Category: Global News

  • OSCAR PISTORIUS AMEHUKUMIWA JELA MIAKA MITANO

    OSCAR PISTORIUS AMEHUKUMIWA JELA MIAKA MITANO

    MWANARIADHA wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

    Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia.

    Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.

    Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia. Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

    Oscar Pistorius Is Sentenced For Killing Girlfriend

  • MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA MAFUTA YA TOTAL YA UFARANSA AUAWA KWA AJALI YA NDEGE

    MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA MAFUTA YA TOTAL YA UFARANSA AUAWA KWA AJALI YA NDEGE

    KAMPUNI kubwa ya mafuta ya Ufaransa, Total imetangaza kwamba mkurugenzi wake mkuu, Christophe de Margerie ameuawa katika ajali ya ndege iliyotokea katika uwanja wa ndege wa Moscow nchini Urusi.

    Taarifa zimeeleza kuwa ndege ya binafsi aliyokuwa akisafiria afisa huyo imeanguka kwenye uwanja wa nukovo ulio nje kidogo ya jiji la Moscow.

    Vyombo vya habari vya Urusi vimesema kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria mmoja tu, pamoja na wahudumu watatu, wote wakiwa raia wa Ufaransa.

     

  • RAIS WA NIGERIA AELEZEA MAFANIKIO NA NJIA WALIZOTUMIA KUONDOA EBOLA

    RAIS WA NIGERIA AELEZEA MAFANIKIO NA NJIA WALIZOTUMIA KUONDOA EBOLA

    RAIS wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema mafanikio ya nchi yake dhidi ya maradhi ya Ebola yametokana na imani ya wananchi wa kawaida kwa maagizo yaliyotolewa na serikali, kuwataka wabadili mienendo yao ya kila siku maishani kama vile kusalimiana kwa kupeana mikono, na utaratibu wa mazishi.

    Amesema serikali yake ilikuwa na wasiwasi kwamba makanisa yangekataa kuitikia wito huo katika suala la komunio ambapo watu wapatao 1,000 wanaweza kushiriki kikombe kimoja. Ameyasifu makanisa kwa kuusimamisha utaratibu huo, na hata ule wa kutakiana amani wakati huu wa kitisho cha Ebola.

    Kauli ya Rais Jonathan inafuatia tangazo la Shirika la afya ulimwenguni WHO hapo jana, kwamba Nigeria sasa ni nchi isiyokuwa na maambukizi ya Ebola, baada ya kutimiza siku 42 bila maambukizi yoyote mapya.

  • MCHEZAJI AFARIKI AKISHEREHEKEA BAO INDIA

    MCHEZAJI AFARIKI AKISHEREHEKEA BAO INDIA

    Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.

    Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.

    Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.

    Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.

    Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : ”imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. ”

    “Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.”

     

  • WHO: EBOLA YAANGAMIZWA NIGERIA

    WHO: EBOLA YAANGAMIZWA NIGERIA

    Shirika la afya duniani linatarajiwa kutangaza rasmi kuwa taifa la Nigeria halina ugonjwa wa bola baadae hii leo, wiki sita baada ya kutoripotiwa kwa visa vya ugonjwa huo .

    Nchi giyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, alipokea sifa tele kwa hatua zake za haraka kukabiliana na Ebola baada ya mwanmadiplomasia Mliberia mwenye ugonjwa huo kwenda Nigeria mwezi Julai.

    Shirika la afya duniani lilitangaza Senegal kutokuwa tena na Ebola mnamo siku ya Ijumaa.

    Mlipuko unaoshuhudiwa wa Ebola, umewaua watu 4,500 katika kanda ya Afrika Magharibi hasa nchini Liberia , Guinea na Sierra Leone.

    Inakisiwa 70% ya wale walioambukizwa ugonjwa huo wamefariki katika mataifa hayo.

    WHO

    Shirika la afya duniani linaweza tu kutangaza nchi kutokuwa na Ebola ikiwa siku 21 zitapita bila ya kuripotiwa kwa visa vipya vya Ebola.

