Category: Sports

  • Fabrice Mugheni Atajwa kutua Young Africans awaaga Rayon Sports.

    Hatimaye kiungo anayehusishwa kujiunga na Young Africans, Fabrice Mugheni, amewaaga rasmi mashabiki wa timu yake ya Rayon Sports ya Rwanda kwa kuwaambia ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

    Fabrice raia wa DR Congo aliwahi kusema kuwa, aliombwa video zake na Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambaye pia anahusika na masuala ya usajili ndani ya Young Africans.

    Fabrice kupitia mtandao wake wa Instagram, aliwaaga rasmi mashabiki wa timu hiyo jambo ambalo linatafsiriwa kama huenda akawa alishamalizana na Young Africans kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.

    Young Africans wamekua wanahusishwa na mipango ya usajili wa baadhi ya wachezaji wa kimataifa, hii ni kwa ajili ya kujipanga vyema kwa msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, endapo watapata fursa ya kuiwakilisha nchi kupitia michuano ya Kombe La Shirikisho.

  • Man Utd na Real Madrid zagongana kwa Lautaro Martinez

    Man Utd na Real Madrid zagongana kwa Lautaro Martinez

    Manchester City wamejiandaa kuanza mapambano dhidi ya Chelsea kuhusu huduma za mlinzi wa pembeni wa Leicester City Ben Chilwell, 23, baada ya kuonyesha kiwango murua akiwa kwa mbweha hao.

    Napoli hawatapunguza bei ya beki wao raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 28, ambapo wanataka Pauni Milioni 100, haya yanakuja kipindi ambacho anahusishwa kujiunga na miamba kama Manchester United, Manchester City na Paris Saint Germain.

    Manchester United na Real Madrid wanamchunguza mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez 22, baada ya mazungumzo ya kujiunga na miamba ya Catalunya FC Barcelona kusimama kwa hivi sasa.

    Kiungo wa Bosnia-Herzegovina na Juventus Miralem Pjanic, 30, amekataa ofa za kujiunga na Chelsea na Paris Saint Germain kwani anahitaji kujiunga na Barcelona.

    Kiungo wa zamani wa Chelsea Michael Ballack ameukubali kwa asilimia 100 uamuzi wa klabu yake  kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 24, kwani anaamini ataiga mapema mazingira ya soka la EPL.

    Kiungo mshambuliaji wa Croatia na Fc Barcelona Ivan Rakitic, 32, anafikiria kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2021 ambako kandarasi yake inatamatika.

    Kiungo wa Paris St-Germain Ander Herrera, 30, amesema mshambuliaji wa Uruguay ambaye wanacheza pamoja Edinson Cavani, anatamani kucheza soka katika taifa la Hispania, Strika Cavani, 33, amekuwa akihusishwa kujiunga na Atletico Madrid.

    Beki wa Manchester United Brandon Williams, 19, anawindwa na mawakala wawili juu ya kumsaini mlinzi huyo kisha wakawa wanamtafuti timu, masoko, usimamizi na masuala kama hayo.

  • Kocha mkuu Luc Eymael kurejea Tanzania Juni 06/07 kunoa kikosi chake.

    Kocha mkuu Luc Eymael kurejea Tanzania Juni 06/07 kunoa kikosi chake.

    Kocha mkuu wa Young Africans Luc Eymael amethibitisha kupokea tiketi ya ndege, kwa ajili ya safari ya kurejea Tanzania kuendelea na kazi ya kukinoa kikosi chake.

     

     

    Eymael amethibitisha taarifa za kupokea tiketi ya safari, baada ya kueleza wazi namna uongozi wa Young Africans ulivyokua umekaa kimya kuhusu mpango wa kumrudisha nchini ili aendelee na kazi.

    Kocha huyo amesema amepanga kuanza safari ya kuja nchini Juni 06 ama 07 na atakuwa sehemu ya benchi la ufundi kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya kikosi chake yanayoendelea jijini Dar es salaam.

