Category: Sports

  • mtikisiko na vishindo vyaikumba 95.5 morogoro

    mtikisiko na vishindo vyaikumba 95.5 morogoro

    Mtikisiko na vishindo vya wana mazoezi wa  95.5 morogoro vyasikika mapema asubuhi ya leo

    MATUKIO KWA PICHA

  • Wallace Karia; mchezo wa October 12 ni Muhimu sana

    Wallace Karia; mchezo wa October 12 ni Muhimu sana

    “Mchezo wa October 12 ni muhimu sana kabla ya October 16, 2018 kwa hiyo sasa hivi tuangalie wa October 12 kwa sababu inabidi tukacheze kule Cape Verde halafu October 16 tunamalizia hapa Wallace Karia, Rais TFF.
    Watanzania waiunge mkono Taifa Stars, Waziri Mwakyembe na serikali yetu kwa kuchangia lakini mchango huo ni nauli yao wenyewe ya kuwafikisha Cape Verde.

    Cape Verde tutakwenda kwa mambo mawili, tangu ndege yetu imenunuliwa mipango yake ilikuwa ni kuwa na safari za nje ya nchi. Hii itakuwa safari yake ya kwanza nje ya nchi kwa hiyo tutaweka historia lakini tutaweka historia kwenda kuishangilia timu yetu na tuweke historia ya kupata ushindi kule.

    Tutaondoka October 9 usiku na alfajiri ya October 10 tutakuwa tumefika Cape Verde na jioni wachezaji watafanya mazoezi, baada ya mchezo wa October 12, usiku tutaondoka kurudi nyumbani.

    Kikubwa ni kwamba, ndege haitaweza kuondoka kama haitakuwa na watu wa kutosha. Ndege ina viti 22 vya Business class ambapo tayari viti 15 vimeshalipiwa, viti 31 vya Economy class vimeshalipiwa kwa ajili ya wachezaji na benchi la ufundi.”

  • Naby Keita: Nyota wa Liverpool alazwa baada ya kuumia akiwa uwanjani dhidi ya Napoli UEFA

    Naby Keita: Nyota wa Liverpool alazwa baada ya kuumia akiwa uwanjani dhidi ya Napoli UEFA

    Kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita alikimbizwa hospitalini baada ya kuondolewa uwanjani kwa machela alipoumia akicheza mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Napoli hatua ya makundi.

    Liverpool walilazwa 1-0 ugenini Italia.

    Keita, aliyejiunga na klabu hiyo kutoka RB Leipzig ya Ujerumani kwa £48m majira ya joto mwaka huu, aliondolewa uwanjani baada ya kucheza dakika 19 pekee. Aliumia mgongoni.

  • Kelvin De Bruyne arejea mazoezini

    Kelvin De Bruyne arejea mazoezini

    Kelvin De Bruyne arejea mazoezini kuungana na Nyota wenzake wa Manchester City

    Kiungo huyo raia wa uberigiji alipata majeraha septemba 19 mwaka huu kwenye dhidi ya Arsenal

  • Jonesia Rukiyaa Kupuliza Kipenga Mechi ya Watani wa Jadi Bongo

    Jonesia Rukiyaa Kupuliza Kipenga Mechi ya Watani wa Jadi Bongo

    Licha ya Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama kutangaza kuwa Mwamuzi wa pambano la watani wa jadi atatangazwa Alhamis ya wiki hii, taarifa za ndani zinasema Jonesia Rukiyaa atachezesha pambano hilo.

    Imeelezwa kuwa Rukiyaa atashika filimbi katikati ya Uwanja huku akisaidiana na Ferdnand Chacha pamoja na Mohammed Mkono.

    Aidha, chanzo hicho kimesema Mwamuzi wa mezani atakuwa ni Elly Sasii.

    Jana ilielezwa pia kuwa Mwanamama Florentino Zabron kutoka Dodoma angechezesha mechi hiyo lakini kumefanyika mabadiliko tena mengine.

    Kikao cha Kamati ya Waamuzi na Wanahabari kinatarajiwa kukutana kesho kunako Makao Makuu ya Shirikisho la Soka mitaa ya Ilala Karume, ili kuweka bayana zaidi juu ya Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo.