    Kisa cha mwisho kilichoripotiwa cha maambukizi mapya ya Ebola, kiliripotiwa tarehe 5 Septemba.

    Janga hilo, lilianza kuripotiwa,wakati raia mmoja wa Liberia kuripotiwa kuwa na Ebola mwezi Julai.

    Nigeria ilitangaza hali ya tahadhari kiafya huku bwana Sawyer akifariki baadaye kutokana na ugonjwa huo pamoja na raia wengine saba wa Nigeria.

    Raia hao walikuwa pamoja na Daktari Ameyo Stella Adadevoh, aliyetambua kuwa Sawyer alikuwa na Ebola na alisifika kwa kusaidia katika harakati za kudhibiti ugonjwa huo.

    Balozi wa Liberia alipeleka virusi vya ebola mjini Lagos mwezi Julai.

    Alikuguliwa kuwa na Ebola hospitalini alipofanyiwa uchunguzi wa awali .

    Mkurugenzi wa hospitali hiyo Daktari Benjamin Ohiaeri, amesema kuwa mlipuko huo umekuwa na athari kubwa.

    Mawaziri mambo ya nje wa muungano wa ulaya wanakutana hii leo kujadili mikakati ya kudhibiti maambukizi ya ebola .

    Zaidi ya watu 4500 wamekufa kutokanma na mlipuko wa ugonjwa huo wengi wao raia wa Afrika Magharibi .

     

  • SALVA KIIR, MACHAR KUKUTANA TANZANIA

    SALVA KIIR, MACHAR KUKUTANA TANZANIA

    SUDAN
    Wakaazi wa Sudan Kusini walioathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika jimbo la Juba

    Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake waliyehasimiana Riek Machar, leo wamealikwa kuhudhuria uzinduzi wa mazungumzo ya kutafuta muafaka ndani ya chama cha SPLM kinachoongoza taifa hilo lenye machafuko ya kisiasa.

    Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Arusha chini ya usimamizi wa CCM, chama tawala nchini Tanzania.

    Endapo mahasimu hao wawili watafika na kukaa meza moja itakuwa ni hatua muhimu katika jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika na jumuiya ya kimataifa kupata muafaka wa machafuko yanayoendelea katika taifa hilo changa kuliko yote barani Afrika.

    Tangazo la kualikwa kwao lilitolewa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana, baada ya mkutano wa siku tano uliofanyika Arusha kuandaa misingi itakayosimamia mazungumzo ya muafaka kufuatia maombi ya chama cha SPLM.

    Mchakato huo unaosimamiwa na CCM unafanyika kuunga mkono jitahada zinazoendelea kumaliza mgogoro ambao mpaka sasa umesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine mamilioni kuyakimbia makazi yao.

    Mazungumzo ya awali yaliwakutanisha wawakilishi kutoka SPLM KUU, SPLM UPINZANI na KUNDI LA WANACHAMA waliowahi kuwekwa kizuzini, lengo likiwa ni kuyaunganisha makundi hayo na kumaliza tofauti zao.

    Viongozi hao inaaminika wataitikia wito wa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye anafanya kazi hiyo kwa kofia ya mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.

    Na kama wakifika Arusha kukaa meza moja ya mazungumzo itakuwa ni hatua ambayo haijafanikiwa tangu watofautiane na machafuko kuzuka nchini Sudan Kusini mwezi Desemba mwaka jana.

    Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa mstari wa mbele kusaidia upatanishi barani Afrika, katika miaka ya karibuni imesaidia kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 uliosababisha mauaji na maelfu ya watu kukimbia makazi yao.

  • JESHI LA MAREKANI KUPAMBANA NA EBOLA AFRIKA MAGHARIBI

    JESHI LA MAREKANI KUPAMBANA NA EBOLA AFRIKA MAGHARIBI

    Rais wa Marekani Barack Obama amethibitisha wito wa kulitumia jeshi la nchi hiyo na wale wa akiba iwapo watahitajika kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika magharibi.

    Rais Obama amesema wanajeshi hao wataongeza nguvu ya jeshi katika kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.

