Category: Slider

  • Wafanyabiashara Kariakoo Wafunga Maduka Kukwepa Ukaguzi Wa Mashine Za EFD

    Wafanyabiashara Kariakoo Wafunga Maduka Kukwepa Ukaguzi Wa Mashine Za EFD

    DUKA 4

    Wafanyabiashara mbali mbali wenye maduka eneo la kariakoo wamefanya mgomo usio rasmi wa kufunga maduka yao ili kutokaguliwa na watendaji wa TRA ambao wanaendesha msako wa kuwakamata wale wote ambao wanatumia mashine za EFD kinyume na matumizi yake halisi.

    DUKA 3

    Kwa mujibu wa hali halisi ambayo imeonekana leo katika eneo hilo  maduka mengi yamefungwa katika kile kinachoonekana kukwepa kufanyiwa tathmini ya matumizi ya mashine za ki Electroniki za EFD zinazofanya kazi ya kutoa risiti na kutunza kumbukumbu za mahesabu za mwenye duka.

    Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi ambaye aliongea na ripota wa EFM Bwana  Sosthenes Shayo alisema wao hawapingi matumizi au kutumia mashine za EFD wanapinga mfumo mbaya uliowekwa kwa ajili ya matumizi ya mashine hizo.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Mamalaka ya Mapato -TRA -amesema kuwa kufuatia Uhakiki huo yapo mambo kadha wa kadha ambayo wameyabaini kufuatia zoezi hilo ikiwemo uhafifu wa matumizi ya  mashine hizo.

    Wafanyabiashara mara nyingi wanalalamika lakini tukiitisha vikao hawafiki. Na pia baadhi yao kwa maana ya wachache wenye hitilafu ndio wanachochea wengine kugoma ili waendelee na kutotumia mashine hizo. Efm itakuletea habari zaidi juu ya sakata hilo.

     

     

  • Christiano Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya

    Christiano Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya

    Ronaldo

    Mchezaji wa kimataifa wa Portugal anayechezea timu ya Real Madrid Christiano Ronaldo Jana usiku alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa mwaka 2014/2015.

    Ronaldo alitwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji Arjen Robben wa Bayern Munich Emmanuel Neur wa Bayern Munich katika sherehew iliyofanyika jijini Monaco nchini Ufaransa.

  • Okwi Arudi Simba Asaini Mkataba Kama Mchezaji Huru Kulinda Kipaji Chake

    Okwi Arudi Simba Asaini Mkataba Kama Mchezaji Huru Kulinda Kipaji Chake

    Okwi

    Aliyekuwa msambuliaji wa Yanga Emmanuel Okwi jana jioni amesaini Simba SC kwa mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.
    Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.
    “Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.
    Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni.
    “Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.
    Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia.
    Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu.
    Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.
    Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.
    Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo.
    Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.
    Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo(Jana) baina ya mchezo huyo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.
    Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema.

