Category: Sports

  • MANCHESTER UNITED YAFIKIA MAKUBALIANO NA AS MONACO JUU YA ADA YA KUMSAJILI RADAMEL FALCAO

    MANCHESTER UNITED YAFIKIA MAKUBALIANO NA AS MONACO JUU YA ADA YA KUMSAJILI RADAMEL FALCAO

     

    Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na klabu ya AS Monaco juu ya ada ya kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao.

    Falcao alijiunga na klabu ya Manchester United kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea AS Monaco kwa dau la euro million 8 huku kukiwa na kipengele kinachomruhusu kujiunga na mashetani wekundu mwisho wa mkataba huo.

    Manchester United chini ya Ed-Woodward wamesema wapo teyari kulipa kiasi cha euro million 56 na mshahara wa kiasi cha euro laki tatu na elfu tano ili kupata huduma za EL TIGER.

    Raia huyo wa Colombia bado anapigania nafasi katika kikosi cha kwanza kilicho chini ya Louis Van Gaal ambacho kimejaa mastaa kama Wayne Rooney, Robin Van Persie na Angel Di Maria.

    radamel-falcao
    RADAMEL FALCAO
  • SIMBA YAMTAKA HANS POP KUTOZUNGUMZA CHOCHOTE KUHUSU CLUB HIYO

    SIMBA YAMTAKA HANS POP KUTOZUNGUMZA CHOCHOTE KUHUSU CLUB HIYO

    Siku moja tu baada ya kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba kumpiga stop mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zakaria Hans pop kutozungumza chochote kuhusu Simba kwa kuwa taarifa zake hazina Baraka ya uongozi, mwenyekiti huyo wa usajili ameibuka na kusema hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kumzuia isipokuwa rais wa Simba pekee.

    hans ameyazungumza hayo baada ya E.sports kutaka kujua msimamo wake baada ya kauli ya iliyotolewa jana na katibu wa Simba stephen Ally.

    Wakati hayo yakiendelea Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara wanalambalamba Azam fc wanapanda basi kesho kuelekea Mtwara kuwafata vijana waliokatika hali mbaya kwa sasa Ndanda fc, ambao watashuka nao dimbani Nangwanda sijaona.

    Msemaji wa Azam Jaffer Idd Maganga amezungumza na E.sports na kuthibitisha pia wachezaji wao waliokuwa majeruhi wamerejea katika hali nzuri.

  • MENEJA WA KASEJA AMFUNGUKIA MAXIMO, KAGERA SUGA YAANZA TAMBO DHIDI YA YANGA

    MENEJA WA KASEJA AMFUNGUKIA MAXIMO, KAGERA SUGA YAANZA TAMBO DHIDI YA YANGA

    Wakati kikosi cha Yanga kikiendelea na mazoezi huko Kahama ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera sugar, uongozi wa Yanga umepewa masharti magumu kuhusu mlinda mlango wao Juma kaseja anaeonekana kusugua benchi kila kukicha ndani ya Klabu hiyo

    Akizungumza na E.sports, meneja wa Kaseja, Abdulfatah Saleh, amesema haoni sababu ya kocha Maxio Maximo kuendelea kumkalisha benchi mchezaji huyo mwenye sifa kuubwa hapa nchini

    Kikosi cha watengeneza sukari – Kagera sugar cha mjini Bukoba kimetoa tahadhari kwa vijana wa kocha maxio Maximo wasiingie kichwakichwa katika mchezo wao utakaopigwa siku ya jumamosi katika dimba la Kaitaba huiko Bukoba.

    kocha msaidizi wa Kagera sugar Mrange Kabange amesema Yanga wanatakiwa wajue kuwa wao Kagera wamechoshwa na sare mbili mfululizo katika uwanja wa nyumbani na badala yake wanazitaka kwa udi na uvumba pointi 3 toka kwao

  • DONDOO ZA TENNIS- PARIS MASTERS

    DONDOO ZA TENNIS- PARIS MASTERS

    Bingwa nambari moja duniani katika mchezo wa Tennis, Novak Djokovic amefanikiwa kutinga katika hatua ya raundi ya pili baada ya kumchapa Mjerumani, Phillip Kohlschreiber kwa seti 6-3 6-4.

    Djokovic mwenye umri wa miaka 27, alionekana akiwa katika kiwango kizuri dhidi ya Phillip huku akipambana kutopoteza taji la ubingwa nambari moja dhidi ya Mswisi Roger Federer.

    Federer anayetarajiwa kushuka leo uwanjani dhidi ya Mfaransa Jeremy Chardy anaalama 9,280 nyuma ya Djokovic mwenye jumla ya alama 11,510 kuelekea katika michuano ya ATP World Tours Finals huko O2 Arena, London.

    Ushindi huo wa Mserbia Djokovic umekuja wiki moja tu baada ya mke wake kujifungua mtoto wa kiume waliyempa jina la Stefan.

    novak-djokovic-training
    Novak Djokovic

    djokovic-training

    novak-djokovic-sharapova-training

  • CHELSEA NA LIVERPOOL ZATINGA ROBO FAINALI ENGLAND

    CHELSEA NA LIVERPOOL ZATINGA ROBO FAINALI ENGLAND

    Chelsea na Liverpool zatinga katika hatua ya robo fainali ya kombe la ligi nchini England kwa ushindi wa magoli 2-1 kila mmoja.

