Author: EFM

  • WANAFUNZI KUMSHTAKI MKE WA RAIS MUGABE

    WANAFUNZI KUMSHTAKI MKE WA RAIS MUGABE

    Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Zimbabwe al maarufu Zinasu, umesema kwamba unawasilisha kesi mahakamani hii leo kutafuta ufafanuzi zaidi wa namna mkewe rais Grace Mugabe alivyopata shahada ya udaktari wa falsafa.

    140929113157_grace_mugabe_512x288_bbc_nocredit
    Bi. Grace Mugabe kulia

    Mwanafunzi mmoja mwanaharakati amesema kuwa ni muhimu kwa taifa hilo kuhifadhi hadhi yake ya elimu.

    Baadhi ya watu wamehoji kasi aliyosomea shahada hiyo huku wengine wakidai ni njama za kumuandaa kwa urithi wa kiti cha rais baada ya rais Mugabe.

    Gazeti moja linalomilikiwa na serikali , the Herald limechapisha kuwa Bi Grace Mugabe alipata shahada hiyo kwa utafiti wake juu ya mabadiliko ya mfumo wa kijamii na miundo ya familia.

     

  • PETER OKOYE WA P SQUARE AANGUKA JUKWAANI

    PETER OKOYE WA P SQUARE AANGUKA JUKWAANI

    Muimbaji kutoka kwenye kundi la P square Peter Okoye jana alianguka jukwaani siku ya jumanne usiku  wakati anatumbuiza kwenye tamasha lililoandaliwa na Beat 99.9 FM’s Triple 9 huko Lagos Nigeria

    tulio hilo lilitokea wakati P square wanaimba wimbo wao “BRING IT ON”   kutoka kwenye albam yao ya ‘Double Trouble’ wakati Peter aliposogea mbele kwenye ukingo wa jukwaa

    Peter-Okoye-falls2
    peter akiwa chini bada ya kuanguka

     

     

     

     

     

     

     

     

     

     

    baada ya show hiyo Peter aliandika kwenye kurasa zake za Twitter na Instagram maneno yafuatayo

    I fell off on stage and it wasn’t funny… Like we said” keep ur head up high and standing tall… I will surely bring it on” #sadFace #headingToTheHospital love u all!”

     

    peter

     

  • HOFU YA EBOLA YATANDA MAREKANI

    HOFU YA EBOLA YATANDA MAREKANI

    Hali hiyo imekuja mara baada ya Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola kugundulika nchini Marekani, na kuthibitishwa katika mji wa Dallas, Texas.

    Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.

    ebola_suit
    watoa huduma wa afya

    Jumatatu, maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.

    Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.

    Nchini Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19 waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watu wanane wamekufa tangu mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai..

    Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.

    Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.

  • NICKI MINAJ KUHOST TUZO ZA  MTV EMA 2014

    NICKI MINAJ KUHOST TUZO ZA MTV EMA 2014

    Mkali wa Anaconda Nicki Minaj ametajwa na MTV kwamba mbali na kuperfom atakuwa  host wa awamu ya 20th kwenye tuzo za MTV EMA 2014 ambapo mapema baada ya kutangazwa Nicki alitweet kupitia akaunti yake ya Twitter akisema maneno haya

    So excited to announce that I will not only perform, but I have the honorable task of HOSTING this…

    tuzo hizi zinatarajiwa kufanyika huko Glasgow Uingeleza mapema mwezi November mwaka huu

  • DIAMOND ATAJWA KUWANIA TUZO ZA The Headies NIGERIA

    DIAMOND ATAJWA KUWANIA TUZO ZA The Headies NIGERIA

    Headies-Print-602x280

    Tuzo hizo ambazo hapo zamani zilijulikana kama Hip-Hop World ambapo kwa mara ya kwanza zilifanyika mwaka 2006 huko Lagos. mwaka huu zinatarajiwa kufanyika tarehe 25th October 2014  Lagos ikiwa ni msimu wake wa 9

    Diamond ametajwa kuwania kipengere cha  BEST AFRICAN ARTIST 

    kipengere hicho kinahusisha wasanii kutoka mataifa ya Afrika wanaofanya vizuri Nigeria

    Diamond atachuana na

    MAFIKIZOLO
    SARKODIE
    R2BEES

     

  • HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KIBAHA KWENYE KAMPENI YA BAR KWA BAR MUZIKI MNENE

    HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KIBAHA KWENYE KAMPENI YA BAR KWA BAR MUZIKI MNENE

    Picha ni umati wa wakazi wa kibaha na maeneo ya jirani waliokusanyika katika kampeni za redio EFM 93.7

    kampeni hii imekuwa ikiendelea maeneo tofauti kwa kuwakutanisha wafanyakazi yani watangazaji na ma rdj wa 93.7efm pamoja na wadau mbalimbali wa redio hii  na kuweza  kutoa zawadi mbalimbali kwa wananchi.

    kampeni hii wiki hii itakuwa maeneo ya Ukonga siku ya jumamosi muziki utaongea

    DU7C0164 DU7C0181 DU7C0306 DU7C0313 DU7C0328 DU7C0334

     

  • RAIS MPYA WA AFGHANSTAN ASAINI MKATABA NA NATO

    RAIS MPYA WA AFGHANSTAN ASAINI MKATABA NA NATO

    afughan2
    Ashraf Ghani rais mpya wa Afghanstan

    Siku moja baada ya kuapishwa kuwa rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani, serikali yake imetia saini mkataba mpya wa usalama na shirika la kujihami la NATO.

