Category: Entertanment

  • Tanzia; Mtayarishaji maarufu  wa Muziki afariki dunia

    Tanzia; Mtayarishaji maarufu wa Muziki afariki dunia

    Mtayarishaji wa muziki Pancho Latino amefariki dunia.

    Taarifa za awali zinaeleza kuwa Pancho amefikwa  na umauti kwa ajali ya maji katika kisiwa cha Mbudya jijini  Dar es Salaam leo Octoba 9/2018.

    Tunatoa pole kwa ndugu na jamaa na marafiki pamoja na wadau wa muziki kufuatia msiba huu.

    Mungu ampuzishe ndugu yetu mahali pema peponi.(amen)

  • mziki mnene 2018 morogoro

    mziki mnene 2018 morogoro

    Matukio kwa picha

    Rdj AutoRan

  • Picha: Singeli Michano Morogoro 2018

    Picha: Singeli Michano Morogoro 2018

    Hii ndio njia pekee inayotumika kwenye kusaka vipaji vya wasanii wa Singeli Pale ambapo Team ya Efm Radio inapofika Mkoani iki kuhamasisha vijana na kukuza vipaji walivyo navyo badala ya kujihisisha na makundi ya uhalifu

    Leo baaaya ya Jogging ya Asubuhi sana kwenye viwanja vya Jamhuri vipaji vya vijana kutoka sehemu mbali mbali za Mji wa Mororgoro walijitokeza kwa wingi na kuonyesha uwezo walionao

  • BASATA LAKANUSHA KUUFUNGIA WIMBOA WA PARAPANDA YA ROSTAM

    BASATA LAKANUSHA KUUFUNGIA WIMBOA WA PARAPANDA YA ROSTAM

    Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limesema halijaufungia wimbo wa Parapanda ulioimbwa na wasanii wa kundi la Rostam, Roma Mkatoliki na Stamina na kusema kuwa labda wameamua kujifungia wenyewe kwa lengo la kutafuta ‘kiki’.

    Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Roma kupitia ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno ya kuilaumu Basata kwamba inaua vipaji na ubunifu wa wasanii na kuhoji wimbo wao huo una tatizo gani.

    Mbali na kuandika hayo pia alizungumza na baadhi ya vyombo vya habari na kudai kuwa amepewa wito wa kufika Basata.

    Akilizungumzia hilo, Katibu wa Baraza la Sanaa, Godfrey Mngereza, amesema hawajaufungia wimbo huo na haujapitishwa mikononi mwao hadi sasa kwa ajili ya kuhaririwa.

    “Labda kama wameamua kujifungia wenyewe ili kuufanya wimbo wao ujulikane na watu, lakini sisi hata hatujauona na kuupitia kama taratibu zetu zinavyotaka na mnajua tukifungia wimbo huwa tunatangaza sasa labda Roma awaonyeshe wapi tumesema hivyo,” amesema Mngereza.

    Wasanii hao, Agosti 2 waliachia wimbo huo Parapanda, unaoelezea masuala mbalimbali yanayoendelea nchini yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

    Wimbo huo ambao umeachiwa sauti tu (audio) katika mtandao wa YouTube, umesindikizwa na picha za hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na aliyekuwa mwanasiasa mkongwe marehemu Kingunge Ngombare Mwiru.

    Hata hivyo, katibu huyo alikiri kuwa juzi wasanii hao wawili kufika katika ofisi za Basata kwa ajili ya kushiriki jukwaa la wasanii ambalo hufanyika kila siku ya Jumatatu katika ukumbi wao uliopo Ilala Gereji huku mada kuu kwa siku hiyo ilikuwa kuhusu kanuni mpya za sanaa zilizoanza kutumika Julai mwaka huu.

    Pia Basata limesema iliwaita Roma na Stamina kwa kuwa walikiuka taratibu za kufikisha wimbo kwenye baraza ili ukaguliwe kabla kuutoa rasmi

    Katika jukwaa hilo anasema mmoja wa waandishi aliuliza swali kuhusu matumizi ya picha za waasisi wa mbalimbali wa nchi hii katika sanaa, ambapo Mngereza anadai alimjibu kuwa msanii anapaswa kupata kibali kutoka kwa familia au Serikali.

    “Huenda majibu haya labda ndiyo yalimfanya Roma akaondoka pale na tafsiri yake na kuandika hicho alichokiandika, lakini kiukweli hatujamfungia wala kumuita kumuhoji kuhusiana na wimbo hiyo,” amesema Katibu huyo.

  • Ndoa ya Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ Hatari

    Ndoa ya Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ Hatari

    Prince Harry na mchumba wake Meghan Markle.

    MAMILIONI ya watu duniani leo wanatarajiwa kushuhudia ndoa ya kifahari ya mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ na mwigizaji maarufu wa Marekani, Meghan Markle.

