Author: EFM

  • Winnie Mandela afariki dunia Afrika Kusini akiwa na miaka 81

    Winnie Mandela afariki dunia Afrika Kusini akiwa na miaka 81

    Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81.
    Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.
    Winnie alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe – Nelson Mandela – walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw Mandela.
    Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27.
    Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata.
    Msemaji wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa: “Amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka hospitalini mara kwa mara tangu mwnazo wa mwaka.
    “Alifariki kwa amani mapema Jumatatu adhuhuri akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake.”
    Askofu mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama “ishara kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi,” kwa mujibu wa AFP.
    Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa.
    Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa.
    Katika kipindi chote cha miaka 27 mumewe alipokuwa gerezani bila matumaini ya kuachiwa huru kutokana na hukumu ya kifungo cha maisha jela alichopewa mwaka 1964, Bi Winnie alilazimika kubeba jukumu la ulezi wa watoto na pia kuendeleza kampeni za kisiasa kutaka mashujaa wa kupigania nchi yao waachiwe huru hasa mumewe.
    “Kamwe hatutapoteza matumaini na watu wangu hawatapoteza matumaini kamwe, bila shaka tunatarajia kwamba kazi itaendelea,” alisema wakati huo.
    Kutokana na hayo Bi Winnie Mandela alilazimishwa kusalia tu huko Brandford katika jimbo lao la Orange Free katika miaka ya 70 baada ya operesheni mojawapo za kupambana na ubaguzi wa rangi zilizokuja kujulikana zaidi kama the Soweto Uprising.

    Kama ilivyomtokea mumewe, Bi Winnie alifungwa gerezani, na hata kuwekwa katika kizuizi cha pekee yake ambacho ni mojawapo ya vifungo vigumu zaidi gerezani vinavyowaathiri wafungwa kisaikolojia.
    Lakini baada ya kuachiwa kwake mtindo wa mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangi ulianza kupata sifa mbaya hasa pale alipoonekana kuendekeza tabia ya kuwavisha tairi shingoni wale waliolengwa kwa tuhuma za usaliti na kisha kuwachoma moto.
    “Kwa ‘mikufu yetu’ tutaikomboa nchi hii,” alizoea kusema.
    Mambo yalizidi kumwendea mrama kutokana na matendo ya baadhi ya walinzi wake katika kile kikundi kilijulikana kama the Mandela United Football Club.
    Walipatikana kuhusika katika kitendo cha kumteka nyara na kumuua kijana mmoja mwenye umri wa miaka 14 aitwae Stompie Moeketsi -kwa tuhuma za kwamba alikuwa akitoa siri kwa maadui zao.
    Japo Bi Winnie Mandela aliepuka hukumu ya kifungo jela – baadaye tume ya ukweli na maridhiano iliyoongozwa na askofu Desmond Tutu, iliyokuwa inachunguza ukweli kuhusu matendo tata katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta maridhiano, ilimpata Bi Mandela na hatia ya kutowajibika kisiasa wala kimaadili wakati wa kitendo hicho.

