Category: Sports

  • Chicharito Apelekwa Real Madrid Kwa Mkopo

    Chicharito Apelekwa Real Madrid Kwa Mkopo

    Chicharito

    Huku dirisha la usajiri ulaya llikitarajiwa kufungwa usiku wa leo, tiimu ya Manchester United wamempeleka kwa mkopo Javie Hernandez “Chicharito kwenda timu ya Real Madrid  na wako mbioni kumwachia Danny Welbeck kwenda Tottenham au Everton.

    Katika siku za hivi karibuni timu zote mbili yaani Manchester United na Real Madrid  zimeonyesha udhaifu katika safu ya ushambuliaji, ambapo  katika mechi dhidi ya Burnley Manchester United ilitoka suluhu huku Real Madrid ikichapwa jana usiku na Real Sociedad kwa mabao 3-1.

    Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico amekuwa hapati namba ya uhakika ya kudumu katika kikosi cha kwanza hata baada ya kocha mpya Mholanzi Louis Van Gaal kujiunga na timu hiyo mwezi uliopita.

    Tayari mchezaji Chicharito ametambulishwa rasmi hii leo na bado haijaeleweka dili la mchezaji huyo kuhamia Real Madrid ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria.  Duru nyingine zikiarifu kuwa kulikuwa na mpango wa chini chini ambao ulikuwa umhusishe Falcao kwenda Real Madrid lakini baada ya mazungumzo Falcao amekwenda Manchester United na Chicharito kuhamia Real.

  • Christiano Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya

    Christiano Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya

    Ronaldo

    Mchezaji wa kimataifa wa Portugal anayechezea timu ya Real Madrid Christiano Ronaldo Jana usiku alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa mwaka 2014/2015.

    Ronaldo alitwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji Arjen Robben wa Bayern Munich Emmanuel Neur wa Bayern Munich katika sherehew iliyofanyika jijini Monaco nchini Ufaransa.

  • Okwi Arudi Simba Asaini Mkataba Kama Mchezaji Huru Kulinda Kipaji Chake

    Okwi Arudi Simba Asaini Mkataba Kama Mchezaji Huru Kulinda Kipaji Chake

    Okwi

    Aliyekuwa msambuliaji wa Yanga Emmanuel Okwi jana jioni amesaini Simba SC kwa mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.
    Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.
    “Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.
    Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni.
    “Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.
    Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia.
    Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu.
    Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.
    Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.
    Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo.
    Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.
    Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo(Jana) baina ya mchezo huyo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.
    Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema.

  • Arsenal Yaifunga 1-0 Besiktas Na Kufuzu UEFA Kwa Msimu Wa 17 Mfululizo

    Arsenal Yaifunga 1-0 Besiktas Na Kufuzu UEFA Kwa Msimu Wa 17 Mfululizo

    Arsenal

    Timu Ya Arsenal ya nchini Uingereza jana usiku iliweza kufuzu kucheza mashindano ya kombe la UEFA kwa msimu wa 17  mfululizo kwa timu za Ulaya baada ya kuichapa timu ya Besiktas ya Uturuki kwa bao 1-0.

    Katika mchezo wa awali wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana na hivyo kusubiri uamuzi wa nani atavuka katika mechi ya pili ya marudiano ambayo ilichezwa jana usiku. Alikuwa ni mchezaji mpya wa timu ya Arsenal aliyejiunga msumu huu akitokea timu ya FC Barcelona Alex  Sanchez, ambaye ndiye aliyeiwezesha Arsenal kusonga mbele baada ya kuipatia timu yake bao hilo pekee la ushindi kwa timu yake katika dakika ya 46 ya kipindi cha kwanza.

    Arsenal ilipata nafasi ya kumaliza mchezo huo mapema lakini washambuliaji wake Santi Cazorla na Alex Chamberlain walipoteza nafasi nyingi za wazi walizopata.

    Timu ya Arsenal ilipata pigo la kupungukiwa na mchezaji mmoja uwanjani, zikiwa zimesalia dakika 15 kabla ya kumalizika kwa mchezo,  baada ya mchezaji wake Mathieu De Buchy kutolewa nje ya mchezo kwa kadi mbili za njano na kufanikiwa kupambana wakilinda ushindi wao kiduchu hadi mwisho wa mchezo.

    Timu nyingine zilizofuzu pamoja na Arsenal katika kinyang’anyiro cha kufuzu jana usiku ni pamoja na Atletico Bilbao 3-1 dhidi ya Napoli,  Bayer 04 Leverkusen 4-0 dhidi ya FC Copenhagen, Ludogorets Razgrad 1-0 dhidi ya Steau Bucharest na Malmo FF – 3-0 dhidi ya Fc Red Bull Salzburg.

     

     

     

     

  • Man UTD Yachapwa 4-0. Van Gaal Alaumu Wachezaji Wake

    Man UTD Yachapwa 4-0. Van Gaal Alaumu Wachezaji Wake

    Van GaalBaada ya kipigo cha magoli 4-0 dhidi ya timu yake,  Meneja wa klabu ya Man Utd Van Gaal amelia na kikosi chake ambacho jana usiku kiliendelea kupata matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu mpya wa soka huko nchini Uingereza Agosti 16.
    Kocha Van Gaal amesema kikosi chake hakikucheza vizuri wakati wa mchezo wa michuano ya kombe la ligi dhidi ya klabu ya Milton Keynes Dons ambao waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri na kuwatupa nje ya michuano hiyo mashetani wekundu.
    Pia Van Gaal amesema makosa madogo madogo yaliyofanywa na wachezaji wake wa safu ya ulinzi yalitoa mwanya mkubwa kwa wapinzani wao kupata mabao kwa urahisi. Akiendelea kulalamika kocha huyo alisema hana budi kuwasilisha lawama zake kwa wachezaji aliokuwa amewapa jukumu la kucheza mechi ya jana usiku.

