Usiku wa klabu bingwa Ulaya umeshuhudia jumla ya magoli 23 yakifungwa usiku jana kwa michezo mbalimbali kupigwa katika viwanja maarufu barani humo.
Haya ni matokeo ya michezo hiyo iliyochezwa hapo jana:

Usiku wa klabu bingwa Ulaya umeshuhudia jumla ya magoli 23 yakifungwa usiku jana kwa michezo mbalimbali kupigwa katika viwanja maarufu barani humo.
Haya ni matokeo ya michezo hiyo iliyochezwa hapo jana:

Klabu ya Manchester City imejikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea kipigo cha magoli mawili kwa moja dhidi ya CSKA Moskva ndani ya uwanja wao wa nyumbani Etihad,
Magoli mawili ya Seydou Doumbia mnamo dakika ya pili ya mchezo huo na lile jengine mnamo dakika ya 34 yalitosha kuwaangamiza mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini England huku goli lao la kufutia machozi likifungwa na Yaya Toure ambae baadae alionyeshwa kadi nyekundu.
Toure alipewa kadi nyekundu dakika ya 81 huku City ikiwa teyari ishampoteza kiungo wa kiBrazil Fernandinho aliyelimwa kadi nyekundu dakika ya 70 hivyo kumaliza mchezo huo wakiwa 9 tu uwanjani.
Matokeo hayo yameshuhudia City ikitupwa mpaka mkiani mwa kundi E ikiwa na jumla ya alama 2 hivyo kuwalazimu kushinda michezo miwili iliyobakia dhidi ya Bayern Munich mwenye alama 12 na AS Roma mwenye alama 4.

Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona, Lionel Messi afikia rekodi ya magoli 71 ndani ya michuano ya klabu bingwa Ulaya iliyokuwa inashikiliwa na legendari Raul Gonzalez.
Messi amefikia rekodi hiyo baada ya kufanikiwa kupachika magoli mawili katika mchezo dhidi ya Ajax Amsterdam kwa kuisadia klabu ya Barcelona kupata ushidi wa magoli mawili kwa sifuri na kukata tiketi ya kutinga raundi ya 16 bora.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid na S04, Raul ilimchukua takribani michezo 142 kuweza kufikisha idadi ya magoli 71 ila imemchukua jumla ya mechi 90 tu kwa nahodha wa Argentina, Lionel Messi kufikia mafanikio hayo.
Messi na Ronaldo mwenye magoli 70 wanachuana kuweza kufikisha magoli 72 na kuweka rekodi mpya katika michuano hiyo ila Muargentina huyo ana nafasi kubwa zaidi ya kuweza kufikisha idadi hiyo pale Barcelona watakapochuana na klabu ya Apoel Nicosia mnamo tarehe 25 mwezi wa 11 mwaka 2014 kabla ya Ronaldo na kikosi cha Real hakijashuka dimbani kesho yake dhidi ya FC Basel.

Usiku wa klabu bingwa Ulaya kuendelea tena leo kwa kuvitukanisha vilabu mbalimbali vinavyosaka tiketi ya kuvuka hatua ya makundi ikiwa ni michezo ya raundi ya pili katika hatua hiyo.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza, Manchester City itashuka dimbani Majira ya saa nne na dakika arobaini na tano kuwakaribisha klabu ya CSKA MOSKVA ya nchini Urusi.
Mabingwa wa Bundesliga klabu ya Bayern Munich itakuwa wenyeji wa klabu ya AS Roma ya huko nchini Italy wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupokea kichapo cha magoli 7-1 kwenye mchezon uliopigwa uwanja wa Stadio Olimpico.
FC Barcelona watasafiri mpaka huko nchini Uholanzi kuivaa Ajax Amsterdam, wakiwa na nahodha wa Argentina Lionel Messi anayefukuzia rekodi ya Raul na mchezo huu utakuwa maalum kwa Luis Suarez aliyewahi kuichezea Ajax kabla ya kuhamia Liverpool.
Michezo mengine ya leo 5/11/2014
PSG VS APOEL
Sporting CP vs Schalke 04
Maribor vs Chelsea
Shakhtar Donestk vs BATE Borisov
Athletic Club vs Porto.

