Author: EFM

  • WANAFUNZI 40 MEXICO WAPOTEA

    WANAFUNZI 40 MEXICO WAPOTEA

    Mamia ya wanafunzi nchini Mexico katika jimbo la Guerrero wameandamana katika mji mkuu wa jimbo la Chilpancingo kulalamikia kutoweka kwa zaidi ya wanafunzi wenzao arobaini wiki iliyyopita.

    Wanafunzi hao wanasemekana kuwa mwisho walionekana kusombwa katika magari ya polisi kufuatia maandamano walioshiriki wakilalamikia ubaguzi katika ajira ya walimu wa maeneo ya vijijini.

    Polisi walifyatua rissasi kwenye basi na kwa waandamaji na kuua watu sita na wengine 17 kujeruhiwa.

    Maafisa ishirini na wawili wa polisi wanashikiliwa na kwa kutuhuma za kufyatua risasi.

    Ndugu ya waliouawa wanaosaidiwa na polisi waliingia mlango kwa mlango katika eneo la Iguala wakiwa wameshikilia picha za wapendwa wao na kutafuta eneo ambalo miili ya ndugu zao ilipofichwa. Serikali ya jimbo hilo imetoa dola 75,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa kueleza wanafunzi hao walipo.

     

  • LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA WIKIENDI HII

    LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA WIKIENDI HII

    Kivumbi cha ligi kuu soka Tanzania bara kinaendelea tena wikiendi hii kwa timu kumi kushuka katika madimba matano tofauti,ambapo katika uwanja wa taifa jijini wenyeji simba watawakaribisha vijana toka shinyanga-stand united,Mtibwa dhidi ya mgambo jkt,ruvu shooting dhidi ya mbeya city,prisons na azam na polisi morogoro wakikipiga dhidi ya kagera.

  • TFF YATANGAZA DHAMIRA YA KUVIKATA VILABU VYA LIGI KUU ASILIMIA TANO YA FEDHA

    TFF YATANGAZA DHAMIRA YA KUVIKATA VILABU VYA LIGI KUU ASILIMIA TANO YA FEDHA

    Kamati ya utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF,jana tarehe 2 oct imetamka hadharani kuwa inadhamira ya kweli ya kuvikata vilabu vya ligi kuu asilimia 5 ya fedha za mdhamini,na kwamba yeyote anayepinga agizo hilo anajisumbua.

    Hatua ya tff,kujitokeza hadharani kutoa msimamo wake,imekuja baada ya umoja wa vilabu kumteua mwanasheria atakayewakingia kifua kupinga agizo hilo,ambalo wanaliona kama unyonyaji kwenye kiasi kidogo wanachokipata toka kwa mdhamini wa ligi.

    Tayari kwa upande wake bodi inayosimamia ligi kuu na ile ya daraja la kwanza Tanzania bara,imeshaweka wazi kuwa msimamo wake ni kutaka vilabu hivyo visikatwe hiyo asilimia tano kama tff inavyotaka.

    Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za shirikisho,rais wa tff Jamal Malinzi,amesema bodi ya ligi itake isitake ni lazima kutekeleza agizo hilo la kuvikata vilabu asilimia tano ya fedha toka kwa mdhamini.

  • SERIKALI IMEFANIKIWA KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO

    SERIKALI IMEFANIKIWA KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO

     

    Serikali imefanikiwa kupunguza tatizo la Vifo vya Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 kutoka vifo 165 hadi kufikia vifo 54 ikiwa ni mojawapo ya malengo waliowekewa na Umoja wa Mataifa,Zaidi Dokta DONAN MMBANDO anafafanua

    Kwa upande wake MONIKA MALLOMO ambaye ni Daktari wa watoto kutoka hospitali ya Sokoine Mkoani Lindi, amesema

     

  • SERIKALI IMEAHIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZINAZOLIKABILI JESHI LA ZIMA MOTO

    SERIKALI IMEAHIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZINAZOLIKABILI JESHI LA ZIMA MOTO

     

    Serikali imeahidi kushughulikia changamoto zinazolikabili Jeshi la Zima Moto na Uokoaji nchini ili kuliwezesha kutekeleza maajukumu yake kwa kuzingatia ongezeko la Ajali za Barabarani ambapo jeshi hilo pia lina jukumu la uokoaji katika Ajali mbalimbali.

