Category: Global News

  • Iran imefanya kosa  kubwa sana

    Iran imefanya kosa kubwa sana

    Rais wa Marekani aliidhinisha majeshi ya Marekani kuishambulia siku ya Alhamisi na kisha kubadili msimamo, vyombo vya habari vya nchi hiyo viaripoti.

    Mashambulizi hayo ilikuwa yawe ya kulipiza kisasi baada ya Iran kuitungua ndege isiy na rubani ya Marekani.

    Kwa mujibu wa gazeti mashuhuri la The New York Times, tayari matayarisho ya awali ya mashambulizi hayo yalikuwa yakiendelea wakati Trump alipobadili mawazo na kuamuru yasitishwe.

    Gazeti hilo linamnukuu afisa mmoja mwanandamizi wa Ikulu ya White House.

    Hata hivyo bado hakuna taarifa rasmi kutoka Ikulu hiyo juu mipango hiyo ya mashambulizi.

    Iran inasema ndege hiyo ya kijasusui ilikuwa ndani ya anga lake wakati wakiitungua, lakini jeshi la Marekani limekanusha na kusema ilikuwa ikipaa katika anga la kimataifa.

    Tukio hilo linaendeleza suitafahamu baina ya mataifa hayo mawili hususani katika eneo la mpaka baina ya Ghuba ya Omani na Ghuba ya Uajemi.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Javad Zarif amesema nchi yake itapeleka malalamiko Umoja wa Mataifa (UN) kuwa Marekani inavamia eneo lake.

    Balozi wa Iran wa UN Majid Takht Ravanchi amesema ni dhahiri kuwa ndege hiyo ilikuwa inafanya operesheni ya kijasusi wakati ikitunguliwa, kitu ambacho amesema ni uvunjifu wa wazi wa sheria za kimataifa.

    Katika barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama, Bw Ravanchi amesema, Japo Iran haitaki kuingia vitani, lakini ina haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vya maadui.

    Trump amesema nini?

    Rais Trump mpaka sasa hajazungumza chochote kuhusu mipango ya mashambulizi ya kulipa kisasi.

    Akizungumza awali kutokea Ikulu ya White House, amesema Iran imefanya makosa makubwa kwa kuitungua ndege hiyo na kuwa kuna ushahidi kuwa ilikuwa katika anga la kimataifa na si eneo la Iran.

    Hata hivyo Trump amewaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo yawezekana lilisababishwa na makosa ya kibinaadamu.

    “Ni vigumu sana kwangu kuamini kwamba tukio hilo lilikuwa la makusudi,” amesema Trump.

    “Nafikiri, huenda Iran ilifanya kosa – Yawezekana kuna jenerali ama mtu mwengine ambaye alifanya kosa hilo la kutungua ndege ile,” amesema.

    “Yawezekana alikuwa ni mtu mmoja mpuuzi (ndio alitoa amri ya kutungua).”

    Viongozi wengine wamesema nini?

    Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuwa vita baina ya mataifa hayo mawili italeta janga ambalo madhara yake hayayumkiniki.

    Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres amezitaka pande zinazokinzana kujizuia.

    Nchini Marekani, Spika wa Bunge la Wawakilishi kutoka chama cha upinzania cha Democrats Nancy Pelosi amesema Marekani haina hamu ya vita dhidi ya Iran.

    Aliyekuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo, na kinara wa kutaka tiketi ya urais kupitia Democrats, Joe Biden, amemkosoa Trump kwa kusema sera zake dhidi ya Iran ni “janga la kujitakia”.

    Kiongozi wa wawakilishi wa chama tawala cha Republicans bungeni, Kevin McCarthy, ametaka kuchukuliwe hatua za kipimo baada ya kufuatia tukio hilo.

    Viongozi wengine wamesema nini?

    Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuwa vita baina ya mataifa hayo mawili italeta janga ambalo madhara yake hayayumkiniki.

    Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres amezitaka pande zinazokinzana kujizuia.

    Nchini Marekani, Spika wa Bunge la Wawakilishi kutoka chama cha upinzania cha Democrats Nancy Pelosi amesema Marekani haina hamu ya vita dhidi ya Iran.

    Aliyekuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo, na kinara wa kutaka tiketi ya urais kupitia Democrats, Joe Biden, amemkosoa Trump kwa kusema sera zake dhidi ya Iran ni “janga la kujitakia”.

    Kiongozi wa wawakilishi wa chama tawala cha Republicans bungeni, Kevin McCarthy, ametaka kuchukuliwe hatua za kipimo baada ya kufuatia tukio hilo.

    cc;BBCswahili

  • Morsi Azikwa saa chache baada ya kifo

    Morsi Azikwa saa chache baada ya kifo

    Rais wa zamani wa Misri, Mohamed Morsi amezikwa saa chache baada ya kufariki dunia akiwa mahakamani siku ya Jumatatu.

