SALVA KIIR ASISITIZA KUENDELEZA MAKUBALIANO YA AMANI

SALVA KIIR ASISITIZA KUENDELEZA MAKUBALIANO YA AMANI

Like
180
0
Thursday, 19 November 2015
Global News

RAIS  wa  Sudan  kusini  Salva  Kiir  amesisitiza  nia yake ya kuendeleza makubaliano  ya  Amani  yaliyotiwa  saini mwezi  Agosti, siku  mbili  baada  ya  serikali  na  waasi kushutumiana  kwa  kukiuka  makubaliano  hayo.

Rais Kiir  ameliambia bunge  la nchi hiyo kwamba Sudan  kusini inapaswa  kufikia   maridhiano na  kufungua  kurasa mpya  na  kuitaka  jumuiya  ya  kimataifa  kusaidia nchi hiyo  kutekeleza  makubaliano  ya  amani.

Mvutano  wa  kuwania  madaraka  kati  ya  rais Salva Kiir na  makamu  wake  wa  zamani Riek Machar  uligeuka kuwa  machafuko  makubwa  katikati  ya mwezi Disemba  mwaka 2013.

Comments are closed.