Msanii wa muziki kutoka Kenya, Nyota Ndogo amewaomba wana Afrika Mashariki kumsaidia kutafuta ndugu wa mama yake mzazi ambao hadi leo hii hawajui walipo.
Nyota Ndogo amesema kuwa mama yake mzazi alifika nchini Kenya akitokea Zambia akiwa na miaka 14 akisafirishwa na rafiki na baba yake (Babu wa Nyota Ndogo) kwa lengo la kwenda kusoma.
Nyota Ndogo amesema kuwa mama yake hakufanikiwa kwenda shule kama alivyoahidiwa bali aliishia kuwa kijakazi wa nyumbani.
Baadaye Mama yake alipata bahati ya kuolewa na mwanaume kutoka Tanzania ambaye ndio baba yake mzazi, na kwa maelezo ya mama yake kwenye familia yao walizaliwa watoto 15 na mama yake alikuwa ndiye mtoto wa mwisho.
“Anatokea Zambia kisha baba anatokea Tanzania lakini sisi tumezaliwa pale makadara hospital. Mimi ni 001 damu kisha my mum alitoka kwao akiwa 14 years but kasahau kikwao. hatujui mtu hata mmoja wakutoka upande wa mama, anasema kwa wapo kumi na tano na yeye ndio alikua wa mwisho hajui kama babake yupo au hayupo anasema anatokea Tunduma.“ameandika Nyota Ndogo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Kwa upande mwingine Nyota Ndogo amesema kuwa kwa sasa anahitaji kufanya ziara nchini Tanzania maeneo ya Tunduma, ambapo amesema kuwa anachohitaji kutoka kwa watu wa Afrika Mashariki ni kumsaidia kutambua lugha anayozungumza mama yake ili apate wepesi wa kutafuta ndugu wa mama yake.
“Nataka kufanya tour ya kumtafutia familia yake alikuja vipi Kenya? Rafiki ya babake alikwenda kumchukua kwa wazazi wake nakusema anakuja kumsomesha badala yake akamgeuza kijakazi,” ameeleza Nyota Ndogo.
Baba mzazi wa Nyota Ndogo ni Mtanzania lakini kwa upande wa mama yake bado haijajulikana asili yake ingawaje wameishi Kenya kwa muda mrefu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai kwa wawekezaji wazawa na wafanyabiashara nchini kujenga viwanda vya dawa na vifaa vya tiba hapa nchini ili kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza ajira.
Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo Jijini Dar es Salaam, kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7 ya kusambaza dawa na vifaa vya tiba yaliyotolewa msaada na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD).
“Asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi, hivyo wawekezaji wazawa watumie changamoto hii kama fursa ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa hapa nchini kwetu,” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alibainisha kuwa ujenzi wa viwanda hapa nchini utasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania hasa vijana pamoja na kupunguza gharama za kuagiza bidhaa nje ya nchi zikiwemo dawa na vifaa vya tiba.
Aidha Rais Magufuli ametoa wito kwa wataalamu na wasomi wazawa wa masuala ya afya na tiba kujiunga pamoja na kuanzisha viwanda vya dawa ili kuchochea uchumi wa viwanda na kuongeza mapato.
“Tunapoteza shilingi bilioni 500 kila mwaka kwa ajili ya kununua dawa nje ya nchi lakini tungekuwa na viwanda vyetu fedha hizo tungetumia kwenye mambo mengine ya maendeleo,” alisisitiza Rais Magufuli.
Pia Rais Magufuli alisisitiza kuwa madereva watakaoajiriwa kuendesha magari hayo mapya wachaguliwe kwa umakini ili kupata watu waaminifu watakaoweza kuyatunza kwa manufaa ya Watanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) Bw. Laurian Bwanakunu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kwa kuongeza bajeti ya ununuzi wa dawa kutoka bilioni 31 mwaka 2015/2016 hadi kufikia bilioni 269 mwaka 2017/2018.
Tony Hage ameishi Liberia kwa zaidi ya miaka hamsini.
Na ndipo mahali alipo kutana na mke wake kisha kuanzisha biashara yake yenye mafanikio.
Aliendelea kuishi Liberia katika kipindi ambacho raia wengi wa nchi hiyo wali kimbia ili kuepuka machafuko akilenga kuiona nchi anayoipenda ikipata mafanikio.
