Author: EFM

  • Teknolojia ya VAR yaibeba Italia dhidi ya Uingereza

    Teknolojia ya VAR yaibeba Italia dhidi ya Uingereza

    Teknolojia ya video (VAR) imeibeba timu ya taifa ya Itali kufanikiwa kuchomoza na sare ya bao 1 – 1 dhidi ya Uingereza mchezo wa kirafiki.

    Wakati Uingereza ikifanikiwa kuongoza mchezo huo baada ya kupata bao lake dakika ya 26 kupitia kwa Jamie Vardy kunako dakika ya 87 mchezaji wa Itali, Lorenzo Insigne akaisawazishia timu hiyo kwa msaada wa teknolojia ya VAR huko Wembley.

    Timu ya taifa ya Uingereza ilikuwa ikitarajia kupata ushindi wake wa pili baada ya kuifunga Netherlands kwa bao 1-0 lakini mwamuzi wa mchezo huo Deniz Aytekin aliamuru penati na kuifanya Italia kusawazisha na kumalizika kwa sare ya 1 – 1 baada ya kupitia VAR.

    Kikosi cha Uingereza: Butland (6), Young (7), Walker (7), Stones (6), Tarkowski (6), Trippier (7), Dier (7), Oxlade-Chamberlain (7), Sterling (8), Lingard (7), Vardy (7).

    Wachezaji wa akiba: Rose (6), Lallana (6), Rashford (6), Cook (6), Henderson (6).

    Kikosi cha Italia: Donnarumma (7), Zappacosta (6), Rugani (6), Bonucci (6), De Sciglio (7), Pellegrini (6), Jorginho (7), Parolo (6), Candreva (6), Immobile (6), Insigne (7).
    Wachezaji wa akiba: Chiesa (7), Belotti (6), Gagliardini (6).

    Kwenye mchezo huo uliyokuwa na kasi na ushindani mkubwa aliyeibuka nyota wa mchezo ni Raheem Sterling

     

  • Taifa Stars Yajiliwaza kwa DRC Congo, Yaifunga Mabao 2-0

    Taifa Stars Yajiliwaza kwa DRC Congo, Yaifunga Mabao 2-0

    Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana.

    Stars ilifunga mabao yake kipindi cha pili baada ya kile cha kwanza kwenda suluhu ya 0-0  kupitia kwa Mbwana Samatta na Shiza Ramadhan Kichuya.

    Stars ilipata ushindi huo ikiwa imetoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Algeria kwa jumla ya mabao 4-1 huko Algiers.
    Kocha wa Taifa Stars, Mayanga ameeleza kuwa mchezo huo ulikuwa vizuri kutokana na vijana wake kuonesha nidhamu na kuwa imara zaidi kwenye safu ya ulinzi, kitu ambacho kilipelekea wapinzani washindwe kupata bao.

    Aidha, Mayanga amesema Congo walishindwa kuisumbua Stars kutokana na kuwa wazito miguuni na kuwapa faida Stars kupata mabao hayo mawili.

  • Imethibitishwa Kweli Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amezuru China

    Imethibitishwa Kweli Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amezuru China

    Baada ya siku ya uvumi wa siku nyingi, imethibitishwa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amezuru China.

    Ziara hiyo, ambayo ilithibitishwa na China na Korea Kaskazini, ndiyo ya kwanza inayofahamika ya Bw Kim nje ya taifa lake tangu alipochukua mamlaka mwaka 2011.

    Bw Kim alifanya “mazungumzo ya kufana” na kiongozi wa China Xi Jinping mjini Beijing, shirika la habari la China, Xinhua liliripoti.

    China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kiuchumi na baadhi ya wachambuzi wanasema uwezekano wa wawili hao kabla ya mkutano mkuu wa Bw Kim na viongozi wa Korea Kusini na Marekani ulitarajiwa.

    Bw Kim amepangiwa kukutana na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in mwezi Aprili na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Mei.