    “Nikiwasili moja kwa moja nitaanza kazi, ninafahamu kwa sasa msaidizi wangu Mkwasa anafanya kazi nzuri ya kuwanoa vijana, nitakapofika nitaongeza nguvu katika benchi la ufundi na mambo yatakuwa sawa kabla ya kucheza mchezo wetu dhidi ya Mwadui.” Alisema Eymael

    Kikosi cha Young Africans kilianza kujiandaa na michezo ya ligi kuu Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho (ASFC), juma lililopita chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.

    “Ni vizuri kusaini mkataba na La Liga lakini kama unataka kuwa klabu kubwa kwanza jaribu kumrudisha kocha wako haraka iwezekanavyo kama una muheshimu”

    Young Africans watarejea dimbani Juni 13 kuendelea na michezo ya ligi kuu dhidi ya Mwadui FC kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, kisha watapambana na JKT Tanzania Juni 17 mjini Dodoma, Uwanja wa Jamuhuri.

     

     

     

     

     

     

  • uongozi wa klabu ya Yanga waachia ngazi

    uongozi wa klabu ya Yanga waachia ngazi

    Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Samwel Lukumay na aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji, akishikilia nyadhifa za Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili, Hussein Nyika, wamejiuzulu nafasi zao leo Machi 27, 2019.

    Nyika na Lukumay wametangaza hilo, kwenye makao makuu ya klabu hiyo ambapo wamesema kuwa wamefanya hivyo ili kupisha uchaguzi utaowezesha klabu hiyo kupata viongozi wapya.

    Aidha, viongozi hao ndio waliokuwa wamebaki kwenye uongozi wa Yanga ambao uliingia madarakani mwaka 2016 baada ya wengine kujizulu, hivyo sasa timu hiyo inabaki bila uongozi mpaka pale uchaguzi mkuu utakapofanyika.

    ”Ninajiuzulu nafasi zangu zote nikiwa kama Mjumbe wa kamati ya utendaji lakini pia Mwenyekiti wa kamati ya usajili na kamati ya mashindano na niombe msamaha kwa wale niliowakosea katika utekelezaji wangu wa majukumu,” amesema Nyika.

    Kwa upande wake Lukumay amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa uchaguzi mkuu kupata viongozi wote tofauti na awali ambavyo ilikuwa ni uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi.

    Hata hivyo, siku za hivi karibuni Baraza la wadhamini la Yanga liliweka wazi kuwa, badala ya kufanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi zilizowazi ikiwemo ile ya Mwenyekiti, utafanyika uchaguzi mkuu kwaajili ya kupata viongozi.

  • Kombe la FA: Mabingwa watetezi Chelsea kuminyana na Man Utd

    Kombe la FA: Mabingwa watetezi Chelsea kuminyana na Man Utd

    Mabingwa watetezi wa kombe la FA, Chelsea, wataminyana na mabingwa mara 12 wa kombe hilo, Manchester United, katika mzunguko wa tano wa michuano hiyo.

    Mechi ya miamba hiyo itakuwa ni marudio ya fainali ya mwaka jana mabapo Chelsea waliibuka na ushindi.

    Timu ya Ligi Daraja la Pili ya Newport County wanaweza kuminyana na mabingwa wa Ligi ya Premia Manchester City iwapo watawang’oa Middlesbrough katika mechi yao ya marudiano.

    Timu ya Ligi Daraka la Kwanza Doncaster Rovers wamenuwia kuwang’oa Crystal Palace iliyopo kwenye Ligi ya Premia baada ya kutoka sare mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa nne.

    Michezo ya raundi ya tano ya michuano ya FA itapigwa kati ya tarehe 15 na 18 ya mwezi Februari.

