Category: Global News

  • MFANYAKAZI WA UN ALIEAMBUKIZWA EBOLA AFARIKI UJERUMANI

    MFANYAKAZI WA UN ALIEAMBUKIZWA EBOLA AFARIKI UJERUMANI

    Madaktari katika hospitali ya Leipzig wamesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 56, alifariki dunia mapema Jumanne asubuhi.

    Mlipuko huo umeua zaidi ya watu 4,000 tangu mwezi Marchi, mwaka huu hususan katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria.

    Shirika la Afya Duniani limeuelezea ugonjwa huo kama tatizo la dharura la kiafya kuwahi kuonekana katika maisha ya sasa ya binadamu. Marekani na Uingereza ni miongoni mwa nchi zilizoanzisha utaratibu wa upimaji afya za abiria kuhusiana na ugonjwa wa Ebola katika viwanja vya ndege.

    Mtu huyo alikuwa akifanyakazi kama afisa wa afya wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia- moja ya nchi zilizoathirika zaidi na maambukizi ya ugonjwa huo Afrika Magharibi- wakati alipoambukizwa Ebola.

    Upimaji wa hali ya joto mwilini

    Aliwasili Ujerumani Alhamisi iliyopita kwa ajili ya matibabu na aliwekwa katika kitengo maalum cha uangalizi.

    “Licha ya matibabu ya kina na jitihada za hali ya juu za madaktari katika kumhudumia mwaajiriwa huyo wa Umoja wa Mataifa, hawakuweza kunusuru maisha yake kutokana na maambukizo makubwa”. Imesema taarifa kutoka hospitali ya St Georg.

    Wafanyakazi wa Afya wako katika hatari kubwa ya maambukizo.

  • GERRIE NEL AMPINGA MARINGA KWENYE KESI YA PISTORIUS

    GERRIE NEL AMPINGA MARINGA KWENYE KESI YA PISTORIUS

    Idara ya kurekebisha tabia nchini Afrika Kusini inataka Oscar Pistorius apewe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu kwa kumpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

    Bwana Joel Maringa afisa anayehusika na masuala ya urekebishaji tabia aliiambia mahakama mjini Pretoria kuwa hawamuadhibu tu Pistoruiis bali pia wanataka kumbadili kitabia akisema kuwa anaweza kutoa huduma za jamii kwa saa 16 kwa mwezi.

    Awali daktari wa Pistorius anayehusika na matatizo ya akili Lore Hartzenberg aliiambia mahakama kuwa mwanariadha huyo mlemavu amevunjika moyo baada ya kumuua mpenziwe.

    Shahidi wa tatu ambaye ni meneja wa shirika la Pistorius la Peet Van Zyl aliiambia mahakama kuhusu orodha ya huduma zake zikiwemo za shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa kama balozi mwema. Kesi hiyo inatarajiwa kuchukua muda wa siku tatu.

    Kwa upande wake mwendesha mashitaka Gerrie Nel ameelezea pendekezo hilo la Bwana Maringa kuwa “linashtua na si sahihi”akisema zaidi kuwa ingekuwa bora kusiwe na adhabu kabisa, huku akihoji kama Bwana Maringa alijua ukubwa wa kosa la Pistorius.

    Baba wa Bi Steenkamp, Barry, alishika kichwa wakati Bwana Maringa akizungumza, huku marafiki wa marehemu wakitikisa vichwa kwa mshangao wa kile kilichoelezwa na Bwana Maringa.

    Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua Bi Steenkamp bila kukusudia mwezi uliopita -lakini aliondolewa mashitaka ya kuua.

    Uamuzi huo ulishutumiwa na ndugu wa familia ya marehemu.

    Pistorius anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela, japokuwa Jaji Thokozile Masipa anaweza kuondoa kifungo hicho au kumtoza faini.

    Amesema mwanariadha huyo alifanya “uzembe” wakati alipompiga risasi mpenzi wake kupitia mlango wa choo, akidhani ni mhalifu kutoka nje.

     

  • HOFU YA EBOLA YATANDA MAREKANI

    HOFU YA EBOLA YATANDA MAREKANI

    Uongozi wa rais Barack Obama wa Marekani umetoa wito wa kuwepo hali ya utulivu kufuatia kupatikana kwa mgonjwa wa ebola nchini kwake.

    Taarifa zinasema Marekani inajiandaa kupambana na mzozo wa ugonjwa wa ebola kote nchini mwake na katika eneo.