Mpaka sasa bwana Hage si raia wa Liberia, amezuiwa kupata uraia wa kudumu wa nchi hiyo kwa sababu ya rangi ya ngozi yake na asili ya familia yake kutoka huko Lebanon.
‘Tutakuwa watumwa’
Nchi ya Liberia iliyoko mashariki mwa Afrika, ilianzishwa kama makazi ya watumwa wanaorejea Afrika kutoka huko Marekani sehemu ambayo walikuwa wakinyanyasika.
Lakini cha ajabu tangu ilipo tengenezwa katiba mpya kiliwekwa kipengele cha kutoa uraia kwa watu wenye asili ya Afrika tu na kutoa kizuizi kwa watu weupe.
Miaka mingi baadae, rais mpya wa Liberia na mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu George Weah anapingana na kipengele hicho na kusema ni kitu kisicho cha lazina lakini pia ni ubaguzi.
Anaongeza kuwa ubaguzi wa rangi unaondoa kabisa tafsiri ya Liberia, neno ambalo linamaanisha uhuru.
Msimamo huo wa Rais wa Liberia umezua tafrani katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.
“Watu weupe watawatawala wa Liberia weusi” mfanyabiashara Rufus amesema.
Anaamini kuwa mpango wowote ule wa kutoa nafasi za uraia kwa watu tofauti na wenye asili ya Afrika utaharibu nafasi ya wa Liberia kuendeleza nchi yao.
Pia anasema ni hatari kuruhusu watu wa nchi nyingine kuwa na umiliki wa mali huko Liberia.
Bwana Oulagbo sio mtu pekee kuweka wazi hofu yake, kundi jipya la utetezi wa raia ‘Citizen’s Action Against Non-Negro Citizenship and Land Ownership’ limejipanga kupambana na mipango ya Rais.
Kila nchi imejengwa kwa misingi maalumu, kama ukii shusha thamani misingi hiyo nchi lazima iyumbe, kiongozi wa kundi hilo Fubbi Henries ameiambia BBC.
Anaongeza kuwa Bwana Weah anatakiwa kushughulikia sera sahihi kwa wa Liberia.
“Tunahitaji kuweka biashara zetu sawa, sekta ya elimu na kilimo na si uraia au umiliki wa ardhi kwa watu weupe” amesema.
Licha ya utajiri wake wa mali asili, linapo kuja swala la wastani wa mapato kwa kila mtu Liberia ni nchi ya 225 kati ya 228 ambapo kwa mwaka 2017 pekee mtu mmoja alipata dola za kimarekani 900 tu.
Hata hivyo asilimia tatu ya pato la taifa la Liberia inatokana na wale wanaoishi nje ya nchi – na baadhi ya familia hutegemea fedha kutoka Marekani.
Lakini Bwana Weah anashutumiwa kwa kutoitathimini vyema hali hiyo anasema liberia ina hali mbaya kiuchumi na yeye anakwenda kutatua hilo.
Baada ya miaka mingi ya vita vya kiraia na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mwaka 2014 ahadi za George Weah zimekuwa kama muziki masikioni mwa raia wa Liberia.
Kubadilishwa kwa sheria sasa ni sawa na kumweka mtoto wa miaka miwili na mtu wa miaka 45 katika ulingo wa ngumi kuona kama wanaweza pigana kwa haki. Anasema Fubbi Henries kiongozi wa kundi la kiraia.
Anasisitiza kuwa lazima mtoto wa miaka miwili ataonewa hivyo basi wa Liberia bado hawana nguvu hiyo.
‘Usikizano‘
Hofu ya watu kutoka mataifa mengine sio kitu kipya, jamii ya wa lebanoni wameizoe sasa.” Baadhi ya watu wanaweza chukulia hii kama kitisho, kwamba wageni wanakuja kuchukua fursa zetu lakini si hivyo, bwana Hage anaiambia BBC akiwa nyumbani kwake Monrovia.
Hata hivyo kuna kipindi familia za Kilebanoni zilikuwa na biashara katika maeneo mengi ya nchi, na mpaka sasa wanamiliki baadhi ya hoteli na biashara kubwa katika nchi hiyo lakini hii isiwatie hofu majirani zetu wazaliwa wa Liberia.