    Chelsea bila ya mshambuliaji wao tegemezi msimu huu, Diego Costa ilibidi wamgeukie Didier Drogba aliyefunga goli la kwanza katika mchezo huo likiwa ni goli lake la tatu katika michezo mitatu iliyopita ndani ya uzi wa The Blues.

    Mnamo dakika ya 77 klabu ya Shrewsbury ilifanikiwa kusawazishakabla ya beki wa klabu hiyo Grandison kujifunga katika daika ya 81.

    Wakati huohuo klabu ya Liverpool imepata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Swansea huku Mario Balotteli akionyersha kiwango kizuri baada ya kutokea benchi kuchukua nafasi ya Rickie Lambert ambapo The Kops walikuwa nyuma kwa goli moja.

    Beki ya Swansea ilionekana iko imara mpaka mnamo dakika ya 94 beki wa kimataifa wa Croatia, Dejan Lovren alipounganisha krosi kwa kichwa na kupeleka furaha kwa vijana wa Brendan Rodgers.

  • URUSI YAZINDUA NEMBO YA KOMBE LA DUNIA 2018 KWENYE CHOMBO CHA ANGA

    URUSI YAZINDUA NEMBO YA KOMBE LA DUNIA 2018 KWENYE CHOMBO CHA ANGA

    Kuelekea michuano ya kombe la dunia mwaka 2018, Taifa la Urusi lazinduwa rasmi nembo itakayotumika katika michuano hiyo mikubwa ya mpira wa miguu iliyo chini ya FIFA.

    Nembo hiyo ilizinduliwa katika chombo cha uchunguzi wa kisanyasi wa anga na baadaye kuonyeshwa katika jiji la Moscow.

    Urusi ilipata haki ya kuandaa michuano hiyo ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza kwa kuzipiku nchi kama England, Spain-Ureno na Uholanzi-Ubelgiji mwaka 2010.

    Shirikisho la soka duniani (FIFA) ilijikuta katika kashfa nzito kwa kuwatangaza Urusi kama washindi wa kuandaa michuano hiyo pamoja na ile ya mwaka 2022 huko nchini Qatar

    RASHIA

     

  • NAHODHA WA BAFANABAFANA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA RISASI

    NAHODHA WA BAFANABAFANA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA RISASI

    Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi.

    Jeshi la polisi la nchi hiyo limesema.

    bafana
    Senzo Meyiwa Ezi ya uhai wake

    Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya taifa katika mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya Afrika.

    Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.

    Katika maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.

     

  • OSCAR TAVERAS AFARIKI DUNIA KWA AJARI YA GARI

    OSCAR TAVERAS AFARIKI DUNIA KWA AJARI YA GARI

    Oscar mwenye umri wa miaka 22 ambae ni nyota iliyokuwa ikichukia kwa kasi kwenye ulimwengu wa Baseball mzaliwa wa Dominican Republic, amaefariki yeye pamoja na mpenzi wake  Edilia Arvelo, mwenye umri wa miaka 18.

    kwa mujibu wa msemaji wa timu ambayo Oscar alikluwa akiichezea enzi za uhai wake amesema ajari hiyo imetokea mara baada ya gari alilokuwa akieendesha mchezaji huyo kuacha njia na kupoteza uelekeo

    AP_TAVERAS3_141026_DG_4x3_992
    oscar Taveras enzi za uhai wake

     

     

     

     

     

     

     

     

     

    AP_TAVERAS5_141026_DG_4x3_992
    Oscar Taveras

     

     

    kupitia mtandao wa twitter moja ya wachezaji wenzake Kolten Wong aliandika hivi”Wow! My heart truly hurts to hear the passing of Oscar! I’ve played with him every year and we truly lost a great person! #RIPOscarTaveras

    tasnia ya mchezo wa Baseball imekuwa ikipata na mikasa ya ajari kwa baadhi ya wachezaji wake kama Nick Adenhart. Josh Hancock. Brian Cole. Mike Darr. And now, Oscar Francisco Taveras ambae alikuwa akitazamiwa kuwa mchezaji nyota siku za mbeleni

     

  • DONDOO ZA LIGI KUU YA UINGEREZA

    DONDOO ZA LIGI KUU YA UINGEREZA

    Katika ligi kuu ya England mechi 12 zimechezwa usiku wa kuamkia leo ambapo Tottenham wamewabamiza bila huruma Asteras Tripolis kwa magoli 5 -1.

    Ilikuwa ni hat-trick ya Harry Kane ambayo imeisaidia Tottenham kuwabamiza wagiriki hao.

    Wakati Evarton imewatunishia misuli Wafaransa, Mpaka dakika ya 90, si Lilli wala Everton aliyechezea nyavu za mwenzie.

    Mchezo huo uliotanguliwa na mapambano kati ya Polisi na Mashabiki wa Evarton ukaisha bila bila.