    Harry akiwasalimia mamia ya watu waliofika kushuhudia ndoa yake.

     

    Harry ni mtoto wa Prince Charles wa Uingereza ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili. Prince Charles ambaye ndiye mfalme-mtarajiwa, anajulikana pia kama Prince of Wales.

    Ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa katika Kasri la St George, eeo la Windsor, jijini London ambapo inakadiriwa tukio la kufunga ndoa kanisani litahudhuria na watu 1,200 ambao ni jozi 600 za waume na wake zao watakaoshuhudia hafla hiyo viunga vya kasri hilo.

    Harry akiingia na kaka yake, Prince William.

     

    Vilevile watu zaidi ya 100,000 watajipanga kwenye barabara za eneo hilo wakiwa na bendera za nchi hiyo kuwatakia pongezi wanandoa hao baada ya kutoka kanisani. Prince Charles atamsindikiza Prince Harry katika ndoa yake na Markle kwenye madhabahu ya Kasri hilo wakati baba wa Markle, Thomas, hatohudhuria harusi hiyo kutokana na kufanyiwa upasuaji wa moyo.

    Meghan na mama yake.

     

    Meghan na Prince Harry jana walitumia muda wao kukaa na familia zao katika maandalizi ya mwisho. Harry alitumia muda mwingi wa jioni kukaa na kubadilishana mawazo na msimamizi wake (mpambe) ambaye ni Prince William.

    Kwa upande wa Markle,mwenye umri wa miaka 36, atasindikizwa kwenda kanisani na Ragland. Pia atakutana na wapambe wengine wa harusi wa kike na kiume ambao ni pamoja na mpwa wa Harry mwenye umri wa miaka minne aitwaye Prince Charlotte, pamoja na watoto wasimamizi wa kidini wa Markle.

    Kwa upande wa pete ya harusi hiyo itatokana na pete ya ndoa ya mwaka 1923 ya mama wa Malkia Elizabeth wa Pili iliyotokana na dhahabu ya Ki-Welsh ambapo sehemu yake imekuwa ikituika katika kila pete ya ndoa za jamii ya kifalme.

    Kuna tetesi kwamba pete ya Markle huenda ikawa ndiyo ya mwisho kutokana na pete hiyo ya kihistoria. Vilevile, kutokana na fahari ya kijeshi aliyo nayo Prince Harry ni dhahiri atavaa sare zake za kijeshi.

    Kutokana na utaratibu wake wa kuwashirikisha wanajeshi katika hafla mbalimbali, panategemewa kuwepo zaidi ya askari 250 kutoka vikosi mbalimbali vilivyo na uhusiano na Prince huyo.

    Katika harusi zote za kifalme tangu enzi za Malkia Victoria mwaka 1840, biharusi wote wamekuwa wakivaa nguo za rangi nyeupe, na pamoja na kwamba gauni la Markle bado linafanywa kuwa siri kubwa, bado panategemewa kwamba litakuwa na rangi ileile.

    Makao ya Kensington yamethibitisha pia kwamba Prince Harry na Markle watafuata utaratibu wa siku nyingi ulioanza kutumika tangu enzi za Malkia Victoria, yaani kutumia farasi wa rangi ya kijivu wa Windsor kwa kuvuta gari la harusi.

    Na iwapo hali ya hewa itakuwa nzuri, inasemekana wanandoa hao watapita katika eneo la Mji la Windsor katika moja ya magari maalum ya kifalme yanayojulikana kama Ascot Landau.

    Hata hivyo, kuna baadhi ya wanasiasa mashuhuri ambao hawamo miongoni mwa washiriki wa harusi hiyo.

    Nao ni pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Teresa May, na marafiki za Prince Harry ambao ni rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle.

    Harusi itaongozwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby katika kanisa la Mt. George na shughuli yote hiyo itatangazwa kwa mamilioni ya watu duniani kote.

     

     

  • MATUKIO KWA PICHA, SHIKA NDINGA PWANI 93.7

    MATUKIO KWA PICHA, SHIKA NDINGA PWANI 93.7

    Swebe Akichimba Mashimo kwa ajili ya Kuweka Alama ndani ya uwanja wa mapambano
    Team ya EFM ikiandaa kiwanja kwa ajli ya kushika ndinga ndani ya viwanja vya Bwawani Kibaha

     

    Team ya Efm imewasili salama kwenye viwanja hivi vya Bwawani, Kibaha, na Maandalizi yanaanza

    Washiriki wanaanza kupewa semina kuwa tayari kuingia kwenye mpambano wa kushika ndinga.