    #BBC

  • Tiangong-1: Kituo cha safari za anga cha Uchina kinaweza kuanguka duniani ”karibuni”

    Tiangong-1: Kituo cha safari za anga cha Uchina kinaweza kuanguka duniani ”karibuni”

    Kifusi kutoka kwa kituo cha maabara cha safari za anga cha China, kinaweza kupasuka na kuanguka duniani Ijumaa,wanasayansi wanaokifanyia uchunguzi wanasema.
    Kituo hicho cha Tiangong-1 ni sehemu ya mpango wa safari za anga za mbali wa Uchina, na wa sampuli ya kituo cha safari za anga za mbali cha binadamu wa mwaka 2022.
    Kiliwekwa kwenye uzio mwaka 2011 na miaka mitano baadae kikamilisha shughuli yake, na baadae kilitarajiwa kuanguka duniani.
    Muda na mahala kitakapoangukia ni vigumu kutabiri kwasababu sasa hakidhibitiwi.
    Makadirio ya hivi karibuni ya kurejea kwa chombo hicho ni kati ya tarehe 30 Machi na 2 Aprili.

  • Uvumi waenea kuhusu ziara ya Kim Jong-un Beijing

    Uvumi waenea kuhusu ziara ya Kim Jong-un Beijing

    Kim Jong-un
    Kim Jong-un

    Uvumi waenea kuhusu ziara ya Kim Jong-un Beijing
    Uvumi kuhusu ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un mjini Beijing umehanikiza katika wakati ambapo kukiwa na gumzo kuhusu maandalizi ya mkutano wa kilele kati ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini na rais Trump.

    Mji Mkuu wa China Beijing, ulikuwa chini ya usalama mkali Jumanne, huku kukiwa na uvumi kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alikuwa anafanya ziara ya kustukiza, kufuatia ripoti za kuwasili kutoka Pyongyang, kwa treni maalumu iliyopokelewa kwa gwaride la heshima.

    Ikiwa itathibitika, hii itakuwa ziara ya kwanza ya nje ya Kim tangu alipoingia madarakani mwaka 2011, na inaashiria mabadiliko ya kushangaza katika zoezi la kidiplomasia ambalo limefungua mlango wa mikutano tofauti ya kilele kati ya Kim na marais wa Korea Kusini na Marekani.

    Baadhi ya wachambuzi wanasema China — mshirika pekee mkubwa wa Korea Kaskazini — ilikuwa imewekwa kando katika mazugumzo ya awali ya Pyongyang na Korea Kusini na Marekani, lakini ziara ya Kim itairudisha Beijing katika mlinganyo wa kidiplomasia.

    Treni maalumu inayotumiwa na familia ya kina Kim nchini Korea Kaskazini.

    Bill Bishop, mchapishaji wa jarida la habari la Cinocism China, amesema rais Xi Jinping huenda alitaka kukutana na Kim kabla ya mkutano wa kilele na Rais Donald Trump, ambao unatazamiwa kufanyika mwezi Mei.

    Bishop amlimabia shirika la habari la AFP kwamba Wachina wanahofia kuachwa nje wakati Korea Kaskazini ikitafuta kufikia makubaliano ya moja kwa moja na Marekani ambayo hayaakisi maslahi ya China.

    Usiri mkubwa

    Uwezekano wa ziara hiyo uliripotiwa kwa mara ya kwanza na shirika la habari la Japan la Kyoto, likinukuu vyanzo ambavyo halikuvitaja vikisema kwamba afisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini alikuwa amewasili katika mji mkuu wa China usiku wa Jumatatu.

    Kituo cha Televisheni cha Nippon cha nchini Japan kilitangaza picha za video zikionesha treni inayofanana na ile iliyokuwa ikitumiwa na yake Kim, marehemu Kim Jong Il — ikiwasili katika kituo cha treni cha Beijing na kupokelewa kwa heshima za kijeshi na msafara wa magari ya rangi nyeusi.

    Katika nyumba ya wageni ya Diaoyutai, ambako Kim Jong Il alikuwa akiishi wakati wa ziara zake mjini Beijing, kulikushuhudiwa uwepo mkubwa wa polisi isivyo kawaida, ambapo maafisa walikuwa wamewekwa kila baada ya mita 50 hadi 100 mbele ya jengo la kuvutia.

    Hakukuwa na utajo wa ziara yoyote katika vyombo vya habari vya ama China au Korea Kaskazini, na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua chunying, alipoulizwa iwapo Kim au afisa mwingine wa Korea Kaskazini alikuwa anaizuru Beijing, alisema hana taarifa kuhusu suala hilo.

