Author: EFM

  • Je Mugabe atamrithisha mkewe mamlaka?

    Je Mugabe atamrithisha mkewe mamlaka?

     

     

     

     

     

     

    MUGABE
    Rais Mugabe akiwa na mkewe bi.Grace Mugabe

    Hivi karibuni kumekuwa na swali ambalo linawatatiza watu wengi hususani raia wa Zimbabwe kufuatia mtukio ya rais wa nchi hiyo kumkabidhi mkewe nyazfa mbalimbali za juu kiutawala.

    Kuzaliwa kwa utawala wa kinasaba sio jambo jepesi kubashiri.

    Lakini wananchi wengi wa Zimbabwe kwa sasa wanaonekana kushawishika kuwa kuna uwezekano wa familia ya Mugabe kuingia katika orodha hiyo ya kurithishana madaraka.

    Rais Mugabe ana umri wa miaka 90. Mke wake, Grace, ana umri wa miaka 49.

    Uvumi wa kurithishana madaraka umekuwa gumzo la kisiasa nchini Zimbabwe kwa miaka mingi, lakini Grace Mugabe katika miaka ya karibuni ameibuka kama mtu ambaye ataweza kumrithi mumuwe madaraka ya uongozi wa nchi ya Zimbabwe.

    Watu wa nje wamesikia tabia ya mke wa Rais Mugabe ambaye ni karani muhtasi wake wa zamani kutuhumiwa kufanya manunuzi yasiyo na mpangilio na katika tukio lingine kumpiga ngumi mwandishi wa habari wa Uingereza huko Hong Kong; na kufanya mambo mengine ambayo yanavuka mpaka kama mke wa kiongozi.

    Vyombo vya habari vya Zimbabwe, kwa kulinganisha vimedhamiria kumjenga Bi Grace Mugabe kuwa mtu wa kujitolea kwake katika kazi za kijamii.

     

    MUGABE2

    “Wakati mume wake akiondoka ndiyo mwisho wake wa kazi ya uanasiasa, kama kweli kuna kazi ya aina hiyo” anasema mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Zimbabwe,anasema Ibbo Mandaza, akitupilia mbali wazo la kuendelea kuwa na utawala wa familia ya Mugabe.

    Nadharia nyingine ni kwamba Rais Mugabe anamjenga mke wake ili kuyayumbisha makundi yote ndani ya chama cha Zanu-PF, na kuimarisha nafasi yake ya urais.

    Dewa Mavhinga, kutoka Human Rights Watch, anaamini kuwa rais amefanya kosa kubwa kumleta mtu ambaye hana ujuzi wowote wa siasa.

    “Inaonyesha kuwa Rais Mugabe hamwaamini mtu yeyote karibu naye”Dewa Mavhinga.

     

     

     

  • CHINA YAONYA MATAIFA YA KIGENI KUTOINGILIA HONG KONG

    CHINA YAONYA MATAIFA YA KIGENI KUTOINGILIA HONG KONG

    china
    picha ni maelfu ya waandamanaji huko Hong kong nchini china

    Uchina imeonya kuwa  kuwa haitawavumilia wahaini kutoka nje ya nchi wanaounga mkono maandamano yasiyo halali nchini humo.

    Kundi lijulikanalo kama Occupy Central ndilo linalolengwa kwa sababu limekuwa likiunga mkono juhudi za maandamano ya maelfu ya watu wanaounga mkono kuimraishwa kwa Demokrasia nchini Uchina.

    Katika kile kinachoaminika kulenga maandamano yanayoendelea katika jimbo la Hong Kon, Uchina inaonya mataifa mengine yasijiingize kwa kila inachoamini na maswala ya ndani ya Uchina.Uchina mara kwa mara hutoa onyo kwa mataifa mengine yasijiingize katika jimbo hilo lake linalotaka kuendesha mambo yake kivyake.

    china
    polisi wakipambana na waandamanaji

    kauli hiyo ya serikali imekuja siku chache baada ya matamshi ya Chris Patten, aliyekuwa wakati mmoja Gavana wa Hong Kong, aliposema kwamba Uingereza ina wajibu wa kutoa taarifa kwa niaba ya wakazi wa Hong Kong, eneo lililokuwa koloni yake wakati mmoja.