    Tayari Simba na Yanga wameshaanza kambi kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  • Paul Pogba Hatokuwa Tena Nahodha wa Man United

    Paul Pogba Hatokuwa Tena Nahodha wa Man United

    Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa hana tatizo na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba licha ya kumwambia mchezaji huyo kwamba hatowahi tena kuwa nahodha wa klabu hiyo.

    Mourinho alimwambia Pogba kwamba sio nahodha wa klabu hiyo kutokana na wasiwasi kuhusu tabia yake.

    ”Ukweli ni kwamba nimechukua uamuzi huo ili asiwe nahodha wa pili lakini hakuna tatizo lolote kati yetu”, alisema Mourinho.

    ”Mimi ndio meneja ninaweza kufanya maamuzi kama hayo”.

    Akizungumza na chombo cha habari cha Sky Sports aliongezea: Hakuna tofauti zozote kati yetu ni uamuzi tu ambao sio lazima nieleze.

    Mshindi wa kombe la dunia Pogba 25 aliambiwa kuhusu uamuzi huo kabla ya mechi ya siku ya Jumanne ya kombe la Carabao dhidi ya Derby.

    Mourinho amejaribu kuonyesha uzito wake baada ya kosa la Pogba kuisaidia timu ya Wolves kufunga bao la kusawazisha katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumamosi mbali na mchezaji huyo kukosoa mbinu zinazotumika.

    Pogba alijaribu kupuuzilia mbali matamshi yake katika mtandao wa twitter siku ya Jumatatu. Lakini katika ripoti yake ya mechi ya Jumanne ambayo Derby ilishinda kwa njia ya penalti , Mourinho alisema kuwa hafurahishwi na baadhi ya wachezaji wake.

    ”Mechi dhidi ya Wolves ilikuwa funzo zuri , funzo ambalo ninarejelea kila wiki, funzo ambalo baadhi ya wachezaji hawajifunzi”, alisema.

    Kila timu inayocheza dhidi ya United hucheza kufa kupona, na tunahitaji kuimarika ili kukabiliana nazo , Asilimia 95 haitoshi iwapo wengine wanatoa asilimia 101.

    Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ,Pogba ambaye alitajwa katika kikosi dhidi ya Derby , alitazama kutoka eneo la mashabiki huku Ashley Young akiwa nahodha wa kikosi hicho.

    Kabla ya mechi , Mourinho alisema: “wamepumzishwa . Nilimpumzisha Luke Shaw, Paul, Victor Lindelof, Antonio Valencia na David de Gea. Lazima nicheze na kikosi kizuri. ”

    Kufuatia sare ya 1-1 siku ya Jumamosi. Pogba alisema kwamba angetaka timu hiyo kushambulia mara kwa mara katika uwanja wa Old Trafford. Tuko nyumbani na tunafaa kucheza vizuri zaidi .

    ”Tuko hapa kushambulia”, alisema .Tunapocheza hivyo ni rahisi kwetu sisi.

    Pogba amabaye alijiunga tena na United kutoka Juventus kwa dau lililovunja rekodi mwaka 2016 , alikuwa akiwachwa nje msimu uliopita na kusema kwamba hafurahii kusalia Old Trafford.

    Mkufunzi wa Ufransa Didier Deschamps hivi karibuni alisema kuwa mtazamo wa Pogba kuwa mtu mbinafsi sio wa sawa na kwamba mashabiki na vyombo vya ahabri hawamuelewi.

    Huu unaonekana kama wakati muhimu kwa Manchester United.

    Imekuwa wazi kwa muda kwamba Paul Pogba haelewani na mtu aliyechukua jukumu la kulipa dau lililovunja rekodi ya £89m kumsaini kutoka Juventus.

    Ni wazi kwamba Barcelona inamnyatia. Swali ni je ni nani kati yao atakayeoondoka?

    Kumwachilia Pogba kuondoka kutaonekana kuwa kufeli kwa Mourinho na afisa mkuu mtendaji Ed Woodward, ikiwa ni muda mchache uliopita ambapo mchezaji huyo aliwafurahisha mashabiki katika kombe la dunia.