  • Mbowe Akabidhiwa Fomu Ataka Ushindani Na Anayeona Anaweza Kummudu

    Mbowe Akabidhiwa Fomu Ataka Ushindani Na Anayeona Anaweza Kummudu

    mbowe

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali na kufungua milango kwa wanachama wengine ‘kupimana naye kifua’.
    “Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,” alisema Mbowe ambaye ameongoza chama hicho kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
    Makada wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiongozwa na kada maarufu, Athuman Mzigo (Mapigo Saba) kutoka Kigoma, walikutana na Mbowe na kuwasilisha maombi yao ya kumtaka awanie tena nafasi hiyo.
    “Kutokana na sifa za mwenyekiti wetu, tumechangishana Sh200 kila mmoja hadi zikafika Sh50,000,” alisema Mapigo Saba huku akishangiliwa na makada wenzake alioambatana nao na kuongeza:
    “Tumemwomba mwenyekiti agombee nafasi hiyo kwa kuzingatia sifa; kwanza anaijua vizuri idadi ya Watanzania na matatizo yao, pili anaungwa mkono na watu wengi na amekisaidia chama kukua. Tulikuwa na madiwani 40 leo wamefika 500, wabunge watano leo 48. Halafu hana ubaguzi ndiyo maana ameunganisha vyama vya upinzani na kuunda Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”
    Huku akichomekea maneno ya lugha ya Kiha, Mapigo Saba alisema kuwa maombi ya kumtaka Mbowe agombee pia yametolewa katika mikoa ya Rukwa, Manyara, Iringa, Njombe, Jimbo la Same Magharibi, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro.
    Hotuba ya Mapigo Saba ilifuatiwa na salamu kutoka kwa wazee wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke, Baraza la Wanawake (Bawacha) na Baraza la Vijana (Bavicha).
    Akitoa salamu za Bavicha, mwenyekiti wa baraza hilo Njombe, Emmanuel Masonga alisema Mbowe ni sawa na Joshua aliyemalizia kuwaongoza wana wa Israel kuingia nchi ya Kanaani:
    “Sisi Wakristo tunajua kuwa Mussa alianzisha safari ya Waisrael kwenda Kanaani, ila hakuwafikisha. Kina Mtei (Edwin), Kimesera (Victor), Bob Makani na wengineo walianzisha safari ya kwenda Ikulu, ila hawakutufikisha. Mbowe ni sawa na Joshua atakayetufikisha Ikulu,” alisema Masonga.
    Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Susan Lymo alimsifu Mbowe akisema ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa katika chama hicho.
    “Mwaka 2000, kulikuwa na mwanamke mmoja katika viti maalumu, mwaka 2005 waliongezeka na kufikia sita na mwaka 2010 wamefikia 26. Mwenyekiti pia ameufanya mwaka huu kuwa wa wanawake kitaifa na ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa,” alisema Lymo.
    Mbali na viongozi wa chama, alikuwapo pia Sheikh Rajab Katimba kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ambaye alimsifu Mbowe na kuomba agombee tena nafasi hiyo.
    Baada ya Mratibu wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Nickson Tugara kummwagia sifa Mbowe, Mapigo Saba alimkabidhi fomu, huku makada wakiimba, ‘Jembe, jembe, jembe…”
    Mbowe aliishukuru Kamati Kuu ya chama hicho kwa kupanga uchaguzi Septemba 14, mwaka huu ambayo ni siku yake ya kuzaliwa huku akiahidi kujenga chama imara.
    “Mtaiona Chadema mpya ifikapo Septemba 14. Hiki chama hakitakufa na hatutamvumilia mtu yeyote wa kabila lolote atakayekivuruga,” alisema.
    Mbowe alisema hajawahi kuomba kugombea uenyekiti wa chama hicho tangu aliponza mwaka 2000… “Napata wakati mgumu ninapofikia wakati huu.
    Chadema ina watu mbalimbali wenye taaluma na uzoefu, kwa nini mimi? Makundi haya yaliyojitokeza kunichukulia fomu yanaweza kutafsiriwa na wapenda majungu kuwa nimepanga mimi.
    “Leo ni mara ya tatu naombwa kugombea uenyekiti, sijawahi kuomba. Mwaka 2004, Mzee Makani aliniomba nikamkatalia, lakini akaunda kikundi cha wazee walionichukulia fomu.
    Mwaka 2005, chama hakikuwa na mgombea urais, awali alijitokeza Profesa Mwesiga Baregu lakini akajitoa, nikaambiwa nibebe mzigo. Mwaka 2009 nikaombwa tena kugombea.”
    Alisema amedhamiria kujenga chama kimtandao na kimfumo ili kuondokana na mfumo wa kienyeji… “Huko nyuma wakati wa uchaguzi watu walipeana tu nyadhifa kiundugu tukadhani chama kimeongezeka. Lakini wakati huu uchaguzi umefanyika kwa miezi tisa.
    Tulisema hatuwezi kufanya uchaguzi wa Taifa bila kupata viongozi wa mkoa, wilaya, kata, kijiji na mtaa, kitongoji na shina.
    Tumefanya uchaguzi, watu wamepima na kuona mambo magumu, mara unasikia wanakimbia wakisema wameacha uenyekiti, uache wakati chama kinakua?”

     