    Milipuko wa ugonjwa wa ebola kwa miaka 40 iliyopita ilidhibitiwa. Marekani inatuma vikosi elfu mbili nchini Liberia kusaidia kupambana na mlipuko wa ebola ambao umeuwa takriban watu elfu tatu katika bara la Afrika magharibi.

    Marekani pia inajaribu kuondoa hofu kuhusu kuzuka kwa ugonjwa wa ebola nchini mwake.

    Raia wa Liberia Thomas Duncan yuko katika hali mbaya lakini inayoweza kudhibitiwa katika hospitali moja kwenye jimbo la Texas baada ya kuambukizwa virusi vya ebola kabla ya kuondoka Liberia kuingia marekani.

     

    ebola

  • HATIMAE KENYATTA AIKABILI ICC LEO NA KUWEKA REKODI

    HATIMAE KENYATTA AIKABILI ICC LEO NA KUWEKA REKODI

    Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.

    Yeye ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya mahakama hiyo.

    Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi muhimu.

    Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.

    Kikao cha leo kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi mahakama hiyo ushahidi unaohitajika kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.

    Upande wa utetezi nao unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea.

    Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda, amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko katika awamu muhimu sana.

    Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea kwa niaba yake.

     

  • PAPA APOKEA TAARIFA YA KUJIHUZURU KWA ASKOFU KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAPENZI

    PAPA APOKEA TAARIFA YA KUJIHUZURU KWA ASKOFU KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAPENZI

    Baba Mtakatifu Francis amekubali kujiuzulu kwa Askofu Kieran Conry kutoka majimbo ya Arundel na Brighton baada ya kupokea barua ya Askofu huyo alieomba radhi mara baada ya taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari

    Conry, mwenye umri wa miaka 64, aliomba radhi katika barua kwa kutokuwa mwaaminifu kwa ahadi yake kama kuhani Katoliki lakini alisisitiza matendo yake yalikuwa si ​​kinyume cha sheria na hawakuwa kuhusisha watoto.

    Kanisa katoliki limekuwa likipata shinikizo juu ya kubadilisha tamaduni hivyo kuwaruhusu watumishi hao kuingia kwenye mahusiano lakini kanisa katoliki bado linaendelee na msimamo wake kwa kuyazingatia mafundisho hayo

  • RAIS KENYATTA NIPO RADHI KWENDA ICC

    RAIS KENYATTA NIPO RADHI KWENDA ICC

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili.

    Akiwahutubia wabunge mjini Nairobi,aliwaambia kuwa yuko tayarti kuhudhuria kikao maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote.

    Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai kuwa serikali yake imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili.

    KENYATA12Anakabiliwa na tuhuma za kupanga ghasia za kikabila zilizokumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.

    Aliarifu bunge kuwa anajiamini mwenyewe kiasi cha kuwa tayari kufika mbele ya ICC na kwamba anajua hana hatia katika kesi inayomkabili.

    Alisema Kenya ni nchi huru na kwamba haitawahi kuwa chini ya mamlaka nyingine yoyote.

    KENYATA RUTO
    Kenyatta na naibu Rais William Ruto ambaye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama ya ICC
  • MGONJWA WA EBOLA ABAINIKA HISPANIA

    MGONJWA WA EBOLA ABAINIKA HISPANIA

    Uchunguzi unaendelea katika hospitali ya Madrid nchini Hispania kutokana na muuguzi mmoja nchini humo kuwa mtu wa kwanza kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola anaodaiwa kuwa aliambukizwa virusi vya ugonjwa huo kutoka nchi za Afrika Magharibi.

    EBOLA MADRID

    Muuguzi huyo alikuwa miongoni mwa kikosi cha madaktari waliowatibia raia wamisionari wawili waliokufa kutokana na ugonjwa huo baada ya kurejeshwa nyumbani kwao wakitokea nchi za Afrika Magharibi.

    Hata hivyo hospitali hapo kwa sasa kuna uangalizi mkubwa huku vifaa vya kujikinga na vifaa vya kiafya ili kuzuia maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

    zaidi ya watu 3000 kutoka Afrika Magharibi wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola katika mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea hivi karibuni.