    Divock Okoth Origi mchezaji kinda ameonyesha mchezo mzuri katika mechi hiyo, Divock aliyezaliwa mwaka 1995 ni mtoto wa

    aliyekuwa mchezaji wa Timu ya Taifa ya Kenya na Mchezaji wa kulipwa Mike Origi.

    Hata hivyo kijana huyo ni binamu wa Arnold Origi, Mkenya anayesukuma ngozi ya ngombe huko Norway.

    Matoke mengine ni Villarreal imemchapa FC Zürich mabao 4 – 1. Hapo Kesho Jumamosi, West Ham wanapambana na Man City,

    Liverpool watakuwa uso kwa uso na Hull, Southampton kutoana jasho na Stoke, Sunderland jumamosi iliyopita walipigwa bao 8

    kiasi wakaamua kuwarudishia kiingilio mashabiki wao, je! watapona mbele ya bunduki za Arsenal.

    TOTEN

     

  • REAL MADRID YAICHAPA LIVERPOOL 3-0 HUKO ANFIELD

    REAL MADRID YAICHAPA LIVERPOOL 3-0 HUKO ANFIELD

    Katika ligi ya mabingwa barani Ulaya Liverpool imechabangwa nyumbani Anfield kwa mabao 3-0 kutoka kwa Real Madrid huku Mario Balotelli akiingia lawamani.

    140922164822_mario_balotelli_304x171_getty_nocredit
    Mario Balotelli

    Meneja wa mchezaji huyo mtukutu, Brendan Rodgers amemlaumu mshambuliaji huyo kwa kitendo chake cha kubadilishana Jezi na Pepe mara tu baada ya dakika 45 za kwanza.

    140411171051_brendan_rodgers_304x171_getty_nocredit
    Brendan Rodgers

    Baadhi ya mashabiki wa jijini Dar es Salaam,Tanzania wamemtupia lawama mchezaji huyo ambaye pamoja na kununuliwa kwa pauni milioni 16 ameifungia Liverpool goli moja tu msimu huu.

    Wakati huo huo Arsenal wamepata ushindi wa dakika za mwisho wa 2-1 baada ya Anderletch kuwakimbiza mchakamchaka kwa muda mrefu.

    Mara baada ya mchezo huo nimezungumza na shabiki wa Arsenal ambaye anasema pamoja na ushindi walioupata lakini kuna haja ya Arsene Wenger kubadillika

    Matokeo mengine ni Atletico Madrid wameifumua Malmo 5-0 na Olimpiakos imeichapa Juventus bao 1-0

    Kwa upande wa michuano ya Uropa Ligi, leo Tottenham inakipiga na Asteras Tripolis, Inter Millan inakutana na St Etienne, Lille itamenyana na Evaton, wakati ambapo Viareale watacheza na FC Zurich

     

  • MCHEZAJI WA QPR ASEMA HANA UZANI MKUBWA

    MCHEZAJI WA QPR ASEMA HANA UZANI MKUBWA

    Mchezaji wa QPR Adel Taarabt amemjibu kocha wake Harry Redknapp aliyesema kuwa mchezaji huyo ana uzani mkubwa hivyobasi hafai kucheza.

    Redknapp alitoa madai hayo alipoulizwa ni kwa nini hakumjumuisha kiungo huyo wa kati katika kikosi kilichocheza mechi dhidi ya Liverpool waliposhindwa kwa mabao 3-2. Hata hivyo Taarabt alipokuwa akiongea na kituo cha habari cha Daily Mail alijitetea kwamba madai hayo si ya kweli.

    “Nilikuwa na tamaa kubwa ya kucheza kabla ya mechi kuanza. Nilikasirika sana niliponyimwa nafasi ya kucheza.”alisema Taarabt.

    Taarabt, ambaye hajakuwa akishirikishwa katika vipindi vya kwanza vya mechi za QPR tangu Agosti 27 alisema: “Mwanahabari alikuwa akifanya wajibu wake kwa kuuliza kama nilikuwa na jeraha”. ” Angesema ”atakapokuwa sawa atacheza”. Yeye ni meneja mwenye tajriba kubwa na angedhibiti hali ilivyokuwa”

    “Sikushiriki mechi za kabla ya msimu kuanza kwa sababu nilikuwa na jeraha la kisigino, kwa hivyo hali yangu haikuwa asilimia mia kwa mia.”

    Taarabt alirudi kuichezea Loftus Road msimu huu baada ya kuzichezea Fulham na AC Milan msimu uliopita kwa mkopo.

    ” Sipendi chakula tunachopewa katika kambi ya kufanyia mazoezi lakini nala chakula bora kama wachezaji wengine.

    “Uzani mkubwa ambao nimewahi kuwa nao ni kilo 86 nikiwa AC Milan, uzani mdogo Zaidi ukiwa kilo 84 na kwa sasa nina uzani wa kilo 85.”

    Timu ya QPR inashika mkia katika orodha ya ubora wa timu katika ligi ya Uingereza baada ya kujipatia pointi nne tu katika mechi nane za mwanzo wa msimu huu walizoshiriki.

    QPR2
    Taarabt wa QPR