Category: Sports

  • ERIC ABIDAL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

    ERIC ABIDAL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

    Beki wa Kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Olympiacos, Eric Abidal ametangaza kustaafu kucheza soka ikiwa ni takribani miaka kumi na nne toka aanze kucheza soka la kulipwa.

    Abidal alijiunga na klabu ya Olympiacos msimu huu na kusaini mkataba wa miaka miwili uliokuwa uishe msimu wa 205/2016 lakini ameamua kuuvunja kwasababu za kiafya.

    Beki huyo wa kushoto amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa toka mwaka 2011 na kumfanya akose michezo mingi akiwa na klabu ya FC Barcelona walioamua kumpa heshima ya kubeba taji la klabu bingwa Ulaya baada ya kuifunga klabu ya Manchester United kwa magoli 3-1.

    Abidal sasa atajiunga na klabu ya FC Barcelona kama mkufunzi wa vijana wa La Masia, moja kati ya vituo vya soka vinavyosifika kwa kutoa vipaji mbalimbali kama Messi, Iniesta, Xavi, Fabregas na Puyol.

    Fuatilia kipindi cha E sport kila siku kuanzia saa moja jioni kwa habari zaidi

  • FA YAMUADHIBU BALLOTELI KUFUATIA VITENDO VYA UBAGUZI WA RANGI

    FA YAMUADHIBU BALLOTELI KUFUATIA VITENDO VYA UBAGUZI WA RANGI

    Chama cha soka cha nchini England (FA) kimemuadhibu mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mario Balloteli kwa kumfungia kutocheza mchezo mmoja wa ligi kuu nchini England na kumtaka alipe fidia ya kiasi cha paundi ishirini na tano elfu baada ya mchezaji huyo kukutwa na hatia ya vitendo vya ubaguzi.

    Hatua hiyo imefikiwa na chama hicho baada ya Muitaliano huyo kutuma ujumbe ulionyesha vitendo vya kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa twitter kwa kuandika “ruka juu kama mtu mweusi ila tafuta fedha kama jew (watu wenye asili ya Israel).” Balotelli

    Pamoja na adhabu hiyo mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Italia ametakiwa kuweza kuhudhuria mafunzo maalum uya elimu dhidi ya vita ya kupinga ubaguzi wa rangi katika kituo atakachopangiwa.

    Balotelli aliyejiunga na majogoo hao wa jiji akitokea klabu ya AC Milan kwa daua la paundi million 16 atakosa mchezo wa jumapili dhidi ya Arsenal huku klabu ya Liverpool ikiwa inashika nafasi ya kumi na moja katika msimamo wa ligi kuu nchini England.

  • AZAM YASHINDWA KUTAMBA KWA URA

    AZAM YASHINDWA KUTAMBA KWA URA

    Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC jana usiku walipokea kichapo cha pili mfululizo katika ziara yao ya huko nchini Uganda. Wanalambalamba hao imechapwa goli 1-0 dhidi ya URA katika mchezo uliochezwa jijini Kampal, Uganda.

    Kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Mganda, George “Best” Nsimbe imeweka kambi Uganda kujiandaa na Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyosimama kwa mwezi mmoja, ambayo itarejea wiki ijayo.

    Katika dirisha dogo la usajili Azam FC imewasajili beki Serge Wawa Pascal raia wa Ivory Coast, Brian Majwega na Amri Kiemba ili kuimarisha kikosi hicho kinachoshika nafasi ya pili nyuma ya vinara Mtibwa Sugar.

  • RAHEEM STERLING AIPELEKA LIVERPOOL NUSU FAINALI CAPITAL ONE CUP

    RAHEEM STERLING AIPELEKA LIVERPOOL NUSU FAINALI CAPITAL ONE CUP

    Kiungo wa kimataifa wa England Raheem Sterling aipeleka klabu ya Liverpool katika hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi (Capital One Cup) baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo dhidi ya klabu ya Bournemouth.

    Liverpool iliingia katika mchezo huo wa robo fainali ikiwa na jeraha la kuchapwa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya mahasimu wao Manchester Unired, ilipata goli la kwanza mnamo dakika ya 20 kupitia kwa Sterling kabla ya Lazar Markovic kuongeza goli la pili mnamo dakika ya 27. Sterling alifunga goli la tatu mnamo dakika ya 51 huku mshambuliaji Gosling akiwafungia Bournemouth goli la kufutia machozi mnamo dakika ya 57.

    rahi

    Liverpool inayonolewa na kocha Brendan Rodgers inataraji kucheza na klabu ya Arsenal mwishoni mwa wiki hii huku mchezo wa nusu fainali dhidi ya Chelsea itachezwa tarehe 19 Jan 2015.

    rah3

    Wakati huohuo klabu ya Spurs imeibuka na ushindi wa magoli manne kwa sifuri dhidi ya Newcastle United na kutinga hatua ya nusu fainali ambapo watamenyana na Sheffield United waliitoa Southampton.