    Wakili wake ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kiongozi huyo wa zamani alizikwa Mashariki mwa jiji la Cairo asubuhi ya Jumanne familia yake ikiwepo

    Morsi,aliyekuwa na miaka 67, alikuwa kizuizini tangu alipoondolewa madarakani mwaka 2013.

    Makundi ya watetezi wa haki za binaadamu , ambayo yalikosoa mazingira ambayo Morsi aliwekwa,wametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu kifo chake.

    Familia yake na wanaharakati wamezungumzia kufo chake na muda ambao aliwekwa katika seli ya peke yake, akizuiwa kutembelewa na wanasheria na familia yake.

    Mtoto wake, Abdullah Mohamed Morsi, ameliambia shirika la habari la Uingereza, Reuters siku ya Jumatatu kuwa mamlaka za Misri ziliikatalia familia yake kufanya maziko katika mji yalipo makazi yake.

    Kiongozi wa juu wa zamani wa kundi lililopigwa marufuku nchini humo, Muslim Brotherhood, Morsi alikua kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia mwaka 2012.

    Aliondolewa na kushikiliwa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka mmoja baadae baada ya kufanyika maandamano makubwa kupinga utawala wake.

    Abdul Fattah al-Sisi, Kiongozi wa zamani wa kijeshi, amekuwa madarakani tangu mwaka 2014.

    Baada ya kuondolewa madarakani, mamlaka zilipambana na wafuasi wake na wapinzani wengine, na kukamata maelfu ya watu.

    Muslima Brotherhood na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, mshirika wa karibu wa Morsi ni miongoni mwa walioshutumu utawala wa Misri kuhusu kifo cha Morsi.

    Kulitokea nini Mahakamani ?

    Morsi alikua mjini Cairo siku ya Jumatatu kwa shutuma za kufanya vitendo vya kijasusi ikihusisha kuwa na mawasiliano na kundi la wanamgambo wa kiislamu la kipalestina, Hamas.

    Maafisa wanasema aliomba kuzungumza mahakamanu na kuongea kwa dakika tano kutoka kwenye kizimba kilichokua na kioo ambacho alikuwamo ndani yake na washtakiwa wengine.

    Dakika chache baadae alizimia wakati wa mapumziko mahakamani hapo.

    ”Alipelekwa hospitali ambapo alithibitishwa kupoteza maisha,”taarifa ya mwendesha mashtaka ilieleza.

    Maafisa wamesema katika ripoti yao kuwa , hakuna majeraha yeyote ambayo yalionekana kwenye mwili wake.

    Televisheni ya taifa ilieleza awali kuwa chanzo cha kifo chake ni mshtuko wa moyo.

    Mosri tayari alikuwa anatumikia kifungo kutokana na mashtaka matatu yaliyokuwa yakimkabili.Awali alihukumiwa adhabu ya kifo,ambayo baadae ilitenguliwa.

    Watu wanazungumza nini baada ya kifo chake ?

    ”Kifo cha Rais wa zamani, Morsi kimetokea kutokana na kutendewa isivyo haki na serikali, kuwekwa katika gereza la peke yake, alipatiwa huduma mbovu za matibabu, kumzuia kuonana na familia yake na mawakili wake.Alieleza Bi Whitson kwenye taarifa yake.

    Shirika la Amnesty International pia limetaka uchunguzi ufanyike kuhusu kifo chake.

    Shirika limesema Morsi alikua akiruhusiwa kutembelewa mara tatu tu kwa kipindi cha takribani miaka sita na hakuruhusiwa kuonana na mawakili wake wala daktari.

    Mfalme wa Qatar,Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, mshirika mwingine wa Morsi ameeleza masikitiko yake kutokana na kifo chake.

    Mbunge wa nchini Uingereza, Crispin Blunt, aliyeongoza jopo la wanasiasa na kutoa tahadhari kuhusu kutendewa kwa Morsi mwaka 2018, ametaka ufanyike ”uchunguzi huru kimataifa”

    Tawi la kisiasa la kundi la Muslim Brotherhood, chama cha Freedom and Justice, kimesema kuwa kifo cha Morsi ni ”mauaji”.

    Rais wa Uturuki ameshutumu ”wakandamizaji” wa Misri kwa kifo chake na kumuelezea Morsi kuwa shahidi.

    Morsi ni nani?

    Mohammed Morsi alizaliwa katika kijiji cha El-Awwadh katika jimbo lililopo kwenye delta za mto Nile la Sharqiya mwaka 1951.

    Alisomea Uhandisi katika chuo Kikuu cha Cairo katika miaka ya 70 kabla ya kuhamia nchini Marekani ambapo alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Uhandisi.

    Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru mwaka 2012, akiwa kiongozi mwandamizi wa kundi la kiislamu la Muslim Brotherhood ambalo limepigwa marufuku kwa sasa nchini humo.

    Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano ya wanaharakati ambao walimshutumu yeye na kundi la Muslim Brotherhood kujilimbikizia madaraka.

    Baada ya maandamano kuwa makubwa, na wafuasi wa Morsi kushambulia wapinzani wake, jeshi likiwa chini ya rais wa sasa Abdel Fattah el-Sisi liliendesha mapinduzi na kumng’oa Morsi madarakani, Juni 2013.

    Jeshi liliendelea kupambana na wafuasi wa Morsi baada ya mapinduzi, na zaidi ya wafuasi wake 1,000 waliuawa Agosti 2013.

  • Omar All bashir ashtakiwa kwa Ufisadi

    Omar All bashir ashtakiwa kwa Ufisadi

    Rais aliyeng’olewa madarakani nchini Sudan Omar al-Bashir ameshtakiwa kwa kosa la ufisadi.

    Mashtaka yanahusiana na sheria zinazohusu “utajiri haramu na maagizo ya dharura “,imesema ofisi ya mwendesha mashtaka, ambayo haikutoa taarifa zaidi.

    Jeshi lilimuondoa madarakani rais huyo wa muda mrefu mwezi April kufuatia miezi ya maandamano dhidi yake.

    Msemaji wa jeshi aliesma Alhamisi kuwa makosa yalifanyika wakati majeneraliwalipoamrisha kumalizika kwa mhgomo wa kukaa mbele ya makao makuu ya jeshi ambapo waandamanaji wanadai kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini humo.

    Ghasia za mwezi Juni zilisababisha vifo vya watu 61, kwa mujibu wa maafisa, au 118,kwa mujibu wa madaktari wanaounga mkono waandamanaji wanaodai demokrasia.

    Mazungumzo baina ya waandamanaji na baraza la kijeshi la mpito yalivunjika baada ya ghasia.

    Viongozi wa maandamano baadae waliyaita maandamano kuwa ni ukaidi wa raia , ambayo walisema hayana budi kukoma ili kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani.

    Baada ya mkutano baina ya Tibor Nagy, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika ,na Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan,jeshi lilisema kuwa lina matumaini Marekani inaweza “kuwa na mchango mzuri”.

     

    Bwana Bashir alipinduliwa na kukamatwa tarehe 11 Aprili baada ya miongo mitatuya utawala wa kiimla nchini Sudan. Hajawahi kuonekana kwa umma tangu alipokamatwa.

    Mwezi May alishtakiwa kwa makosa ya kuchochea nana kuhusika na mauaji ya waandamanaji.

    Mashtaka hayo yametokana na uchunguzi uliofanywa kuhusu kifo cha ddaktari aliyeuawa wakati wa maandamano yaliyosababisha kumalizika kwa utawala wake mwezi uliopita.

    Hatma ya Bwana Bashir haijawa wazi. Aliripotiwa kutiwa nguvuni mara baada ya kupinduliwa.

    Mnamo mwezi Disemba, waandamanaji walianza maandamanano dhidi ya uamuzi wa serikali wa kupandisha mara tatu kwa bei ya mkate.

    Maandamano hayo ghafla yalibadilika kuwa hasira iliyosambaa kote nchini dhidi ya kiongozi huyo ambaye alikuwa mamlakani kwa miaka 30, yakiongozwa na madaktari.

    Maandamano yalifanyika kwa wiki tano na shahidi mmoja anasema tarehe 17 Januari, vikosi vya usalama viliwafyatulia risasi waandamanaji na kumuua daktari.

    Utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir uligubikwa na mapigano.

    Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameiongoza taifa hilo lililokuwa kubwa zaidi barani Afrika zama hizo hadi mwaka 2011 alipochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

    Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini.

    Japo serikali yake ilitia saini makubaliano ya kumaliza vita mwaka 2005, vita vingine vilizuka tena – katika eneo la magharibi mwa Darfur.

    Bw. Bashir alituhumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC kwa kupanga uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika eneo hilo.

    Licha ya ICC kutoa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwake, ameshinda uchaguzi mara mbili mwaka 2010 na 2015, japo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi uliyopelekea ushindi wake.

     

  • wanne waripotiwa kuuawa nchini Sudan

    wanne waripotiwa kuuawa nchini Sudan

    Watu wanne wameripotiwa kuuawa nchini Sudan katika siku ya kwanza ya maandamano ya kitaifa ya kupinga utawala wa Kijeshi nchini humo.

    Vikosi vya Usalama nchini Sudan viliwarushia mabomu ya machozi baridi na kutumia risasi halisi kuwatawanya waandamanaji hao katika mkuu wa nchi hiyo Khartoum.

    Wanaharakati wameitisha maandamano ya kupinga utawala huo kuanzia Jumapili, siku kadhaa baada ya msako wa kijeshi uliosababisha vifo vya mamia ya watu katika mji mkuu wa Khartoum.