    Baraza Kuu la Kitaifa la Uchina, ambalo ni kiungo muhimu katika Serikali, limesema kuwa lina imani kwamba Serikali ya Jimbo la Hong Kong, ina uwezo wa kukabiliana na maandamano hayo kibinafsi bila kuingiliwa na yeyote.

    Kuna hofu kuu Hong Kong kuwa huenda Serikali Kuu ikatumia polisi wenye silaha kuzima maandamano hayo.

    kumekuwa na mijadala mbalimbali duniani juu ya kauli hiyo ya serikali ya China na maoni tofauti yamekuwa yakitolewa na wasomi pamoja viongozi lakini pia watu mashuhuri duniani

     

     

  • MEEK MILL KUTOKA JELA HIVI KARIBUNI

    MEEK MILL KUTOKA JELA HIVI KARIBUNI

     

    Rapa kutoka kundi la MMG Meek Mill ambae jina lake halisi ni Robert Williams alihukumiwa kutumikia kifungo kisichopungua miezi mitatu hadi sita jela baada ya rufaa yake kukataliwa alipokutwa na hatia ya kutofuata taratibu alizowekewa wakati anatumikia kifungo cha nje ikiwemo fujo na vurugu. Meek Mill alitiwa hatiani baada ya kukamatwa na silaha pamoja na madawa ya kulevya mwaka 2008 ambapo alitumikia miezi nane jela kabla hajaachiwa kutumikia kifungo cha nje ndani ya miaka mitano.Kupitia mtandao wa twitter rick rosey alitweet picha ya rapa huyo akiwa jela na kuandika #FreeMeekMill Dreams Worth More than $$$$.” Ikiwa ni siku chache rapa huyo kutarajiwa kurudi uraiani pamoja na kutoa albam yake ya Dreams Worth More Than Money baada ya kusogezwa mbele 

     

     

     

     

     

     

     

  • DIAMOND PLUTNUM AMZAWADIA GARI WEMA SEPETU

    DIAMOND PLUTNUM AMZAWADIA GARI WEMA SEPETU

    wema

    Kupitia mtandao wa instagram jana msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasib Abdul yani Diamond amepost picha ya gari alilomnunulia mpenzi wake muigizaji Wema Sepetu gari aina ya Nisani kama zawadi katika siku yake ya kuzaliwa september 28. wawili hawa ambao wamekuwa wakimake Headlines kwenye vyanzo vya habari tofauti kuhusiana na mapenzi yao mbali na hayo wema anamiliki kampuni ya Endless fame inayojihusisha na uandaaji wa filam lakini pia Diamond ndie mmiliki wa brand ya Wasafi classic inayojihusisha zaidi na maswala ya mavazi jina la Diamond limekuwa likipata umaarufu zaidi kufuatia kutajwa kushiriki kwenye tuzo kubwa Afrika na dunia kiujumla kama MTV na Chanel O

  • Jason Derulo amethibitisha rasmi kuachana na Jordin Sparks

    Jason Derulo amethibitisha rasmi kuachana na Jordin Sparks

    GTY_jason_derulo_jordin_sparks__16x9_992

    mkali wa r&b kutoka marekani Jason Derulo ambae alikuwa na mahusiano na mwimbaji mwenzake Jordin Sparks.Jason Derulo  amethibitisha kuachana kwao kupitia ABC News kwa kusema hakuna ubaya baina yao wala usaliti ama kukwazana. Jason ameongeza kuwa licha ya mahusiano yao kuwa ni maswala binafsi ila anayaweka wazi kuepuka kuvuma kwa taarifa zisizo za kweli kupitia vyao tofauti vya habari, wawili hao ambao wamedumu kwa miaka mitatu mara baada ya kuingia rasmi kwenye mahusiano mwaka 2011 na kuamua kuyaweka wazi mwaka uliofuata 2012. kwa upande wake Jordan Sparks aliandika pia kupitia mtandao wa twitter maneno haya kuthibitisha hayo “Don’t cry because it’s over, smile because it happened,” wawili hao walimake headline zaidi mwaka jana baada Jason ngoma ya “marry me” iliyosemekana kuwa maalum kwa Jordan sparks baada ya kuonekana pia kwenye Video hiyo