Category: Sports

  • DAVID GINOLA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS FIFA

    DAVID GINOLA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS FIFA

    Mchezaji wa zamani wa Ufaransa David Ginola amesema kuwa atasimama dhidi ya Sepp Blatter kuwania Urais wa shirikisho la kandanda duniani,Fifa.

    Lakini richa ya kuwa imetangazwa hivyo hakuna uhakika kama Ginola ataendelea na nia yake.

    Hali hii inakuja kwakuzingatia vigezo ambapo mgombea anahitajika kuungwa mkono na vyama vitano vya soka na kigezo kingine anapaswa kuwa amejihusisha na soka kwa miaka miwili kati ya mitano iliyopita

    Mchezaji huyo mwenye miaka 47 , aliichezea Ufaransa, pia club ya nchi hiyo Paris St Germain kabla ya kujiunga na New Castle United kwa kitita cha Pauni milioni 2.5 mwaka 1995.

    Zoezi la Uteuzi wa nafasi ya urais wa fifa litafungwa tarehe 29 mwezi huu.Blatter amekuwa Rais wa Fifa tangu mwaka 1998 anawania muhula wa tano sasa.

  • MAKALA YA UCHAMBUZI KUELEKEKEA AFCON 2015 TAIFA LA EQUTORIAL GUINEA

    MAKALA YA UCHAMBUZI KUELEKEKEA AFCON 2015 TAIFA LA EQUTORIAL GUINEA

    Miezi michache iliyopita Shirikisho la soka barani afrika CAF linalo ongozwa na raisi wake Issa Hayatou lilikuwa katika wakati mgumu kutokana na taarifa iliyotolewa na walio kuwa waandaaji wa michuano hiyo mwaka huu MOROCO kujivua uwenyeji muda mchache kuelekea kuanza kwa michuano hiyo kwa kuogopa ugonjwa wa Ebola.

    Shirikisho hilo kwa wakati tofauti likachagua mataifa ya GHANA,SOUTHAFRIKA na NIGERIA kuandaa michuano hiyo nayo yakatolea njee ombi hilo na kuibuka hali ya sintofahamu.

    Mashabiki wengi walitahamaki kuona Raisi wa EQUTORIAL GUINEA Teodoro Obiang Nguema Mbasogo kutangaza yakua yupo tayari kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwakahuu bila ya kuogopa ugonjwa huo na CAF kupitisha ombi hilo.

    EQUTORIAL GUINEA wakiwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa barani afrika kwa mara ya pili huku wakionekana kufanya maandalizi ya zimamoto kwa kuwa nyuma ya muda.

    EQUTORIAL ipo katika kundi A ikiwa pamoja na BUKINAFASO,GABON na CONGO,Kikosi hicho kwa sasa kinanolewa na kocha ESTEBAN BECKER raia wa argentina ambaye pia anakinoa kikosi cha timu ya taifa hilo cha wanawake.

    Wachezaji tegemezi wa timu hio ni capten Emilio Nsue anae kipiga katika klabu ya Middlesbrough ya nchini uingereza Aitor Embela,wa Malaga ya Hispania RAUL FABIANA wa olyimpic xativa ya Hispania.

    Taifa hilo liliomba kuandaa michuano hiyo mwaka 2012 wakishirikiana na GABON huku EQUTORIAL ikiwa na viwanja viwili nakufanikiwa kujenga vingine viwili,viwanja hivyo ni ESTADIO DE BATA na kile cha ESTADIO DE MALABO.EQUTORIAL GUINEA imewahi kushiriki michuano hiyo mara 1 ikiwa wenyeji mwaka 2012 na ikaishia hatua ya robo fainal.

    Ushindi mkubwa walio wahi kupata katika hitoria ya soka ni ule wa goli 3-0 dhidi ya Mauritania wakati wakiwania kufudhu katika michuano ya mwaka huu na hatimaye kushindwa,mchezo huo ulichezwa mwaka jana katika uwanja wa ESTADIO DE MALABO uliopo mjini malabo.

    Mchezo wa kwanza wa timu hiyo utapigwa saa 12 jioni tarehe 17/01/2015 dhidi ya Congo ukiwa ni wa ufunguzi wa michuano hiyo mchezo utakaochezwa katika uwanja wa ESTSDIO DE BATA wenye uwezo wa kubeba mashabiki 357,00 uliopo mjini BATA huko EQUTORIA GUINE.