  • Mtangazaji Wa Michezo Omari Katanga Naye Ajiunga EFM

    Mtangazaji Wa Michezo Omari Katanga Naye Ajiunga EFM

    Omari Katanga

    Aliyekuwa mtangazaji wa Redio One katika kipindi cha “Spot Leo” Omary Katanga amefuata nyayo za pacha wake Maulid wa Kitenge aliyejiunga na kituo cha redio 93.7 E FM mapema wiki hii.Katanga na Kitenge walikuwa wote Redio One, na wataanza kusikika E FM kesho(Leo) katika kipindi cha michezo cha E Sports, ambacho kitakuwa kikiruka kila siku saa 7:00 – 7:30 usiku.Watangazaji hao wanajiunga na watangazaji wengine maarufu kama Dennis Ssebo, Dickson Ponnela (Dizzo 1), DJ Majay, na Kanky

     

  • Maulid Kitenge Na Omari Katanga Waanza Rasmi Kazi EFM

    Maulid Kitenge Na Omari Katanga Waanza Rasmi Kazi EFM

    DU7C9347

    Watangazaji mahiri wa michezo nchini, Maulid Kitenge na Omari Katanga jana usiku wameanza kazi rasmi katika kituo chako cha Radio EFM.

    Watangazaji hao mahiri ambao wote wamejiunga  wiki hii watakuwa wakitangaza katika kipindi cha michezo cha E Sports kinachoruka hewani kuanzia mida ya saa moja kamili usiku. Kwa kuanzia pia Mtangazaji Maulid Kitenge alikuwa uwanja wa ndege wa Kimataifa jana usiku kukutangazia moja kwa moja yaani live kuwasili kwa nyota wa timu ya wakongwe wa real madrid.

  • Fifa nayo yaishukia Gor Mahia

    Fifa nayo yaishukia Gor Mahia

    NI taabu tupu kwenye ngome ya Gor Mahia kwani baada ya kuandamwa na Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) kwa kutokulipa ushuru wa Sh118 milioni, sasa iko hatarini kufungiwa na Fifa kusajili wachezaji.

    Kwa wiki chache zilizopita, mambo hayajawa mazuri kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Kenya ambao wamefilisika na kwa sasa wanawategemea mashabiki wao kutoa mchango ili kuwanusuru na janga la kifedha.

    Huku hayo yakizidi kuwaumiza kichwa, Fifa ambalo ni shirikisho la kimataifa la vyama vya soka, imetishia kuwashushia rungu hilo baada ya klabu hiyo kukikuka kanuni katika kumsajili, Patrick Oboya, kutoka klabu ya Vietnamese.

    Habari zilizopatikana zinasema shirikisho hilo limenusa mchezo mchafu unaodaiwa kufanywa Gor kutokufuata kanuni zinazotakiwa kumnunua mchezaji huyo na sasa limeitaka klabu hiyo kujieleza kinagaubaga jinsi gani walivyomsajili Oboya.

    “Tunataka Gor Mahia itueleze kwa mapana na marefu ni utaratibu upi walioufuata hadi kumpata mchezaji huyo. Oboya amekuwa akishiriki mechi bila ya kuwa na cheti cha kimataifa cha uhamisho na hilo ni kosa kubwa,” taarifa kutoka Fifa imeeleza.

    Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ambrose Rachier amekiri kupokea barua ya Fifa kuhusu usajili wa Oboya na amesema katika hatua za awali wamemwomba mchezaji huyo aketi pembeni kidogo mpaka mzozo huo utakapotatuliwa.

    Ofisa Mkuu wa uhamisho wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Nick Mwendwa, naye amethibitisha nao kuwa na nakala ya barua hiyo, lakini analitetea shirikisho lisilaumiwe.

    Kwa kawaida Fifa huwa inazifungia usajili klabu zinazofanya faulo katika suala hilo. Pia huenda Gor Mahia ikapokonywa pointi za mechi ambazo Oboya alicheza kama itathibitika kanuni zilikiukwa katika usajili wake.

    Kabla ya kujiunga na Gor mwanzoni mwa msimu huu, Oboya alikuwa akiichezea Thanh Hoa inayoshiriki Ligi Kuu Vietnam ambako mkataba wake ulisitishwa. Alikwenda Vietnam akitokea Ligi ya Slovakia ambako aliichezea klabu ya MFK Ruzomberok.

    source mwanaspoti

  • Msanii LADY JAY DEE (@jidejaydee) ameula katika michuano ya Kombe la Dunia 2014

    Msanii LADY JAY DEE (@jidejaydee) ameula katika michuano ya Kombe la Dunia 2014

    Msanii Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameula katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kupata nafasi ya kuandaa wimbo kwa a jili ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka duniani.

    Jaydee anayefahamika pia kama Komandoo au Anaconda, amepata fursa ya kuandaa wimbo maalum wa michuano hiyo ‘FIFA World Cup Anthem’ akishirikiana na wakali wawili David Correy wa Brazil na rapa Octopizzo wa Kenya.

    Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha ya Kiingereza huku Octopizzo ‘akichana’ kwa Kiswahili.

    Wimbo huo ulipigwa kwa mara ya kwanza jana jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi za robo fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

    Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Yebeltal Getachew alisema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam huku akizitaja zawadi nyingine kuwa luninga, mipira na fulana. Wakati huo huo, Jmosi tarehe 12 April Lady Jaydee anataraji kuachia wimbo wake na video mpya ‘Nasimama’.
    CHANZO: Nipashe