Category: Sports

  • BBC KUTOA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

    BBC KUTOA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

    Wachezaji watano watajwa kuweza kuwania tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika inayotolewa na Shirika la utangazaji habari nchini Uingereza (BBC).

    Wachezaji waliopata nafasi ya kuingia katika kiny’ang’anyiro hicho ni Yaya Toure (Ivory Coast, Man City), Yacine Brahimi (Algeria, Porto), Vicent Enyeama (Nigeria, Lille), Gervinho (Ivory Coast, Roma) na Pierre Emerick Aubameyang (Gabon, Borussia Dortmund).

    Tuzo hiyo inayoshikiliwa na mchezaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na klabu ya Man City, Yaya Toure inatoa nafasi kwa mashabiki wa soka kuweza kumchanga mchezaji wanayemtaka kwa kupiga kura kwa njia ya mtandao au kwa kutumia simu ya kiganjani.

    Mchakato wa kupiga kura utaendeshwa mpaka tarehe 24 mwezi Nov huku mshindi kutangazwa mnamo tarehe 1 mwezi Desemba mwaka 2014.

  • OSCAR DOS SANTOS AMWAGA WINO MIAKA 5 NDANI YA CHELSEA

    OSCAR DOS SANTOS AMWAGA WINO MIAKA 5 NDANI YA CHELSEA

    Kiungo wa kimataifa wa Brazil Oscar Dos Santos Emboaba Jr. asaini mkataba wa miaka mitano ndani ya klabu ya Chelsea utakaomfunga ndani ya Stamford Bridge mpaka mwaka 2019.

    Oscar alijiunga na Chelsea msimu wa mwaka 2012 akitokea klabu ya Internacional kwa dau lililoripotiwa kuwa ni kiasi cha paundi million 20 chini ya utawala wa kocha Di Matteo.

    Chelsea inayonolewa na kocha Jose Mourinho imekuwa katika kiwango kizuri sana msimu ikiwa inaongoza ligi kuu nchini England bila ya kupoteza mchezo wowote mpaka sasa kwa kupata alama ishirini na tisa, alama nne juu ya Southampton inayoshika nafasi ya pili.

    Wachezaji kama Diego Costa, Cesc Fabregas na Eden Hazard wamekuewa wakitajwa kuwa msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho ila Oscar na Nemanja Matic wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana ya kupora mipira kutoka kwa wapinzani.

  • DAVID MOYES ATEULIWA KUWA MENEJA WA REAL SOCIEDAD

    DAVID MOYES ATEULIWA KUWA MENEJA WA REAL SOCIEDAD

    Aliyekuwa kocha wa kikosi cha Manchester United, David Moyes ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa klabu ya Real Sociedad inayokipiga ndani ya ligi kuu nchini Hispania (LA LIGA).

    Moyes amesaini mkataba wa miezi kumi na nane akichukua nafasi ya kocha aliyefungashiwa virago Jacob Arraste ikiwa ni miezi nane tu toka alipotimuliwa ndani ya Manchester United.

    Klabu ya Real Sociedad inashika nafasi ya kumi na tano katika msimamo wa La Liga ikiwa imejikusanyia jumla ya alama tisa tu sawa na vilabu vinne vilivyo chini ya klabu hiyo na alama tatu tu juu ya klabu inayoshika mkia katika ligi hiyo.

    Moyes anatarajia kuanza kazi rasmi tarehe ishirini na mbili mwezi huu katika mchezo dhidi ya Deportivo La Coruna huku michezo minne inayofuatia ni dshidi ya Elche, Oviedo (kombe la mfalme), Villareal na Athletic Club Bilbao.

    Real-Sociedad-v-Olympique-Lyonnais-UEFA-Champions-League-Play-offs-Second-Leg

  • PAZIA LA ATP WORLD TOUR LIMEFUNGULIWA RASMI LONDON

    PAZIA LA ATP WORLD TOUR LIMEFUNGULIWA RASMI LONDON

    TENNIS

    Pazia la michuano ya ATP World Tour limefunguliwa rasmi hapo jana usiku katika viwanja vya O2 huko jijini London nchini England.

    Andy Murray anayetokea katika visiwa hivyo vya Uingereza amejikutan akipokea kichapo kikali cha seti 6-4 6-4 kutoka kwa MJapan Kei Nishikori ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki katika michuano hiyo ya kufunga mashindano ya mwaka.

    Kichapo hicho kinamuweka Murray katika wakati mgumu sana ndani ya kundi B linalojumuisha mchezaji bingwa namba mbili duniani, Roger Federer anayeshikilia rekodi ya kutwaa mataji mengi katika historia ya michuano hiyo.

    Wakati huohuo MCanada Milos Raonic amepoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Federer kwa seti 6-1 7-6 (7-0). Mechi nyengine za kundi hilo zitapigwa siku ya jumanne kwa kuwakutanisha Murray vs Raonic huku Federer vs Nishikori.

    ATPNNN

  • DONDOO ZA FORMULA 1 – LANGALANGA

    DONDOO ZA FORMULA 1 – LANGALANGA

    FORMULA 1 – LANGALANGA

    Dereva wa timu ya Mercedes Nico Rosberg apunguza tofauti ya alama katika msimamo wa mashindano ya langalanga (Formula 1) baada ya kuibuka kidedea kwenye mashinadno ya huko nchini Brazil (Brazilian Grand Prix).