    Ziara za huko zilizofanywa na Kim Jong Il nchini China zilikuwa pia zikigubikwa na usiri, ambapo Beijing ilikuwa ikithibitisha uwepo wake baada ya kuvuka mpaka na kurudi Korea Kaskazini kwa usafiri wa treni.

  • WAKILI ALIYEMUAPISHA RAILA ODINGA AZUHIRIWA UWANJA WA NDEGE

    WAKILI ALIYEMUAPISHA RAILA ODINGA AZUHIRIWA UWANJA WA NDEGE

    Bw Miguna

    Wakili wa upinzani aliyeidhinisha kiapo cha Bw Raila Odinga alipokuwa anajiapisha kuwa ‘Rais wa Wananchi’ mwezi Januari bado amekwama katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi.

    Bw Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

    Wakili huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea.

    Taarifa zinasema Bw Miguna, ambaye pasipoti yake ya Kenya ilitwaliwa na polisi kabla ya kuondolewa kwake Kenya mwezi jana, alikuwa ametakiwa kuwasilisha ombi la kupata visa ya kukaa Kenya kwa miezi sita kwa kutumia pasipoti hiyo yake ya Canada.

    Alikataa jaribio hilo na badala yake kutoa kitambulisho chake cha taifa kuonesha kwamba yeye ni Mkenya na kutaka aruhusiwe kuingia.

    Bw Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.

    Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.

    Wakili wa upinzani James Orengo, seneta ambaye majuzi alichaguliwa kuwa kiongozi wa upinzani Bunge la Seneti, ameambia Reuters kwamba maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliojaribu kumlazimisha Bw Miguna kupanda ndege hiyo iliyokuwa inaondoka.

    Lakini wakili huyo alikataa kuingia ndani ya ndege hiyo na mtafaruku ukazuka.

    Video iliyopeperushwa moja kwa moja na runinga ya kibinafsi ya Citizen ilimuonesha Bw Miguna akiwa kwenye lango la ndege akiwaambia wahudumu: “Siendi popote, hamuwezi kuniondoa kutoka kwa nchi yangu kwa nguvu.”

    Bw Orengo ameambia Reuters kwamba maafisa hao wa polisi baadaye walimuondoa mwanasiasa huyo kutoka kwenye ndege hiyo na kumzuilia kwa muda katika afisi za uhamiaji katika uwanja huo wa JKIA.

    Baadaye asubuhi, walimhamishia kituo cha polisi cha uwanja huo na kuendelea kumzuilia.

    Bw Odinga alikuwa amefika uwanjani humo Jumatatu usiku kujaribu kutatua mzozo huo.

    Kwa mujibu wa Bw Orengo, Bw Odinga alikuwa ametoa wito kwa serikali kumrejeshea Miguna pasipoti yake ya Kenya.

    Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uhamiaji mapema Jumanne ilisema Bw Miguna alianza “kuzua fujo na kulalamika” uwanja wa ndege na kwamba alikuwa anataka kuruhusiwa kuingia Kenya bila kuidhinishwa na maafisa wa uhamiaji.

    Wizara hiyo imesema inafanikisha utaratibu wa kumuwezesha Bw Miguna kuwasilisha tena ombi la kuwa raia wa Kenya.

    Taarifa ya wizara hiyo ilisema fomu za kuwasilisha maombi hayo zimetumwa uwanja wa Ndege.

    Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji Joseph Munywoki kwenye taarifa alisema: “Badala ya kuonesha hati za kusafiria alizotumia kwenda Canada, Miguna alianza kuzua fujo na kulalamika akisema kwamba yeye ni Mkenya na anafaa kuruhusiwa kuingia Kenya bila kupitia kwa meza ya idara ya uhamiaji kama inavyotakiwa kwa abiria wote wanaowasili bila kujali uraia wao.”

    “Hatujamzuia kuingia Kenya, tunamtaka tu afuate utaratibu kama watu wengine wote,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani

    Mwenda Njoka aliambia Reuters kwa njia ya simu

     

  • MICHAEL PETTER MSHINDI WA SHIKA NDINGA 2017

    MICHAEL PETTER MSHINDI WA SHIKA NDINGA 2017

    Michael Petter

    Michael Petter ambae ni mshiriki na mshindi wa #ShikaNdinga2017 akitoa mrejesho wa maisha yake ya biashara baada ya ushindi.