     

     

     

  • PAMBANO LA FLOYD MAYWEATHER V MANNY PACQUIAO LINAKARIBIA

    PAMBANO LA FLOYD MAYWEATHER V MANNY PACQUIAO LINAKARIBIA

    Lile pambano la uzito wa juu lililokuwa likisubiliwa kwa hamu kati ya bondia anaesifika kwa kutopigika raia wa Marekani Floyd Mayweather na bondia mfilipino Pacquiao lipo kwenye hatua za mwisho za maandalizi.

    Pacquiao ambae anashikilia mkanda wa dunia wa WBO wakati Mayweather anashikilia mkanda wa WBC na WBA

    Pambano hili linasubiriwa kwa hamu saana maana hawa mabondia wawili wanatajwa kuwa mabondia bora katika kipindi hiki ila hawajawahi kukutana kwenye ulingo

     

  • GENOVEVA ANONMA: NILILAZIMIKA KUVUA NGUO KUTHIBITISHA KUWA MIMI NI MWANAMKE

    GENOVEVA ANONMA: NILILAZIMIKA KUVUA NGUO KUTHIBITISHA KUWA MIMI NI MWANAMKE

     

    Richa ya kutukanwa na kudharaulika zaidi kupitia nyakati ngumu mpaka kwenye maisha ya Familia yake mchezaji huyu hakukatishwa tamaaa katika kuifikia ndoto yake.

    Nyota yake ilianza kung’aa pale alipoitumikia Equatorial Guinea mnamo mwaka 2008 katika michuano ya kombe la mabingwa Afrika wanawake

    Alipokuwa Mfungaji wa bao la ushindi katika ardhi ya nyumbani na kuifanya timu yake kua ya kwanza kwa kuipiku Nigeria

    Hapa ndipo changamoto zilizidi kwa Anonma kutokana na uwezo wake mkubwa kiuchezaji pamoja nguvu hii ilipelekea timu pinzani zianze kumtilia mashaka ya kuwa yeye ni mwanaume

    Ndipo shirikisho la soka barani Afrika lilichagua njia ya kumkagua

    Anonma amenukuliwa akisema

    Waliniambia nivue nguo zote mbele ya maofisa wa CAF kiukweli nilichukizwa saana na nililia saana kutokana na udhalilishaji

  • MENEJA WA ENGLAND AMEAHIRISHA KIKAO BAADA YA WACHEZAJI KUBANWA NA RATIBA

    MENEJA WA ENGLAND AMEAHIRISHA KIKAO BAADA YA WACHEZAJI KUBANWA NA RATIBA

    Meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amejikuta akilazimika kufuta ratiba ya kukutana na wachezaji wake na kupata chakula cha usiku pamoja kufuatia ratiba kuwabana wachezaji hao.

    Roy Hodgson alikuwa na lengo la kukutana na wachezaji hao mwishoni mwa mwezi wa kwanza ili kuweza kujadili pamoja ikiwemo ushindi dhidi ya Scotland.

    Shirikisho la mpira wa miguu nchini humo limeeleza kuwa timu hiyo pia ilikuwa ipo kwenye utayari wa kikao hicho ila kufuatia kile kilichotokea wamejikuta wakiahirisha kukutana na hakuna upande uliopanga siku ya kukutana tena

  • SIMBA KINARA KOMBE LA MAPINDUZI

    SIMBA KINARA KOMBE LA MAPINDUZI

    Fainali za kombe la mapinduzi zimemalizika jana katika uwanaja wa Amani mjini Unguja huko zanzabar kwa kuwakutanisha vinara wa ligi kuu ya bara mtibwa sugar na wekundu wa msimbazi Simba

    Ambapo imeshuhudiwa katika fainali hiyo Simba wakilibeba kombe kwa kuifunga mtibwa kwa mikwaju 4 – 3 baada ya kwenda suluhu kwa sare tasa katika dakika 90 za mchezo

    Ushndi huo wa simba ni mwanzo mzuri kwa kocha wao mpya kabisa Mserbia Goran kopunorvic ambae amejiunga na club hiyo hivi karibuni kurithi mikoba ya kocha mzambia patrick phill alietimuliwa kwa staili ya aina yake

  • RADAMEL FALCAO HUENDA HATOICHEZEA MANCHESTER UNITED MSIMU UJAO

    RADAMEL FALCAO HUENDA HATOICHEZEA MANCHESTER UNITED MSIMU UJAO

     

    Kiungo mshambuliaji kutoka Colombia Radamel Falcao anaepokea kiasi cha paundi 265,000 kwa wiki kuna uwezekano wa kutochezea tena katika klabu ya Man Utd

