Author: EFM

  • Brazil: Lula da Silva kufungwa miaka 12 jela

    Brazil: Lula da Silva kufungwa miaka 12 jela

    Luiz Inacio Lula da Silva

     

    Mahakama ya rufaa nchini Brazil imeagiza kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva, ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka kumi na miwili gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na ufisadi.
    Majaji sita kati ya kumi na mmoja wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasi wasi wa kisiasa nchini humo.

    Hatia hiyo imetokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata la rushwa linalojulikana kama ”Operation Car Wash”
    Lula aligundulika kukubali rushwa yenye thamani Euro laki saba na tisini.

    Lula da silva amekua akitarajiwa na watu wengi kusimama kama mgombea asie na ushindani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi octoba,
    Lakini ndoto hizo zimeisha baada ya mahakama kuu kuamuru mwanasiasa huyo mkongwe aanze kifungo cha miaka 12 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya ufisaidi.
    Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali, waandamanaji katika mji wa Sao Bernardo wanataka Da silva aachiwe huru.
    ” mkusanyiko wetu wa leo ni kuhakikisha kuwa rais wetu wa zamani Lula, ana haki ya kurudi kuwa mgombea wa Urais na kama kweli hawataki kumuona basi njia pekee ni kumshinda katika uchaguzo”
    Baadhi ya watu wanapinga kuachiwa huru kwa Lula Da Silva na badala yake jeshi ndio liongoze nchi hiyo.
    ”Kama mahakama kuu haitamuweka Lula jela, basi tunataka jeshi ndio lishike madaraka kwasababu taasisi zimejaa rushwa , zote hadi mahakama”
    Mbali na kukutwa na hatia Lula amekua akipinga vikali kuhusika na kashfa yoyote ya rushwa anasema kuwa amekua akipinga vikali uonevu wa aina yoyote hivyo hatakubali uonevu wa mahakama.

    Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 72 atabaki uraiani kwa muda hadi pale nyaraka za kifungo chake zitakapo kamilika.
    Lula Da silva amekua madaraki kati yam waka 2003 hadi 2011. Kama angeingia kama mgombea katika uchaguzi wa mwezi oktoba huenda angeshinda kwa kishindo kutokana na umaarufu wake.

     

  • Rufani ya Michael Richard Wabura Bado Kitendawili

    Rufani ya Michael Richard Wabura Bado Kitendawili

    Rufani ya Michael Richard Wambura bado kitendawili na hili ni baada ya kamati ya rufaa kuchelewa kutoa maamuzi. Je ni sahihi maamuzi kuchelewa ili haki itendeke au si sahihi kwa kuwa kamati hii imepokea taarifa ya pande zote mbili? Hebu tuzungumze hapa juu ya kile unachokiona kwenye sakata hili kwa kutoa comment yako.

     

  • Yanga kuwakosa wachezaji wanne kikosi cha kwanza kombe la shirikisho

    Yanga kuwakosa wachezaji wanne kikosi cha kwanza kombe la shirikisho

    Klabu ya soka ya Yanga ambayo Jumamosi hii inatarajiwa kucheza na Welayta Dicha ya Ethiopia katika kombe la shirikisho barani Afrika, itawakosa wachezaji wake wanne muhimu

    Wachezaji hao ambao wataukosa mchezo huo ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Said Makapu.

    Wachezaji hao wataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi nyingi za njano ambazo walipata kwenye michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika.

    Wapinzani hao wa Yanga wanatarajiwa kuwasili mchana wa leo (Jumatano) kwenye uwanja wa ndege wa Mwl. JK Nyerere jijini Dar es Salaam.

     

  • Gavana atuhumiwa kwa ubakaji DRC

    Gavana atuhumiwa kwa ubakaji DRC

    Naibu Gavana wa jimbo la Ikweta kusini magharibu nchini Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo ,Tathy Bikamba ameshtakiwa kwa tuhuma za ubakaji wa binti wa miaka 20 ambaye inadaiwa kuwa alimfanyia unyama huo baada ya kumpa dawa za kulevya.