    Winnie Mandela mkutano mkuu wa ANC 54th ANC Johannesburg.Haki miliki ya pichaAFP
    Image caption
    Winnie Mandela alidumisha uhusiano na mumewe wa zamani licha yao kutalikiana mwaka 1996
    Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81.
    Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.
    Winnie alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe – Nelson Mandela – walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw Mandela.
    Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27.
    Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata.
    Msemaji wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa: “Amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka hospitalini mara kwa mara tangu mwnazo wa mwaka.
    “Alifariki kwa amani mapema Jumatatu adhuhuri akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake.”
    Askofu mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama “ishara kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi,” kwa mujibu wa AFP.
    Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa.
    Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa.
    Katika kipindi chote cha miaka 27 mumewe alipokuwa gerezani bila matumaini ya kuachiwa huru kutokana na hukumu ya kifungo cha maisha jela alichopewa mwaka 1964, Bi Winnie alilazimika kubeba jukumu la ulezi wa watoto na pia kuendeleza kampeni za kisiasa kutaka mashujaa wa kupigania nchi yao waachiwe huru hasa mumewe.
    “Kamwe hatutapoteza matumaini na watu wangu hawatapoteza matumaini kamwe, bila shaka tunatarajia kwamba kazi itaendelea,” alisema wakati huo.
    Kutokana na hayo Bi Winnie Mandela alilazimishwa kusalia tu huko Brandford katika jimbo lao la Orange Free katika miaka ya 70 baada ya operesheni mojawapo za kupambana na ubaguzi wa rangi zilizokuja kujulikana zaidi kama the Soweto Uprising.
    Bi Mandela (pichani mwaka 1988) alihusika makubwa kukabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangiHaki miliki ya pichaREUTERS
    Image caption
    Bi Mandela (pichani mwaka 1988) alihusika makubwa kukabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangi
    Kama ilivyomtokea mumewe, Bi Winnie alifungwa gerezani, na hata kuwekwa katika kizuizi cha pekee yake ambacho ni mojawapo ya vifungo vigumu zaidi gerezani vinavyowaathiri wafungwa kisaikolojia.
    Lakini baada ya kuachiwa kwake mtindo wa mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangi ulianza kupata sifa mbaya hasa pale alipoonekana kuendekeza tabia ya kuwavisha tairi shingoni wale waliolengwa kwa tuhuma za usaliti na kisha kuwachoma moto.
    “Kwa ‘mikufu yetu’ tutaikomboa nchi hii,” alizoea kusema.
    Mambo yalizidi kumwendea mrama kutokana na matendo ya baadhi ya walinzi wake katika kile kikundi kilijulikana kama the Mandela United Football Club.
    Walipatikana kuhusika katika kitendo cha kumteka nyara na kumuua kijana mmoja mwenye umri wa miaka 14 aitwae Stompie Moeketsi -kwa tuhuma za kwamba alikuwa akitoa siri kwa maadui zao.
    Japo Bi Winnie Mandela aliepuka hukumu ya kifungo jela – baadaye tume ya ukweli na maridhiano iliyoongozwa na askofu Desmond Tutu, iliyokuwa inachunguza ukweli kuhusu matendo tata katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta maridhiano, ilimpata Bi Mandela na hatia ya kutowajibika kisiasa wala kimaadili wakati wa kitendo hicho.
    ANC leader Nelson Mandela and wife Winnie raise fists upon his release from Victor Verster prison, 11 February 1990 in PaarlHaki miliki ya pichaAFP
    Image caption
    Nelson na Winnie Mandela baada yake kuachiliwa huru Februari 1990
    Licha ya misukosuko hiyo Bi Mandela alibaki kuwa mtu muhimu sana katika siasa za Afrika kusini na kuwa mwakilishi muhimu waa wanawake waliopambana kufa na kupona dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi uliokuwa unaendelezwa na Wazungu walio wachache nchini humo.
    Katika siku za baada ya uhuru wa Afrika Kusini anakumbukwa zaidi kwa kuwa miongoni mwa wachache katika uongozi wa ANC waliomuunga mkono aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo mbeki katika kushtumu na kulaani vikali vitendo vya kuwashambulia wahamiaji wa Kiafrika huko nchini Afrika Kusini.
    KUSINI – mashambulio yaliyobadikwa jina xenophobic attack. Pia amekuwa muungaji mkono mkubwa wa kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters CHA Julius Malema , kilichojimegua kutoka ANC ambacho kilimkosoa vikali rais aliyelazimika kung’atuka Jacob Zuma.
    Historia ya Bi Winnie Madikizela Mandela, hadi kifo chake inabaki akikumbukwa zaidi kama mama wa taifa la Afrika kusini aliyesimama kidete dhidi ya ubaguzi wa rangi katika umri wake wote.

  • Waziri mkuu Kassim Majaliwa awasihi viongozi wa kidini wakumbatie amani

    Waziri mkuu Kassim Majaliwa awasihi viongozi wa kidini wakumbatie amani

    Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa

    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini popote walipo wahakikishe wanaipigania na kuilinda amani kwa kila hali ikiwani pamoja na kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani.
    Wito huu unatolewa siku chache baada ya baadhi ya makanisa ya kikristo kukosoa utendaji wake.

    Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) kusema kuwa Umoja na amani ya Tanzania viko hatarini.
    Katika waraka wa ujumbe wa pasaka uliosambaa katika mitandao ya kijamii , baraza hilo liliorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.
    Waraka uliyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.
    Maaskofu waonya kuhusu Umoja na amani ya Tanzania
    Ujumbe huo kutoka baraza la maaskofu wa KKKT ulitolewa siku chache tu baada ya ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki.
    “Shughuli za kisiasa kama vile maandamano, mikutano ya hadhara, ambayo ni haki ya kila raia, vinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola”, ilieleza sehemu ya waraka huo wa Maaskofu wa kanisa Katoliki
    Akizungumza na viongozi wa kiislam Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali inatambua umuhimu wa dini: ”dini ni taasisi muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku ndio maana Serikali inaheshimu na kuzitambua dini zote kutokana na mchango wake mkubwa katika amani ya nchiyetu. Niwaombe viongozi wangu popote mlipo muilinde amani yetu”

    Cc:- BBCswahili

  • Mtibwa Sugar Wawapania Azam, Kombe la FA

    Mtibwa Sugar Wawapania Azam, Kombe la FA

    Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amejipambanua na amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha leo lazima wawafunge Azam FC na kutinga hatua ya Nusu Fainali Kombe la FA.