  • Aliyekuwa Mkurugenzi TBS Ekelege Apatikana Na Hatia Afungwa Mwaka

    Aliyekuwa Mkurugenzi TBS Ekelege Apatikana Na Hatia Afungwa Mwaka

    ekelege

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jana imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege na kumwamuru kurejesha Dola za Marekani 42,543 (Sh68,068,800).
    Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando alimtia hatiani Ekelege baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka, vielelezo na ushahidi wa utetezi uliotolewa na mshtakiwa.
    Hakimu Mmbando alisema katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulithibitisha mashtaka yote yanayomkabili Ekelege pasipo kuacha shaka na kumhukumu kifungo hicho.
    Mmbando alisema viongozi wapo kwa ajili ya kulinda masilahi na rasilimali za nchi ili wananchi waweze kuifurahia keki ya Taifa na siyo kufuata matakwa yao.
    Alisema kiongozi kama Ekelege aliaminiwa na kuteuliwa na Rais ili aweze kuiongoza TBS ambayo ni sehemu ya chanzo cha mapato ya nchi, hivyo kuzembea kwake na kusababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha, hapaswi kuonewa huruma ili iwe fundisho kwa viongozi wengine.
    Katika shtaka la kwanza la kutumia madaraka yake vibaya kwa kuziondolea asilimia 50 ya ada ya utawala, Kampuni za Jaffar Mohamed Ali na Quality Motors, Ekelege alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.
    Katika shtaka la pili la kuondoa ada za kampuni hizo bila idhini ya Baraza la Utendaji kinyume na utaratibu wa TBS pia alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na katika shtaka la tatu la kusababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha alifungwa tena kifungo kingine cha mwaka mmoja jela.
    Hakimu Mmbando alisema vifungo hivyo vitakwenda pamoja, hivyo mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela na kurejesha Sh68,068,800 anazodaiwa kulisababishia shirika hilo hasara kwa uzembe.
    Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Janeth Machulya alisema kwa kuzingatia uzito wa mashtaka aliyotenda Ekelege na alivyoshindwa kuitumikia dhamana aliyopewa, anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa viongozi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.
    Machulya aliiomba mahakama wakati ikifikiria kutoa adhabu kwa Ekelege izingatie sheria ya uhujumu uchumi.
    Wakili aliyekuwa akimtetea Ekelege, Majura Magafu aliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwa kuwa ni kosa lake la kwanza, ana familia ya mke, watoto na wazee wanaomtegemea.
    Katika utetezi wake, Ekelege alikana kusababisha hasara kwa kutoa msamaha, akisema hali hiyo ilitokana na udanganyifu uliofanywa na kampuni husika.
    Alidai kuwa kampuni hizo zilidanganya na kusababisha kutoa uamuzi mwingine ambao haukuwa sahihi na bodi ya wakurugenzi ya TBS ilipoitishwa iliridhia kuwa msamaha huo haukutolewa kwa makusudi.
    Alisema kwa kuwa TBS haikuwa na historia ya kutoa msamaha hiyo na kwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza na kampuni hizo hazikuwa na uaminifu, aliiomba Mahakama imwachie huru.
    Akijitetea, alisema kampuni ya Jaffar Mohamed Ali ilipata msamaha baada ya kuwasilisha maombi yake ikidai kuwapo kwa ushindani uliotokana na wakala mwenzake, Total Otomotive Services, aliyekuwa akifanya mchezo mchafu wa kuvuta wateja kwa kutokagua viwango vya ubora wa magari yao na kuwapa vyeti vya ubora.
    Alidai kuwa menejimenti ya TBS iliijadili na kukubaliana na matatizo hayo na ikatoa msamaha kwa kipindi cha Oktoba 2007 na Machi 2008 na alitakiwa kuanza kulipa tozo na gharama zake ifikapo Aprili Mosi, 2008.

     

  • HALIMA MDEE AMWAGA MACHOZI BAADA YA KUKABIDHIWA FOMU YA KUGOMBEA UENYEKITI!

    HALIMA MDEE AMWAGA MACHOZI BAADA YA KUKABIDHIWA FOMU YA KUGOMBEA UENYEKITI!

    Halima Mdee

    Vigogo wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), watachuana katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyekiti wa baraza hilo baada ya jana baadhi ya wanawake kujitokeza kumchukulia fomu Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.Mbunge huyo anaungana na Mbunge wa Viti Maalumu, Chiku Abwao na wanachama wengine, Lilian Wasira na Sophia Mwakagenda ambao nao wamesharejesha fomu kuwania nafasi hiyo inayoshikiliwa na Suzan Lyimo. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Agosti 30 na uchaguzi unatarajiwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu.
    Wanawake zaidi ya 30 kutoka Kinondoni, Kawe, Pwani na Ubungo jana saa 5.20 asubuhi, walifika katika ofisi za Bawacha jijini Dar es Salaam kumchukulia fomu Mdee wanayedai kuwa ndiye anayestahiki kuliongoza baraza hilo kutokana na msimamo wake wa uongozi wa kutotaka kuyumbishwa.
    “Tumekaa na kutafakari ili kumpata mwanamke atakayeweza kuliongoza baraza hili kwa kututoa hapa tulipo na kutupeleka mbele zaidi, tumeona Halima Mdee anatufaa zaidi ndiyo maana tumeamua kuja kumchukulia fomu,” alisema Felister Njau, Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kawe.
    Huku akishangiliwa na wenzake alisema, “Tunakwenda kumtafuta sehemu yoyote alipo ili tukamkabidhi hii fomu na tutamwomba akubali ombi letu.”
    Msafara wa wanawake hao wakiwa na fomu yao mkononi ukiongozwa na Mwenyekiti wa Wazee Kata ya Kunduchi, Elefedina Mali ulikwenda makao makuu ya chama hicho ambako walimkuta Mdee na kumkabidhi fomu hiyo.
    Huku akibubujikwa na machozi, Mdee (pichani) alisema; “Nimewaelewa naombeni nikajitafakari kwanza, nitawaeleza nitakachoamua.” Wanawake hao pia walichangishana fedha Sh53,000 walizomkabidhi Mdee kwa ajili ya kurejeshea fomu hiyo.Aliwashukuru na kuwaomba wamvumilie kwani anahitaji muda wa kulitafakari ombi hilo.