    Aidha, Wafanyikazi kadhaa wa benki, Viwanja wa Ndege pamoja na wa shirika la umeme nchini humo walikamatwa kabla ya mgomo wa kitaifa wa kupinga utawala wa kijeshi, limedai kundi kuu la waandamanaji

    Wanaharakati wa kupigania demokrasia nchini humo wanasema kuwa baraza la jeshi haliwezi kuaminiwa baada kuzuka kwa ghasia ambapo wafuasi wengi wa Upinzani waliuawa jijini Khartoum na wamekataa kufanya mazungumzo ya amani na viongozi wa baraza hilo.

    Jeshi lilichukua uongozi baada ya kumng’oa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Omar al-Bashir mwezi Aprili mwaka huu na kuahidi kurejesha utawala wa kiraia baada ya kipindi cha mpito.

    Hata hivyo, mpaka sasa baraza la Kijeshi linalotawala nchi hiyo (TMC) halijatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.

     

  • Njiwa amuepusha dereva  na faini

    Njiwa amuepusha dereva na faini

    Dereva aliyekua akiendesha Gari kwa kasi nchini Ujerumani alinusurika kulipa faini ya pauni 93 baada ya njiwa mweupe kumuepusha kutambulika sura yake.

    Dereva alinaswa kwenye kamera za mwendo kasi lakini sura yake ilifichwa na mabawa ya ndege huyo alipokua akiruka mbele ya kioo cha gari.

    Taarifa ya polisi inasema pengine ”Roho mtakatifu” aliingilia kati- ishara ya njiwa mweupe kama alama ya uwepo wa Mungu katika imani ya dini ya kikristo.

    ”Tumeelewa ishara hiyo na kumuacha dereva kwa amani wakati huu.”

    Lakini maafisa katika mji wa Viersen, karibu na mpaka wa Ujerumani waliongeza: ”Tuna matumaini kuwa dereva huyo aliyesaidiwa anaelewa ‘onyo hili kutoka juu’ na kuwa ataendesha vizuri siku za usoni.”

    Dereva alikua akisafiri kwa kasi ya kilometa 54 kwa saa katika barabara ambayo alipaswa asafiri kwa kilomita 30 kwa saa, polisi wameeleza

    Kutokana na gari pekee kubainika na si dereva, alinusurika kulipa faini hiyo ”ashukuriwe malaika yule mwenye mabawa ambaye mbawa zake zilizuia sura ya dereza”.

    Polisi wa mji wa Viersen amesema kuwa Njiwa huyo naye angetozwa faini kwa kupita kwa kasi kwenye eneo asilopaswa kupita.

     

  • Brexit ilivyomuondoa madarakani Theresa May

    Brexit ilivyomuondoa madarakani Theresa May

    Waziri mkuu wa pili mwanamke Uingereza, kama ilivyo kwa wa kwanza, mwishowe ameondolewa madarakani kutokana na mvutano wa ndani ya chama cha Conservative kuhusu Ulaya.

     

    Lakini huenda Theresa May asiwe kama Margaret Thatcher katika orodha ya viongozi walioacha alama ya kudumu katika nchi yao.

    Angalau sio kwa namna ambavyo angetamani wakati alipoingia Downing Street mnamo Julai 2016.

    Maazimio aliyokuwa nayo – kufikia maenoe yaliosahauliwa katika taifa hilo, au kusahihisha masuala nyeti ya dhulma katika jamii ya Uingereza – yaligubikwa kwa neno moja: Brexit.

    Takriban muda wa miaka mitatu aliyohudumu yote yalifafanuliwa kwa uamuzi wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya na jitihada zake kupata ufumbuzi wa matokeo ya kura ya maoni iliyoitishwa na mtangulizi wake David Cameron.

    Hata wakosoaji wake wakali walishangazwaa kwa uwezo wake wa kuhimili adhabu na aibu iliyofuata wimbi baada ya wimbi kutoka Brussels na Westminster.

    Mpambano wa kuwasilisha Brexit

    Kujiuzulu kwa mawaziri na wabunge wa upinzani ambayo yote yangebaini mwisho wa uhusiano wa kawaida kwa waziri mkuu yalioonekana kutomtetelesha.

    Aliendelea ni kana kwamba hata hatambui kizaa zaa kinachomzungka na kuwamabia wabunge “hakuna kilichobadilika” na kuahidi kutekeleza “wanachotaka” raia wa Uingereza, hata wakati nguvu zake bungeni na udhibiti wa chama chake kilichoshuka umaarufu ukiendelea kupungua.

    Huenda taswira ingekuwa tofuati iwapo angeshinda katika uchaguzi mkuu aliouitisha mnamo 2017.

    Lakini badala ya kurudi Downing Street na jukumu kubwa mikononi, kama alivyotarajia, alipoteza uwingi katika bunge la wawakilishi na imbidi ategemee uungwaji mkono wa kutoka chama cha Ireland kaskazini Democratic Unionist Party.

