Category: Sports

  • KUNA UWEZEKANO WA KURUDISHA CHENJI KWA MASHABIKI AFRIKA?

    KUNA UWEZEKANO WA KURUDISHA CHENJI KWA MASHABIKI AFRIKA?

    Wachezaji wa Sunderland wameamua kuwarudishia Mashabiki wao gharama walizotumia kuutizama mchezo ambao mwisho wa siku walipokea kichapo cha bao 8-0 kutoka kwa Southampton.

    Hicho kilikuwa kisago kikubwa kabisa kwa Sunderland katika miaka 32.

    Mashabiki wana nafasi ya kudai pesa yao mpaka kufikia tarehe 5 ya Novemba mwaka huu.

    Akizungumza kwa niaba ya wenzake, nahodha John O’Shea amesema, “Tunashinda na kushindwa kama timu, wachezaji, uongozi na mashabiki lakini tungependa kuwatambua na kuwashukuru mashabiki waliosafiri umbali mrefu kuja kutuunga mkono na pamoja na yote yaliyotokea walibaki nasi mpka filimbi ya mwisho”

    Mashabiki wameombwa kurejesha tiketi au hata kuzituma kwa njia ya posta wakiambatanisha na majina na anwani zao kamili.

    Mashabiki ambao hawatadai pesa yao basi pesa hiyo waliyoitumia katika manunuzi ya Tiketi zitapelekwa katika kituo cha kutunzia watoto.


     

  • FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA ZAINGIA UTATA KUFUATIA KUENEA KWA EBOLA

    FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA ZAINGIA UTATA KUFUATIA KUENEA KWA EBOLA

    Kuenea kwa ugonjwa wa Ebola umefanya fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kuwa mashakani.

    Fainali hizo zimepangwa kufanyika nchini Moroco kuanzia Januari 17 lakini nchi hiyo iliwaeleza waandaji wa mashindano hayo kwamba wangependa kusogeza mbele mashandano hayo.

    Serikali ya Moroco imekuwa na wasi wasi maambukizo ya virusi vya ebola kutoka nchi za magharibi mwa Afrika.

    Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF linatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho mwezi novemba kama nitasogeza mbele mashindano hayo au la japo limekuwa likisisitiza kuwa mashindano hayo yatafanyika kama kawaida

    Wakati huo huo kumekuwa na taarifa kuwa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limeizungumzia nchi za Ghana na Afrika kusisni ili kama zinaweza kukubali kuwa fainali hizo.

    DONDOO ZA LIGI KUU UINGEREZA

    EPL_Logo

    Baada ya ligi mbalimbali duniani kusimama kwa muda ili kupisha mechi za timu za taifa, hekaheka za ligi hizo zinataraji kuendelea tena kesho.

    Huko England nyasi za viwanja kadhaa zitakuwa matatani pale timu mbalimbali zitakaposhuka dimbani.

    Katika uwanja wa Etihad wenyeji Manchester City watajitupa dimbani kuwakaribisha Tottenham katika mechi itakayotangazwa moja kwa moja na Idha ya Kiswahili ya BBC kuanzia saa saa nane na nusu kwa saa Afrika Mashiriki.

    Mechi nyingine zitakazochezwa hiyo kesho ni kati ya Arsenal watakapowakaribisha Hull City, Burnley itapepetana West Ham, Crystal Palace watawakaribisha Chelsea, huku Everton watakuwa nyumbani kumenyana na Aston Villa.

    Nayo Newcastle watavaana na Leicester City wakati Southampton itakuwa nyumbani kukwaana na Surnderland.

    Siku ya Jumapili Liverpool watakuwa ugenini dhidi ya QPR nayo Stocke City watacheza dhidi ya Swansea City.

     

  • SIMBA NA YANGA KUKICHAPA KESHO KWENYE MCHEZO WA LIGI KUU

    SIMBA NA YANGA KUKICHAPA KESHO KWENYE MCHEZO WA LIGI KUU

    Kikosi cha wekundu wa msimbazi Simba, kimerejea nnchini kimyakimya toka Afrika kusini baada ya kumaliza kambi yake na sasa wapo tayari kuwavaa watani wao wa jadi Yanga katika mchezo wa ligi kuu uatakaopigwa keshokutwa jumamosi kwenye uwanja wa taifa jijini Daresalaam.

    ikiwa huko Afrika kusini Simba chini ya kocha wake Mzambia Patrick Phiri, imecheza mechi tatu za kujipima nguvu, ambapo imekwenda sare mechi mbili na kuchezea kichapo mechi moja

    Tumezungumza na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tulli, na kuthibitisha kuwasili kwa kikosi hicho, lakini pia ameeleza kuwa mlinda mlango wao namba 2 Husen Sharifu maarufu kama Casilas amejiondoa rasmi kushiriki katika mechi hiyo ya Octoba 18

