BAFANABAFANA WAIPISHA GHANA ROBO FAINALI AFCON

Written by

in

,

Andre Ayew Amefanikiwa kuipeleka Ghana robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika  afcon baada ya kuwapa kichapo cha 2-1 afrika ya kusini na kuibuka washindi wa kundi c.

Black Stars wa Ghana, wamewahi fikia  nusu fainali mara nne mfululizo katika michuano ya afcon, Walihfiwa kutolewa katika dakika ya 17 ambapo Mandla Masango kuipatia Afrika Kusini goli la kwanza.

Matumaini ya ghana yalirejea Wakati mlinzi John Boye aliposawazisha katika dakika 73 na baadae dakika saba kabla kumalizika kwa mchezo ayew akafanikisha goli la pili kutokana na mpira wa kona uliopigwa na abdul rahman baba

Wakati huo huo, Algeria waliibuka na ushindi wa magoli mawili  dhid iya wapinzani wao Senegal