MAN UNTD NAMBARI 5 KWA UTAJIRI DUNIAN

MAN UNTD NAMBARI 5 KWA UTAJIRI DUNIAN

Like
312
0
Thursday, 14 July 2016
Slider

Klabu ya Manchester United imeorodheshwa ya tano kwa utajiri duniani na jarida la Forbes, thamani yao ikiwa imepanda kwa asilimia saba.

Klabu ya NFL, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011.

United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya $3.32bn (£2.52bn).

Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na Barcelona wa tatu $3.55bn (£2.69bn).

United, klabu pekee ya Uingereza katika orodha hiyo, walisaidiwa sana na mkataba wao wa £750m na Adidas, jambo lililoongeza thamani yao licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Hata hivyo, Manchester United, ndio wenye deni kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizo katika 25 bora.

Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na Liverpool (41) ndizo klabu hizo nyingine za Uingereza zilizofanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo.

Comments are closed.