    Kwa upande wao Yanga kupitia mwenyekiti wake wa mashindano, Seif Ahmed maarufu kama Seif Magari, wamesema kikosi hicho chini ya kocha Mbrazil Maxio Maximo, kipo kamili na kinachosubiriwa ni muda tu ufike wa kumchinja mnyama

  • HATIMAE THEO WALCOTT AREJEA UWANJANI BAADA MIEZI 9

    HATIMAE THEO WALCOTT AREJEA UWANJANI BAADA MIEZI 9

    Mshambuliaji nyota wa Arsenal Theo Walcott ambae alikaa nje kwa miezi tisa akiwa majeruhi, ameanza mazoezi rasmi akiwa na kikosi hicho chini ya Arsenal Wenger.

    LIVE-A-dejected-Theo-Walcott-of-Arsenal-looks-on

    article-2535533-1A749A0300000578-921_634x420

    article-0-1A778A4500000578-105_634x448

     

  • SHABIKI AMUOMBA NEYMAR AMUOE DADA YAKE

    SHABIKI AMUOMBA NEYMAR AMUOE DADA YAKE

    Shabiki amuomba Neymar amuoe dada yake baada ya mshambuliaji huyo  wa Brazil kupiga goli nne peke yake dhidi ya Japan.

    shabiki huyo amemuomba  striker  wa Barcelona amuoe dada yake  Amanda Recla, ambae ni model alieingia kwenye  15 bora  ya Miss Brazil.

    Bz6dd0ICMAMY-BJ

    ingawa dada wa shbiki huyo Amanda amesema hana analofikiria juu ya uamuzi wa kaka yake Stephan, na kusema kuwa atamuua kufatia kitendo hicho

    Hata hivyo Stephan ameendelea na msimamo wake kwa kudai dada yake ametoa kauli hiyo tu lakini ukweli ni kwamba yupo single na endapo Neymar atamkubali basi atamshukuru kaka yake katika kipindi chote cha maisha yake

    Bz6d9xrCUAAcggt.jpg-small
    Amanda Recla
  • TFF YAFANYA YAFANYA MAREKEBISHO YA MECHI LIGI DARAJA LA KWANZA

    TFF YAFANYA YAFANYA MAREKEBISHO YA MECHI LIGI DARAJA LA KWANZA

    UWANJA+WA+ALI+HASSAN+MWINYI

    Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, imefanya marekebisho ya mechi nne za kundi A za Ligi Daraja la kwanza ili kutoa fursa ya matumizi ya uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.

    Timu za African Lyon na Kimondo FC ambazo awali zilikuwa zicheze Octoba 25 kwenye uwanja wa mabatini mkoani Pwani sasa zitacheza Octoba 26 uwanja wa Karume, Dar es salaam.

    Nayo mechi ya Polisi Dar es salaam na majimaji ya Songea ilikuwa ichezwe Octoba 26 sasa itachezwa Octoba 27, huku mechi ya Friends rangers na Ashanti UNITED ilikuwa ichezwe mabatini mkoani pwani, Octoba 26, sasa itachezwa uwanja wa Karume octoba 28

    mechi nyingine ni kati ya Lipuli FC na JKT Mlale iliyokuwa ichezwe Octoba 25 kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa, imesogezwa mbele na itachezwa octoba 26 kwenye uwanja huohuo

     

    Katika hatua nyingine TFF imeongeza muda wa usajili wa wachezaji kwa timu za ligi daraja la pili kwa sikun saba, ambapo sasa utamalizika octoba 21 mwaka huu

    Awali usajili huo unaofanyika kwa njia ya mtandao (online) ulikuwa umalizike octoba 14 mwaka huu lakini ni klabu chache zilizoweza kusajili ndani ya muda uliopangwa.

    Klabu ambazo hazijakamilisha shughuli hiyo ya usajili, zinatakiwa kukamilisha ndani ya siku hizo saba kwani TFF haitaongeza tena muda wa usajili

  • RAIS MUSEVEN AIGHARAMIA UGANDA CRANES

    RAIS MUSEVEN AIGHARAMIA UGANDA CRANES

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amegharamia safari ya timu ya soka ya taifa Uganda Cranes kwenda Togo, kucheza mechi ya marudiano siku ya jumatano ya kufuzu kucheza fainali ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 kundi E.

    Rais Museveni amewapatia dolla laki moja na efu arobuni kusafirisha timu ya Uganda Cranes kwenda Togo kwa mechi ya Jumatano.

    Hicho ni kikosi cha Uganda Cranes kilichovalia jezi nyekundu yaani yenye kuishia 42 na yenye 40 ni Togo.

    Katika mechi ya jumamosi Uganda Cranes ilinyamazishwa na Togo kwa bao 1 kwqa nunge hivyo Uganda wanahitaji ushindi mechi ya Jumatano kuongeza matumaini ya nafasi ya kushiriki fainali ya kombe la Afrika mwaka 2015 nchini Morocco.