    Gavana huyo anatarajiwa kufikishwa kinshasa kujibu tuhuma hizo mahakamani , ingawa wakili wake ametupia mbali tuhuma hizo.
    Taarifa kutoka duru za karibu za uchunguzi wa kesi hiyo ya kubaka vinasema kwamba gavana huyo alimbaka binti huyo siku ya Jumamosi.
    Bwana Bikamba ambaye kwa sasa yuko gerezani anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo ili aweze kujibu mashtaka yake ya kumwekea dawa ya kulevywa na kumfanyia tendo la ngono binti bila idhaa yake.
    Wakili wa gavana huyo, Imbambo Engulu ametupilia mbali tuhuma hizo na kushutumu mahakama ya jimbo hilo kwa kumzuia gavana huyo bila kujali na cheo chake
    “Kushikwa kwake ni kama uonevu, tuliomba wamuzuie kwanza nyumba kwake badala ya kumuweka gerezani moja kwa moja, majaji hawakukubali ombi letu, Nawambia kweli kuwa gavana hakufanya kitendo hicho, ni uongo.”
    Waziri wa sheria ,Faida mwangiliwa ambaye pia ni miongoni mwa wanaharati wa haki za wanawake ameomba sheria kumhukumu vikali gavana huyo ikiwa tuhuma hizo zitathbitishwa na mahakama

    Kesi za ubakaji zimeripotiwa nyingi nchini jamuhuri ya kidemokrasi ya kongo, idadi kubwa ya kesi imefanywa na waasi na wanajeshi wa taifa husuan mashariki mwa DRC.
    Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya kongo tayari kuathibu vikali askari kadhaa na maafisa wa jeshi la Kongo wengi kwa kuwapa kifungo cha maisha .

  • RONALDO REKODI MPYA UGENINI

    RONALDO REKODI MPYA UGENINI

    Ni Cristiano Ronaldo tena anaendelea kuwanyamazisha wapinzani wa Real Madrid, dakika ya 3 tu alipiga shuti lake la 9 kwa Gianluigi Buffon na kufunga bao lake la 8 dhidi ya golikipa huyo, hili likiwa bao la kwanza katika mchezo huu.

    Dakika ya 64 Cristiano Ronaldo tena aliifungia Real Madrid bao la pili na kumfanya kuwa mchezaji katika historia aliyewafunga Juve mabao mengi (9) kabla ya Marcelo kufungia bao la 3 Real Madrid.

    Hii ni mara ya kwanza Juventus wanaruhusu kufungwa mabao 3 nyumbani tangu mwaka 2009 walipofungwa bao 4-1 na Bayern Munich, Juventus walimaliza wakiwa pungufu baada ya Paulo Dyabala kuoneshwa kadi nyekundu.

    Kama hujui tu ni kwamba bao la kwanza la Madrid ndio bao la mapema zaidi kwa Cristiano Ronaldo kuwahi kufunga katika Champions League, huku sasa Mreno huyo akiwa na mabao 38 katika msimu huu(michuano yote) ikiwa ni idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote barani Ulaya.

    Tangu klabu ya Juventus wahamie katika uwanja wao mpya mwaka 2011 hawajawahi kupokea kipigo kama hiki katika uwanja huo katika mashindano yoyote yale.

     

  • TETESI: Man United kumuongezea mkataba mrefu zaidi De Gea, kumpatia mshahara wa kufa mtu

    TETESI: Man United kumuongezea mkataba mrefu zaidi De Gea, kumpatia mshahara wa kufa mtu

    Klabu ya soka ya Manchester United hawana mpango kabisa ya kumuachia David de Gea kwenda Real Madrid.

    Man United inampango wa kumuongeze mkataba wa miaka mitano mchezaji huyo na kumlipa mshahara wa paundi 350,000 kwa wiki kabla ya kuanza kwa kombe la dunia, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la The Sun.

    De Gea ambaye alitua United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid, anatarajia kumaliza mkataba wake mwaka 2019.

