Category: Sports

  • ALIEKUWA KOCHA WA STOKE CITY NA CRYSTAL PALACE YUPO MBIONI KUSAINI NA WEST BROMWHICH ALBION

    ALIEKUWA KOCHA WA STOKE CITY NA CRYSTAL PALACE YUPO MBIONI KUSAINI NA WEST BROMWHICH ALBION

    Aliyekuwa kocha wa klabu ya Stoke City na Crystal Palace yu mbioni kusaini mkataba wa kukinoa kikosi cha klabu ya West Bromwhich Albion kwa kuziba nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Alan Irvine.

    Pulis ambaye ni mshindi wa tuzo ya ya kocha bora msimu uliopita amekubali kujiunga na klabu ya West Brom na kuitosa Newcastle baada ya mazungumzo ya kina baina yake na wamiliki wa pande zote mbili.

    Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 amesema hakuwa teyari kujiunga na Newcastle kwasababu mmiliki wa klabu hiyo, Mike Ashley hayupo teyari kumuachia kocha afanye maamuzi katika masuala ya usajili wa wachezaji.

    Pulis ataungana na aliyekuwa kocha msaidizi wakati yupo Stoke City, David Kemp huku mechi yake ya kwanza inatarajiwa kuwa siku ya mwaka mpya dhidi ya wagonga nyundo wa London klabu ya West Ham United.

  • KOCHA WA WEST BROMWHICH ALBION AFUNGASHA VIRAGO

    KOCHA WA WEST BROMWHICH ALBION AFUNGASHA VIRAGO

    Klabu ya West Bromwhich Albion nimemfungashia virago kocha Alan Irvine ikiwa ni miezi saba tu toka apewe mikoba ya kukinoa kikosi hicho kinachokipiga katika uwanja wa Hawthorns.

    Irvine raia wa Scotland mwenye umri wa miaka 56 aliteuliwa kukinoa kikosi cha WBA baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Pepe Mel kutimuliwa, amekuwa akipata matokeo mabovu na kuwaacha klabu hiyo katika nafasi ya 16 ndani ya msimu wa ligi kuu nchini England.

    West Brom inataraji kusafiri kwenda jijini London kumenyana na klabu ya West Ham United itaongozwa na makocha Robby Kelly na Keith Downing waliokuwa wsasaidizi wa Irvine.

    Makocha mbalimbali wameanza kuhusishwa na kuchukua mikoba ya Irvine akiwemo Tim Sherwood aliyekuwa kocha wa Spurs pamoja na Tony Pulis aliyewahi kuvinoa vikosi vya Stoke City na Crystal Palace.

  • CRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA MCHEZAJI WA ULIMWENGU

    CRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA MCHEZAJI WA ULIMWENGU

    Nahodha wa timu ya taifa ta Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji wa ulimwengu (Globe Soccer Award) huko nchini Dubai.

    Ronaldo amepata tuzo hiyo mbele ya wachezaji mbalimbali kama Messi, Neuer ambao ndio wapinzani wake wakubwa katika tuzo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka duniani ballon d’Or inayotarajiwa kutolewa tarehe 12 januari 2015.

    RR

    Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utoaji wa tuzo hizo, Ronaldo amesema anashukuru kwa kushinda tuzo hiyo na anamatumaini makubwa itakuwa ni kichocheo cha yeye kushinda ballon d’Or kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuitwaa januari mwaka huu.

    Cristiano amekuwa na msimu mzuri kwa kufanikiwa kuvunja rekodi mbalimbali huku akiiongoza klabu ya Real Madrid kushinda mechi takribani 22 mfululizo huku akiwa anaongoza kwa ufungaji wa magoli ndani ya ligi kuu nchini Hispania.

  • MOUNRINHO: KUNA KAMPENI INAENDESHWA KUIANGUSHA CHELSEA LIGI KUU YA ENGLAND

    MOUNRINHO: KUNA KAMPENI INAENDESHWA KUIANGUSHA CHELSEA LIGI KUU YA ENGLAND

    Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema kuna kampeni inaendeshwa dhidi ya klabu yake ili isifanye vizuri ndani ya ligi kuu nchini England kwa kuwashawishi marefarii kutotoa maamuzi sahihi.