     

  • Uchaguzi kuingia duru ya pili Brazil

    Uchaguzi kuingia duru ya pili Brazil

    Huku zaidi ya asilimia 97 ya kura zilizopigwa zikiwa zimehesabiwa kwenye uchaguzi mkuu nchini Brazil, rais Dilma Roussef ameshinda awamu ya kwanza ya kura hizo, lakini bado hajapa ushindi unaohitajika ili kuzuia kuwepo duru ya pili.

    Mpinzani wake wa karibu Aecio Neves amechukua nafasi ya pili.

    Matokeo haya hata hivyo yanamaanisha kuwa mgombea mwingine ambaye ni waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva ameondolewa kwenye kinyanganyiro hicho hata baada ya kuonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa rais wa Brazil.

    Takriban watu milioni 150 walipiga kura katika uchaguzi wa saba wa nchi hiyo tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1985.

     

    brazil2

    Bi Rousseff aliendesha kampeni yake akitumia rekodi yake ya kubuni programu ambazo zimesaidia kukwamua mamilioni ya watu kutoka umaskini nchini Brazil.

    Cha kushangaza zaidi katika uchaguzi huu ni dalili ya kupoteza uungwaji mkono kwa waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva.

    Mwezi mmoja uliopita Bi Silva alikuwa aking’aa kwenye kura ya maoni baada ya kuchukua usukani kama mgombea wa urais kupitia kwa chama cha Kisoshiolisiti kufuatia kuaga dunia kwa mgombea mwenza kwenye ajali ya ndege.

    Lakini mijadala yake isiyo ya kuridhisha na pia uamuzi wa wapiga kura wa kutotaka kupigia kuya vyama vya zamani ina maana kuwa Bi Silva amendoka kabisa kwenye kinyanganyiro hicho.

  • WANAFUNZI 40 MEXICO WAPOTEA

    WANAFUNZI 40 MEXICO WAPOTEA

    Mamia ya wanafunzi nchini Mexico katika jimbo la Guerrero wameandamana katika mji mkuu wa jimbo la Chilpancingo kulalamikia kutoweka kwa zaidi ya wanafunzi wenzao arobaini wiki iliyyopita.

    Wanafunzi hao wanasemekana kuwa mwisho walionekana kusombwa katika magari ya polisi kufuatia maandamano walioshiriki wakilalamikia ubaguzi katika ajira ya walimu wa maeneo ya vijijini.

    Polisi walifyatua rissasi kwenye basi na kwa waandamaji na kuua watu sita na wengine 17 kujeruhiwa.

    Maafisa ishirini na wawili wa polisi wanashikiliwa na kwa kutuhuma za kufyatua risasi.

    Ndugu ya waliouawa wanaosaidiwa na polisi waliingia mlango kwa mlango katika eneo la Iguala wakiwa wameshikilia picha za wapendwa wao na kutafuta eneo ambalo miili ya ndugu zao ilipofichwa. Serikali ya jimbo hilo imetoa dola 75,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa kueleza wanafunzi hao walipo.

     

  • WANAFUNZI KUMSHTAKI MKE WA RAIS MUGABE

    WANAFUNZI KUMSHTAKI MKE WA RAIS MUGABE

    Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Zimbabwe al maarufu Zinasu, umesema kwamba unawasilisha kesi mahakamani hii leo kutafuta ufafanuzi zaidi wa namna mkewe rais Grace Mugabe alivyopata shahada ya udaktari wa falsafa.

    140929113157_grace_mugabe_512x288_bbc_nocredit
    Bi. Grace Mugabe kulia

    Mwanafunzi mmoja mwanaharakati amesema kuwa ni muhimu kwa taifa hilo kuhifadhi hadhi yake ya elimu.

    Baadhi ya watu wamehoji kasi aliyosomea shahada hiyo huku wengine wakidai ni njama za kumuandaa kwa urithi wa kiti cha rais baada ya rais Mugabe.

    Gazeti moja linalomilikiwa na serikali , the Herald limechapisha kuwa Bi Grace Mugabe alipata shahada hiyo kwa utafiti wake juu ya mabadiliko ya mfumo wa kijamii na miundo ya familia.

     

  • HOFU YA EBOLA YATANDA MAREKANI

    HOFU YA EBOLA YATANDA MAREKANI

    Hali hiyo imekuja mara baada ya Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola kugundulika nchini Marekani, na kuthibitishwa katika mji wa Dallas, Texas.

    Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.

    ebola_suit
    watoa huduma wa afya

    Jumatatu, maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.

    Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.

    Nchini Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19 waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watu wanane wamekufa tangu mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai..

    Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.

    Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.