karibu wa rais.

    Bi Choi anashutumiwa kutumia urafiki wao kuingilia kati siasa na utoaji wa zabuni za kibiashara.

    Samsung imeithibitishia BBC kuwa uvamizi huo ulifanyika ikisema “hakuna maelezo zaidi “.

    Rais Park ameomba msamaha kwa uhusiano wa karibu na Bi Choi lakini anakabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu.

  • RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SPIKA WA BUNGE KUFUATIA KIFO CHA SPIKA MSTAAFU, SAMWEL SITTA

    RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SPIKA WA BUNGE KUFUATIA KIFO CHA SPIKA MSTAAFU, SAMWEL SITTA

    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo mkoani Tabora
    Samwel Sitta.
    Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujeruman alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.

    Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko na masikitiko taarifa hizo na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.

  • MADINI MAPYA YAGUNDULIWA MERERANI, TANZANIA

    MADINI MAPYA YAGUNDULIWA MERERANI, TANZANIA

    Madini mapya yamegunduliwa nchini Tanzania, katika eneo lenye madini ya kipekee la Manyara, na kupewa jina Merelaniite.

    Jina hilo limetokana na eneo ambalo madini hayo yalipatikana, Merelani (Mererani) katika milima ya Lelatema katika wilaya ya Simanjiro katika eneo la Manyara.

    Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite.

    Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, chuo kikuu cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia ya Smithsonian ya Washington.

    Wataalamu sita waliofanya uchunguzi, kwenye makala iliyochapishwa kwenye jarida la Minerals (Madini) wanasema madini hayo yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu vya urefu wa milimita moja hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi mililita 12.

    Kipenyo cha vipande hivyo ni mikrometa kadha.

    Madini hayo yanakaribiana na madini ya zoisite (aina ya tanzanite), prehnite, stilbite, chabazite, tremolite, diopside, quartz, calcite, graphite, alabandite na wurtzite.

    “Madini haya mapya yametambuliwa na taasisi inayoyapa majina madini, IMA CNMNC (2016-042), na kupewa jina linalotokana na eneo yalipogunduliwa kwa heshima ya wachimba migodi wa eneo hilo wa zamani, wanaoishi na wanaofanya kazi,” makala ya wataalamu hayo inasema.

    “Wilaya ya Merelani imekuwa maarufu tangu mwishoni mwa miaka ya 1960 kutokana na aina ya madini ya thamani ya rangi ya samawati kwa jina zoisite yafahamikayo kama tanzanite, lakini ni eneo muhimu sana kwa wanaotafuta madini ya kipekee na ni eneo la kusisimua sana kutafuta madini mapya,” John Jaszczak, mwanafizikia katika Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan, na aliyeongoza katika kuandika makala kuhusu ugunduzi wa madini hayo anasema.

    Madini hayo yalitambuliwa mara ya kwanza mwaka 2012 na Simon Harrison na Michael Wise, bila wataalamu hao kuyafahamu vyema, pale walipogundua vitu vilivyoonekana kama nyaya ndogo zilizokuwa zimedunga na kuingia ndani ya vipande vya madini ya chabazite.

    Baadaye uchunguzi zaidi ulifanywa na ikagunduliwa kwamba yalikuwa madini tofauti.

  • MGOMO WAPELEKEA CHUO CHA MAKERERE KUFUNGWA

    MGOMO WAPELEKEA CHUO CHA MAKERERE KUFUNGWA

    Wanafunzi wameanza kuondoka kutoka Chuo Kikuu cha Makerere baada ya Rais Yoweri Museveni kutangaza kifungwe mara moja Jumanne jioni.

    Rais alisema amechukua hatua hiyo “kuhakikisha usalama wa watu na mali.”

    Chuo kikuu hicho kilikuwa kimekumbwa na vurugu kutokana na mgomo wa wahadhiri na wanafunzi.

    Chama cha wahadhiri Jumatatu kiliamua kuendelea na mgomo hadi wahadhiri walipwe marupurupu ya miezi minane ambayo yamefikia Sh32bn (dola 9.2 milioni za Marekani).

    Wanafunzi walijiunga na mgomo Jumanne, na walitaka kukutana na Rais Museveni badala ya mwenyekiti wa baraza simamizi ya chuo chini ya uenyekiti wa Dkt Charles Wana-Etym.

    Naibu chansela wa chuo hicho Prof Ddumba Ssentamu wiki iliyopita alikuwa amewasihi wahadhiri wakubali kurejea kazini huku suluhu ya kudumu ikiendelea kutafutwa.

  • MFALME MTEULE WA THAILAND KUTHIBITISHWA DECEMBER

    MFALME MTEULE WA THAILAND KUTHIBITISHWA DECEMBER

    imetaarifiwa kwamba mfalme mteule mtarajiwa wa Thailand Vajiralongkorn atathibitishwa rasmi kama mfalme ajaye mnamo Desemba mosi.

    Mwana wa mfalme huyo ambaye pia ni mfalme mtarajiwa alitarajiwa kupakwa mafuta na kutawazwa katika kipindi ama baada ya maziko ya babake , mfalme King Bhumibol Adulyadej, aliyefariki wiki tatu zilizopita, kutokana na yeye mwenyewe kuomba muda wa kumuomboleza babake.

    Mpaka sasa haijafahamika wazi, ni uhusiano wa namna gani mfalme huyo mtarajiwa atakuwa nao baina yake na vikosi vya jeshi la serikali ambavyo hivi karibuni vilikuwa vinaiongoza Thailand, ama ni namna gani atapokelewa na raia wake.