Category: Sports

  • MPINZANI WA MAYWEATHER ATANGAZA KUACHA MUZIKI

    MPINZANI WA MAYWEATHER ATANGAZA KUACHA MUZIKI

    Hii ndio kauli ya bingwa wa masumbwi duniani kutokea nchini Ufilipino Manny Pacquiao kwenye vyombo vya habari

    Pacquiao ametangaza rasmi kuachana kabisa na shughuri za kimuziki na kusema kwamba anaupenda muziki ila hadhani kama muziki unampenda

    “I love music, but I don’t think music loves me.”

    Pacquiao amesema hatotoa albam mpya tena .

    Pacquiao kwa sasa anapromote documentary lakini hadi hivi sasa amesema anajivunia mafanikio aliyoyapata kupitia muziki, aidha Pacquiao ameongeza ya kuwa albam yake ya kwanza ilifikia mauzo ya platinum huko Ufilipino hivyo inatosha kwa yeye kuacha muziki

  • TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO

    TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO

    TETESI ZA MAGAZETI:

    Klabu ya Manchester United ipotayari kuvunja rekodi ya usajili kwa kuweka mezani kitita cha paundi milioni 112 ili kumsajili beki wa kati wa klabu ya PSG MARQUINHOS.

    (Daily Mirror)

    Klabu ya Everton ipotayari kumpiga bei mshambuliaji wao KEVIN MIRALLAS katika dirisha hili la usajili.

    (Metro) 

    Klabu ya Chealsea ipotayari kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Fiorentina JUAN CUADRADO endapo watafanikiwa kuwauza wakina MOHAMED SALAH  na ANDRE SCHURRLE.

    (Daily Mirror) 

    Kiungo wa klabu ya Manchester City JAMES MILNER amesema kuwa anaweza kuihama timu hiyo wakati wowote kuanzia sasa na kutimkia katika ligi za Italy au Hispania.

    (Guardian)

    Klabu ya arsenal ipotayari kumsajiri beki wa kati wa klabu ya Villarreal GABRIEL PAULISTA katika kipindi hiki cha usajili.

    (Telegraph)

    Klabu ya Cristal Palace ipotayari kumsajili kiungo wa klabu ya Sevilla STEPHANE MBIA.

    (Daily Mail)

  • CRISTIANO RONALDO AMWAGANA NA SHAYK

    CRISTIANO RONALDO AMWAGANA NA SHAYK

    Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo na mwanamitindo wa Urusi Irina Shayk wameripotiwa kuachana baada ya miaka mitano ya mahusiano yao.

    Tetesi hizo zilianza kusambaa mara baada ya Shyk kukosa kuhudhuria kwenye sherehe za kutoa tuzo za mchezaji bora duniani wiki iliyopita na utata ulikuja zaidi pale muwakilishi wa mwanamitindo Shayk kuzungumza na waandishi wa habari huko marekani na kuweka wazi kuwa wawili hao hawapo pamoja tena

    Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 29 alijizolea umaarufu zaidi duniani baada ya kucheza kwenye filamu yake ya kwanza ya ‘Hercules’ huko Hollywood mwaka jana.

  • KATANGA ATEULIWA KUWA AFISA HABARI WA DRFA

    KATANGA ATEULIWA KUWA AFISA HABARI WA DRFA

    Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA jana kilimtangaza Mwandishi na mtangazaji wa Habari za michezo kutoka kwenye kituo hiki cha

    EFM kwenye dawati la michezo la E sport Omary Katanga kuwa msemaji Mpya wa chama hicho.

    Katanga anachukuwa nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mohamed Mharizo ambae amekubaliana na uongozi kuachia nafasi hiyo.

    Katanga maarufu kama mlinda mlango namba moja ulimwenguni anawika katika medali ya utangazaji wa habari za kimichezo katika kipindi cha Esport,kinachoruka kila siku sa moja hadi saa mbili usiku, ameahidi kutopepesa macho wala kung’ata maneno katika majukumu yake.

    “Nimepokea uteuzi huu kwa moyo mkunjufu kabisa”alisema Katanga “Nafasi hii ambayo nimepewa ni nafasi ngumu lakini itakuwa rahisi kama ushirikiano utatoka kwenu(waandishi wa habari,)”

    “Lakini changamoto kubwa ambayo naiona DRFA ni kwamba chama hiki  kinafanya mambo mengi makubwa sana lakini mambo hayo hayasikiki kwa upana wake, kwa hiyo kwa nafasi hii ambayo nimepewa,nitahakikisha nayafikisha kwa wananchi” alifafanua Katanga.

  • TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO

    TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO

     

    Beki wa kati wa klabu ya Borussia Dortimund MATS HUMMEL amesema kuwa hana mpango wa kuihama klabu hiyo kwa sasa.

