Author: EFM

  • WATANZANIA LEO WANAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA MIAKA 15 TANGU KUFARIKI KWA HAYATI BABA WA TAIFA

    WATANZANIA LEO WANAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA MIAKA 15 TANGU KUFARIKI KWA HAYATI BABA WA TAIFA

    WATANZANIA leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere .

    Kufuatia maadhimisho hayo, Wananchi jijini Dar es salaam wamewataka viongozi wa serikali kufuata miongozo na maadili mbalimbali katika kujenga, kulinda na kudumisha amani ya Nchi.

    Akiongea na EFM mmoja wa wananchi amesema pamoja na juhudi za viongozi waliopo madarakani bado zipo changamoto mbalimbali.

    Hayati baba wa taifa Julius Nyerere alifariki Dunia Oktoba 14 mwaka 1999.

    ***

     

  • GERRIE NEL AMPINGA MARINGA KWENYE KESI YA PISTORIUS

    GERRIE NEL AMPINGA MARINGA KWENYE KESI YA PISTORIUS

    Idara ya kurekebisha tabia nchini Afrika Kusini inataka Oscar Pistorius apewe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu kwa kumpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

    Bwana Joel Maringa afisa anayehusika na masuala ya urekebishaji tabia aliiambia mahakama mjini Pretoria kuwa hawamuadhibu tu Pistoruiis bali pia wanataka kumbadili kitabia akisema kuwa anaweza kutoa huduma za jamii kwa saa 16 kwa mwezi.

    Awali daktari wa Pistorius anayehusika na matatizo ya akili Lore Hartzenberg aliiambia mahakama kuwa mwanariadha huyo mlemavu amevunjika moyo baada ya kumuua mpenziwe.

    Shahidi wa tatu ambaye ni meneja wa shirika la Pistorius la Peet Van Zyl aliiambia mahakama kuhusu orodha ya huduma zake zikiwemo za shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa kama balozi mwema. Kesi hiyo inatarajiwa kuchukua muda wa siku tatu.

    Kwa upande wake mwendesha mashitaka Gerrie Nel ameelezea pendekezo hilo la Bwana Maringa kuwa “linashtua na si sahihi”akisema zaidi kuwa ingekuwa bora kusiwe na adhabu kabisa, huku akihoji kama Bwana Maringa alijua ukubwa wa kosa la Pistorius.

    Baba wa Bi Steenkamp, Barry, alishika kichwa wakati Bwana Maringa akizungumza, huku marafiki wa marehemu wakitikisa vichwa kwa mshangao wa kile kilichoelezwa na Bwana Maringa.

    Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua Bi Steenkamp bila kukusudia mwezi uliopita -lakini aliondolewa mashitaka ya kuua.

    Uamuzi huo ulishutumiwa na ndugu wa familia ya marehemu.

    Pistorius anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela, japokuwa Jaji Thokozile Masipa anaweza kuondoa kifungo hicho au kumtoza faini.

    Amesema mwanariadha huyo alifanya “uzembe” wakati alipompiga risasi mpenzi wake kupitia mlango wa choo, akidhani ni mhalifu kutoka nje.

     

  • CRISS BROWN AONYESHA HOFU YAKE JUU YA EBOLA

    CRISS BROWN AONYESHA HOFU YAKE JUU YA EBOLA

    Criss Brown mapema leo asubuhi kuipitia mtandao wa twitter aliweka wazi mawazo yake juu ya ugonjwa wa Ebola kwa kusema kuwa

    “I don’t know … But I think this Ebola epidemic is a form of population control. Shit is getting crazy bruh.”

    akimaanisha kuwa yeye hajui ila anadhani janga la Ebola ni namna ya kudhibiti idadi ya watu, haya yanakuja siku chache mara baada ya mtu mmoja kugundulika na virusi vya ugonjwa huo nchini marekani

    baadhi ya watu wameichukulia kauli hiyo ya Criss Brown kama ni hali ya hofu aliyonayo mara baada ya ugonjwa kupenya kwenye taifa lao huku Afrika ya magharibi ikikadiliwa kupoteza zaidi ya watu elfu nne (400) kwa mujibu wa W.H.O tangu kuzuka kwa ugonjwa huo

    TWITER

  • TIWA SAVAGE AWA MUHUDUMU KWENYE KITUO CHA MAFUTA

    TIWA SAVAGE AWA MUHUDUMU KWENYE KITUO CHA MAFUTA

     

    Mwimbaji kutoka Nigeria Tiwa Savage mapema mwaka huu alichaguliwa kuwa balozi wa brand ya  Forte Oil Petroleum Company 

    mwimbaji huyo kutoka  323 Entertainment Records alipost picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa kwenye kituo cha mafuta akitoa huduma kwa wateja kama wahudumu wengine

    aina hii ya promotion imekuwa ikifanyika sehemu mbalimbali duniani ambapo watu maarufu yani mastar hutumika na makampuni waliyoingia nayo mikataba kushiriki kwenye shughuri tofauti ikiwemo za kijamii

    Wakati umefika pia kwa hapa nyumbani makampuni kuwekeza kwa wasanii ili kukuza vipato vyao lakini pia kuongeza ukubwa wa mauzo ya bidhaa husika

  • STEVE R&B AUAGA UBACHELA

    STEVE R&B AUAGA UBACHELA

    Msanii wa muziki wa kizazi kipya Steve r&b ameuaga ubachela baada ya kufunga ndoa na Naimana Kuyangana juzi Jumamosi, Oktoba 11

    Steve ambae hivi karibuni ameachia ngoma yake mpya aliyoipa jina la polepole ni miongoni mwa wasanii wachache wanaotumia muda mrefu kuachia kazi zao kwa kuzipa nafasi ziendelee kufanya vizuri

    kwa niaba ya timu nzima ya Efm 93.7 tunawatakia maisha mema yenye furaha na amani pia

    MkewaSteve
    mke wa Steve r&b Naimana Kuyangana
  • JUKATA YAWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI,KUISOMA NA KUILEWA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA

    JUKATA YAWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI,KUISOMA NA KUILEWA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA

    Jukwaa la Katiba Tanzania- JUKATA limewasihi wananchi kushiriki katika kuhamasishana na kupata Elimu itakayowawezesha Kuisoma na Kuielewa Katiba inayopendekezwa ili kujiandaa na zoezi la upigaji Kura za Katiba hiyo.

    Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa JUKATA- DEUS KIBAMBA

    Pia imesema inaunga mkono makubaliano kati ya Vyama vya Siasa na Mheshimiwa Rais juu ya kufanyika kwa kura ya maoni baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015

    Amesema kuwa ili uelimishaji ufanikiwe kwa kiasi kikubwa ni vyema kwa mamlaka husika kuwezesha upatikanaji wa kutosha wa nakala za katiba inayopendekezwa na rasimu ya katiba

     

  • WANANCHI WATOA MAONI YAO KUELEKEA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWL.NYERERE

    WANANCHI WATOA MAONI YAO KUELEKEA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MWL.NYERERE

     

    Kuelekea kuadhimisha siku ya Kumbukumbu Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu JULIUS NYERERE Taasisi ya Mwalimu Nyerere foundation, Makumbusho ya Taifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ wameandaa maonyesho na mdahalo wa kumuenzi Baba wa Taifa ili kujenga, kulinda na kudumisha amani ya nchi.

    Mdahalo huo pamoja na maonesho kwa pamoja vitafanyika katika jumba la Makumbusho jijini Dar es salaam kuanzia Oktoba 13 hadi 17 baadhi ya Watanzania wamekua na maoni tofauti juu ya namna ambavyo wanamkumbuka na kumuenzi Mwalimu Nyerere.

  • D’BANJ ATEULIWA KUWA BALOZI WA KWANZA WA APPLE/BEATS BY DRE AFRIKA

    D’BANJ ATEULIWA KUWA BALOZI WA KWANZA WA APPLE/BEATS BY DRE AFRIKA

    Msanii kutoka Nigeria D’banj amesaini mkataba wa kuwa balozi wa brand ya apple/beat by Dre

    D’banj ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza barani Afrika kuwa balozi wa bidhaa hiyo

    DBanj-Tedx-Conference-Beats-By-Dre-Music-October-BellaNaija-4-600x597

     

  • YAMEBAKI MASAA MACHACHE KUPIGA KURA ILI KUMWEZESHA MTANZANIA E.NAPOLEON KUSHIRIKI KWENYE MOVIE YA THE DRIVER

    YAMEBAKI MASAA MACHACHE KUPIGA KURA ILI KUMWEZESHA MTANZANIA E.NAPOLEON KUSHIRIKI KWENYE MOVIE YA THE DRIVER

    Ernest Napoleon ni Mtanzania MUIGIZAJI amefanya movie inayoitwa Going Bongo.
    Anahitaji Kura yako ili kushirikishwa katika filamu ya kampuni ya Forest Whitaker (Idi Amin, Last King of Scotland) inayoitwa “The Driver”.
    Unaombwa msaada wa ku SHARE habari hii pamoja na maelekezo ya jinsi ya kumpigia kura:
    1) TUMIA kompyuta badala ya simu kama inawezekana
    2) Bonyeza link hiyo hapo Bit.ly/castErnest kisha una log in kwa kutumia Facebook account.
    3) Unabonyeza “newest” Unasukuma kidogo.
    4) Unaibeba picha (drag) hadi kwenye kibox kilichopo juu na kuipachika.
    Tafadhalini fata maagizo ili kumnyanyua Mtanzania mwezetu, kwani kesho ndio mwisho wa kuchukua mahesabu ya upigaji kura yako. Mwisho wa kura ni usiku wa leo.
    forest
    ern

     

  • WIZ KID AZUNGUMZIA COLLABO YAKE NA CRISS BROWN

    WIZ KID AZUNGUMZIA COLLABO YAKE NA CRISS BROWN

     

    Mkali kutoka Nigeria Wiz kid Ayo amezungumzia collabo yake na Criss Brown kupitia Capital Extra ya Uingereza jumamosi iliyopita

    Wiz kid amesema kuwa anatarajia kuiweka ngoma hiyo ambayo amemshirikisha Criss Brown aliyoipa jina la African bad girl   kwenye Albam yake ijayo

  • ITAZAME VIDEO MPYA YA RICH MAVOKO BAADA YA PACHA WANGU

    ITAZAME VIDEO MPYA YA RICH MAVOKO BAADA YA PACHA WANGU

    Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rich mavoko jana kupitia mtandao wa instagram alipost picha zinazoonyesha uandaaji wa video yake mpya ikiwa ni siku chache baada ya kutoka South Afrika ambapo alifanya video ya wimbo wake wa Pacha wangu chini ya director Adam Juma

    mara kadhaa rich amekuwa akiulizwa kuhusu gharama za video hiyo inayoonekana kugharimu kiasi kikubwa cha pesa hata hivyo Rich mavoko hakuwahi kuweka wazi kwa kusema Adam Juma ndie anaefahamu gharama zake

    itazame teaser hapa

    Screenshot_2014-10-09-16-27-51-1