    Iliobakia ni kusalia naye , lakini hatua hiyo itamaanisha kwamba wadhfa wa Mourinho hauna nguvu tena baada ya kuzuiwa kuwanunua wachezaji wapya aliotaka msimu uliopita.

  • Kocha Msaidizi wa Simba Aendelea kuwa Mbali na Benchi la Ufundi la Simba

    Kocha Msaidizi wa Simba Aendelea kuwa Mbali na Benchi la Ufundi la Simba

    Masoud Djuma Kocha Msaidizi wa Simba ataendelea kubaki Dar es Salaam, ikiwa timu inakwenda Mkoani Mwanza kwa ajili ya kucheza michezo miwili ya Ligi kuu ampapo tarehe 20, September Simba SC itacheza na Mbao Fc kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na Mchezo  mwingine ni ule dhidi ya Mwadui FC kwenye uwanja huo huo wa CCM Kirumba utakao pigwa tarehe 22, September.

    Hatua hiyo inakuja baada ya viongozi wa kumkabidhiwa majukumu mengine ya kuwanoa wachezaji waliobakia Dar wakiwemo Juuko Mushid na Haruna Niyonzima kwa ajili ya mechi zingine za ligi.

     

    Swali Linabaki Je Kweli Kocha Mkuu anajitosheleza mwenyewe bila kuhitaji Msaidizi ??

     

    #SportHQ

  • WAFUNGAJI WA MABAO BORA LIGI KUU ENGLAND

    WAFUNGAJI WA MABAO BORA LIGI KUU ENGLAND

    Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard anaweza kufunga mabao 40 msimu huu na kujishindia tuzo ya mfungaji mabao bora Ligi ya Premia, kwa mujibu wa meneja wa klabu hiyo Maurizio Sarri.

    Kwa mujibu wa BBC, Hazard alifunga mabao matatu dhidi ya Cardiff Jumamosi na kuwawezesha The Blues kupata ushindi wa 4-1.

    Kufikia sasa amefunga mabao matano katika mechi tano zilizochezwa, moja kushinda mchezaji anayemfuata.

    Baada ya mechi hiyo ya Jumamosi, Sarri alisema Mbelgiji huyo huenda akawa ndiye mchezaji bora zaidi Ulaya.

    Alisema zamani alikuwa anaamini alikuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi Ulaya lakini kwa sasa anaamini huenda ndiye bora zaidi.

    “Tumezungumza naye na kumwambia anaweza kufunga mabao 40,” alisema Sarri.

    “Kuna baadhi ya mambo anayoweza kuboresha, lakini anaweza.”

    Miongoni mwa anayotaka Hazard aboreshe, ni kutumia nguvu zake nyingi katika maeneo ya wapinzani uwanjani badala ya eneo la timu yake.

    Kimsingi anamtaka ashambulie zaidi.

    Hazard alijiunga na Chelsea mwaka 2012 na amewafungia jumla ya mabao 94 lakini hajawahi kufunga mabao 20 akichezea klabu mechi za ushindani msimu mmoja.

    Mabao ya juu zaidi aliyofunga ilikuwa ni msimu wa 2014-15 alipofunga mabao 19, na misimu miwili iliyopita alifunga amabo 17 kila msimu.

    Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah alishinda tuzo ya mfungaji mabao bora msimu uliopita baada ya kufunga mabao 32 Ligi ya Premia, na jumla ya mabao 44 mashindano yote.

  • SERENGETI BOYS DIMBANI TAIFA LEO

    SERENGETI BOYS DIMBANI TAIFA LEO

    Michuano ya vijana walio chini ya miaka 17 inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaa kufuzu fainali za Afcon leo Tanzania (Serengeti Boys ) watakuwa dimbani dhidi ya Rwanda (Amavubi Junior )vijana wa Kagame katika mchezo ambao utatoa matokeo ya nani atakuwa kinara katika kundi A.

    Mpaka sasa Rwanda na Tanzania zimetinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ikiwa Tanzania ndio inaongoza kundi hilo kwa idadi ya magoli ya kufunga ,katika Kundi B Burundi na Sudani tayari zimeyaaga mashindano hayo.