    (Daily Express) 

    Klabu ya Manchester United imeandaa paundi milioni 15 ili kumsajili beki wa klabu ya Barcelona GERARD PIQUE

    (Telegraph)

    Klabu ya Wolfsburg ipotayari kutoa kitita cha paundi milioni 23 ili kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Chealsea ANDRE SCHURRLE lakini klabu hiyo imekataa dau hilo inahitaji paundi milioni 30.

    (Daily Star) 

     

    Kiungo wa klabu ya Arsenal FRANCIS COQUELIN yupotayari kusani mkataba mpya katika klabu hiyo marabaada ya kuonekana kuwa na kiwango toka aliporudi kutoka katika klabu ya chalton alipokua anakipiga kwa mkopo.

     

    (Independent)

    Mshambuliaji wa klabu ya Palermo  PAULO DYABALA amesema kuwa hana mpango wa kuihama timu hiyo kwa sasa.

    (Daily Mail)

    Klabu ya Bayer Leverkusen ipotayari kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Liverpool ROBERTO SOLDADO.

    (Sky Sports) 

     

    Kiungo wa timu ya taifa Norway MARTIN ODEGARD amesema kuwa siku yoyote anaweza kujiunga na klabu ya Real Madrid.

    (Evening Standard) 

  • AFCON: MAKALA MAALUM YA UCHAMBUZI WA SOKA TAIFA LA AFRIKA KUSINI

    AFCON: MAKALA MAALUM YA UCHAMBUZI WA SOKA TAIFA LA AFRIKA KUSINI

    Ikiwa michuano ya Afcon tayari imeanza kwenye hatua za makundi huko EQUTORIAL GUINEA   macho yetu leo hii yanalitazama taifa la Afrika kusini, Afrika kusini ni nchi inayopatikana kusini mwa bara la Afrika ikiwa karibu na bahari ya Atlantic na bahari ya Hindi,nchi hiyo imepakana na Zimbabwe,Botswana,Namibia,Lesotho na Swaziland.Taifa hilo limepata uhuru kutoka kwa wadachi mwaka 1994

    Afrika kusini ni nchi ya pili inayoongoza kiuchumi barani Afrika na inashika nafasi ya 34 kiuchumi duniani, Taifa la Afrika Kusini linamchanganyiko wa watu wa aina mbalimbali duniani na Taifa hilo linatumia jumla ya lugha 11 ambazo zote ni rasmi.Maendeleo ya Taifa hilo yanakuja kutokana na kuendelea katika teknolojia,kiviwanda,miundombinu na uongozi bora.

    Afrika kusini ina makabila zaidi ya 10 na kabila kubwa nchini humo ni wazulu, taifa hilo lina raia milioni 54 na 2000.

    Katika soka Timu ya taifa ya Afrika Kusini maarufu Bafana Bafana imeshiriki mara 8 katika michuano hiyo ya AFCON ikichukua kombe hilo mara moja mwaka 1996 walipokua wenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

    Taifa hilo linaenda katika michuano hiyo likiwa na pigo la kumpoteza nahodha wao SENZO MEYIWA aliyefariki 26 October 2014 baada ya kupigwa risasi mbele ya mpenzi wake KELLY KHUMALO

    Katika michuano ya AFCON mwaka huu Bafana Bafana ipo katika kundi C pamoja na Ghana,Senegal na Algeria,mchezo wa kwanza Bafana Bafana ulichezwa jana wakati timu hiyo iliposhuka dimbani kuminyana na Algeria siku ya tarehe 19/mwezi huu saa 3 usiku katika uwanja wa estadio de mongomo uliopo mjini mongomo na matokeo ya mchezo huo Algeria iliibuka na ushindi wa mabao 3-1

     

     

  • AFCON: MOUSSA SOW AIINUA SENEGAL

    AFCON: MOUSSA SOW AIINUA SENEGAL

    Mshambuliaji wa Senegal Moussa Sow jana aliinua timu yake baada ya kufunga bao la muda wa lala salama hivyo kuifanya Senegal kuibuka na ushindi dhidi ya Black stars ya Ghana

     

    Bao hilo lilipatikana mnamo dakika ya 90 na kuipa Senegal alama zote tatu

    Mchezaji wa Ghana Andrew Ayew alifunga mkwaju wa Penalti baada ya kiungo wa kati wa Everton Christian Atsu kuangushwa katika eneo la hatari.

    Lakini Senegal ilijitahidi na kupiga chuma cha goli la Ghana kupitia mchezaji Kara Mbodj,kabla ya mshambuliaji wa Stoke Mame Biram Diouf kufunga bao la kusawazisha huku Mousa Sow akifunga bao la Ushindi.

    SOU SAOU2

     

     

  • MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA BARA

    MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA BARA

    Polisi Moro imeibana Coastal Union kwao Mkwakwani mjini Tanga.