Hage anaamini kuwa kama pendekezo la Rais litapia, hii itafungua njia ya ushirikiano zaidi. Sasa anasherekea sikukuu yake ya kuzaliwa ya 15 akiwa ndani ya Liberia, na haja wahi kujuta kuishi Liberia.
“Nina furaha si kwa sababu sina uraia wa Liberia, ninafuraha kwa sababu Rais Weah anatazamia mwelekeo wa nchi hii”
KIKOSI cha mabingwa wa Tanzania, Yanga SC kinatarajiwa kuondoka leo Dar es Salaam kwenda Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Singida Aprili 1, mwaka huu.
Robo Fainali za Azam Sports Federation Cup zitaanza Machi 30, Singida United wakiikaribisha Njombe Mji FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Machi 31 kutakuwa na mechi mbili, Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa JKT Tanzania Uwanja wa Namfua mjini Singida na Azam FC wakiikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
Wachazaji wote wa yanga wanapanda basi leo kwenda Morogoro, kasoro wanne waliopo katika kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars kipa Ramadhan Kabwili, mabeki Hassan Kessy, Gardiel Michael na Kelvin Yondan na kiungo Ibrahim Ajib pamoja na watatu waliopo timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, wote viungo Maka Edward, Said Mussa ‘Ronaldo’.
Taifa Stars itakuwa na mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na bila shaka mapema Jumatano Kabwili, Kessy, Yondan na Ajib watakwenda kuungana na wenzao kambini mjini Morogoro.
Ngorongoro nao watakuwa mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON –U20) Machi 31 Uwanja wa Taifa na baada ya mchezo huo Maka na Side Ronaldo nao watakwenda kambini.
Yanga inatarajiwa kugeuka Dar es Salaam mapema tu baada ya mechi yao ya ASFC mjini Singida ili kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania tiketi ya hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia Aprili 7 Uwanja wa Taifa.
Wakili na mwanaharakati mzaliwa wa Kenya ambaye alilazimishwa kwenda uhamishoni nchini Canada mwezi Februari mwaka huu alitarajiwa kurejea mjini Nairobi siku ya Jumatatu Machi 26, 2018 huku kukiwa na wasiwasi kwamba huenda asiruhusiwe na serikali ya Kenya kuingia nchini.
Katika taarifa aliyoituma kwa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika siku ya Jumapili akiwa mjini London Uingereza, Miguna Miguna alisema kuwa ataingia Kenya hata bila pasipoti au viza kumruhusu kufanya hivyo.
“Ndege yetu itatua Nairobi Jumatatu saa nane na dakika kumi na tano alasiri,” alisema Miguna.
Wakati wa kuchapisha ripoti hii, serikali ya Kenya haikuwa imetekeleza maagizo ya mahakama kuu, kuitaka imrejeshee hati yake ya kusafiria.
Miguna, ambaye amejitangaza kuwa kiongozi wa vuguvugu la National Resistance Movement (NRM- Kenya), amekuwa akiishi uhamishoni tangu maafisa wa polisi walipomlazimisha kuabiri ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi mapema mwezi Februari, kwa madai kwamba yeye si raia wa Kenya.
Mapema mwezi Februari, serikali ya Kenya iliwasilisha hoja mahakamani na kudai kuwa Miguna aliukana rasmi uraia wake na kwa hivyo hastaili kudai kuwa Mkenya.
Lakini mwanasiasa huyo mwenye utata ameshikilia kwamba katiba ya Kenya inaeleza bayana kuwa mtu aliyezaliwa katika nchi hiyo hawezi kupoteza uraia wake.
Akizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu siku ya Jumapili kabla ya kuabiri ndege mjini London akiwa njiani kwelekea Kenya, Miguna alisema hakuna mtu yeyote aliye na nguvu kuliko amri ya mahakama, na kupuzilia mbali kauli zilizokuwa zikitolewa kwamba huenda seriakli isimruhusu kuingia nchini Kenya, licha ya mahakama kuamuru asizuiliwe kuingia na kwamba arejeshewe hati yake ya kusafiria.
“Ninasafiri na pasipoti yangu ya Canada kwa sababu mahakama iliamuru iwapo watakataa kurudisha cheti cha kusafiria, nina uhuru wa kutumia pasipoti ya Canada kusafiria. Nitaenda huko na sitaomba viza kwa sababu mahakama ilisema hivyo,” alisema Miguna.