    Ratiba kamili ya raundi ya tano ya FA:

    Bristol City v Shrewsbury Town/Wolverhampton Wanderers

    AFC Wimbledon v Millwall

    Doncaster Rovers v Crystal Palace

    Middlesbrough/Newport County v Manchester City

    Chelsea v Manchester United

    Swansea v Barnet or Brentford

    Portsmouth/Queens Park Rangers v Watford

    Brighton & Hove Albion/West Bromwich Albion v Derby County

  • Real Madrid yafunika kwa ukwasi, ‘yaichapa’ Barcelona

    Real Madrid yafunika kwa ukwasi, ‘yaichapa’ Barcelona

    Klabu ya Real Madrid imetangazwa kuwa klabu ya soka duniani kote iliyoongoza kwa kuingiza fedha nyingi zaidi kati ya mwaka 2017/2018.

    Klabu hiyo ya Hispania yenye rekodi ya kushinda makombe ya misimu mitatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa, imeripotiwa kutengeneza $854.8 milioni katika kipindi hicho, kwa mujibu wa Deloitte Football Money League la mwaka 2019.

    Klabu ya Barcelona ambayo sasa inaongoza La Liga imechukua nafasi ya pili katika orodha hiyo ikiwa imeingiza $785.5 milioni, na magwiji wa Uingereza, Manchester United ambao mwaka uliopita waliongoza orodha hiyo wameangukia katika nafasi ya tatu wakiwa wametengeneza $758 milioni.

    Hii ni mara ya kumi na mbili katika historia kwa Real Madrid kuongoza katika orodha hiyo lakini ni mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 2014/15.

    Kwa mujibu wa uchambuzi wa Deloitte, timu 20 za juu kwenye orodha hiyo zilikuwa na ukuaji wa mapato yao kwa ujumla kwa 6%. Walioshika nafasi tatu za juu zaidi yaani Real Madrid, Barcelona na Manchester United kwa pamoja waliingiza $2.3 bilioni ikiwa ni zaidi ya mara mbili zaidi ya mapato yao ya miaka kumi iliyopita.

    Jana, mashabiki wa Real Madrid wameipokea habari hiyo kwa furaha iliyosindikizwa na ushindi wa 4-2 dhidi ya Girona.

     

  • Ronaldo aingia katika makubaliano na mahakama ili kukwepa kifungo jela

    Ronaldo aingia katika makubaliano na mahakama ili kukwepa kifungo jela

    Nyota wa soka Cristiano Ronaldo ameingia katika makubaliano na mahakama ya Madrid kuhusu madai ya kukwepa kulipa kodi baada ya kubali kupigwa faini ya €18.8m (£16.6m) fine. makubaliano yaliofikiwa yanashirikisha kifungo cha miezi 23 jela

    Jaji mmoja alikataa ombi la mchezaji huyo kuhudhuria kesi hiyo kupitia kanda ya video ama hata kuingia katika jumba hilo kwa kutumia gari ili kuzuia kuandamwa na vyombo vya habari.

    Nchini Uhispania, wafungwa huwa hawahudumii kifungo cha chini ya miaka miwili.

    Hali ya makosa ya Ronaldo inamaanisha kwamba hatohudumia kifungo jela.

    Kesi hiyo ilichukua dakika chache baada ya Ronaldo kukubali makubaliano yaliotolewa na viongozi wa mashtaka

    Mchezaji huyo wa Juventus ambaye aliichezea klabu hiyo usiku wa kuamkia mashtaka hayo aliwasili akiwa anatabasamu.

    Wakili wake alikuwa amehoji kwamba kutokana na umaarufu wake , alipaswa kutotumia lango kuu la mahakama kutokana na hali ya usalama.

    Ronaldo ambaye ni bingwa mara tano wa taji la Ballon d’Or na miongoni mwa wachezaji bora duniani, anatuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi nchini Uhispania kati ya 2011 na 2014 wakati alipokuwa akiichezea klabu ya Real Madrid wakati huo akiwa na makao yake nchini Uhispania.

    Kesi hiyo inaangazia mikataba ya haki za picha zake.

    Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa fedha hizo zilipitishwa kupitia kampuni zinazotozwa kodi ya chini katika mataifa ya kigeni ili kukwepa kulipa kodi iliohitajika.

    Kitita hicho kilidaiwa kuwa cha €14.8m.