    Wageni hao wameikomalia Coastal na kuilazimisha sare ya bila kufungana.

    Polisi Moro ilipoteza nafasi mbili za kufunga katika kipindi cha kwanza. Lakini Coastal nayo ilishindwa kufunga katika kipindi cha pili baada ya kupata nafasi zaidi ya mbili.

    Hata hivyo, Polisi ilionyesha soka safi la pasi za uhakika na kumiliki mpira muda mwingi licha ya kuwa ugenin

    MECHI YA COASTAL UNION DHIDI YA YANGA YAAHIRISHWA

    Mechi kati ya Coastal Union dhidi Yanga kwenye Uwanja Mkwakwani imeahirishwa.

    Awali mechi hiyo ilikuwa ichezwe Jumatano, lakini sasa imeahirishwa. Hata hivyo bado haijaelezwa mechi hiyo itachezwa lini.Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amethibitisha hilo.

    “Kweli nimepewa taarifa hizo baada ya timu yetu kuwa na wachezaji kwenye kikosi cha Taifa Stars Maboresho, hivyo mechi imeahirishwa,” alisema Sanga.

    Kutokana na hali hiyo, Yanga inaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi nyingi dhidi ya timu ngumu ya Polisi Moro, Jumamosi.

    MTIBWA YAREJEA KILELENI

    Kikosi cha Mtibwa Sugar kimerejea kileleni kikiwa na pointi 17 ikiwa ni baada ya sare ya leo.

    Mtibwa imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu JKT katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

    Sare hiyo inaifanya iringane pointi 17 sawa na Azam FC na Ruvu JKT.

    Vijana hao wa Mecky Maxime wanakaa kileleni kutokana na kuwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

  • AFCON: BAADA YA MBABE KUKOSEKANA KUNDI B LEO TIMU ZA KUNDI C ZITASHUKA DIMBANI

    AFCON: BAADA YA MBABE KUKOSEKANA KUNDI B LEO TIMU ZA KUNDI C ZITASHUKA DIMBANI

    Mataifa yanayounda kundi B ambayo ni Drc, Tunisia, Cape verde na Zambia katika michuano ya kombe la mtaifa Afrika zimejikuta zikikosa mbabe baada timu zote kuibuka na sare ya kufungana 1-1

     Mchezo wa kwanza wa kundi hilo ulipigwa kwakuikutanisha Zambia na Congo ambapo Zambia ilitangulia kuziona nyavu za Drc kupitia mnamo dakika ya pili bao lililofungwa na mchezaji wake Given Singuluma na kudumu hadi mapumziko

    Bao hilo lilisawazishwa na mchezaji wa Drc Yannick Bolasie kwenye dakika ya 66 hadi mwisho wa mchezo ambapo timu zote ziliibuka na pointi moja

     

    Cape verde ilishuka dimbani na Tunisia katika mchezo wa pili wa kundi B ambapo Tunisia ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 70 lililofungwa na Ali Moncer ambapo dakika 7 baadae Cape verde ilisawazisha bao hilo kupitia mchezaji wake Almeida Ramos, mchezo huo pia ulimalizika kwa sare ya kufungana1-1

    Leo ni mechi za kundi C ambapo Ghana itaonyeshana kazi na Senegal, zikifuatiwa na mchezo kati ya Algeria na Afrika Kusini.

    Kundi A linaongozwa na timu ya Gabon ambayo iliirarua Burkina Faso 2-0 katika mchezo wa Jumamosi, huku wenyeji Equatorial Guinea wakitoka sare ya 1-1 na Congo.

  • MAKALA MAALUM YA UCHAMBUZI WA SOKA TAIFA LA DRC

    MAKALA MAALUM YA UCHAMBUZI WA SOKA TAIFA LA DRC

    Katika harakati za maandalizi ya vikosi vya timu za mataifa 16 kutoka katika bara la afrika kuelekea kunako michuano mikubwa yakusaka taifa bingwa katika mchezo wa soka inayo taraji kuanza mnamo tarehe 17/01/2015.

    Leo hii macho na masikio ya mashabiki walio wengi yanataka kusikia ama kuona ni taifa gani litaibuka kidedea katika michuano hiyo? Tutazame ubora na mafanikio ya timu mojamoja ambapo kwa sasa machoyetu yanaitazama timu ya taifa ya CONGO DRC ikiwa katika kundi “B” likiongozwa na Zambia,Tunisia na Cape Verde Island.

    Kikosi cha timu ya taifa CONGO DRC almaarufu(the leopards) kimetangaza kikosi cha wachezaji 24 pamoja kiongozi wa wachezaji hao YOUSSOF MULUMBU anaekipiga kunako klabu ya West Brom Wich Albion inayo shiriki ligi kuu nchini uingereza.