Mabingwa watetezi wa michuano ya klabu bingwa Ulaya klabu ya Real Madrid imefanikiwa kutinga katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo kwa kuilaza klabu ya Liverpool kwa goli 1-0.
Goli la Real limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Karim, Benzema aliyeunganisha krosi safi iliyojazwa na beki wa kushoto wa Brazil Marcelo.
Mechi hiyo iliyokuwa inatazamiwa kuwa ya kipekee kwa mchezaji Cristiano Ronaldo aliyekuwa anafukuzia rekodi ya ufungaji magoli 71 iliyowekwa na Raul Gonzalenz, alishindwa kutamba mbele ya beki KoloToure aliyeonekana kumbana vilivyo.
Wakati huohuo klabu ya Borussia Dortmund nayo imefanikiwa kukata tiketi ya hatua ya 16 bora baada ya kupata ushindi mnono wa magoli 4-1 dhidi ya Galatasaray.
Matokeo mengine ya michezo ya jana 5/Nov/2014
Arsenal 3-3 Anderlecht
Juventus 3-2 Olympiacos Piraeus
Malmo FF 0 vs 2 Atletico Madrid
FC Basel 4 vs 0 Ludogorets
Benfica 1 vs 0 Monaco
Zenith 1 vs 2 Bayer Leverkusen

Beki wa Azam fc Erasto Nyoni amekutwa na mkasa mkubwa baada ya kumgonga dereva wa bodaboda katika enero la tiptop Manzese lakini akaendeklea kukimbia akiyagonga baadhi ya magari hadi katika eneo la Kijitinyama jijini Dar ambako alikwama baada ya kugonga gari la grobal publisheer.
Bada ya tulio hilo Nyoni beki wa Taifa stars alitoka kwenye gari lake aina ya toyota grande mark 11 GX 110, akaanza kujitahidi kukimbia kutokana na lundo la bodaboda kuanza kumfukuza wakitaka kumchukulia sheria mkononi hali iliyomtia hofu
kwa mujibu wa watu walioshuhudias tukio hilo walisema kuwa
beki huyo aliteremka kwenye gari wakaanza kumshambulia kama mwizi Nyoni alishambuliwa na lundo la madereva wa bodaboda lakini akafanikiwa kukimbia huku wakiendelea kumpiga na hata baadhi ya watu walipojitokeza kumsaidia waliendelea kumpiga
Nyoni alipopata nafasi ya kukimbia alitokomea pasipojulikana

Michuano ya klabu bingwa ulaya kuendelea tena leo ikiwa ni mechi za raundi ya pili katika hatua ya makundi kwa msimu wa mwaka 2014/2015.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo klabu ya Real Madrid itawakaribisha majogoo wa jiji la Anfield Liverpool katika
uwanja wa Santiago Bernabeu wakiwa na rekodi ya kushinda goli 3-0 katika mchezo uliopita.
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo na Iker Casillas wanatazamiwa kuvunja rekodi mbalimbali usiku wa leo, Ronaldo anafukuzia rekodi ya magoli 71 iliyowekwa na Raul Gonzalez huku Iker atakuwa ndio mchezaji aliyecheza michezo mingi (144) kama atafinikiwa kucheza.
Klabu ya Arsenal itawakaribisha Anderlecht kutoka nchini Ubelgiji huku ratiba ya michezo iliyobakia ikiwa kama ifuatavyo:

Kamati ya maamuzi ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) imewapa muda wa siku tano mpaka siku ya jumamosi ya tarehe nane mwezi wa kumi na moja mwaka huu kutoa tamko rasmi juu ya uaandaaji wa michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2015
Morocco walipewa kibali cha kuandaa michuano hiyo lakini kutokana na hofu ya ugonjwa wa Ebola iliwaomba CAF waisogeze mbele au kuahirisha kabisa michuano hiyo iliyopangwa kuanza tarehe 17 mwezi januari mpaka Februari 8 mwaka 2015.
Wakati huohuo CAF imewaomba nchi wanachama wanaotaka kuandaa michuano hiyo endapo nchi ya Morocco itaamua kujitoa waweze kuwasilisha maombi yao siku hiyohiyo ya tarehe nane mwezi wa kumi na moja ili wafikie maamuzi tarehe kumi na moja mwezi wa kumi na moja mwaka 2015.
Nchi mbalimbali zimeshaanza kuonyesha nia ya kuandaa ikiwemo Nigeria ambayo pia ilikumbwa na ugonjwa wa Ebola huku Afrika ya Kusini kupitia Rais wa shirikisho la soka nchini humo Danny Jordan ilijitoa katika kinyang’anyiro cha kuandaa.

TENNIS
Kuelekea katika michuano ya ATP World Tours pale jijini London nchini England, makundi na ratiba ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza tarehe 9 mpaka 16 mwezi huu yapangwa rasmi hapo jana usiku.
Bingwa namba moja katika mchezo huo, Novak Djokovic amepangwa katika kundi A pamoja na wachezaji wengine watatu nafasi zao duniani katika mabano, Satnislas Wawrinka (4), Tomas Berdych (7) na Marin Cilic (9).
Katika kundi B limewakutanisha vigogo Roger Federer anayesika nafasi ya pili kwa ubora duniani, Muingereza Andy Murray huku Kei Nishikori (5) na Milos Raonic (8) wakikamilisha washiriki wa kundi hilo.
Wachezaji wawili watakaomaliza nafasi mbili za juu katika makundi hayo watatinga moja kwa moja kwenye hatua ya nusu fainali huku Djokovic na Federer wakiwa wanachuana kumaliza mwaka kama bingwa namba moja.

Mtendaji wa bodi ya TFF inayosimamia ligi kuu na ile ya daraja la kwanza, Sylas Mwakibinga ameamua kuachana na kibarua chake kwenye taasisi hiyo nyeti ya soka nchini.
Uchunguzi wa E.sports umegundua kwamba Mwakibinga ameamua kuachia ngazi katika nafasi yake kutokana na mvutano mkubwa unaoendelea kati ya rais wa TFF -Jamali Malinzi na wakali Damas ndumbaro aliyezawadiwa kifungo cha miaka 7 kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje nchi kwa madai ya kutoa siri nzito zilizojificha ndani ya shirikisho wakati akivitetea vilabu kupinga agizo la makato ya asilimia tano ya fedha ya mdhamini.
E.sport imefanya mahojiano na wajumbe wa bodi hiyo ya ligi, Charz Mguto, uthibitisho juu ya hatua ya Mwakibinga kujiengua kwenye wadhifa wake.
hata hivyo E.spot ikamtafuta silas Mwakibinga mwenyewe kutaka kujua kilichojificha nyuma ya pazia kuhusu kuondoka kwake

Winga wa klabu ya Celtic, Aleksandar Tonev amepewa adhabu ya kutokucheza mechi nne baada ya kukutwa na hatia ya kitendo cha ubaguzi wa rangi.
Raia huyo wa Bulgaria mwenye umri wa miaka 24 alifanya kitendo hicho kwa beki wa klabu ya Aberdeen, Shay Logan mwezi tisa mwaka huu mchezo ambao Celtic waliibuka na ushindi wa goli 2-1.

Uongozi wa klabu ya Celtic umesema adhabu hiyo ni kali na hawaamini kama mchezaji huyo ambaye yupo kwa mkopo akitokea klabu ya Aston Villa sio mbaguzi na hajawahi kufanya vitendo hivyo.
Hivi karibuni wachezaji kama Luis Suarez na John Terry waliadhibiwa kwa vitendo vya ubaguzi.