  • FORMULA 1 – LANGALANGA LEWIS AHAIDI MAKUBWA BAADA YA USHINDI

    FORMULA 1 – LANGALANGA LEWIS AHAIDI MAKUBWA BAADA YA USHINDI

     

    Dereva wa magari ya Mercedes, Lewis Hamilton ameahidi kufanya makubwa zaidi katika mashindano mashindano ya Formula 1 baaada ya kufanikiwa kubeba taji la mwaka huu.

    Hamilton amefanikiwa kubeba taji kwa tofauti ya alama sitini na saba dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Nico Rosberg likiwa ni taji lake la pili baada ya lile la kwanza kulitwaa mwaka 2008 akiwa na timu ya McLaren.

    Akiwa ni mmoja kati ya madereva saba kuwahi kutwaa taji hilo mara mbili katika historia ya Formula 1 na wanne kutoka visiwa vya Uingereza amepanga kuvunja rekodi ya Michael Schumacher ya kutwaa mataji saba.

    Hamilton amesema anajua fika kuwa kabla ya kufikia rekodi ya Schumacher anatakiwa kufikia rekodi ya Juan Manuel Fangio aliyetwaa taji hilo mara tano huku Sebastian Vettel ambaye amehamia timu ya Ferrari akiwa na mataji manne kibindoni.

  • HATMA YA MAKUNDI KUFAHAMIKA COPA AMERIKA

    HATMA YA MAKUNDI KUFAHAMIKA COPA AMERIKA

    Mataifa mbalimbali kutoka barani Amerika ya Kusini yatajua hatma yao katika upangwaji wa makundi ya michuano ya Copa Amerika inayotarajiwa kufanyika mwaka 2015 huko nchini Chile.

    Katika jiji la Vina Del Mar mataifa kumi na mbili yatagawanywa katika makundi matatu yatakayojumuisha timu nne kila kundi kwenye hatua ya kwanza.

    Chile ambaye ndio mwenyeji wa michuano hiyo amewekwa katika kapu namba moja pamoja na timu ya Brazil na Argentina huku Uruguay ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo amewekwa katika kapu namba mbili linalojumuisha na timu za Colombia na Mexico (kaalikwa).

    Mataifa mengine yanasubiri upangwaji huo wa makundi ni Ecuador, Peru, Paraguay, Venezuela, Bolivia na Jamaica ambaye ni mualikwa katika michuano hiyo iliyoanzishwa miaka tisini na nane iliyopita.

  • CASILLAS AWANIA TUZO YA GOLIKIPA BORA 2014

    CASILLAS AWANIA TUZO YA GOLIKIPA BORA 2014

    Iker Casillas ateuliwa kuwania tuzo ya golikipa bora katika kikosi cha shirikisho la soka duniani (FIFA) cha mwaka 2014.

    Casillas ambaye ni golikipa wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania amejumuishwa katika kiny’ang’anyiro hicho pamoja na Manuel Neuer (Bayern Munich, Germany), Gigi Buffon (Juventus, Italy), Thibaut Courtois (Chelsea, Ubelgiji) na Claudio Bravo (FC Barcelona, Chile).

    Kujumuishwa kwa nahodha huyo wa Hispania kumewashangaza watu wengi kwani Casilllas alicheza mechi mbili tu katika msimu wa 2013/2014 ndani ya La Liga huku akifanya vibaya katika michuano ya kombe la Dunia huko nchini Brazil huku timu ya taifa ya Hispania ikitupwa nje katika hatua ya makundi.

    Mshindi wa nafasi hiyo ya golikipa ambaye hupigiwa kura na wachezaji wapatao ishirini elfu kutoka duniani kote atatangazwa mnamo tarehe kumi na mbili mwezi wa kwanza mwaka 2015 kwenye ugawaji wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka (Ballon d’Or).

  • BARTOMEU AMMWAGIA SIFA MESSI

    BARTOMEU AMMWAGIA SIFA MESSI

    Rais wa klabu ya FC Barcelona amemmwagia sifa nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji wa klabu hiyo, Lionel Messi kuwa ndio mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea.