    Akizungumza katika uzinduzi wa baraza dogo la zima moto na uokoaji mjini Bagamoyo Mkoani Pwani, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi MUBARAKA ABDULWALIKI amesema

     

  • WANAFUNZI ELIMU YA JUU WAIOMBA SERIKALI KUTOA MIKOPO BILA KUGAWA MATABAKA

    WANAFUNZI ELIMU YA JUU WAIOMBA SERIKALI KUTOA MIKOPO BILA KUGAWA MATABAKA

    Wanafunzi wa Elimu ya juu nchini wameiomba Serikali kuhakikisha kuwa Wanafunzi wote wenye sifa ya Elimu ya Kati –Diploma wanapewa mikopo kama ilivyo kwa wanafunzi wanaosoma Kada nyingine mbalimbali katika Elimu ya juu.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Elimu ya Juu –TAHLISO MUSSA MDEE amesema

     

  • AKON AFANYA SHOW NDANI YA PUTO KUEPUKA EBOLA!

    AKON AFANYA SHOW NDANI YA PUTO KUEPUKA EBOLA!

    Msanii kutoka Senegal mwenye mafanikio makubwa duniani aishie kikazi huko Marekani hivi karibuni amezua mijadala juu ya mtindo wake wa kufanya show ndani ya puto kubwa

    Akon alifanya hivyo kwenye show yake ya huko Goma Congo mwezi uliopita katika maazimisho ya siku ya amani duniani.

    akon2
    Akon kwenye moja ya show zake huko Montreal Canada

    lakini pia Akon alionekana kwenye moja ya show zake huko Canada, wachunguzi wa mambo wanasema huenda ikawa sehem ya kampeni yake ya AKON LIGHTING  AFRICA ambapo sio chini ya makazi milioni moja yatapatiwa huduma ya umeme kupitia mradi huo

     

  • SHINIKIZO LA NDOA LAVUNJA UCHUMBA WA JORDIN SPARKS NA JASON DERULO

    SHINIKIZO LA NDOA LAVUNJA UCHUMBA WA JORDIN SPARKS NA JASON DERULO

    kupitia mtandao wa TMZ mwimbaji Jordan Sparks amedai kuwa chanzo cha kuvunjika kwa mahusino ya wawili hao yaliyodumu kwa muda wa miaka mitatu ni kitendo cha yeye kudai ndoa baina yao ili kuhalalisha mapenzi yao.

    Jordan aliongeza kwa kusema kuwa haitaji kuwepo kwa aina yeyote ya mikwaruzano ama kusemana vibaya kati yake na aliyekuwa mpenzi wake na ndio maana aliamua kukaa kimya

     

  • JUSTIN BIEBER AMPIGA NGUMI MWANDISHI PARIS

    JUSTIN BIEBER AMPIGA NGUMI MWANDISHI PARIS

    Tukio hilo limetokea wakati Bieber na kundi la watu wake wakaribu wanaingia hotelini baada ya chakula cha usiku kwenye moja ya hoteli za huko Paris

    picha inamuonyesha Justin Bieber akiwa katikati ya mapaparazi wakikwaruzana wakati anataka kupita katika eneo hilo kitendo kilichopelekea arushe ngumi kwa mmoja wa wapiga picha.

    mwanamuziki huyo amekuwa akiandamwa na kesi za mara kwa mara ambapo  siku chache nyuma alituhumiwa kugonga Min Van ya mwanahabari.

  • UKAWA YALAANI UKIUKWAJI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

    UKAWA YALAANI UKIUKWAJI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

    Kamati ya Ufundi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi -UKAWA imetoa tamko la kulaani Ukiukwaji wa Kanuni za Bunge Maalum la Katiba linaloendelea mjini Dodoma pamoja na kulaani shutma dhidi ya viongozi wa dini zinazotolewa na Bunge hilo kuwa nao wamejiunga na UKAWA.

    Kauli hiyo imetolewa na  Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara Mheshimiwa JOHN MNYIKA wakati Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam

    Naye Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mwanasheria wa CHADEMA Mheshimiwa TUNDU LISSU alifafanua kwa upande wake.

    Mh. Mnyika akizungumzia swala hilo

  • WANANCHI WAMETAKIWA KUTUMIA VYEMA MIUNDOMBINU YA NCHI IKIWEMO BARABARA

    WANANCHI WAMETAKIWA KUTUMIA VYEMA MIUNDOMBINU YA NCHI IKIWEMO BARABARA

    Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Rais JAKAYA KIKWETE wakati akifungua rasmi barabara ya Mwenge –Tegeta.

    Naye Balozi wa Japani nchini MASAKI OKADA amezungumzia juu ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali yake na Tanzania

    kikwete3

     

    Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 imegharimu kiasi cha Sh. bilioni 77.85, fedha
    ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa
    la JICA. Serikali ya Tanzania imechangia asilimia 7.64 katika gharama za ujenzi
    wa Barabara hiyo.

    kikwete
    Mh.Rais akifungua barabara

    Katika ufunguzi wa barabara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam SAIDI MECK SADIKI amesema kuwa hali hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa magari.

    Naye Mhandisi Mkuu wa TANROAD PATRICK MFUGALE amesema ujenzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta imejengwa kwa kiwango chenye ubora