    Kocha huyo raia wan chini Ureno anayesifika kwa ubwatukaji amewashutumu makocha wenzake, watangazaji wa michezo pamoja na wachambuzi kuwa wanachangia kwa kiasi kikubwa klabu ya Chelsea kuandamwa na maamuzi ambayo siyo sahihi ndani ya uwanja.

    Maneno hayo ameyatoa baada ya kushuhudia mchezaji Cesc Fabregas kunyimwa penalty katika mchezo wa jana dhidi ya Southampton na matokeo yake alilimwa kadi ya njano kwa kile refarii wa mchezo huo Taylor kutafsiri kuwa alijiangusha ndani ya eneo hilo la hatari.

    Fabregas_3179732

    Wachezaji wa Chelsea wamekuwa wakishutumiwa kujiangusha kutafuta penalty, kocha wa West Ham alimshutumu beki wa klabu hiyo Branoslav Ivanovic huku Cahill, Diego Costa nao pia walishutumiwa.

  • MALI YATANGAZA KIKOSI CHA AWALI KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA 2015

    MALI YATANGAZA KIKOSI CHA AWALI KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA 2015

    Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Mali, Cheick Omar Kone ametangaza kikosi cha awali kinachotaraji kwenda kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwezi januari mwaka 2015 huko nchini Equatorial-Guinea.

    Kikosi hicho ambacho ni cha awali kabla ya kile cha mwisho kutangazwa mnamo tarehe tatu januari 2015 kimeshuhudia mshambuliaji wa klabu ya Metz, Modibo Maiga akirejea kundini baada ya kutoitwa kwa kipindi kirefu ndani ya timu hiyo.

    Abdou Traore na Cheick Diabate wanaokipiga katika klabu ya Bordeaux nao nwamejumuishwa huku golikipa wa klabu ya Ajaccio Oumar Sissoko akiachwa.

    Mali inayoongozwa na kocha raia wa Poland Henry Kasperczak inataraji kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Afrika ya kusini na Tunisia kujiandaa na michuano hiyo itakayoanza tarehe 17 januari 2015.

  • GIANFRANCO ZOLA ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA WA CAGLIARI

    GIANFRANCO ZOLA ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA WA CAGLIARI

    Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Italy, Gianfranco Zola ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Cagliari kwa kuchukua nafasi ya Zdenek Zeman.

    Uongozi wa Cagliari umefikia maamuzi hayo baada ya kuona matokeo mabovu chini ya kocha Zeman aliyewaacha katika nafasi ya 17 ndani ya ligi kuu nchini Italy (Serie A).

    Zola aliyewahi kuvinoa vikosi mbalimbali kama West Ham na watford anataraji kuanza kukinoa kikosi cha Cagliari mnamo siku ya jumapili ya tarehe 28 mwezi wa 12, 2014 huku mechi yake ya kwanza itakuwa tarehe 6 mwezi januari dhidi ya Palermo.

    Legendari huyo wa klabu ya Chelsea alimalizia maisha yake ya soka ndani ya Cagliari na sasa anakazi ya kuweza kuikomboa klabu hiyo iliyopata ushindi katika michezo miwili tu ndani ya michezo kumi na sita ya mwanzo isishuke daraja.

  • DONDOO ZA MCHEZO WA CRICKET

    DONDOO ZA MCHEZO WA CRICKET

    Nahodha wa timu ya taifa ya Cricket, Micahel Clark amepata matumaini mapya ya kurudi uwanjani mapema kabla ya michuano ya kombe la dunia baada ya madaktari kumfanyia upasuaji wa misuli.

    Clark aliumia katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya India huko Adelade kwa timu ya taifa ya Australia kuibuka na ushindi wa rani 48 kwac sifuri.

    Australia itaanda michuano ya kombe la dunia kwa kushirikian na taifa la New Zealand kuanzia tarehe 14 mwezi wa pili mwaka 2015.

    Micahel Clark mwenye umri wa miaka 33 amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara mwaka huu ikiwamo kuumia bega na mgongo.

