Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali aliyemwakilisha Dkt. Yamungu Kayandabila Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha akifungua semina ya siku tano ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu masuala ya uchumi na fedha inayofanyika kwenye ukumbi wa (BOT) jijini Dodoma.
Katika semina hiyo wanahabari watapata ufafanuzi wa masuala yanayoshughulikiwa na benki hiyo pamoja na mabenki ya biashara ya kifedha nchini Tanzania kwa kufuata sheria kanuni na taratibu zinazosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na kushoto ni Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT).










Leave a Reply