    Mkataba huo utaidhinisha zaidi ya wanajeshi elfu kumi na mbili, wengi wakiwa wamarekani, kusalia nchini Afghanistan hata baada ya kumalizika kwa kandarasi yao mwaka huu.

    Mkataba huo ulitiwa sahihi katika hafula iliyotangazwa moja kwa moja katika televisheni na mshauri wa maswala ya usalama wa kitaifa wa Afghanistan Hanif Atmar na balozi wa Marekani nchini humo Jim Cunningham, huku Rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani akishuhudia.

     

    afughan

    Rais aliyeondoka Hamid Karzai alikataa kwa muda mrefu kusaini mkataba wa kuwaongezea wanajeshi wa Marekani muda wa kukaa huko, na hivyo kusababisha mvutano kati yake na Marekani.

    Bwana Karzai alikuwa anasisitiza kuwa la muhimu zaidi ni kuanzisha mpango wa amani na kusitisha mapigano na wanamgambo wa Taleban.

    Vikosi vya NATO vimekuwa vikipunguzwa nchini Afghanistan na taratibu kurudisha udhibiti wa usalama wa nchi hiyo kwa vikosi vya Afghanistan.

     

  • MKUTANO WA KIMATAIFA WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO WAANZA RASMI JIJINI DAR

    MKUTANO WA KIMATAIFA WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO WAANZA RASMI JIJINI DAR

    chinaleo

    Mkurugenzi wa Kampuni ya Tekinologia ya Huawei Tanzania, Vincent

Wen(kushoto) akizungumza na washiriki katika mkutano huo.

    chinaleo2

    chinaleo3chinaleo3

    baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa

wa Tekinolojia ya Mawasiliano wakifatilia kwa makini mkutano huo ulioanza rasmi siku ya jana katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam kwa 

udhamini wa HUAWEI.

  • KAMPENI YA MUZIKI MNENE BAR KWA BAR NDANI YA BAGAMOYO

    KAMPENI YA MUZIKI MNENE BAR KWA BAR NDANI YA BAGAMOYO

    3

    umati wa watu huko bagamoyo wakicheza na kufurahi

    kwenye kampeni ya Muziki mnene bar kwa bar

    10679793_829111660466523_5055820328853436508_o

    Swebe moja ya watangazaji wa EFM akizungumza

    jambo na wakazi wa bagamoyo

    4

    Wananchi wa Bagamoyo wakijiachia kwa shagwe

    2

    kampeni hiyo bado inaendelea maeneo mbalimbali

  • Big Fendi, NICK MINAJ BADO YUPO CHINI YA DIRTY MONEY

    Big Fendi, NICK MINAJ BADO YUPO CHINI YA DIRTY MONEY

    Big Fendi_09-29-2014

    Aliekuwa meneja wa Msanii Nick Minaji, Big Fendi ameelezea kiundani jinsi alivyokutana na msanii huyo kati ya mwaka 2006 au2007 kupitia mtandao wa MySpace ambapo alimchukua na kumbadilisha jina kutoka Nicki Maraj kwenda Nicki Minaj kitendo kilichomsababishia Nick Minaj matatizo na familia yake lakini baadae Big Fendi alimuelewesha ikiwemo pia kumtumia Jadakiss na Busta Rhymes

    Fendi amedai kumiliki sehem ya jina na vyanzo vya mapato vya Nick ikiwemo NickiMinaj.com.

     

    Fendi Baadae alipata mkataba wa kumuuza nick Minaj kwenda Young money ambapo aliukataa kwa sababu za kimaslahi lakini pia alimkutanisha na Debra Antney kutoka Waka Flocka Flame ambae amedai kuwa chanzo cha kumbadilisha Nick kwa Kumshawishi aachane na Dirty money Company

    Big Fendi aliyasema hayo wakati anahojiwa kupitia Power 105.1’s The Breakfast Club

    http://youtu.be/MFsJmCFNslE

  • CRISS BROWN KWENYE UTATA NA TMZ

    CRISS BROWN KWENYE UTATA NA TMZ

    Chris-Brown

    Mkali wa ngoma zinayofanya vizuri kwa sasa New frame na loyal Criss brown jana kupitia mtandao wa Instagram alimtukana meneja wa TMZ mtandao unaotoa ripoti na tetesi za mastar huko marekani.

     

    tmz
    Harvey Levin C.E.O wa TMZ

     

     

     

     

     

     

     

     

     

    Criss brown alimtukana CEO . Harvey Levin kwa kumuita shetani na kumtaka aache kumfuatilia mara moja.

    Criss Brown amedai meneja huyo amekuwa akimfuatilia kwa miaka kadhaa kwa lengo la kumshusha. Hii inakuja siku chache baada ya mtandao huo kuchapisha habari inayosema mama mzazi wa Crisss brown anahofia usalama wa maisha ya mwanae kufuatia tuhuma za kujihusisha na makundi ya wahuni huko LA.