    Hakupoa kidonda hichi, na kumekuwana hisia kwamba wabunge wake wengi walikuwa wamemaucha aendele kuhdumu mpaka pale atakapofanikiwa kuwasilisha mpango wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya kabla ya kumtema baada ya kupata mpango mbadala unaovutia.

    Kwa wakati mmoja, ilibidi aahidi atajiuzulu kabla ya uchaguzi ujao wa 2022 wakati akijizatiit kuponea kura ya kutokuwana imani naye iliyooidhinishwa na wabunge wake mwenyewe.

    Na baada ya kutengwa na wabunge wengi kwa kuwalauamu kwa mkwamo wa Brexit, alilazimika hatimaye kukubali kwamba chama chake, cha Conservative hakikumtaka aendelee kuhudumu tena.

    Ajitolea mara ya mwisho

    Amejitolea kuondoka kama hatua ya mwisho kwa wakosoaji wakena kuwamabi kwamba atajiuzulu iwapo wtaapiga kura kukubali mpango wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya aliyoupigia upatu huko Brussels.

    Januari 2019, bunge lilipinga mpango huo kwa uwingi mkubwa kuwahi kufanyika dhiid ya serikali Uingereza katika historia.

    May amejaribu tena mara mbili kupata ridhaa ya bunge, kwa kukarabati mpango huo na alishindwa tena mara zote.

     

    Watu wanaounga mkono kusalia walidhani kwamba makubaliano hayo ni makali mno, huku wa Conservative wakisema haujatimiza Uingereza kujitoa kikamilifu kutoka Umoja wa Ulaya.

    Katika jitiahada ya kujadiliana makubaliano ya Brexit ambayo yanaweza kupita katika bunge la wawakilishi alishauriana na kiongozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn.

    Lakini mazungumzo ya wiki sita pasi kufikiwa makubaliano , matokeo ambayo wabunge wengi wa Conservative wanasema yalitabirika na ni ya kuvunja moyo.

    Izara nyingine ilifuata wakati alilazimika kukubali Uingereza kushiriki katika uchaguzi kwenye Umoja wa Ulaya – jambao ambalo hapo awali alisema halitokubalika.

    Kufikia hatua hii wabunge waliacha kumsikiliza, kwa kufikia uamuzi kwamba May ni kizuizi kwa Brexit wanayoitamani- au ya aina yoyote ile.

    Hatimaye May alilazimika kukubali kwamba hawezi kuendelea “katika kazi anayeoipenda” na muda wake huko Downing Street sasa umemalizika.

    Sauti yake ilitetereka na alikuwa mwingi wa hisia alipomaliza hotuba yake akisema: “Nitaondoka katika wadhifa huu hivi karibuni lakini imekuwa heshima kubwa maihsani mwangu kuhudumu.

    Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.

     

    cc;BBCswahili

     

  • Cardi B amehairisha tamasha kisa upasuaji

    Cardi B amehairisha tamasha kisa upasuaji

    Kutokana na upasuaji wa kuongeza mwili unaojulikana kama (liposuction) alioufanya  rappa Cardi B umesababisha kujitoa kutumbuiza kwenye tamasha la 92Q Spring Bling lilipangwa kufanyika ijumaa hii mjini Maryland.

    Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ rapa Cardi b amejitoa baaada ya kupata tatizo mara tu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongea baadhi ya sehemu za mwili wake.

    kwa mujibu wa vyanzo vya karibu vya rapa huyo vimeeleza kuwa kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kupona baada ya kufanya pia upasuaji wa maziwa yake.

    Hata hivyo Madaktari wameshauri kuwa Cardi B anahitaji mapumziko ya muda mrefu ili mwili wake urudi kama zamani kutokana na baadhi ya sehemu alizofanyiwa upasuaji kuwa hazijapona vizuri.

    Imeelezwa kuwa Cardi B alifanya upasuaji huo mara tu baada ya kumpata mtoto wake wa kwanza Kulture, May 5,2019

    Aidha Cardi B alisikika akiwaambia mashabiki zake katika tamasha lilofanyika Memphis kuwa alitaka kuahirisha tamasha hilo kwasababu kucheza sana kunaweza kumsababishia matatizo.

     

  • Kundi la IS kuvamia Mashariki mwa DRC

    Kundi la IS kuvamia Mashariki mwa DRC

    Wakuu wa vyombo vya usalama katika kanda ya Maziwa Makuu wanakutana nchini Uganda kupanga mikakati ya kukabiliana na tishio la kundi la Islamic State ambalo linasemekana limeanza kuendesha harakati zake katika maeneo ya Mashariki na Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Hayo ni kwa mujibu wa upelelezi wa chombo cha usalama kinachowaleta pamoja wakuu wa usalama katika kanda ya maziwa makuu, kuna uwezekano wa eneo hilo kuingiliwa kirahisi na wanamgambo wa kundi hilo kutokana na ukosefu wa usalama na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao unatatiza juhudi za kukabiliana nao.