    Mtibwa Sugar inacheza mechi ya robo fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam na Katwila anaamini wamejiandaa hasa.

    “Azam wana timu nzuri lakini kweli tumejiandaa sana na tuko Dar es Salaam kutafuta matokeo ya mechi hiyo,” alisema.

    Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uwezo wa wachezaji wa timu hizo ambao wamekuwa wakiuonyesha katika mchuano hiyo na Ligi Kuu Bara msimu huu.

    Mshindi katika mechi hiyo ataingia nusu fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

     

  • Yanga VS Singida United, Kesho Mtoto Hatumwi Dukani Kombe la FA

    Yanga VS Singida United, Kesho Mtoto Hatumwi Dukani Kombe la FA

    Kikosi cha Yanga kesho kitashuka dimbani Uwanja wa Namfua kwa ajili ya kucheza dhidi ya Singida United kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la FA.

    Yanga ambayo ilikuwa imeweka kambi ya muda mfupi mjini Morogoro, tayari ipo Singida huku ikielezwa wachezaji wake wote wapo fiti kiafya.

    Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema wachezaji wote wapo sawa kuelekea mchezo huo, na jukumu limesalia kwa Mwalimu, George Lwandamina, kuamua nani amuanzishe.

    Singida itakuwa inaikaribisha Yanga ikiwa na kumbukumbu za kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya ligi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Namfua Stadium.
    Timu itakayoshinda katika mechi hiyo itaungana na Stand United ya Shinyanga kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho iliyotinga jana kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC.

  • Tanzania Yaombwa Kuwa Mwenyeji Kombe la Kagame

    Tanzania Yaombwa Kuwa Mwenyeji Kombe la Kagame

    Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepokea barua kutoka CECAFA ikiomba Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame kwa ngazi ya klabu.

    TFF imepokea barua hiyo leo ikiitaka Tanzania iwe mwenyeji wa michuano hiyo ambayo mara nyingi hufanyika jijini Dar es Salaam inapotokea Tanzania kwa mwenyeji.

    Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amethibitisha shirikisho hilo kupokea barua hiyo na kuahidi kuifanyia kazi.

    “Ni kweli tumepokea barua ya CECAFA ikiomba Tanzania tuwe wenyeji wa michuano ya Kagame, tutaifanyia kazi na tujajua kipi cha kufanya” amesema Ndimbo.

    Michuan hiyo inayohusisha nchi za Afrika Mashariki na Kati inatarajia kuanza Juni mwaka huu.

  • Madereva wa Daladala Mwanza Wagoma Kutoa Huduma ya Usafiri

    Madereva wa Daladala Mwanza Wagoma Kutoa Huduma ya Usafiri

    Mwanza Madereva wa Daladala wanaofanya safari zao Airpot Nyashishi na Kisesa Nyashishi wilayani Misungwi wamelazimika kugoma baada ya Sumatra kuongeza ruti bila kuongeza nauli.
    Madereva hao wamelalamikia kitendo hicho kwakuwa ruti iliyopangwa sumatra haijatoa bei elekezi nauli itakuwa sh
    Ngapi, kutokana na umbali.

    Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Anthon Bahebe ameliomba Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani pamoja na mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa Majini na nchi kavu sumatra kusimamia suala hilo ili kuepusha adha wanayoipata Abiria.

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Madereva wa Daladala mkoani Mwanza Hassan Dede amekiri kuwepo kwa suala hilo na kusema kuwa bado kuna baadhi changamoto katika ruti hiyo hali ambayo imekuwa ikisababisha kuwepo kwa tatizo hilo.
    Akizungumzia changamoto hiyo afisa leseni wa sumatra mkoani Mwanza Daniel Chilongani amesema kuwa tayari mamlaka hayo yanaendelea kushughulikiwa.