    Mwaka 2017, wakati madai hayo yalipochipuka, viongozi wa mashtaka walisema kuwa ulikuwa ukiukaji wa ahadi yake nchini Uhispania.

    Lakini wakili wa Ronaldo alisema kuwa kutoelewana kuhusu kile kilichohitajika na kili ambacho hakikuhitajika chini ya sheria za Uhispania na kuzuia jaribio lolote la kukwepa kulipa kodi.

    Ronaldo

    Xabi Alonso anakabiliwa na mashtaka kama hayo

    Makubaliano hayo yaliofanyika mwezi Juni mwaka uliopita yaliafikiwa na mamlaka ya ushuru nchini Uhispania.

    Yatawasilishwa mbele ya jaji siku ya Jumanne mahakamani.

    Jaji huyo atatangaza uamuzi wake katika kipindi cha siku zijazo.

    Ronaldo sio mchezaji wa kiwango cha juu wa pekee kukabiliana na mkono wa mamlaka ya ushuru nchini Uhispania.

    Mchezaji mwezake wa zamani Xabi Alonso pia anatarajiwa kuwasili mahakamani siku hiyohiyo kwa mara ya kwanza akishtakiwa na shataka kama lake la makosa ya haki za picha zake ya takriban €2m.

    Katika siku za hivi karibuni:

    • Nyota wa Barcelona Lionel Messi alizuia kifungo kwa mashtaka kama hayo yanayohusisha haki za picha zake , akilazimika kulipa mamilioni kama faini na ushuru.
    • Neymar da Silva Santos Junior alikuwa katikati ya mgogoro wakati Barcelona ilipopigwa faini ya mamilioni ya fedha baada ya kushtakiwa kwa kukwepa kulipa kodi lakini akazuia kukiri shtaka hilo.
    • Mchezaji wa Real Madrid Marcelo Vieira alikiri mashtaka ya kukwepa kulipa kodi na kukubali kuondolewa kifungo cha miaka minne jela kufuatia hatua yake ya kutumia kampuni za kigeni kumpitishia takriban Yuro nusu milioni ya mapato yake.

    Ronaldo pia anakabiliwa na shtaka jingine: Mchezaji huyo anatuhumiwa kutekeleza ubakaji mjini Las Vegas 2009, mashtaka ambayo anapinga.

    cc;BBCswahili

  • Mourinho agoma kuzungumzia kufutwa kazi

    Mourinho agoma kuzungumzia kufutwa kazi

    Jose Mourinho anasema kwamba, hawezi kuzungumzia kuhusu kuondoka kwake kutoka kwenye ukufunzi mkuu wa timu ya soka ya Manchester United, kwa sababu ya “heshima kubwa aliyo nayo” kwa Mashetani Wekundu.

    Mreno huyo alifutwa kazi siku ya Jumanne baada ya kukifunza timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili u nusu.

    Timu ya Man United ipo kwenye nafasi ya 6 katika jedwali la mchuano wa Ligi kuu ya Premia, alama 19 nyuma ya viongozi Liverpool.

    “Nilikuwa na furaha kubwa kuvalia nembo ya Manchester United, tangu siku ya kwanza kufika hapa, na nina imani kuwa mashabiki wote wa Man United, walitambua hilo,” Mourinho amesema kwa njia ya taarifa.

    “Kila mara ukurasa unapofungwa, mimi huonyesha heshima kubwa kwa kutosema lolote kuwahusu wenzangu wa zamani.”

    Siku ya Jumatano, mshambulizi wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, aliteuliwa kusimamia kwa muda klabu hiyo, hadi mwisho wa msimu huu.

    Mourinho amekwenda nyumbani kwake Jijini London, huku mkufunzi huyo wa zamani wa timu za Chelsea na Real Madrid, akiviomba vyombo vya habari kumpa heshima na kutoingilia mambo yake ya ndani, kabla hajarejea tena katika ukufunzi wa soka.

    kizungumza na Sky Sports News, mapema siku ya Jumatano, alisema: “Daima nilikuwa nashangazwa sana na wakufunzi wanaohama hama vilabu vya soka, na kisha wanaanza kuzungumzia maswala ya ndani ya kile kilichotokea, hasa ni nani wa kulaumiwa.