    Vyombo vya usalama katika eneo hilo sasa vinataka kuhakikisha kuwa kundi hilo halipati nafasi kuendesha shughuli zake katika matatifa ya eneo hilo baada ya kutimuliwa mashariki ya kati.

    ”Kuna vitisho kwa hivyo ni onyo kwetu kulishughulika mapema kabla halijawa tatiza kubwa katika kanda ya maziwa makuu” alisema Mkuu wa Jeshi la Uganda, Jenerali David Muhoozi’

    Kulingana na wakuu hao wa usalama kuna haja ya wao kushirikiana na majeshi ya mataifa ya kigeni yaliyochangia katika juhudi za kuvunja kundi hilo mashariki ya kati.

    ”Tishio la kundi hilo la kigaidi ni kubwa kiasi ya kuhamasisha Serikali za eneo hili lote la Maziwa Makuu, kuona ya kwamba zinaongeza juhudi za kukabiliana masuala ya kigaidi iwe ni kutoka kwa kundi la al-Shabab, ISIS, Boko Haram au Al-Qaeda”, alisema katibu mtendaji wa mataifa ya maziwa makuu, Zakaria Mubuli Mwita.

    Aliongeza kuwa wamepokea ripoti kutoka kwa serikali za eneo hilo kwamba kundi la kigaidi la ADF linashirikiana na na makundi hayo ya kigaidi.

    Hivi karibuni kundi la kigaidi la Islamic State lililo na chimbuko lake nchini Iraq, lilidai kufanya mashambulizi katika kijiji cha Kamango mkoani Kivu Kaskazini.

    Maafisa wa kanda hiyo walisema hapakuwa na ushahidi wa IS kuhusika na shambulio hilo japo waliyoshuhudia walilaumu kundi la Allied Democratic Forces (ADF) ambalo wanadai limekuwa likishirikiana na IS.

    Shambulio hilo la mwezi Aprili lilizua taharuki kuhusu hali ya usalama katika Mataifa ya Kanda ya Maziwa Makuu.

    Bw. Zakaria Mwita ambaye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Mataifa ya Maziwa Makuu amesema kuwa wanapania kushirikiana na vikosi vya Umoja wa Mataifa kame vile MONUSC, Serikali na Jeshi la DRC pamoja na nchi zote za Maziwa Makuu ili kuona kuwa wanakabiliana vilivyo na makundi hayo ya kigaidi yasitie fora katika eneo hilo.

    Ingawa maeneo karibu yote ya DRC yamekuwa yakikumbwa na changamoto za usalama kama vita ama kushambuliwa na waasi mara kwa mara, eneo la mashariki ya nchi hiyo ndiyo lililoathirika zaidi.

     

    Usalama mashariki ya DRC

    Akiongea na BBC siku chache kabla ya kuondoka madarakani mwishoni mwa maka 2018, rais mataafu wa nchi hiyo, Joseph Kabila alisema katika mambo ambayo angekuwa na muda zaidi kuyashughulikia ni kurudisha amani kwa taifa hilo.

    Mashariki mwa DRC kuna makundi ya kijeshi ya waasi na ya kikabila.

    Baadhi ya makundi yanaondwa na raia wa nchi hiyo, lakini kuna amakundi mengine makubwa ambayo yanafadhiliwa ama kupambana za serikali za nchi jirani.

    Makundi ya waasi yanayotokea nchi jirani ni FDLR ambalo lilitekeleza mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 na wapiganaji wake wakakimbilia DRC.

    Waasi wa ADF wanatokea nchini Uganda.

    Makundi hayo ya waasi yanatumia misitu mizito iliyopo kwenye eneo hilo kujificha na kuendesha shughuli zao huku wakitangaza nia ya kushambulia nchi zao walizozikimbia.

    Uganda na Rwanda zimeshavamia DRC mara mbili kwa lengo la kusambaratisha makundi hayo na vita hizo kupelekea mamilioni ya watu kufariki.

     

     

     

    cc;BBCswahili

  • Mfalme  amgeuza mlinzi  kuwa  Malkia wake

    Mfalme amgeuza mlinzi kuwa Malkia wake

    Mfalme wa Thailand amemuoa Naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wake , na kumpa cheo cha malkia, imesema taarifa ya ufalme huo.

    Tangazo hilo la kushitukiza limetolewa huku sherehe za kutawazwa kwake zikitarajiwa kuanza Jumamosi, wakati atakapochukua wadhfa wake.

    Mfalme Maha Vajiralongkorn, mwenye umri wa miaka 66, alikuwa mfalme kikatiba baada ya kifo cha baba yake aliyependwa sana kilichotokea mwaka 2016.

    Amekwisha wataliki wanawake mara tatu na ana watoto saba.