  • Trump apongeza mazungumzo kati ya rais Xi na Kim

    Trump apongeza mazungumzo kati ya rais Xi na Kim

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema leo kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yuko tayari kukutana naye. Kauli hiyo inaashiria kuwa mkutano wa kihistoria unaopangwa kati yake na kiongozi huyo anayetengwa wa nchi ya bara Asia utaendelea. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Trump ameandika kuwa alipokea ujumbe jana usiku kutoka kwa rais wa China Xi Jinping ukimweleza kuwa mkutano kati yake na Kim Jong Un uliendelea vizuri na kwamba Kim anatarajia kukutana naye. Ameendelea kusema kuwa kwa sasa shinikizo pamoja na vikwazo vya juu vilivyowekwa dhidi ya Korea Kaskazini sharti vitekelezwe kwa vyovyote vile. Trump ameongeza kuwa yeye pia anatarajia kukutana na Kim. China ilitangaza leo kuwa Kim alizuru nchi hiyo na kukutana na Rais Xi. Kim alisema nchi yake iko tayari kuachana na mipango ya silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea.

  • Miguna Miguna : Mwanasiasa wa upinzani atimuliwa tena kutoka Kenya na kupelekwa Dubai

    Miguna Miguna : Mwanasiasa wa upinzani atimuliwa tena kutoka Kenya na kupelekwa Dubai

    Mwanasiasa wa upinzani Kenya aliyeidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa ‘Rais wa Wananchi’ Januari Miguna Miguna ametimuliwa tena kutoka nchini humo.
    Mwanasiasa huyo ametimuliwa huku mzozo kuhusu uraia wake ukiendelea.
    Bw Miguna ameandika kwenye Facebook kwamba ameamka na kujipata yuko Dubai na kwamba anahitaji matibabu.
    Amesema anafahamu kwamba kuna mpango wa kumpeleka London lakini anataka kupanda ndege ya kurejea Nairobi pekee.
    Mwanasiasa huyo amesema amesindikizwa na afisa wa idara ya ujasusi.

    Serikali imechukua hatua hiyo licha ya kuwepo kwa maagizo ya mahakama ya kuzuia kutimuliwa kwake na ya kuitaka serikali kufanikisha kurejea kwake nchini humo.
    Mawakili wa Bw Miguna wamethibitisha kwamba aliondolewa nchini humo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates iliyokuwa inaelekea Dubai.
    Bw Miguna alikuwa amezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) tangu alipowasili Jumatatu adhuhuri.
    Mwanasiasa huyo alikuwa anajaribu kurejea kutoka Canada ambako alikuwa amepelekwa baada ya kufurushwa kutoka Kenya kwa lazima mwezi Februari.

    Jaji wa Mahakama Kuu George Odunga Jumatano alisema waziri wa usalama nchini humo, mkuu wa polisi na mkuu wa idara ya uhamiaji watakuwa wamekaidi maagizo ya mahakama iwapo wangekataa kumwachilia huru.
    Alikuwa ametoa ilani kwa watatu hao kufika mahakamani baadaye Jumatano lakini baada yao kukosa kufika akawapata na hatia ya kukaidi agizo la mahakama.
    Aliahidi kutoa adhabu dhidi yao leo asubuhi.
    Maafisa wa Kenya mnamo 6 Febuari walikuwa wamemfukuza kutoka nchini humo kutokana na mchango wake wakati wa kuapishwa kwa Bw Odinga.
    Walisema mwanasiasa huyo hana uraia wa Kenya lakini ana uraia wa Canada.
    Idara ya uhamiaji ya Kenya imekariri kuwa Miguna alipoteza uraia wa Kenya mwaka 1998 alipopewa uraia wa Canada wakati ilipokuwa ni kinyume cha sheria kuwa na uraia wa nchi mbili nchini Kenya.

    Kuzuiliwa kwa Bw Miguna kumejadiliwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii Kenya, baadhi wakiunga mkono hatua hiyo lakini wengine wakiwashutumu maafisa wa uwanja wa ndege na serikali.
    Mmoja wa mawakili wa Bw Miguna, Nelson Havi, ni miongoni mwa waliokuwa wa kwanza kufichua kwamba Bw Miguna alikuwa ametimuliwa tena nje ya nchi hiyo.