Serikali ya Kenya haijatoa kauli yoyote hadharani kuhusu kurudi kwa mwanasiasa huyo ambaye aliwania nafasi ya gavana wa Nairobi kwenye uchaguzi wa mwaka jana.
Safari yake inajiri chini ya wiki tatu baada ya rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta Kukutana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na kukubaliana kushirikiana pamoja kutafuta uwianio wa kitaifa.
Miguna alikuwa amekamatwa na kuzuiliwa na polisi kwa takriban siku tano kwa tuhuma kwamba alitoa kiapo – kinyume na sheria – kwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, mbali na kuwa mwanachama wa vuguvugu la NRM lililopigwa marufuku.
Lakini licha ya mahakama moja mjini Nairobi kumtaka afikishwe mbele ya jaji, polisi walimuwasilisha mbele ya hakimu katika mji ulio mbali na mji mkuu wa Kenya, na baadaye wakampeleka moja kwa moja hadi kwenye uwanja wa ndege, na kuwondosha nchini.
Tangu wakati huo, Miguna amekuwa akishiriki mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari na kufanya mikutano na Wakenya wanaoishi nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kutembelea miji kadhaa ya Canada, Marekani na Uingereza.
Tangu Miguna aondoke nchini, mgawanyiko mkubwa ndani ya muungano wa National Alliance Super Alliance (NASA) umejidhihirisha huku baadhi ya vinara wakuu wakisema kuwa Odinga aliwasaliti na kuashiria kwamba huenda muungano huo unaelekea kusambaratika.
Moses Wetangula, ambaye ni mmoja wa vinara wanne wa muungano huo, alisema yafuatayo siku ya Jumamosi: “Kile walizungumza, hakutuambia. Kile alipewa hakutuambia.”
Wetangula tayari amevuliwa madaraka ya kiongozi wa walio wachache kwenye seneti ya Kenya, na wadhifa huo ukachukuliwa na wakili wa chama cha Raila Odinga, ODM, ambaye pia ni seneta wa kaunti ya Siaya, James Orengo.
“Wanachama wa NRM wako tayari kuhakikisha kwamba hakuna shughuli zitakazoendelea katika mji wa Nairobi hadi pale wanyanyasaji wa raia walionykua madaraka kwa nguvu waachie mamlaka na kukubali kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki nchini Kenya,” Miguna aliuambia mkutano aliohutubia mjini London siku ya Ijumaa.
Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya sisasa wanasema hata ikiwa Miguna Miguna hatazuiliwa kuingia nchini Kenya, huenda ikawa vigumu kwake kutimiza malengo ya vuguvugu la NRM, hususan kufuatia mabadiliko makubwa ya Kisiasa yaliyotokea tangu aende uhamishoni.
Tayari Miguna amemkosoa vikali Raila Odinga kwa kukubali kushirikiana na rais Kenyatta huku akidai kwamba itakuwa vigumu mno kwa masuala waliokuwa wakipigania kama upinzani kutekelezwa.
Watu 37 wamethibitishwa kufariki baada ya moto kuzuka katika jumba moja kubwa la kibiashara katika mji maarufu kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe wa Kemerovo, eneo la Siberia nchini urusi.
Watu zaidi ya 64 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto 41.
Baadhi ya maeneo ya jumba hilo kubwa yanadaiwa kuwa kwenye hatari ya kuporomoka.
Moto huo ulianza katika ghorofa ya juu katika jumba Winter Cherry.
Inadaiwa wengi wa waliofariki walikuwa kwenye kumbi za sinema.
Video zilizopakiwa mitandao ya kijamii zinawaonesha watu wakiruka nje kupitia madirisha kujaribu kujinusuru kutoka kwa moto huo uliozuka Jumapili.
Wazima moto zaidi ya 660 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji.
Chanzo cha moto huo hakijabainika lakini maafisa wameanzisha uchunguzi.
Kemerovo, ni eneo maarufu sana kwa uchimbaji wa mkaa wa mawe.
Ni mji unaopatikana takriban kilomita 3,600 mashariki mwa mji mkuu Moscow.
Kansela wa Austria Sebastian Kurz ametuma salamu zake za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa waathiriwa, sawa na Waziri wa mambo ya nje wa Latvia Edgars Rinkēvičs.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuburuzwa mahakamani mwezi Aprili kwa makosa 16 yakiwemo ya kutumia vibaya ofisi wakati akiwa madarakani na ufisadi.