    Ufalme ulisema kuwa: Mfalme Vajiralongkorn “ameamua kumpandisha cheo Generali Suthida Vajiralongkorn Na Ayudhya, na kuwa Malkia Suthida na atakuwa na cheo cha kifalme na hadhi kama sehemu ya sfamilia ya kifalme”.

    Malkia Suthida ni mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn na amekuwa akionekana hadharani pamoja nae kw amiaka mingi, ingawa mahusiano yao haukuwahi kukubalika rasmi.

    Picha kutoka kutoka katika sherehe za harusi zilionyeshwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni vya Thailand Jumatano, ambapo watu wa wengine wa familia ya ufalme na washauri wa ufalme walihudhuria.

    Mfalme alionekana akimwagia maji ya baraka Malkia Queen Suthida kichwani. Baadae wawiloi hao walisaini cheti cha ndoa.

    Mnamo mwaka 2014 Vajiralongkorn alimteua Suthida Tidjai, ambaye ni mhudumu wa zamani wa Thai Airways,kama naibu kamanda wa kikosi cha walinzi wake. Alimpandisha cheo na kuwa Generali kamili jeshini Disemba 2016.

    Mfalme aliyetangulia Bhumibol Adulyadej, alitawala kwa miaka 70 na kuwa ndiye mfalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani na alifariki dunia mwaka 2016

  • Maisha ya wengi yako hatarini kutokana na maafa ya kimbunga

    Maisha ya wengi yako hatarini kutokana na maafa ya kimbunga

    Msumbiji inahitaji misaada ya haraka kuokoa maisha ya walioathirika na kimbunga Kenneth, shirika la msaada limesema.

    Huku shirika la ‘Save the Children’ limesema hali waliokuwa nayo watu wa Msumbiji inatishia usalama wa maisha yao hivyo ni muhimu misaada zaidi itolewe.

    Umoja wa mataifa umetoa kiasi cha fedha cha dola milioni 13 ili ziweze kuwasaidia wahanga wa kimbunga wa Msumbiji na Comoro kwa ajili ya chakula, maji na kurekebisha miundo mbinu.

    Idadi ya vifo vilivyosababishwa na kimbunga , magharibi mwa Msumbiji vimefika 38 na vifo vingine vinatarajiwa kutokea, utawala umebainisha.

    Kwa sasa wafanyakazi wa mashirika ya msaada yanahangaika kufika katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na kimbunga.

    Mvua kubwa ilipiga kusini mwa Afrika mwishoni mwa wiki iliyoambatana na upepo mkali uliovuma kwa kilomita 220 kwa saa, na kusababisha zaidi ya maelfu ya makazi ya watu kuharibika.

    Kwa sasa mvua si kubwa sana ingawa bado inaendelea kunyesha.

    Mamlaka ya hali ya hewa inatabiri kuwa mvua hizi zitapiga mara mbili kama ilivyotokea kwenye kimbunga cha Idai ambacho kilitokea mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 900 katika maeneo ya kusini mwa Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.

    Afisa wa masuala ya misaada kwa binadamu kutoka Umoja wa mataifa anasema hatari za mafuriko ambayo yamesababishwa na kimbunga Kenneth zinatarajia kuendelea mpaka mwishoni mwa msimu wa mvua ambapo kiwango cha maji kwenye mito kitakuwa juu.

    Tayari mji wa Pemba na Cabo Delgado umeathirika na mvua kubwa na mafuriko.

    Kipi kipya?

    Wafanyakazi wa shirika la msaada wanajaribu kupeleka dawa na kusambaza chakula kabla mvua nyingine kubwa haijaja.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo cha taifa cha kukabiliana na majanga nchini humo, wamesema watu 38 wamefariki kutokana na kimbunga Keneth huku makazi 35,000 yameharibiwa na mvua.

    Mtandao wa kujitegemea wa ‘O Pais’ umeripiti kuwa watu wengine watano wamefariki baada ya nyumba za Pemba kuanguka siku ya jumapili ingawa bado serikali haijathibitisha idadi ya vifo hivyo.

    Watu laki mbili wapo hatarini Pemba peke yake, Ocha ilitoa angalizo.

    Lakini kufika katika maeneo hayo hatari imekuwa kazi ngumu kwa wasaidizi kufanikiwa kufikia.

    “Tumefanikiwa kutuma ndege moja kwa msaada wa shirika la chakula duniani ili kusambaza mchele na biskuti na vitu vingine ambavyo sio vyakula,

    Lakini hali ya hewa imekuwa ikibadilika haraka sana na kuathiri operesheni hiyo ya kutoa misaada. Mvua zinaendelea kunyesha na walishindwa kutuma ndege nyingine”, Bwana Abreu aliiambia AFP

    Kimbunga cha kitropiki huwa inatokea katika sehemu ya bahari ya hindi na huwa nadra kutokea.

    Hata hivyo kwa mujibu wa mwandishi wa mazingira wa BBC ,Matt McGrath,Kimbunga Idai kilikuwa cha saba kupiga katika bahari hindi msimu ambao kilikuwa kimepiga mwezi achi.

