Taasisi ya The Neghesti Sumari yakutanisha wanawake kwenye mjadala wa usawa wa kijinsia

Taasisi ya The Neghesti Sumari yakutanisha wanawake kwenye mjadala wa usawa wa kijinsia

Like
385
0
Wednesday, 09 March 2016
Local News

Taasisi ya The Neghesti Sumari iliwakutanisha wanawake kwenye mjadala kuhusu usawa wa kijinsia uliofanyika kwendana na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Kwenye mjadala huo uliofanyika Buni Hub kwenye jengo la COSTECH jijini Dar es Salaam,  watoa mada walikuwa ni pamoja na mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Anna Mghwira,  Profesa Esther Mwaikambo, muanzilishi wa taasisi ya Doris Mollel na  mjasiriamali na mtaalam wa masuala ya uchumi na Monica Joseph.

Akizungumza kwenye mjadala huo, Mama Mghwira alisema alijifunza kujitegemea mapema sana kwa kujua thamani ya pesa na kwamba usawa wa kijinsia ni usawa wa fursa kati ya wanawake na wanaume.

Bi. Mghwira alikuwa mgombea pekee wa kike wa urais mwaka 2015.

Kwa upande wake Prof. Mwaikambo miongoni mwa mambo aliyosema ni: Enzi zangu za kusoma wanafunzi wote walikua very serious, enzi zetu tulisoma kwa shida, lakini tulisoma, tofauti na sasa. Maishani mwangu niko very committed katika masuala ya msingi. Nilikua najua nataka nini. Nilijua nilikokua natoka.  Mimi nilitaka kuwa daktari kutokana na mama yangu kufariki nikiwa na miaka kumi kwa ugonjwa usiojulikana.  Nasisitiza kwa wazazi kuhakikisha watoto wote wa kike Na kiume wanapata elimu nzuri kuwawewezesha baadaye. Elimu itawawezesha wanawake kupata kila kitu maishani.

Kwa upande wake Doris Mollel alisema usawa utapatikana pale tu utaanza kuzingatiwa katika kazi ya familia.

Kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka huu ni “50 – 50 Ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada.”

MATUKIO KATIKA PICHA

6

5

3

2

index

9

7

Comments are closed.