Author: EFM

  • JAMAL MALINZI AMESEMA YEYE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WAPO MADARAKANI KUENDELEZA SOKA NA SI MALUMBANO

    JAMAL MALINZI AMESEMA YEYE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WAPO MADARAKANI KUENDELEZA SOKA NA SI MALUMBANO

    SHIRIKISHO la kandanda Tanzania Tff,limesema mashindano ya taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12, yatafanyika mkoani mwanza kuanzia mwezi Desemba mwaka huu,ukiwa ni mpango maalumu unaolenga kupata kikosi imara cha kitakachoshiriki michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya 17 (U17), mwaka 2019, ambapo Tanzania imeomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

    Akizungumza na wanahabari hii leo kuelezea mpango huo, Rais wa TFF, Jamal Malinzi,amesema mashindano hayo yatashirikisha kombaini za mikoa yote Tanzania,lakini kwanza amenza kwa kusema yeye pamoja na kamati yake ya utendaji ipo madarakani kuendeleza soka na si kulumbana .

    Kwa upande wao mkurugenzi wa shule za Alliance,James Bwire, pamoja na Kanali mstaafu Idd Kipingu wa Lord Baden,wameridhia kwa kauli moja vituo vyao kutumika katika kuendeleza soka la Tanzania,na kipingu akisisitiza kuwa suala hili ni la watanzania wote.

    Mashindano hayo yatafanyika kuanzia Desemba 6 hadi 12 Mmwaka huu, na timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza, Desemba 5 mwaka huu. Bajeti ya mashindano hayo ni sh. milioni 350.

    Mkurugenzi wa Symbion, Stewart John Hall aliwasilisha kwa waandishi wa habari programu hiyo

  • RAIS KENYATTA NIPO RADHI KWENDA ICC

    RAIS KENYATTA NIPO RADHI KWENDA ICC

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili.

    Akiwahutubia wabunge mjini Nairobi,aliwaambia kuwa yuko tayarti kuhudhuria kikao maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote.

    Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai kuwa serikali yake imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili.

    KENYATA12Anakabiliwa na tuhuma za kupanga ghasia za kikabila zilizokumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.

    Aliarifu bunge kuwa anajiamini mwenyewe kiasi cha kuwa tayari kufika mbele ya ICC na kwamba anajua hana hatia katika kesi inayomkabili.

    Alisema Kenya ni nchi huru na kwamba haitawahi kuwa chini ya mamlaka nyingine yoyote.

    KENYATA RUTO
    Kenyatta na naibu Rais William Ruto ambaye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama ya ICC
  • MGONJWA WA EBOLA ABAINIKA HISPANIA

    MGONJWA WA EBOLA ABAINIKA HISPANIA

    Uchunguzi unaendelea katika hospitali ya Madrid nchini Hispania kutokana na muuguzi mmoja nchini humo kuwa mtu wa kwanza kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola anaodaiwa kuwa aliambukizwa virusi vya ugonjwa huo kutoka nchi za Afrika Magharibi.

    EBOLA MADRID

    Muuguzi huyo alikuwa miongoni mwa kikosi cha madaktari waliowatibia raia wamisionari wawili waliokufa kutokana na ugonjwa huo baada ya kurejeshwa nyumbani kwao wakitokea nchi za Afrika Magharibi.

    Hata hivyo hospitali hapo kwa sasa kuna uangalizi mkubwa huku vifaa vya kujikinga na vifaa vya kiafya ili kuzuia maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

    zaidi ya watu 3000 kutoka Afrika Magharibi wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola katika mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea hivi karibuni.

     

  • SERIKALI IMEWATAKA WANANCHI KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UJENZI MAENEO YA MJINI

    SERIKALI IMEWATAKA WANANCHI KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UJENZI MAENEO YA MJINI

    Katika kuadhimisha Siku ya makazi Duniani Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka Wananchi kufuata sheria na taratibu za ujenzi maeneo ya Mijini ili kuepuka na hasara pamoja na usumbufu wa kubomolewa makazi yao.

    Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Waziri wa Wizara hiyo Profesa ANNA TIBAIJUKA

     

    Amebainisha kuwa kupitia mradi wa kuboresha Miundombinu kwa kushirikiana na jamii kuna baadhi ya maeneo yameboreshwa

    Kauli mbiu isemayo, SAUTI KUTOKA MAKAZI DUNI.

  • SERIKALI KUFUNGA MITAMBO YA VIDEO CONFERENCE KATIKA OFISI ZAKE

    SERIKALI KUFUNGA MITAMBO YA VIDEO CONFERENCE KATIKA OFISI ZAKE

    Serikali imeahidi kufunga Mitambo ya Video Conference katika Ofisi za Halmashauri za Wilaya na Mikoa pamoja na Vituo vya Polisi vya Wilaya ili kurahisisha Mawasiliano na kupunguza gharama za vikao katika taasisi zake ifikapo mwaka 2015.

    Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa MAKAME MBARAWA

    Profesa MBARAWA amesema tayari Serikali imeunganisha baadhi ya Mikoa katika Mkongo wa Mawasiliano

    Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao -TAGLA CHARLES SENKONDO amesema mfumo huo wa umesaidia Watanzania

     

     

     

  • Uchaguzi kuingia duru ya pili Brazil

    Uchaguzi kuingia duru ya pili Brazil

    Huku zaidi ya asilimia 97 ya kura zilizopigwa zikiwa zimehesabiwa kwenye uchaguzi mkuu nchini Brazil, rais Dilma Roussef ameshinda awamu ya kwanza ya kura hizo, lakini bado hajapa ushindi unaohitajika ili kuzuia kuwepo duru ya pili.