    Wachezaji tegemezi wa CONGO DRC ni mlinda mlango ROBERT KIDIABAwa Tp mazembe ,kiungo MIALA NKULUKUTU wa Tp mazembe YOUSSOF MULUMBU wa West Brom Wich, CEDRIC MAKIADI Weder Bremen,washambuliaji ni TRESOR MPUTU mazembe na LELO MBELE wa Petro Atletico

    Kocha wa timu hiyo ni FLORENT IKWANGE IBENGE ambaye ni mzawa wanchi hiyo, IBENGE amesha wahi kuvinoa vilabu mbali mbali ikiwemo klabu ya SHANGHAI SHENHUA LIANSHENG inayo shiriki ligi kuu ya nchini china.

    IBENGE mara ya kwanza kukiongoza kikosi cha CONGO DRC ilikua mwaka 2008-2009 katika harakati za kuwania kufuzu katika michuano ya kombe la mataifa Afrika na hatimaye kushindwa.

    CONGO DRC imewahi kushiriki michuano hiyo mikubwa barani afrika mara 16 toka ilipo anzishwa mwaka 1957na imefika hatua ya robo fainal mara2,hatua ya nusu fainali mara 6 pamoja na kutwaa ubingwa mara 2 ikiwa ni mwaka 1968 na mwaka 1974.

    Mchezo wa kwanza wa timu hiyo utapigwa saa moja usiku tarehe 18/01/2015 dhidi ya Zambia mchezo utakaochezwa katika uwanja wa ESTSDIO DE BATA wenye uwezo wa kubeba mashabiki 357,00 uliopo mjini BATA huko EQUTORIA GUINE.

    # Pos. Player Date of birth (age) Caps Goals Club
    1 GK Robert Kidiaba 1 February 1976 (age 38) 41 0  Mazembe
    16 GK Parfait Mandanda 10 October 1989 (age 25) 7 0  Charleroi
    23 GK Hervé Lomboto 27 October 1989 (age 25) 2 0  Vita Club
    5 DF Miala Nkulukutu 6 September 1982 (age 32) 26 0  Mazembe
    3 DF Kilitcho Kasusula 5 August 1986 (age 28) 25 0  Mazembe
    21 DF Cédric Mongongu 22 June 1989 (age 25) 22 0  Évian
    18 DF Patou Ebunga-Simbi 6 August 1983 (age 31) 13 2  Vita Club
    22 DF Chancel Mbemba Mangulu 8 August 1994 (age 20) 4 0  Anderlecht
    2 DF Bobo Ungenda 19 November 1989 (age 25) 4 0  Motema Pembe
    12 DF Manitu Matondo 3 September 1992 (age 22) 0 0  Motema Pembe
    10 MF Zola Matumona 26 November 1981 (age 33) 45 8  Mons
    14 MF Youssouf Mulumbu 25 January 1987 (age 27) 21 1  West Bromwich Albion
    6 MF Cédric Makiadi 23 February 1984 (age 30) 19 2  Werder Bremen
    13 MF Distel Zola 5 February 1989 (age 25) 7 0  Le Havre
    19 MF Gabriel Zakuani 31 March 1986 (age 28) 5 0  Peterborough
    20 MF Hervé Ndonga 2 May 1992 (age 22) 2 0  Mazembe
    15 MF Mukoko Mayayi 18 March 1988 (age 26) 1 0  Motema Pembe
    4 MF Tychique Ntela 12 December 1987 (age 27) 1 0  AC Léopards
    8 FW Trésor Mputu 10 December 1985 (age 29) 43 14  Mazembe
    17 FW Lelo Mbele 10 August 1987 (age 27) 13 1  Petro Atlético
    7 FW Eric Bokanga 9 October 1989 (age 25) 8 1  Mazembe
    11 FW Mbidi Mavuanga 1 June 1994 (age 20) 1 0  Motema Pembe
    9 FW Jacob Little 6 May 1995 (age 19) 0 0  SPCCFC
  • AMAVUBI KUINGIA MWANZA JAN 21TAYARI KUKIPIGA NA STARS

    AMAVUBI KUINGIA MWANZA JAN 21TAYARI KUKIPIGA NA STARS

    Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) inatarajiwa kuwasili katika jiji la Mwanza, Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars ambapo nyasi zitawaka moto kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

    Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura, Amavubi yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itawasili kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya JB Belmont.

    Baada ya kocha Mdachi, Mart Nooij kutaja kikosi, Stars inaingia kambini keshokutwa (Januari 18 mwaka huu), na siku inayofuata itakwenda Mwanza tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayofanyika Januari 22 mwaka huu.

    Kikosi hicho cha Kocha Mart Nooij ambacho ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo za michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN) kinaundwa na wachezaji 26.