Category: Global News

  • WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA URENO AJIUZULU

    WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA URENO AJIUZULU

    WAZIRI WA MAMBO YA NDANI wa Ureno amejiuzulu kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za rushwa inayohusishwa na utoaji vibali vya mgawo wa makazi.

    MIGUEL MACEDO amesema hahusiki na kashfa hiyo lakini amejiuzulu kulinda heshima ya Taasisi za Serikali.

    Taarifa zimebainisha kuwa Polisi wamewakamata watu 11, akiwemo Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini humo, siku ya Alhamisi.

  • HELIKOPTA NYINGINE YAANGUKA NIGERIA

    HELIKOPTA NYINGINE YAANGUKA NIGERIA

    HELIKOPTA ya kijeshi ya Nigeria imeanguka katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo , ikiwa ni Helikopta ya pili kupata ajali kwa muda wa chini ya wiki mbili .

    Ajali ya hivi karibuni imetokea katika viunga vya mji wa Yola, mji mkuu wa jimbo la Adamawa ambako kwa sasa jeshi linahangaika kukabiliana na Uasi wa wanamgambo wa Jihad.

    Kuna taarifa kutoka jimbo hilo kuwa wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwasukuma wanajeshi nje ya mji muhimu uliopo karibu na mpaka wa Cameroon .

    Wanafunzi katika chuo kikuu cha Modibbo Adama kilichopo katika mji wa Yola wamebainisha kuwa wamesikia Helikopta ikianguka karibu na chuo chao .

  • OBAMA: MAGEUZI KWANZA KISHA DEMOKRASIA MYNAMAR

    OBAMA: MAGEUZI KWANZA KISHA DEMOKRASIA MYNAMAR

    RAIS BARACK OBAMA wa Marekani amesema kuna haja ya Mageuzi zaidi nchini Myanmar katika kuelekea kuipata Demokrasia.

    Akizungumza katika mji mkuu wa nchi hiyo Yangon leo, Rais OBAMA amekosoa jinsi watu wa dini za walio wachache wanavyotendewa na pia hatua ya kumzuia kiongozi wa upinzani, AUNG SAN SUU KYI, kutogombea Urais.

    SUU KYI aliyeachiwa huru miaka minne iliyopita baada ya kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani kwa takribani miongo miwili, sasa ni mjumbe katika Bunge la nchi hiyo, ingawa anashindwa kugombea Urais katika uchaguzi wa Rais wa mwaka ujao kutokana na kuzuiwa kikatiba.

     

  • MAREKANI, INDIA MAMBO SHWARI

    MAREKANI, INDIA MAMBO SHWARI

    MAREKANI na India zimesema zimepata muafaka juu ya mzozo uliohusu ruzuku ya chakula nchini India, ambayo mwaka jana ilikwamisha makubaliano ya kibiashara katika Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO.

    India imekataa kutia saini makubaliano hayo muhimu Julai mwaka jana, ikitaka kwanza kuhakikishiwa hazina kubwa ya chakula nchini humo.

    Kulinagana na makubaliano yaliyofikiwa, hazina ya chakula ya India haitakabiliwa na changamoto zozote kutokana na kanuni za WTO, hadi pale suluhisho la kudumu kuhusu suala hilo litakapokuwa limepatikana.

  • LIBERIA YAONDOA SHERIA YA EBOLA

    LIBERIA YAONDOA SHERIA YA EBOLA

    RAIS wa Liberia ELLEN JOHNSON SIRLEAF ameondoa sheria ya hali ya hatari ambayo ilikuwa imetangazwa nchini humo katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa maradhi ya Ebola, ambayo yaliizonga nchi hiyo na nyingine mbili jirani katika kanda ya Afrika Magharibi.

    Katika hotuba yake kwa taifa Rais SIRLEAF amesema kuondolewa kwa sheria hiyo hakumaanishi kwamba mlipuko wa ugonjwa huo umemalizika.

    Amebainisha kuwa Maendeleo ya kutosha yamepatikana katika vita dhidi ya maradhi hayo kuwezesha kuondolewa kwa sheria hiyo.

  • BOTI YA DORIA YASHAMBULIWA MISRI

    BOTI YA DORIA YASHAMBULIWA MISRI

    JESHI la Misri limesema wanamaji wake 8 hawajulikani walipo baada ya kile ilichokiita shambulizi la Kigaidi dhidi ya boti yake iliyokuwa ikifanya doria kwenye bandari za nchi hiyo katika bahari ya Mediterania.

    Msemaji wa jeshi hilo Brigedia Jenerali MOHAMMED SAMIR amesema kupitia ukurasa wake wa Facebook kwamba boti iliyofanya shambulizi hilo imeharibiwa na kwamba wavamizi 32 wamekamatwa.

    Mapema leo, Shirika la Habari la Misri, MENA limesema washambuliaji waliokuwa ndani ya boti 3 wameishambulia kwa bunduki boti ya doria ya Jeshi Kaskazini mwa bandari ya Damietta, na kurushiana risasi.