    Mpinzani wake wa karibu Aecio Neves amechukua nafasi ya pili.

    Matokeo haya hata hivyo yanamaanisha kuwa mgombea mwingine ambaye ni waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva ameondolewa kwenye kinyanganyiro hicho hata baada ya kuonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa rais wa Brazil.

    Takriban watu milioni 150 walipiga kura katika uchaguzi wa saba wa nchi hiyo tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1985.

     

    brazil2

    Bi Rousseff aliendesha kampeni yake akitumia rekodi yake ya kubuni programu ambazo zimesaidia kukwamua mamilioni ya watu kutoka umaskini nchini Brazil.

    Cha kushangaza zaidi katika uchaguzi huu ni dalili ya kupoteza uungwaji mkono kwa waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva.

    Mwezi mmoja uliopita Bi Silva alikuwa aking’aa kwenye kura ya maoni baada ya kuchukua usukani kama mgombea wa urais kupitia kwa chama cha Kisoshiolisiti kufuatia kuaga dunia kwa mgombea mwenza kwenye ajali ya ndege.

    Lakini mijadala yake isiyo ya kuridhisha na pia uamuzi wa wapiga kura wa kutotaka kupigia kuya vyama vya zamani ina maana kuwa Bi Silva amendoka kabisa kwenye kinyanganyiro hicho.

  • SOULJA BOY KUKIKABILI KIFUNGO

    SOULJA BOY KUKIKABILI KIFUNGO

    Rapa kutoka nchini Marekani Soulja boy ambae wiki kadhaa nyuma alitupiana matusi na mwimbaji K michelle kupitia mtandao wa Twitter.

    hivi karibuni amekutwa na hatia ya kumiliki bunduki ya kijeshi kinyume cha sheria na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya aina ya bangi

    maafisa wapolisi wa huko LAPD Loss angels polis department wameeleza kuwa vitu hivyo alikutwa navyo rapa huyo chini ya kiti cha gari lake aina ya  Porsche Panamera ambapo rapa huyo alikamatwa eneo la tukio

  • JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KUFUATIA TAARIFA YA TMA

    JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KUFUATIA TAARIFA YA TMA

    Kufatia taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa -TMA juu ya kuwepo kwa mvua nyingi nchini, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limewataka wananchi kutoendelea na Ujenzi katika maeneo ya Mabondeni ili kuepusha usumbufu pindi mafuriko yanapotokea.

    Akizungumza na EFM ofisini kwake Kaimu Kamishina wa operesheni ya Zimamoti na Uokoaji jijini CHRISTOM MANYOLOGA amesema

    Akizungumzia namna ambavyo Jeshi hilo limejipanga na Majanga MANYOLOGA anasema

     

     

  • DAVID KAFULILA AIBANA IPTL,SERIKALI

    DAVID KAFULILA AIBANA IPTL,SERIKALI

    Serikali imetakiwa kutozuia Utoaji na Kujadiliwa Bungeni kwa Ripoti za Uchunguzi juu ya matumizi Mabaya ya Fedha za ESCROW Shilingi Bilioni 400 kilichofanywa kupitia Kampuni ya PAP na IPTL.

    Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mbunge wa Kigoma Kusini ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi Mheshimiwa

    DAVID KAFULILA

     

  • SHEDY CLEVER DIAMOND NI KITOVU CHA KAZI ZANGU ZA KIMATAIFA TIWA SAVAGE & K CEE

    SHEDY CLEVER DIAMOND NI KITOVU CHA KAZI ZANGU ZA KIMATAIFA TIWA SAVAGE & K CEE

    Mtayarishaji wa kazi za muziki wa Bongo fleva hapa nchini amezungumzia jinsi Diamond alivymuunganisha na Wasanii wa kimataifa na kuweza kufanya kazi nao.

    miongoni mwa wasanii hao ni Tiwa savage  pamoja na K cee wote kutoka Nigeria na mataifa mengine ya Africa, Shedy aliyasema hayo siku ya jana kwenye birthday ya Diamond

  • RONALDO MANCHESTER UNITED NI FAMILIA YANGU

    RONALDO MANCHESTER UNITED NI FAMILIA YANGU

    Mchezaji wa kimataifa kutoka  Portugal ambae nyota yake ilianza kung’aa na kutambulika zaidi duniani kupitia Club ya Manchester united Cristiano Ronaldo.

    hivi karibuni kumekuwa na tetesi juu ya uwezekano wa mchezaji huyo anaeichezea club ya Real Madrid kurudi Manchester united .

    Club ya Real Madrid imeonyesha msimamo wake juu ya mchezaji huyo kwa kumuhitaji kuendelea kukichapa hapo Santiago Bernabeu kwenye msimu wa kiangazi kitendo ambacho Ronaldo amekipokea kwa furaha taarifa hiyo na kusema anafurahi kuitumikia Club hiyo lakini pia aliwashukuru Manchester united kwa mapenzi ya dhati wanayomwuonyesha