    Hii imekuja mara baada ya wakala wa mchezaji huyo kusema Falcao ataichezea moja kati ya klabu kubwa duniani katika msimu ujao

    Hayo yamesemwa na Jorge Mendes. Ambae ndie wakala wa

  • NOVAK DJOKOVIC ATUPWA NJE KWENYE MICHUANO YA WAZI YA QATAR

    NOVAK DJOKOVIC ATUPWA NJE KWENYE MICHUANO YA WAZI YA QATAR

    Bingwa namba moja katika mchezo wa Tennis, Novak Djokovic ametupwa nje katika michuano ya wazi ya Qatar baada ya kupokea kichapo ca seti 6-7 (2-7) 7-6 (8-6) kutoka kwa Ivo Karlovic.

    Djokovic ambaye alijitoa katika michuano iliyopita alionekana anashindwa kuendana sawa na kasi ya mkongwe huyo kutoka katika taifa la Croatia mwenye umri wa miaka 35.

    Kwa matokeo hayo sasa Ivo atacheza na raia wa Hispania, David Ferrer aliyefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwa kumtoa Dustin Brown kwa seti 6-2 6-2.

    Katika mchezo mwengine wa nusu fainali utawakutanisha Tomas Berdych dhidi yaAndreas Seppi.

  • YAYA TOURE ANYAKUA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA KWA MARA YA NNE MFULULIZO

    YAYA TOURE ANYAKUA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA KWA MARA YA NNE MFULULIZO

    Mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester City, Yaya Toure afanikiwa kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa bara la Afrika kwa mara ya nne mfululizo.

    Tuzo hiyo inayotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF), imeshuhudia Yaya Toure akiwapiku wachezaji wawili, Pierre Emerick Aubameyang (Gabon) na golikipa wa timu ya taifa ya Nigeria, Vicent Enyeama.

    Yaya alipata kura 175 dhidi ya mshambuliaji wa klabu ya Borrusia Dortmund, Aubemayang aliyejinyakulia kura 12o huku Enyeama akiangukia nafasi ya tatu kwa kupata jumla ya kura 105.

    Katika hatua nyengine tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kutoka katika ligi za ndani imekwenda kwaFirmin Mubele Ndombe wa AS Vita huku ile ya mchezaji bora wa kike akinyakuliwa na Asisat Oshoala anayekigika katika klabu ya River Angels.

  • AFRIKA MAGHARIBI WAAZIMIA KUMALIZA EBOLA

    AFRIKA MAGHARIBI WAAZIMIA KUMALIZA EBOLA

    WAKATI UGONJWA wa maradhi ya Ebola ukiendelea kuwa tishio katika baadhi ya nchi Afrika Magharibi, Wataalam wa Afya nao wameendelea kuweka jitihada zaidi kuhakikisha kuwa wanaumaliza ugonjwa huo.

    Katika jitihada zao hivi sasa wamebuni mpango wa mawasiliano ya simu ya mkononi wenye mpango maalum inayotoa taarifa kutoka maeneo yaliyokumbwa na Ebola.

  • AC MILAN YATWAA UBINGWA DUBAI CHALLENGE BAADA YA KUILAZA 4-2 REAL MADRID

    AC MILAN YATWAA UBINGWA DUBAI CHALLENGE BAADA YA KUILAZA 4-2 REAL MADRID

    Klabu ya soka ya AC Milan imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Dubai Challenge kwa kuitandika mabingwa wa dunia kwa upande wa klabu na barani Ulaya, Real Madrid magoli 4-2.

    Magoli ya AC Milan yalifungwa na wachezaji Stephen El Shaaraway aliyefunga magoli mawili, Jeremy Menez na Giampaolo Pazzini huku kwa upande wa Real Madrid yakifungwa na mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema.

    MILAN2 MILAN3

    Milan inayonolewa na kocha Phillipo Inzaghi aliyewahi kucheza chini ya kocha wa sasa wa Real Madrid, Carlo Ancelloti kipindi wapo AC Milan ilionyesha kandanda safi n akuendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika michezo mitatu iliyopita ambapo walikutana na klabu za Napoli na Juventus.

    Kipigo hiki hakijaathiri rekodi ya klabu ya Real Madrid ya kushinda michezo 22 mfululizo kwasababu hii ilikiuwa ni mechi ya kirafiki na rekodi hiyo inasimama katika mechi za ushindani tu kama La Liga, Klabu bingwa Ulaya, Kombe la mfalme na mengineyo.