    Kundi la kwanza la wanajeshi hao linatarajiwa kupelekwa kusaidia ujenzi wa vituo 17 vya kutolea tiba ya ugonjwa huo, katikati mwa Liberia, moja ya nchi iliyoathiriwa vibaya na ugonjwa huo.

    Maafisa wa kikosi cha ulinzi wameelezea agizo hilo la Raisi Obama kama agizo la muhumu ili kuongeza kasi ya kutekeleza mipango ya kwenda kuisaidia mapambano ya ugonjwa huo

    na itamfanya rais kutuma majeshi mengine zaidi iwapo watahitajika.

    Marekani imeahidi kupeleka askari wake wapatao elfu nne huko Africa Magharibi kusaidia mapambano ya kuzuia na kuumaliza kabisa ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.

    Rais Obama amesema hajapinga wazo la kutekeleza katazo la kuziuia watu wanaoingia nchini Marekani kutoka nchi zilizo athiriwa na ugonjwa huo,na hadhani kama wazo hilo litafanikiwa.

    Ameyasema hayo mwishoni mwa mkutano aloufanya katika ikulu ya Marekani na maafisa wa shirikisho juu ya ushiriki wa nchi ya Marekani katika mapambano na ugonjwa huo.

    Raisi Obama amesema anaamini hatua za uchunguzi wa ugonjwa huo ni hatua nzuri.

    Sina sababu za kifolosofia ya kupinga katazo la safari, kama hiyo ndiyo itakuwa ndiyo njia bora ya kuwaweka raia wa Marekani salama.tatizo ni kwamba je haya ndiyo majadiliano yangu niliyoyafanya a na wataalamu walioko kwenye maeneo ya tukio yaliyoathiriwa na ugonjwa huo ni kwamba katazo la safari halina nguvu kama hatua tulizochukua hivi karibuni kupambana na ugojwa huo.

    EBOLA MADRID

    Obama pia aesema yupo wazi kumteua atakayesimamia janga la Ebola

    Mpaka hatua hii kila mtu binafsi amefanya kazi nzuri yenye kutukuka ,kazi ambayo ni ngumu kupambana na majimaji ya ugonjwa huu. Hii inatufanya tuwe kama mtu mmoja ,kwa sehemu baada ya janga hili tunaweza kusonga mbele kama kawaida.

    Naye mkuu wa kitengo cha maendeleo ya kimataifa wa Marekani ameahidi kuongeza dola milioni mia moja na arobaini na mbili ili kusaidia mapambano ya ugonjwa wa Ebola huko Guinea.

    Bwana Rajiv Shah aliyeko nchini Guinea kwenye ziara ya kujionea hali halisi ya athari zilizoletwa na ugonjwa huo Africa Magharibi, na kusema kwamba anafikiri msaada huo utarejesha matumaini ya watu waishio nchini humo.

    Natangaza ongezeko la dola milioni moja na eflfu arobaini na mbili ili kuendeleza mapambano nchini Guinea katika ugonjwa wa Ebola,kwa vitengo vinavyojihusisha na ugonjwa huu,ili kuongeza ufanisi katika idara ya afya na wafanyakazi wake na kuongeza nguvu katika elimu juu ya ugonjwa huu.

     

  • WAASI WA ADF WASHAMBULIA DRC

    WAASI WA ADF WASHAMBULIA DRC

    Jeshi la DRC linasema kuwa watu 26 wameuawa nchini humo katika shambulizi liliofanywa katika mji wa Beni Mashariki mwa nchi.

    Wengi, wa waliofariki walikuwa raia wakiwemo watoto.

    Shirika moja la kutetea haki za binadamu, linasema kuwa wapiganaji wa kundi la waasi la Uganda la ADF au Allied Democratic Forces , lilivamia mji huo nyakati za usiku.

    Kikosi cha Umoja wa Matifa kikishirikiana na wanjeshi wa DRC, kimekuwa kikijaribu kuwatimua waasi hao wa ADF kutoka nchini DRC tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

    Lakini waasi hao nao pia wamekuwa wakifanya mashambulizi kadhaa katika meizi ya hivi karibuni.