    “Siwezi kabisa kuzungumzia kitu ambacho hakikuwa kizuri, huyo sio mimi kabisa.

    “Hadi nitakaporejea tena kwenye ulingo wa soka, kwa sasa napenda kuishi maisha yangu tu ya kawaida. “Hatma ya baadaye ya Manchester United iko nzuri bila ya mimi, na pia mimi maisha yangu ya baadaye ni nzuri mno bila ya Manchester United.”…Hiyo ndio taarifa ya kina ya Mourinho.

    Salamu kamili za Mourinho

    Nimekuwa na furaha isiyo na kifani kuvalia nembo ya Manchester United, tangu siku ya kwanza nilipowasili Old Traford, na nina amini kuwa mashabiki wote wa Man U wanatambua hilo.

    Na hivyo ndivyo ilivyo tu na vilabu vyangu vya awali, ambako nilifanya kazi, nimefanya kazi na watu wazuri na nina imani kuwa baadhi yao watakuwa marafiki zangu milele.

    Najua kuwa mnafahamu misingi yangu ya kazi na taaluma yangu. Kila mara ukurasa unapofungwa, mimi huonyesha heshima ya dhati mno kwa wenzangu wa zamani.

    Nadhani vyombo vya habari vitaheshimu msimamo wangu na kuniacha niishi tu maisha ya kawaida, hadi pale nitakapoamua kurejea tena katika ukufunzi wa soka.

    Krismasi njema

    Maoni ya wachezaji

    Mchezaji wa kiungo cha kati Jesse Lingard, alikuwa mchezaji wa kwanza kabisa kumuandikia Mourinho ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii wa Tweeter, “Thank you for the memories and wisdom,” yaani “Asante kwa kumbukumbu na busara yako.”

    Naye mlinzi wa kati Eric Bailly aliandika: “Lolote wasemalo, daima nitamshukuru mtu aliyenipa fursa ya kubobea katika uwanja wa Old Trafford.

    “Asante sana kwa kile ulichonifunza. Heri njema Kocha

  • Samatta kuwindwa na vilabu vya  uingereza

    Samatta kuwindwa na vilabu vya uingereza

    Imeripotiwa kuwa Klabu za Evarton, West Ham , Burnley na Brighton zinaiwinda saini ya mshambuliaji wa Genk na kapteni wa Taifa stars Mbwana Ali Samatta. Samatta ameonesha kiwango cha juu msimu huu ambapo mpaka sasa amefunga magoli 14 katika mechi 16 alizocheza.

     

  • Ballon d’Or: Sergio Aguero na Gareth Bale miongoni mwa wanaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani

    Ballon d’Or: Sergio Aguero na Gareth Bale miongoni mwa wanaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani

    Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, kipa wa Liverpool Alisson, mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema na straika wa Paris St-Germain Edinson Cavani ni miongoni mwa wachezaji walioteuliwa kushindania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu.

    Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale anayechezea Real Madrid pia ameorodheshwa kushindania.

  • John Terry: Kapteni wa zamani wa England na Chelsea astaafu soka

    John Terry: Kapteni wa zamani wa England na Chelsea astaafu soka

    Aliyekuwa kapteni wa timu ya taifa ya England na Chelsea John Terry amestaafu katika soka.

    Terry, mwenye umri wa miaka 37, hajaichezea klabu yoyote tangu aondoke timu ya mabingwa Aston Villa msimu wa joto.

    Mlinzi huyo alitoa tangazo hilo kwenye akaunti yake ya Instagram, akisema: “Baada ya miaka 23 kama mchezaji wa soka, nimeamua sasa ndio muda muafaka kwangu mimi kustaafu kutoka mchezo wa soka.”

    Terry, aliyejinyakulia mataji 78 England, aliondoka Chelsea mnamo 2017 baadaya kuichezea klabu hiyo ya London kwa miongo miwili.