    Raia huyo wa nchini Ujerumani mwenye upinzani mkubwa na dereva mwenzake Lewis Hamilton ilimchukua saa moja dakika thelathini na sekunde mbili ikiwa ni ushindi wake wa tano msimu huu.

    Hamilton anaongoza msimamo wa mashindano hayo akiwa na jumla ya alama 334 dhidi ya Rosber mwenye alama 317 atatangazwa kuwa bingwa wa mwaka huu kama atamaliza japo nafasi ya pili katika mashindano ya mbio za Abu Dhabi.

    Endapo Nico Rosberg ataibuka mshindi wa masindano yam bio hizo za Abu Dhabi mnamo tarehe 23 mwezi huu na Hamilton akamaliza nafasi ya tatu au zaidi ya hapo, Rosberg atatangazawa kuwa bingwa wa michuano ya Formula 1 mwaka 2014.

  • WACHEZAJI WA TENNIS KUKUTANA ARUSHA

    WACHEZAJI WA TENNIS KUKUTANA ARUSHA

    Wachezaji wa Tennis Nchini watakutana mjini Arusha siku ya Jumamosi tayari kwaajili yamichuano ya kupandisha viwango vyao ilikujiwekatayari kwa mashindanombalimbali ya kimataifa

    Kocha wa mchezo huo Kiango Kipingu ameiambia E.sport kuwa wachezaji hao wanaianza safari yao leo kuelekea Arusha huku chama cha Tennis taifa kikiwakimegharamia safari hiyo

     

  • WANACHAMA YANGA WAKOSOA MFUMO WA MAXIMO

    WANACHAMA YANGA WAKOSOA MFUMO WA MAXIMO

    Wanachama Yanga waibuka na kukosoa mfumo wakocha Mbrazil Maxio Maxmokuendelea kuwatumia wachezaji wa kigeni – Jaja na Countinhokatika kila mechi hatakamawachezaji haowanaonekana hawapo vizuri kimchezo

    Akizungumza na E.sport mwanachama aliyewahi kuwania nafasi ya Mwenyekiti klabu hiyo ya Jangwani John Jambele amesema mfumo huo wa kocha maximo pamoja nakuchelewa kufanyamaamuzi kubadilisha wachezaji kutokana na ugumu wamechi husika umechangia kupoteza mechi zao mbili tangu ilipoanzakutimuaVumbi

    Msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto ameipinga kauli hiyo akisema kuwa kazi ya mwalimu haipaswikuingiliwa na wanachama

  • HATMA YA WATOVU WA NIDHAMU BADO KIZUNGUMKUTI

    HATMA YA WATOVU WA NIDHAMU BADO KIZUNGUMKUTI

    Kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba imekutana jana kuzungumzia suala la Wachezaji watatu waliowasimamishwa kutokana naUtovu wa nidhamu, Lakini kikao hicho kimeshindwa kutoamajibu kuhusu hatima ya wachezaji hao

    Wachezaji hao ni pamoja na Shabani Kisiga, Haroun Chanongona, Amry Kiemba ambao wamesimamishwa mara baada ya mchezo wa kati ya Simba dhidi ya Tanzania prison uliopigwa katika dimba la Sokoine huko mkoani mbeya na timu hizo kwenda sare ya kufunganabao 1-1

    Msemaji wa Simba Hamphrey Nyasio, Amezungumza na E.sport na kuthibitisha kufanyika kwa kikao hicho cha kamati ya utendaji

    Katika hatua nyingine msemaji huyo wa Simba amekanusha taarifa ya kuwa imemtelekeza mlinda mlango wao namba mbili Husein Sharif alieumia katika mechi ya majalibio huko Afrikakusini ambapo Simba ilikwenda kuweka kambi kwaajili ya mechi ya wataniwajadi

     

  • ETHIOPIA YAJITOA CECAFA MWENYEJI KUTAFUTWA

    ETHIOPIA YAJITOA CECAFA MWENYEJI KUTAFUTWA

    CECAFA yakuna kichwa kumpata mwenyeji wa mashindano ya Challenge mwaka huu ni baada ya Ethopia kujitoa dakika ya mwisho

    Afisa habari wa CECAFA Rodgers Mulindwaalipozungumza n E.sport kutoka mjini Kampala nchini Uganda amesema baraza hilo kwa sasa lipo katika mazungumzo mazito na nchi YaSudani kuona uwezekano wakubeba jukumu hilo la uenyeji wa challenge

     

  • DONDO ZA MBIO ZA MAGARI ZA FORMULA 1

    DONDO ZA MBIO ZA MAGARI ZA FORMULA 1

    Dereva wa kimataifa kutoka nchini Brazil, Felipe Nasr ameteuliwa kuitumikia timu ya Sauber yenye maskani yake huko nchini Uswisi katika michuano ya langalanga msimu wa 2015.

    Felipe aliyekuwa ni dereva wa akiba wa timu ya Williams atajiunga na timu inayoshika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi huku wakishindwa kukusanya alama yoyote.

    Uteuzi huo unamaanisha kuwa madereva wawili wa sasa Adrian Sutil na Esteban Gutierez watakuwa huru kujiunga na timu nyengine ndani ya klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

    Felipe mwenye umri wa miaka 22 atasaidiwa na Marcus Ericsson, 24 aliyejiunga na timu hiyo akitokea Claterham iliyofilisika mwezi uliopita