    Mawakili kushambuliwa
    Usiku wa kuamkia Jumanne, kabla ya kusafirishwa kwa Miguna kwenda Dubai, mawakili James Orengo, Julie Soweto, Nelson Havi na Cliff Ombeta walikuwa wamefika uwanja wa ndege wa JKIA kujaribu kuwasilisha ilani ya mahakama ya kuwataka maafisa wa uhamiaji kutomsafirisha nje ya nchi Bw Miguna.
    Lakini taarifa za vyombo vya habari zinasema walishambuliwa na kupigwa na maafisa wa usalama katika uwanja huo.
    Wanahabari hawajaruhusiwa pia kuingia tena uwanja huo. Baadhi walidaiwa kupigwa na kuumizwa na maafisa wa polisi wakati wa jaribio la kwanza la kumsafirisha Bw Miguna kwenda Dubai usiku wa kuamkia Jumanne.
    Jumanne Roselyn Aburili alikuwa ametoa agizo Bw Miguna aachiliwe huru. Mawakili Orengo na Otiende Amollo walibandika agizo la mahakama katika milango ya afisi za uhamiaji JKIA na makao makuu ya polisi.
    Baadaye Bw Havi alijaribu kuwapasha habari maafisa hao kupitia mtandao wa Twitter hatua ambayo haikupokelewa vyema na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mwenda Njoka.

    Bw. Njoka alisema hawawezi kupokea ilani ya mahakama kupitia mitandao ya kijamii.
    Kukamatwa kwa Miguna mara ya kwanza
    Bw Miguna alikamatwa na polisi kwa mchango wake katika kuapishwa kwa Bw Odinga kuwa “Rais wa Wananchi”, hafla iliyofanyika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi mnamo 30 Januari.
    Bw Miguna, ambaye pia ni wakili, ndiye aliyetia saini hati ya kiapo ya Bw Odinga.
    Serikali ilikuwa imeeleza hatua hiyo ya kiongozi huyo wa upinzani kuwa uhaini wa hali ya juu.
    Odinga apendekeza serikali ya muda iundwe Kenya
    Bw Odinga anadai kwamba alimshinda Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa 8 Agosti ambao matokeo yake yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu kwa sababu ya kutokea kwa kasoro nyingi.
    Muungano wa upinzani Kenya unaelekea ukingoni?
    Serikali yamfurusha Miguna Miguna kutoka Kenya
    Mahakama iliamuru uchaguzi mpya ufanyike lakini Bw Odinga akasusia uchaguzi huo mnamo 26 Oktoba na kutangaza kwamba hakumtambua Bw Kenyatta kama rais halali wa nchi hiyo.
    Baadaye aliongoza hafla ya kuapishwa kwake mnamo tarehe 30 Januari.
    Mapema mwezi huu, Bw Odinga na Rais Uhuru Kenyatta walikutana katika mkutano ambao haukuwa umetarajiwa na wakahutubia wananchi moja kwa moja kupitia vyombo vya habari.
    Waliahidi maridhiano na pia wakaahidi kuwaunganisha tena Wakenya.
    Bw Miguna mnamo Jumatano alikuwa ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumanne kwamba alikuwa anazuiliwa chooni uwanja wa ndege na kwamba alikuwa amezuiwa kuwaona mawakili wake na jamaa zake.
    Miguna alipoteza uraia wake?
    Chini ya Kifungu 17 cha Katiba ya Kenya, mtu aliyezaliwa nchini Kenya anaweza tu kuupoteza uraia wake iwapo itabainika kwamba aliupata uraia huo kwa njia ya ulaghai, au ibainike kwamba mtu huyo au wazazi wake walikuwa raia wa nchi nyingine, au ibainike kwamba mtu huyo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka minane alipogunduliwa akiishi Kenya.
    Serikali ya Kenya imekuwa ikisisitiza kwamba chini ya katiba ya zamani, Wakenya hawangekuwa na uraia wa nchi mbili.
    Serikali inasema hatua ya Bw Miguna ya kupata pasipoti ya Canada mwaka 1988 ina maana kwamba aliupoteza uraia wa Kenya wakati huo.
    Raila Odinga: ”Hatutambui uchaguzi wa Uhuru Kenyatta”
    Ingawa Bw Miguna aliwasilisha maombi na akapewa pasipoti ya Kenya mwaka 2009, serikali inasema pasipoti hiyo ya Kenya si halali kwa sababu hakufichua kwamba wakati huo alikuwa raia wa Canada pia.
    Serikali imesema mwanasiasa huyo hakuwasilisha tena ombi la kuruhusiwa kuwa raia wa Kenya katiba ilipofanyiwa marekebisho mwaka 2010 na Wakenya wakakubaliwa kuwa na uraia wa nchi mbili.
    Bw Miguna amekuwa akisisitiza kwamba hakuwahi kuukana uraia wake wa Kenya na kamwe hawezi kufanya hivyo.
    “Katiba iko wazi kabisa: hakuna mtu yeytoe anayeweza au anayeweza kudai kuufuta uraia wa Mkenya aliyezaliwa nchini Kenya,” alisema awali.

    cc. :- bbcswahili