    Hii ni zaidi ya mara mbili ya kiwango cha kawaida kwa mwaka.

    Kitu ambacho sio cha kawaida, licha ya kuwa kimbunga Idai na Kenneth vimepiga kwa mfululizo.

    Kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa duniani imesema, kimbunga hiki kilichotokea Msumbiji kimevunja rekodi kwa sababu haijawahi kutokea kupiga mara mbili katika msimu mmoja.

    Si hali ya kawaida kimbunga kuonekana katika maeneo haya na vilipungua kutokea yapata miongo saba iliyopita.

    Lakini ni mapema sana au ni mfano mdogo kusema kuwa mabadiliko ya tabia nchi ndio yamesababisha mabadiliko haya.

    Wataalamu wameainisha kuwa dhoruba hii inahusishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

    cc;BBSswahili

     

  • ‘Hali ni mbaya kuliko ilivyodhaniwa’ Msumbiji

    ‘Hali ni mbaya kuliko ilivyodhaniwa’ Msumbiji

    Hali kaskazini mwa Msumbiji ni mbaya kuliko ilivyodhaniwa, msemaji wa Umoja wa mataifa ameeleza, siku chache baada ya kimbunga Kenneth kutuwa nchini humo.

     

    Kimbunga hicho kilituwa siku ya Alhamisi kwa upepo mkali wenye kasi ya 220km/h (140mph) kilichoviangamiza vijiji.

    Takriban watu 700,000 sasa wanadhaniwa kuwa katika hatari katika eneo hilo wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha.

    Pemba, mji mkubwa wa jimbo la Cabo Delgado kumeshuhudiwa mvua yenye kina cha mita mbili na mafuriko.

    Msemaji katika ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinaadamu (Ocha) Saviano Abreu ameeleza kwamba hali ni mbaya katika miji ya Macomia na Quissanga, akiongeza kwamba kuna wasiwasi pia kwa kisiwa kisichoweza kufikiwa cha Ibo.

    Mawimbi ya hadi mita 4 yanatarajiwa, na mashirika ya misaada yanahofia kwamba mvua itazidi kunyesha.

    “Tuna wasiwasi mkubwa kwasababu, kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa, mvua nzito inatarajiwa kunyesha katika siku nne zijazo,” Deborah Nguyen, msemaji wa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa mataifa , alieliambia shirika la habari la AFP.

    “Tunatarajia mvua iwe na ukubwa wa mara mbili zaidi ya ilioshuhudiwa wakati wa kimbunga Idai,” ameongeza.

    Kimbunga Idai kilisababisha vifo vya watu 900 katika nchi tatu mnamo Machi mwaka huu.

    Ni yapi yanayojiri?

    Inadhaniwa kwamba watu 400,000 wanaishi Pemba , na mvua kubwa imesababisha watu wengi kuwa katika hatari.

    Kuna wasiwasi unaotokana na maporomoko ya ardhi katika mtaa wa Mahate mjini humo, maafisa wa Ocha katika eneo hilo wanasema, na katika mtaa wa Natite, nyumba zimeanza kuporomoka.

    Shirika la mpango wa chakula duniani linaarifiwa kuanza kutoa misaada kwa watu waliokwama, lakini barabara zilizoharibika zimesababisha shughuli zisitishwe katika maeneo yaliotengwa sana.

    Takriban watu watano wamefariki kutokana na kimbunga hicho na takriban nyumba 35000 zimeharibika vibaya au kubomoka kabisa, maafisa wa kitaifa wanasema.

    Mashirika ya Umoja wa mataifa yanasaidia maafisa wa serikali na bwana Guterres ametoa wito wa “rasilmali za ziada” kutoka jumuiya ya kimataifa “kufadhili usaidizi wa sasa, wa siku zijazo na wa kipindi kirefu zaidi”.

    Eneo lililoathirika liko vipi?

    Jimbo la Cabo Delgado halina watu wengi kama eneo lililoathirika na kimbunga Idai na inavyoonekana sehemu kubwa iko katika ardhi ya juu.

    Hilo kwa pamoja na tahadhari za mapema kutoka kwa maafisa husika kabla ya kutokea kimbunga hicho huenda ikasaidia kuzuia hasara ikilinganishwa na wakati wa kimbunga Idai.

    Lakini taarifa zinasema maelfu ya makaazi yameharibiwa kutokana na upepo mkali, na ene hilo limekabiliwa na mashambulio ya wanamgambo wenye itikadi kali za dini ya kiislamu katika miezi ya hivi karibuni, jambo ambalo linaonekana huenda likatatiza utoaji wa msaada.

    Tayari maelfu ya watu walikuwa wametoroka makaazi yao kutokana na ghasia kutafuta hifadhi katika kambi za kuwahifadhi watu walioachwa bila ya makaazi.