     

  • Serikali Yaridhishwa Na Maendelea Ya Mradi Wa Mabasi Yaendayo kasi

    Serikali Yaridhishwa Na Maendelea Ya Mradi Wa Mabasi Yaendayo kasi

    Hawa Ghasia

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia ameridhishwa na tathimini ya mkutano wa mashauriaono wa awamu ya kwanza wa Mradi wa Mabasi yaendeyo Haraka (DART) uliofanyika hivi karibuni ukiwemo pia na wa kampuni ya Simon Group inayomiliki mabasi ya UDA na wamiliki wa usafirishaji jijini Dar es Salaam.

  • Arsenal Yaifunga 1-0 Besiktas Na Kufuzu UEFA Kwa Msimu Wa 17 Mfululizo

    Arsenal Yaifunga 1-0 Besiktas Na Kufuzu UEFA Kwa Msimu Wa 17 Mfululizo

    Arsenal

    Timu Ya Arsenal ya nchini Uingereza jana usiku iliweza kufuzu kucheza mashindano ya kombe la UEFA kwa msimu wa 17  mfululizo kwa timu za Ulaya baada ya kuichapa timu ya Besiktas ya Uturuki kwa bao 1-0.

    Katika mchezo wa awali wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana na hivyo kusubiri uamuzi wa nani atavuka katika mechi ya pili ya marudiano ambayo ilichezwa jana usiku. Alikuwa ni mchezaji mpya wa timu ya Arsenal aliyejiunga msumu huu akitokea timu ya FC Barcelona Alex  Sanchez, ambaye ndiye aliyeiwezesha Arsenal kusonga mbele baada ya kuipatia timu yake bao hilo pekee la ushindi kwa timu yake katika dakika ya 46 ya kipindi cha kwanza.

    Arsenal ilipata nafasi ya kumaliza mchezo huo mapema lakini washambuliaji wake Santi Cazorla na Alex Chamberlain walipoteza nafasi nyingi za wazi walizopata.

    Timu ya Arsenal ilipata pigo la kupungukiwa na mchezaji mmoja uwanjani, zikiwa zimesalia dakika 15 kabla ya kumalizika kwa mchezo,  baada ya mchezaji wake Mathieu De Buchy kutolewa nje ya mchezo kwa kadi mbili za njano na kufanikiwa kupambana wakilinda ushindi wao kiduchu hadi mwisho wa mchezo.

    Timu nyingine zilizofuzu pamoja na Arsenal katika kinyang’anyiro cha kufuzu jana usiku ni pamoja na Atletico Bilbao 3-1 dhidi ya Napoli,  Bayer 04 Leverkusen 4-0 dhidi ya FC Copenhagen, Ludogorets Razgrad 1-0 dhidi ya Steau Bucharest na Malmo FF – 3-0 dhidi ya Fc Red Bull Salzburg.

     

     

     

     

  • P Square Kuachia Nyimbo Tatu Leo Ndani Ya Saa 48, Moja Ni Kolabo Na TI

    P Square Kuachia Nyimbo Tatu Leo Ndani Ya Saa 48, Moja Ni Kolabo Na TI

    Kundi la muziki la Mapacha wawili wa Ki Nigeria P Square kuanzia Alhamisi ya leo na ndani ya masaa 48 wanategemewa kuachia nyimbo tatu mfululizo moja kati ya hizo ikiwa collabo kali ya kimataifa.
    Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa meneja wa wasanii hao Jude Okoye ambaye pia ni kaka yao wasanii hao wataachia nyimbo hizo kupitia record lebo yao ya Square Music. Wasanii hao ambao wamejijengea sifa kubwa ulimwenguni kote kwa sasa wanatamba na kibao cha “Taste The Money”.
    Nyimbo hizo ni pamoja na “Ejeajo” waliyomshirikisha rapa wa Ki Marekani TI ambayo itatoka na Video yake inayosemekana kuwa kali sana ikifuatiwa na wimbo “Shekini “ kabla ya kuhitimisha na wimbo wa tatu “Bring it On” waliomshirikisha Dave Sott.