    Golikipa huyo amekuwa tegemezi katika kikosi cha Man United huku katika msimu huu akiwa anaongoza katika ligi kuu ya Uingereza kwa kuwa na clean Sheet 16 akifuatiwa na golikipa wa Manchester City, Ederson mwenye clean sheet 14.

  • Al-Shabab yauwa wanajeshi 4 wa Uganda

    Al-Shabab yauwa wanajeshi 4 wa Uganda

    Wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabaab la nchini Somalia.

    Wanamgambo wa kundi la kigaidi la al-Shabaab la nchini Somalia wamewauwa wanajeshi wanne wa Uganda katika shambulizi kubwa dhidi ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika, katika kambi iliyo Kusini mwa Mogadishu.

    Shambulizi hilo lilitokea jana Jumapili (Aprili 1) kwenye kambi iliyoko umbali wa kilomita 150 kusini mwa mji mkuu, Mogadishu.

    Awali, naibu gavana wa jimbo lilikotokea shambulizi hilo, Ali Noor Mohamed, hakubainisha idadi ya waliouawa, lakini alikiri kuwa wanajeshi kadhaa wa Uganda walipoteza maisha.

    Baadaye, msemaji wa jeshi la Uganda, Brigedia Richard Karemire, alithibitisha kuwa al-Shabaab imewauwa wanajeshi wao wanne na kujeruhi wengine sita. Kundi la al-Shabaab kwa upande wake limedai kuwauwa wanajeshi 59 wa Uganda.

    Pia, kundi hilo kupitia kituo chake cha redio cha Andalus limesema wapiganaji wake 14 wameuawa katika shambulizi la jana kwenye kambi ya Buula-Mareer. Msemaji wa jeshi la Uganda amesema idadi ya wanamgambo wa al-Shabab waliouawa ni 30. Umoja wa Afrika haukutoa tamko lolote kuhusu kilichotokea.

    ”Tumeona vifaru na magari mengine ya kijeshi ya Umoja wa Afrika yakiwa katika barabara nje ya mji wenye kambi iliyoshambuliwa”, alisema Maryam Ali ambaye ameshuhudia shambulizi hilo, na kuongeza kuwa baadaye aliweza kukimbia yeye na watoto wake sita, kunusuru maisha yao.

    Shambulizi hilo lilitokea jana Jumapili (Aprili 1) kwenye kambi iliyoko umbali wa kilomita 150 kusini mwa mji mkuu, Mogadishu.

    Awali, naibu gavana wa jimbo lilikotokea shambulizi hilo, Ali Noor Mohamed, hakubainisha idadi ya waliouawa, lakini alikiri kuwa wanajeshi kadhaa wa Uganda walipoteza maisha.

    Baadaye, msemaji wa jeshi la Uganda, Brigedia Richard Karemire, alithibitisha kuwa al-Shabaab imewauwa wanajeshi wao wanne na kujeruhi wengine sita. Kundi la al-Shabaab kwa upande wake limedai kuwauwa wanajeshi 59 wa Uganda.

    Pia, kundi hilo kupitia kituo chake cha redio cha Andalus limesema wapiganaji wake 14 wameuawa katika shambulizi la jana kwenye kambi ya Buula-Mareer. Msemaji wa jeshi la Uganda amesema idadi ya wanamgambo wa al-Shabab waliouawa ni 30. Umoja wa Afrika haukutoa tamko lolote kuhusu kilichotokea.

    ”Tumeona vifaru na magari mengine ya kijeshi ya Umoja wa Afrika yakiwa katika barabara nje ya mji wenye kambi iliyoshambuliwa”, alisema Maryam Ali ambaye ameshuhudia shambulizi hilo, na kuongeza kuwa baadaye aliweza kukimbia yeye na watoto wake sita, kunusuru maisha yao.

    Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia
    1. Rais Mohamed aapa kuiangamiza al-Shabab

    Äthiopien Mohamed Abdullahi Mohamed, Präsident Somalia (DW/Y. G/Egziabhare)
    Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia
    Kundi la al-Shabaab, ambalo linapigania kunzisha utawala wa Kiislamu nchini Somalia, mara kwa mara hufanya mashambulizi dhidi ya majengo ya serikali mjini Mogadishu, na pia hoteli na migahawa katika nchi hiyo ya Upembe wa Afrika inayokabiliwa na mzozo wa muda mrefu. Mwezi Oktoba, shambulizi baya zaidi liliuwa watu zaidi ya 500 mjini Mogadishu.