  • BARCELONA MBIONI KUMUONGEZEA MKATABA NEYMAR

    BARCELONA MBIONI KUMUONGEZEA MKATABA NEYMAR

    Uongozi wa klabu ya FC Barcelona upo mbioni kumuongeza mkataba wa miaka miwili nahodha wa timu ya taifa ya Brazil na mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar utakaomalizika mwaka 2018.

    Mkataba wa sasa wa Neymar unataraji kuisha mwaka 2018 ila kiwango kizuri alichokionyesha Mbrazil huyo kimewashawishi viongozi hao kutaka kumsainisha mkataba mpya ili kumzuia asijiunge na klabu nyengine.

    Neymar amefanikiwa kuunda mahusiano mazuri na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji hatari duniani Lionel Messi pamoja na Luis Suarez.

    Neymar ameshafanikiwa kufunga magoli 14 na kutoa pasi 3 za magoli ndani ya michezo 18 msimu huu atakuwa nalipwa kiasi cha euro million 5 kiwango sawa na Mruguay Luis Suarez.

  • CHELSEA YAILAZA 2-0 STOKE CITY

    CHELSEA YAILAZA 2-0 STOKE CITY

    Klabu ya soka ya Chelsea imefanikiwa kupata ushindi wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya Stoke City na kujihakikishia nafasi ya kwanza kuelekea katika msimu wa sikukuu ya Christmas.

    Magoli ya Chelsea yamefungwa na beki na nahodha wa klabu hiyo John Terry huku kiungo wa Kihispania Cesc Fabregas akifunga goli la pili la mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Brittania.

    CH2

    CH

    Chelsea imefikisha alama 42 ikiwa ni 5 dhidi ya klabu ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili huku historia ikionyesha kuwa katika misimu ambayo Chelsea imekuwa ikiongoza mpaka Christmas basi huenda kulitwaa taji hilo.

    Kikosi hicho cha kocha Jose Mourinho kitarejea tena uwanjani mnamo tarehe 26 mwezi huu kwa kuikaribisha mahasimu wao wa jiji la London klabu ya West Ham kabla ya kusafiri kwenda kumenyana na Southampton tarehe 28 mwezi 12 mwaka 2014.

  • BARCLAYS PRIMIER LEAGUE: CHELSEA KUMENYANA NA STOKE CITY LEO

    BARCLAYS PRIMIER LEAGUE: CHELSEA KUMENYANA NA STOKE CITY LEO

    Vinara wa Ligi kuu nchini England, klabu ya Chelsea leo wanashuka tena dimbani kumenyana na klabu ya Stoke City katika uwanja wa Brittania majira ya saa tano kamili usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki.

    Chelsea inayonolewa na kocha Jose Mourinho inaongoza ligi hiyo ikiwa na alama 39 sawa na klabu ya Manchester City iliyopata ushindi mnono wiki iliyopita dhidi ya Crystal Palace.

    Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemuomba refarii wa mchezo huo wa leo, Swarbrick awe makini katika maamuzi yake kwani klabu ya Stoke City inasifika kwa kutumia nguvu sana dhidi ya wapinzani wao.

    Stoke City inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu nchini England ikiwa imeshinda michezo mitano, ikitoka sare mara nne huku wakipoteza michezo saba na kujikusanyia jumla ya alama kumi na tisa.

  • DONDOO ZA MCHEZO WA CRICKET

    DONDOO ZA MCHEZO WA CRICKET

    Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Australia Matthew Hayden ameshangazwa na maamuzi ya timu ya taifa ya England ya kumuacha nahodha wa zamani wa timu hiyo, Kevin Pietersen.

    Matthew amesema kitendo cha England kumuacha mmoja kati ya wachezaji hodari kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya nchi ya England kinaonyesha wazi hawapo teyari kwenda kushindana na timu kama India na Australia.

    England wametangaza majina ya wachezaji 15 watakaoshiriki michuano ya kombe la dunia huku ikimteua Eoin Morgan kuwa nahodha wa timu hiyo mbele ya mchezaji mkongwe Alastair Cook.

    Timu hiyo ipo katika kundi linalojumuisha timu za Australia, New Zealand, Scotland, Sri Lanka, Bangladesh, Afghanistan.