  • Man UTD Yachapwa 4-0. Van Gaal Alaumu Wachezaji Wake

    Man UTD Yachapwa 4-0. Van Gaal Alaumu Wachezaji Wake

    Van GaalBaada ya kipigo cha magoli 4-0 dhidi ya timu yake,  Meneja wa klabu ya Man Utd Van Gaal amelia na kikosi chake ambacho jana usiku kiliendelea kupata matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu mpya wa soka huko nchini Uingereza Agosti 16.
    Kocha Van Gaal amesema kikosi chake hakikucheza vizuri wakati wa mchezo wa michuano ya kombe la ligi dhidi ya klabu ya Milton Keynes Dons ambao waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri na kuwatupa nje ya michuano hiyo mashetani wekundu.
    Pia Van Gaal amesema makosa madogo madogo yaliyofanywa na wachezaji wake wa safu ya ulinzi yalitoa mwanya mkubwa kwa wapinzani wao kupata mabao kwa urahisi. Akiendelea kulalamika kocha huyo alisema hana budi kuwasilisha lawama zake kwa wachezaji aliokuwa amewapa jukumu la kucheza mechi ya jana usiku.

  • Mapigano Baina Ya Israel Na Wapalestina Yasimama Gaza

    Mapigano Baina Ya Israel Na Wapalestina Yasimama Gaza

    Gaza

    Israel na wapiganaji wa Ki Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano kwa muda mrefu katika ukanda wa Gaza.
    Kusitishwa kwa mapigano hayo, kumehitimisha wiki saba za vita vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 2,200, wengi wao wakiwa Wapalestina. Mazungumzo hayo yalisimamiwa na Misri na yalianza kutekelezwa jana kuanzia majira ya saa moja usiku.
    Hamas wamesema mpango huo unawakilisha “ushindi wa upinzani wao”.Maafisa wa Israel wamesema Israel italegeza vikwazo ilivyoiwekea Gaza ili kuruhusu misaada na vifaa vya ujenzi kuingia Gaza.
    Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas ametangaza kukubaliana na mpango wa kusitisha mapigano.Msemaji wa serikali ya Israeli, Mark Regev amesema: “hebu tuwe na matumaini kwamba mpango huu wa kusitisha mapigano utaheshimika”
    Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja katika masuala yenye utata, ikiwa ni pamoja na wito wa Israel wa kuyataka makundi ya wapiganaji yanapokonywa silaha, yataanza mjini Cairo katika kipindi cha mwezi mmoja.
    Marekani imeunga mkono kikamilifu mpango huu, kwa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Jen Psaki kusema: “tunaunga mkono kikamilifu tangazo la kusitisha mapigano.”
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia amepongeza mpango huo wa kusitisha mapigano. Lakini katika taarifa kupitia kwa msemaji wake, Bwana Ban ameonya kuwa “jitihada yoyote ya amani ambayo haishughulikii chanzo halisi cha mgogoro, itafanya kazi kidogo kuliko kutengeneza mzunguko mwingine wa ghasia”.
    Hatua ya kusitisha mapigano imekuja huku Israel na Wapalestina wakiendelea kushambuliana.
    Kombora la dakika ya mwisho ya makabiliano kutoka Gaza limemuua raia wa Israel na kuwajeruhi wengine sita katika Barazala la Jimbo la Eshkol.
    Mapema Jumanne, Wapalestina wapatao sita waliuawa katika mfululizo wa mashambulio ya anga ya Israel huko in Gaza, Wamesema maofisa wa Palestina.
    Maofisa wa Palestina wamesema pendekezo la Misri la kusitisha mapigano linataka kumalizwa kwa uhasama kusiko na kikomo, kufunguliwa haraka kwa mipaka ya Gaza na Israel na Misri na kuongezewa ukanda wa uvuvi katika bahari ya Mediterani..
    Tangazo la kusitisha mapigano lilishangiliwa na Wapalestina katika mji wa Gaza.
    Kabla ya kuanza utekelezaji wa mpango huo, majengo marefu mjini Gaza yalishambuliwa na makombora zaidi yalipiga Israel.
    Mwezi mmoja baadaye Israel na vikundi vya Wapalestina vitajadili ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege huko Gaza na kuwaachilia huru wafungwa 100
    Israel na Misri pia zimesemekana kutaka kuhakikishiwa kuwa silaha hazitaingizwa Gaza kwa njia ya magendo.