    Josep Maria Bartomeu ambaye ni rais wa klabu ya Barcelona inayonolewa na kocha Luis Enrique amezungumza hayo baada ya kushuhudia Messi akivunja rekodi ya magoli ndani ya La Liga iliyokuwa ikishikiliwa na marehemu Telmo Zarra.

    Messi mwenye umri wa miaka ishirini na saba amefikisha jumla ya magoli mia mbili na hamsini na tatu na kuvunja rekodi ya Zarra ya magoli mia mbili hamsini iliyodumu kwa zaidi ya miaka hamsini.

    Mshambuliaji huyo pia anashikilia rekodi ya magoli katika klabu bingwa Ulaya akiwa sawa na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Raul Gonzalez wakiwa na magoli sabini na moja.

  • DJOKOVIC AVUNJA REKODI YA IVAN LENDL

    DJOKOVIC AVUNJA REKODI YA IVAN LENDL

    Bingwa namba moja katika mchezo wa Tennis, Novak atawazwa kuwa mshindi wa michuano ya ATP World Tour Finals huko jijini London baada ya Roger Federer kushindwa kucheza mchezo wa fainali kutokana na maumivu ya mgongo.

    Federer aliyeshinda kwa seti 4-6 7-5 7-6(8-6) ndani masaa mawili na dakika arobaini na nane siku ya jumamosi dhidi ya Wawrinka ameomba radhi kutokana na kitendo hicho.

    Huu ni ubingwa wan ne kwa MSerbia Djokovic ikiwa ni mara yake ya tatu mfululizo kutwaa taji hilo akifikia rekodi iliyowekwa na Ivan Lendl miaka ya themanini.

    Toka mwaka 2014 katika michuano mbalimbali, Novak Djokovic amecheza michezo 66 akifungwa minne na kushinda sitini na mbili na kumfanya amalize akiwa bingwa namba moja duniani.

  • VAN GHAL KUMKOSA KIUNGO BLIND MECHI ZIJAZO

    VAN GHAL KUMKOSA KIUNGO BLIND MECHI ZIJAZO

    Kiungo wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Manchester United, Daley Blind anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita baada ya kupata jeraha la goti katika mchezo wa kuwania kuingia michuano ya Ulaya mwaka 2016 huko nchini Ufaransa.

    Katika mchezo huo ambao timu ya Taifa ya Uholanzi iliibuka na ushindi mnono wa magoli 6-0 dhidi ya Latvia, Blind aliumia mnamo dakika ya 20 ya mchezo kwa kugongana na mchezaji Eduards Visnakovs.

    Kuumia kwa kiungo huyo ni pigo kubwa kwa klabu ya Manchester United chini ya aliyekuwa kocha wa Uholanzi, Louis Van Ghal akiwa mpaka sasa ameshawapoteza wachezaji muhimu katika kikosi cha kwanza akiwemo David De Gea, Phil Jones, Michael Carrick, radamel Falcao huku Cris Smalling akiwa na adhabu.

    Manchester United inayoshika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu nchini England siku ya jumamosi itasafiri kwenda jijini London kumenyana na klabu ya Arsenal inayoshika nafasi ya 6.

  • NOVAK DJOKOVIC AMCHAKAZA MIRIN CILIC MICHUANO YA ATP WORLD TOUR

    NOVAK DJOKOVIC AMCHAKAZA MIRIN CILIC MICHUANO YA ATP WORLD TOUR

    TENNIS

    Bingwa namba moja katika mchezo wa Tennis, Novak Djokovic ameanza vizuri michuano ya ATP World Tour kwa kumchakaza bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani (US OPEN), Marin Cilic kwa seti 6-1 6-1 huko O2 Arena jijini London.

    Djokovic anayesaka taji la tatu mfululizo katika michuano hiyo ikiwa ni rekodi iliyowekwa mara ya mwisho na aliyekuwa kocha wa Andy Murray, Ivan Lendl ilimchukua Mserbia huyo dakika 56 tu kuweza kumpoteza mpinzani wake raia wa Croatia.

    Katika mchezo mwengine wa kundi A uliwakutanisha bingwa wa michuano ya wazi ya Australia, Stanislas Wawrinka dhidi ya Tomas Berdych ambapo raia huyo wa Uswisi alimsambaratisha Berych kwa seti 6-1 6-1 mchezo ulioelemea upande mmoja kwa kipindi kirefu.

    Matokeo hayo yanawaweka pazuri Djokovic na Wwarinka huku mchezo unaofuata utawakutanisha miamba hii miwili na mshindi ataweza kukata tiketi ya kutinga nusu fainali.