    Wenyeji Serengeti Boys walianza vyema michuano hiyo ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Burundi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam huku Rwanda wakianza kwa kuifunga Sudan mabao 3-1 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

    Tanzania kupitia vijana wa Serengeti Boys ndio mabingwa wa Kombe la Vijana la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati Cecafa wa mwaka 2017, walitwaa ubingwa baada ya kuwalaza Somalia mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyochezewa mjini Bujumbura, Burundi.

  • Ronaldo, Modric, Salah Vitani Mchezaji Bora, Messi, Mbappe Waenguliwa

    Ronaldo, Modric, Salah Vitani Mchezaji Bora, Messi, Mbappe Waenguliwa

    Shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya Nyota wanaoshindania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya UEFA kwa mwaka 2017/2018 ambao ni Cristiano Ronaldo wa Juventus, Luka Modric wa Real Madrid na Mohammed Salah wa Liverpool.

    Hii ni baada ya kufanya mchujo wa wachezaji 10 kati ya hao ni washindi wa Kombe la Dunia mwaka huu.

    Luka Modrić (Real Madrid na Croatia)
    Mshindi wa Kombe la Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) 2018, Mchezaji Bora wa Dunia (Kombe la Dunia ‘FIFA World Cup’ 2018.

    Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Juventus and Portugal)
    Mshindi wa Kombe la Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) mara tano na mfungaji Bora wa UEFA Champions League mwaka 2018, mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia (Ballon d’Or) mara tano.

    Mohamed Salah (Liverpool and Egypt)
    Ana rekodi nyingi za michuano ya UEFA Champions League hasa katika msimu wake wa kwanza ndani ya Liverpool. Amefanikiwa kucheza fainali hizo na Hispania licha yakutolewa nje baada ya kuumia.

     

    Wengine walioingia 10 Bora ni;

    4 Antoine Griezmann (Atlético & France) – 72 points
    5 Lionel Messi (Barcelona & Argentina) – 55 points
    6 Kylian Mbappé (Paris & France) – 43 points
    7 Kevin De Bruyne (Manchester City & Belgium) – 28 points
    8 Raphaël Varane (Real Madrid & France) – 23 points
    9 Eden Hazard (Chelsea & Belgium) – 15 points
    10 Sergio Ramos (Real Madrid & Spain) – 12 points.

    Tuzo nyingine ni;

    Goalkeeper wa msimu: Alisson Becker, Gianluigi Buffon, Keylor Navas.
    Beki wa msimu: Marcelo, Sergio Ramos, Raphaël Varane.
    Kiungo wa msimu: Kevin De Bruyne, Toni Kroos, Luka Modrić.
    Mshambuliaji wa msimu: Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Mohamed Salah.
    Mchezaji wa kike wa Mwaka: Pernille Harder, Ada Hegerberg, Amandine Henry.
    Mchezaji wa Ulaya wa Msimu: Diego Godín, Antoine Griezmann, Dimitri Payet.

  • Yanga sc Kucheza na Timu ya Mchangani Leo

    Yanga sc Kucheza na Timu ya Mchangani Leo

    Baada ya siku takribani tano kupita tangu kikosi cha Yanga kiweke kambi mjini Morogoro, imeelezwa Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ameomba mechi moja kukipima kikosi chake.

    Taarifa kutoka Morogoro zinasema Zahera ameomba apatiwe timu moja ambayo haishiriki Ligi Kuu Bara ili aweze kukipima vizuri kikosi chake kabla ya kufikia hatua ya kucheza na timu za daraja la juu.

    Taarifa zinaeleza Yanga wametuma maombi kwa timu zaidi ya moja mjini humo na ambayo itakubali watakipiga nayo leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi dhidi ya USM Alger.

    Ikumbukwe Yanga watakipiga na Alger Agosti 19 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika.

    Katika mechi ya mkondo wa kwanza, Yanga ililala kwa jumla ya mabao 4-0 jijini Algiers, Algeria ambapo sasa ipo mkiani kunako kundi D ikiwa na alama moja pekee.