    Tangu kutokea shambulizi hilo, Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed ameapa kuliangamiza kundi la al-Shabab, akiungwa mkono na umma, ambao umeingia kwa maelfu mitaani, katika maandamano ya kutaka kundi hilo lipigwe vita hadi kushindwa. Hata hivyo, kundi hilo ambalo lilifukuzwa mjini Mogadishu mwaka 2011, bado linashikilia maeneo makubwa ya vijijini.

    Mwezi uliopita, nchi za Mashariki mwa Afrika zinazochangia wanajeshi 22,000 katika ujumbe wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani nchini Somalia, AMISOM, wameutaka Umoja wa Mataifa kutafakari upya azma yake ya kuuhitimisha ujumbe huo ifikapo mwaka 2020, wakisema hatua hiyo inaweza kuhujumu hatua iliyopigwa katika kuleta utulivu nchini Somalia.

  • China  Yaiongezea Ushuru wa Forodha Bidhaa za Marekani

    China Yaiongezea Ushuru wa Forodha Bidhaa za Marekani

    Baada ya kuidhinishwa na Baraza la Serikali ya China, kamati ya Ushuru wa Forodha ya China imeamua kuwa itasimamisha upunguzaji wa ushuru wa Forodha kwa bidhaa 128 za aina 8 zinazoagizwa kutoka Marekani kuanzia jana tarehe 2 Aprili, huku ikiongeza ushuru wa Forodha kwa bidhaa hizo.

    Ikumbukwe kuwa tarehe 22 Machi, Rais Donald Trump wa Marekani amesaini kumbukumbu ya kuiwekea China vikwazo kwa mujibu wa matokeo ya ripoti kuhusu ukaguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara, na kuagiza kutoza ushuru mkubwa Wa Forodha kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China, na kuweka Kikomo kwa kampuni za China kuwekeza na kununua kampuni za Marekani.

    Hili limefanyika Marekani kuwawekea vikwazo China je kwa Tanzania hatuwezi na sisi tukatumia mfumo huo ili kuiongezea Thamani bidhaa zetu za ndani kwa kuwawekea ushuru Mataifa yanayoingiza bidhaa zao nchini kwa wingi kama China ili bidhaa zetu zikanunulika kwa bei ya chini na tukaachana na za nje?

  • Simba Sc Mzigoni Leo Kuikabili Njombe Mji

    Simba Sc Mzigoni Leo Kuikabili Njombe Mji

    Simba itakuwa inakibarua dhidi ya wenyeji wa mji huo, Njombe Mji FC, katika mchezo wa ligi kuu bara utakaopigwa majira ya saa 10 jioni leo.

    Njombe Mji itakuwa inaikaribisha Simba ikiwa na kumbukumbu mbaya za kuondoshwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho na Stand United ya mjini Shinyanga.

    Tayari timu zote mbili zimeshakamilisha maandalizi kuelekea mchezo mchezo huo wa leo.

  • EFM REDIO YATIMIZA MIAKA 4 YA MAFANIKIO

    EFM REDIO YATIMIZA MIAKA 4 YA MAFANIKIO

    – EFM imetimiza miaka 4 tangu kuanzishwa kwake. Nitumie nafasi hii kuishukuru Serikali kuu,TCRA kwakuendelea kutulea na kutuamini hadi sasa tumeongeza wigo wa Matangazo yetu. Niwashukuru MaKampuni na wadau ambao wameendelea kushirikiana nasi kwa namna moja au nyingine.

    Mwisho niwashukuru sana wasikilizaji na watendaji wote wa Efm. DODOMA,MORO,TABORA,KIGOMA na ARUSHA tunawafikia Mwezi huu.. HAPPY BIRTHDAY @efmtanzania