     

  • MFANYAKAZI MWINGINE WA EBOLA AGUNDULIKA MAREKANI

    MFANYAKAZI MWINGINE WA EBOLA AGUNDULIKA MAREKANI

    Mgonjwa mwingine wa Ebola amegundulika huko marekani kwenye hospitali ya  jimbo la Texas ambapo kwa mara ya kwanza kisa cha kuwepo kwa ugonjwa huo kiliripotiwa baada ya Thomas Dancun raia wa Liberia kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

    Baadae Thomas Dancun alifariki dunia oct 8 akiwa chini ya uangalizi wa wahudumu wa afya kwenye kituo cha Texas Presbyterian

    mgonjwa huyo ambae jina lake halikutajwa kuna uwezekano mkubwa alipata virusi hivyo wakati akimuhudumia Texas Presbyterian

    Kwa mujibu wa Daktari David Lakey ambaye ni kamishna wa idara ya afya katika jimbo la Texas amethibitisha kutokea tukio na kusema kwamba ”Tulijua kuna uwezekano wa kisa cha pili kuripotiwa na tumejitayarisha kwa uwezekano huo”

    MAREKAN

     

  • MSUMBIJI YAFANYA UCHAGUZI MKUU WA RAIS NA WABUNGE

    MSUMBIJI YAFANYA UCHAGUZI MKUU WA RAIS NA WABUNGE

    Wapiga kura wanaelekea kwenye vituo vya kupigia kura nchini Musumbiji leo kumchagua rais mpya na wabunge kwenye uchaguzi wenye upinzani mkali tangu taifa hilo lipate uhuru mwaka 1975.

    Takriban watu 11 wamejiandikisha kupiga kura nchini humo wakiwemo wengine 90,00 wanaoishi mataifa ya kigeni.

     

    141014160822_mozambique_election_512x288__nocredit

     

    Zaidi ya watu milioni 10 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa leo, ambao unaonekana kuwa wa kwanza kidemokrasia tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Wareno mwaka 1975.

    Chama tawala, cha Frelimo, ambacho kimekuwa mamlakani tangu mwaka 1975, kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa chama cha upinzani cha Renamo.

     

    141015074418_moza_3
    Rais Arrnando Guebuza (kushoto) na muasi wa zamani wa Renamo Afonso Dhlakama walifikia mkataba wa amani Septemba

     

     

     

     

     

     

     

     

    Kiongozi wa Renamo,Afonso Dhlakama, alitoka mafichoni mwezi jana na kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu katika dakika za mwisho baada ya kufikia makubaliano ya amani na serikali.

    Mgombea wa chama tawala ni Filipe Nyusi, ambaye ni waziri wa zamani wa ulinzi.

    Msumbijini moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi barani Afrika na mshindi wa uchaguzi atahakikisha rasilimali za nchi ikiwemo gesi zinatumiwa vyema.

     

     

     

     

     

     

  • TOYOTA YAAGIZA MAGARI MILIONI MOJA YARUDISHWE KIWANDANI

    TOYOTA YAAGIZA MAGARI MILIONI MOJA YARUDISHWE KIWANDANI

    toy_showroom_lg

    Kampuni kubwa zaidi ya kuunda magari, Toyota, imeagiza kurejeshwa kwa magari milioni moja nukta saba kote duniani kutokana na hitilafu ya breki za magari hayo.

    Kampuni hiyo imesema hitilafu tatu zimetambulika kwenye breki katika miundo mbali mbali za magari ya Toyota ikiwemo muundo wa Lexus.

    Magari yaliyo ndani na nje ya Japan yote yameathiriwa na hitilafu hizo.

    Hata hivyo kampuni yenyewe imesema haina habari yoyote kuhusu ajali za magari au watu kujeruhiwa kutokana na hitilafu hizo.

    Wadadisi wanasema hili ni jambo la kuaibisha sana kwa Toyota ambayo imelazimika kuagiza magari yake kurejeshwa kiwandani zaidi ya mara moja kutokana na hitilafu mbali mbali.