    Katika kundi hilo E Ghana ndiyo wanaongoza na alama 5 wakifatiwa na Uganda alama 4, Ginea alama 4 na Togo alama 3

    Uganda-Cranes
    Uganda-Cranes
  • JAMAL MALINZI AMESEMA YEYE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WAPO MADARAKANI KUENDELEZA SOKA NA SI MALUMBANO

    JAMAL MALINZI AMESEMA YEYE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WAPO MADARAKANI KUENDELEZA SOKA NA SI MALUMBANO

    SHIRIKISHO la kandanda Tanzania Tff,limesema mashindano ya taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12, yatafanyika mkoani mwanza kuanzia mwezi Desemba mwaka huu,ukiwa ni mpango maalumu unaolenga kupata kikosi imara cha kitakachoshiriki michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya 17 (U17), mwaka 2019, ambapo Tanzania imeomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

    Akizungumza na wanahabari hii leo kuelezea mpango huo, Rais wa TFF, Jamal Malinzi,amesema mashindano hayo yatashirikisha kombaini za mikoa yote Tanzania,lakini kwanza amenza kwa kusema yeye pamoja na kamati yake ya utendaji ipo madarakani kuendeleza soka na si kulumbana .

    Kwa upande wao mkurugenzi wa shule za Alliance,James Bwire, pamoja na Kanali mstaafu Idd Kipingu wa Lord Baden,wameridhia kwa kauli moja vituo vyao kutumika katika kuendeleza soka la Tanzania,na kipingu akisisitiza kuwa suala hili ni la watanzania wote.

    Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Desemba 6 hadi 12 Mmwaka huu, na timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza, Desemba 5 mwaka huu. Bajeti ya mashindano hayo ni sh. milioni 350.

    Mkurugenzi wa Symbion, Stewart John Hall aliwasilisha kwa waandishi wa habari programu hiyo

  • RONALDO MANCHESTER UNITED NI FAMILIA YANGU

    RONALDO MANCHESTER UNITED NI FAMILIA YANGU

    Mchezaji wa kimataifa kutoka  Portugal ambae nyota yake ilianza kung’aa na kutambulika zaidi duniani kupitia Club ya Manchester united Cristiano Ronaldo.

    hivi karibuni kumekuwa na tetesi juu ya uwezekano wa mchezaji huyo anaeichezea club ya Real Madrid kurudi Manchester united .

    Club ya Real Madrid imeonyesha msimamo wake juu ya mchezaji huyo kwa kumuhitaji kuendelea kukichapa hapo Santiago Bernabeu kwenye msimu wa kiangazi kitendo ambacho Ronaldo amekipokea kwa furaha taarifa hiyo na kusema anafurahi kuitumikia Club hiyo lakini pia aliwashukuru Manchester united kwa mapenzi ya dhati wanayomwuonyesha

     

  • LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA WIKIENDI HII

    LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA WIKIENDI HII

    Kivumbi cha ligi kuu soka Tanzania bara kinaendelea tena wikiendi hii kwa timu kumi kushuka katika madimba matano tofauti,ambapo katika uwanja wa taifa jijini wenyeji simba watawakaribisha vijana toka shinyanga-stand united,Mtibwa dhidi ya mgambo jkt,ruvu shooting dhidi ya mbeya city,prisons na azam na polisi morogoro wakikipiga dhidi ya kagera.

  • TFF YATANGAZA DHAMIRA YA KUVIKATA VILABU VYA LIGI KUU ASILIMIA TANO YA FEDHA

    TFF YATANGAZA DHAMIRA YA KUVIKATA VILABU VYA LIGI KUU ASILIMIA TANO YA FEDHA

    Kamati ya utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF,jana tarehe 2 oct imetamka hadharani kuwa inadhamira ya kweli ya kuvikata vilabu vya ligi kuu asilimia 5 ya fedha za mdhamini,na kwamba yeyote anayepinga agizo hilo anajisumbua.

    Hatua ya tff,kujitokeza hadharani kutoa msimamo wake,imekuja baada ya umoja wa vilabu kumteua mwanasheria atakayewakingia kifua kupinga agizo hilo,ambalo wanaliona kama unyonyaji kwenye kiasi kidogo wanachokipata toka kwa mdhamini wa ligi.

    Tayari kwa upande wake bodi inayosimamia ligi kuu na ile ya daraja la kwanza Tanzania bara,imeshaweka wazi kuwa msimamo wake ni kutaka vilabu hivyo visikatwe hiyo asilimia tano kama tff inavyotaka.

    Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za shirikisho,rais wa tff Jamal Malinzi,amesema bodi ya ligi itake isitake ni lazima kutekeleza agizo hilo la kuvikata vilabu asilimia tano ya fedha toka kwa mdhamini.