  • MSF KUJARIBU DAWA ZA EBOLA

    MSF KUJARIBU DAWA ZA EBOLA

    SHIRIKA la Madaktari wasio na Mipaka-MSF limesema kuwa wanatarajia kufanya majaribio juu ya aina tatu za dawa zinazoweza kutibu maradhi ya Ebola Mwezi Desemba katika vituo vya shirika hilo nchini Guinea na Liberia.

    Majaribio mengine tofauti na hayo kuhusu aina mbili ya dawa, moja kutoka kampuni ya Chimerix ya Marekani na nyingine iliyotengenezwa na kampuni ya Fujifilm ya Japan yanalenga kutathmini namna Maji ya Damu ya wagonjwa waliopona Ebola yanavyoweza kusaidia kuwatibu watu walio na maradhi hayo.

    Tangazo la MSF limesema matokeo ya mwanzo ya majaribio hayo yanaweza kuwa tayari mwezi Februari mwaka ujao.

     

  • UJERUMANI YAPANGA PUNGUZO LA KODI KUKUZA UCHUMI ULAYA

    UJERUMANI YAPANGA PUNGUZO LA KODI KUKUZA UCHUMI ULAYA

    UJERUMANI  imepanga punguzo  la  Kodi  la Euro  Bilioni  1 kuimarisha  matumizi  mazuri  ya  Nishati  katika  majumba  na kuongeza biashara  ya  magari  yanayotumia  nishati  ya  umeme, katika  mpango wa  kusaidia  uchumi  huo  mkubwa  katika  bara  la Ulaya  kufikia  malengo  yake  ya  utoaji  wa  gesi  zinazochafua mazingira.

    Waraka  wa  Sera  ya  Nishati umeonesha  kwamba  licha  ya kuelekea  katika  Nishati  Mbadala , utoaji  wa  gesi  zinazoharibu mazingira  nchini  Ujerumani  umepanda  kutokana  na  kuachana  na matumizi  ya  nishati  ya  kinyuklia.

    Baraza  la  Mawaziri  la  Kansela  ANGELA  MERKEL  linatarajia kukutana Desemba  3 kukubaliana  kuhusu  mapendekezo  kadhaa  kusaidia kujaza  pengo, ambalo  Mawaziri  wanakadiria  linafikia   asilimia  7, ikiwa  ni  pamoja  na  ongezeko  la  matumizi  mazuri  ya  nishati.

  • WAUGUZI WA EBOLA SIERRA LEONE WAWEKA MGOMO

    WAUGUZI WA EBOLA SIERRA LEONE WAWEKA MGOMO

    ZAIDI ya Wahudumu 400 wa Afya wanaowatibu Wagonjwa wa maradhi ya ugonjwa wa Ebola katika Kliniki moja nchini Sierra Leone wamegoma.

    Wahudumu hao wakiwemo wauguzi na wafanyakazi wengine wanagoma kushinikiza kuwalipa Dola Miamoja kila wiki kwa kuhatarisha maisha yao kutokana na kuwashughulikia wagonjwa wa hao.

    Kliniki hiyo iliyo mjini Bandajuma karibu na eneo la Bo, ni kliniki pekee ambayo wagonjwa wa Ebola wanatibiwa Kusini mwa Sierra Leone.

    Kwingineko nchini Mali, muuguzi mmoja pamoja na mgonjwa aliyetibiwa na muuguzi huyo wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola.

  • CHINA, MAREKANI WATOA MALENGO MAPYA YA TABIA YA NCHI

    CHINA, MAREKANI WATOA MALENGO MAPYA YA TABIA YA NCHI

    Rais wa Marekani BARACK OBAMA na   Rais wa China XI JINPING leo wametangaza malengo mapya ya Mabadiliko ya Tabia nchi mwishoni mwa mazungumzo yao ya siku mbili mjini Beijing.

    XI amesema utoaji wa China wa Gesi zisizochafua mazingira utaongezeka ifikapo mwaka 2030, ambapo vyanzo vya nishati ambayo sio mafuta ikiwa ni asilimia 20 ya Nishati itakayotumika wakati huo.

    Rais wa China hakuweka lengo la viwango vya utoaji gesi ama upunguzaji, lakini ni mara ya kwanza kwa China , ambayo inategemea uzalishaji wa Nishati kupitia Majenereta yanayotumia Maka ya mawe, imeweka muda maalum kuhusiana na Gesi zinazochafua Mazingira.

     

  • PAPA FRANCIS AITAKA G20 KUWAFIKIRIA WATU MASIKINI DUNIANI

    PAPA FRANCIS AITAKA G20 KUWAFIKIRIA WATU MASIKINI DUNIANI

    PAPA Mtakatifu FRANCIS ametaka viongozi Duniani wanaoshiriki Mkutano wa G20 mjini Brisbane kuwafikiria watu Masikini Ulimwenguni.

    Amewataka Viongozi hao kupata ufumbuzi wa kuimarisha hali ya maisha ya watu walio masikini.

    Viongozi wa nchi 20 zilizo na uchumi mkubwa wanakutana Brisbane nchini Australia mwishoni mwa juma hili kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uchumi.