Duru za habari nchini Afrika Kusini kusini likiwemo gazeti la News24 limeeleza kuwa Zuma atafikishwa kizimbani katika Mahakama Kuu mjini Durban tarehe 6 Aprili 2018 kwa makosa 16.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa bodi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo, Brigedia Hangwani Mulaudzi amesema kuwa mwishoni mwa wiki hii watawasilisha barua kwa mawakili wa Zuma juu ya wito huo.
Mulaudzi amesema kuwa Zuma atakabiliwa na mashtaka makubwa 16 ambapo rushwa na Matumizi mabaya ya ofisi yanatajwa kuwa ni moja ya mashtaka yaliyopewa kipaumbele.
Imeelezwa kuwa Jacob Zuma alifanya malipo ya risiti 783 kiholela, kwenye ununuzi wa silaha na vifaa vya jeshi nchini Afrika Kusini ambapo inakadiriwa kuwa ametumia mabilioni ya fedha kwenye ununuzi huo.
Mwaka 2012, Zuma aliingia kwenye kashfa nzito baada ya kutengeneza nyumba yake ya kifahari kwa kutumia fedha za serikali, ambapo alitumia zaidi ya dola milioni 25 za kimarekani.
Hata hivyo, kashfa hiyo ilitetewa na baadhi ya wabunge wa chama tawala nchini humo ANC, ambapo walieleza kuwa ukarabati huo ulizingatia vigezo.
Mnamo Februari 14, 2018. Mzee Zuma alitangaza kung’atuka madarakani baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wanachama wa ANC na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu wake wa Rais, Cyril Ramaphosa.
Pamoja na mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerbag kuomba msamaha kutokana na kupoteza uaminifu kitu kilichowakera watu zaidi ya milioni 50 duniani, soko lake la hisa limeonyesha kutetereka.
Kwa mujibu wa mtandao wa kibiashara MoneyWatch soko la hisa za mtandao huo zilianguka kwa asilimia saba.
Thamani ya hisa ilishuka kutoka Dola 176.80 siku ya Jumatatu hadi Dola 159.30 siku ya Ijumaa jioni.
Siku hiyo hisa za mtandao wa Facebook ziliuzwa kwa $38 kila moja na kuufanya mtandao huo kuwa na thamani ya kibiashara ya Dola bilioni 104.
Hadi Februari 2018 kutokana na kukua kwa matangazo ya kidijitali hisa za facebook zilipanda hadi $190.
Mchambuzi wa masuala ya hisa Raymond James amesema katika ripoti kwa wateja wake kwamba kumekuwa na ongezeko la wasiwasi juu ya Rashia kuendelea kuwalenga wateja na kutumia vibaya taarifa zao kitu ambacho kimekuwa na athari hasi katika hisa za Facebook.
Facebook imesema kuwa hapo awali ilitoa taarifa za wateja wake kwa mtafiti ambaye alidai kuwa zitatumika kwa masuala ya kielimu. Facebook imedai kuwa mtafiti huyo baada ya hapo “alitudanganya” na kuwapa taarifa hizo kampuni ya Cambridge Analytica.
Hali kadhalika Cambridge Analytica inashutumiwa kwamba ilihusika kwenye mzozo wa kupotosha watu na kutumia takwimu visivyo, ambao pia unaikabili kampuni ya Facebook.
Facebook tayari imesitisha uhusiano wake na CA na kuikataza kampuni hiyo kutumia mtandao huo kwa matangazo yake.
Hili lilikuwa ni tatizo kubwa la kupoteza uaminifu. Ninaomba msamaha wa kweli kwa kilichotokea. Tunawajibu wa msingi kulinda taarifa za watu,” Zuckerbag aliliambia shirika la habari la CNN.
Hata hivyo mmiliki huyo wa Facebook hakufafanua ni makosa gani Facebook ilifanya, lakini aliahidi kupitia apps zote na kuzihakiki kikamilifu iwapo zimehusika na vitendo vya jinai.
Wachambuzi wa biashara wanasema kuwa siri ya mafanikio ya modeli ya biashara ya Facebook ni kiwango cha wateja wanaojiunga na facebook, na hivi sasa kutokana na kashfa ya kupoteza uaminifu wake, Facebook imeanza kupoteza wateja wake.