  • MIAKA MINNE (IV) E-FM YAANZA NA MSIMU WA SHIKA NDINGA.

    MIAKA MINNE (IV) E-FM YAANZA NA MSIMU WA SHIKA NDINGA.

     

    Katika kusherekea Miaka minne ya uwepo wa E Fm radio tunayo furaha sana na tuna kila sababu za kusherekea uwepo wetu.

    Wakati tunaanza tulikuwa na wafanyakazi 10 tu lakini leo hii E-fm imeajiri wafanyakazi zaidi ya 100 moja, wakati tunaanza tulikuwa tunasikika Dar-es-alaam pekee lakini leo hii E-fm inasikika kwenye mikoa 6 pia tumeweza kuwawezesha wadau wetu na mdau wetu mkubwa ni msikilizaji wa E-fm tukiwa na bidhaa kama SHIKA NDINGA ambapo tumefanikiwa kutoa magari ya biashara pamoja pikipiki maarufu kama bodaboda, tunayo pia bidhaa ya Sakasaka tumeweza kutoa mitaji lakini pia bidhaa yetu ya mchizi wangu tumemuwesha ‘Single Mother’ kwa kuwapatia mahitaji yao”.

    #SHIKA NDINGA

  • Sergei Skripal: Wanadiplomasia wa Urusi wazidi kufurushwa katika nchi mbalimbali

    Sergei Skripal: Wanadiplomasia wa Urusi wazidi kufurushwa katika nchi mbalimbali

    Malcolm Turnbull, amesema matukio haya ni kutokana na tabia zisizokubalika za Urusi

    Australia imekuwa nchi ya karibuni kufukuza wanadiplomasia wa Urusi kutoka nchini kwake kutokana na shambulio la jasusi wa zamani wa urusi nchini Uingereza Sergei Skripal na binti yake ambao wako katika hali mbaya kiafya.

    Novichok: Sumu iliyotumiwa kumshambulia jasusi wa Urusi
    Waziri mkuu Malcolm Turnbull amesema uamuzi huo unatokana na shambulio hatari la kutumia kemikali za neva zinazotengezwa na Urusi na zilitomiwa mara mwisho vita vya pili vya dunia.Idadi ya wanadiplomasia wa Urusi wanaofukuzwa inazidi kuongezeka, na hii ndio idadi kubwa kuwahi kutokea katika historia.
    Zaidi ya nchi 20 zimeungana na umoja wa Ulaya kuwafukuza zaidi ya wanadiplomasia 100.

    Donald Trump amesema Urusi inapaswa kuachana na tabia zake hatarishi kwa mataifa mengine

    Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amesema hatua hiyo ya nchi nyingine kuungana na Uingereza ni matokeo ya tabia ya Urusi kuingilia nchi za watu.
    ”Ambacho kimesababisha nchi zote hizi kuungana na sisi, ni kutokana na vitu ambayo urusi imefanya, nchi nyingi ndani ya miaka kumi wameshuhudia kama sio jaribio la mauaji kufanyika nchini mwao basi wameingiliwa katika uchaguzi wao na mitandao yao, aina zote za tabia zisizo kubalika za Urusi,” alisema Johnson.
    Seneta wa Urusi Andrey Klimov anasema kuwa hakuna ukweli wowote wa shutuma dhidi ya Urusi bali ni propaganda dhidi yao.

    Iceland imetangaza pia itasimamisha mazungumzo na mamlaka za Urusi na viongozi wake hawatahudhuria michuano ya kombe la dunia mwezi wa sita.
    Nani hudhibiti kemikali hatari zaidi duniani?
    Mapema Uingereza ilisema kuwa hawatatuma mawaziri wake pamoja na familia ya Malkia kushiriki kombe la dunia.

    Boris Johnson amesema Urusi inapaswa kujichunguza mara mbili mbili

    Itakumbukwa kuwa mwaka 1986 rais wa Marekani Ronald Reagan aliwatimua wanadiplomasia 80 wa Urusi.
    Na mwaka 2016 uongozi wa Barack Obama uliwafukuza wanadiplomasia 35 kutokana na kudukua chama cha Democratic.