    Washiriki waliofika katika viwanja hivi vya Bwawani wakiwa tayari kuanza mpambano wa kushika ndinga
    Washiriki waliofika katika viwanja hivi vya Bwawani wakiwa tayari kuanza mpambano wa kushika ndinga
    Watu wa huduma ya kwanza wakiwa tayari kutoa huduma ya kwanza kwa yeyote atakayepatwa na tatizo kwenye eneo hili la Bwawani kibaha, kushika ndinga # Tunapindua Meza Kibabe
    Wananchi walio wahi mapema kabisa kushuhudia watu wakishika ndinga hapa hapa kwenye viwanja vya Bwawani, Kibaha

    Kiwanja ambacho cha kushindanisha washiriki kipo tayari na sasa muda wowote kuto muda huu zoezi la kushika ndinga linakwenda kuanza # tunapindua meza kibabe

    Burudani ikiendelea katika viwanja hivi vya Bwawani, Kibaha,

    Jeshi la polisi likitoa usalama wa wananchi walifika kushuhudia watu wakishika ndinga
    Kila kitu kipo sawa muda wowote tunaanza zoezi la kushika ndinga
    Kwenye Mashine ya Muziki anayetuburudisha kwenye viwanja hivi vya Bwawani Kibaha yupo RDJ AUTO RUN, Akitupa Visingeli
    Timu yetu ya TV E wakiaweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuchukua maukio yote yanayojili hapa kwenye viwanja hvi vya Bwawani Kibaha

    Mpambano wa kushindanisha washindi umeshaanza na washiliki wamenza na zoezi la kujaza maji, hivyo tunasubiri matokeo kutoka kwa majaji, nani atatoka na nani atandelea na mpambano.

    Matokeo ya Majaji yanatoa uamuzi kwamba Mshiriki Abdallah Mohamed, Ramadhani, Ima Lukindo wameaga mashindano baada ya kuwa na point chache ukilinganisha na point za wengine.

    Wananchi wakishuhudia mpambano mkali wa kutafuta washindi wa shika ndinga 2018
    TTCL wakitoa huduma ya kuwapatia wananchi wa pwani line za bure na muda wa maongezi
    Vilainishi vya Shell Advance wakitoa huduma kwa wananchi waliojitokeza eneo hilo
    Baadhi ya Watu waliopanda juu ya miti ili waweze kuangalia kinachotokea
    Muda wa kumtafuta wa kuchukua bodaboda.

    ..

  • MATUKIO KWA PICHA, SHIKA NDINGA 103.3 MBEYA 2018

    MATUKIO KWA PICHA, SHIKA NDINGA 103.3 MBEYA 2018

    Mshindi wa chombo cha moto (Pikipiki) Shika Ndinga Mbeya Bw.SAIDI DAIMON KATEMBWE Mkazi wa Masewe, Mbeya mjini
    Bi.AMIDA HARUNI SELEMANI, akiwa katika hatua za mwisho kabla hajajishindia Chombo cha moto (pikipiki) kwa upande wa wanawake mkoa wa Mbeya. Shika Ndinga 2018.

  • SHIKA NDINGA MBEYA 2018

    SHIKA NDINGA MBEYA 2018

    Hatua za awali za ukaguzi wa uwanja ambao utatumika kubadilisha maisha ya wamiliki wa namba kubwa 103.3 Mbeya na kuwaongezea thamani kwa mtaji wa sikio tu.
    #ShikaNdinga2018Mbeya #TunapinduaMezaKibabe

  • SHIKA NDINGA 2018 TANGA

    SHIKA NDINGA 2018 TANGA

    Kutoka kaskazini mwa Tanzania kwenye mji wenye mahaba tele tumekuja kuongeza thamani ya maisha kwa wakazi wa 88.9 #ShikaNdinga2018Tanga#TunapinduaMezaKibabe

    #Hatupoi Tukiwa nyumbani 88.9 Tanga waja leo wabaki milele.

    Huu ndio muonekano wa leo kwenye uwanja wa Lamore mahali ambapo akili nyingi itatumika na nguvu kiasi kuweza kuwachuja washiriki watakaokwenda kushika ndinga jukwaani.
    #ShikaNdinga2018Tanga#TunapinduaMezaKibabe

    Tukiwa karibu nawe kwa namba 88.9 Tanga ndugu zetu wa @ttcl_corporation wanatupa uthubutu zaidi na habari njema ni kwamba *150*71# ndio namba yako ya kipesa kukuwezesha kununua umeme ili uendelee kusikiliza E-fm na kutazama @tvetanzania
    #RudiNyumbaniKumenoga

  • SHIKA NDINGA; 88.9 TANGA HODI HAPOOOH.

    SHIKA NDINGA; 88.9 TANGA HODI HAPOOOH.

    Timu ya wafanyakazi wa Efm na Tv E ilipo wasili katika uwanja wa Ramore Tanga kwaajili ya shindano la SHIKA NDINGA litakalofanyika kesho April 14 2018.
    Picha ya pamoja wafanyakazi wa Efm & Tv E na TTCL Mara baada ya kuwasili katika mkoa wa Tanga na kufanya ziara fupi kwenye ofisi za TTCL mkoani hapa.