YANGA WAENDA MOROGORO KUIWEKEA KAMBI SINGIDA UNITED

YANGA WAENDA MOROGORO KUIWEKEA KAMBI SINGIDA UNITED

Like
941
0
Monday, 26 March 2018
Local News

KIKOSI cha mabingwa wa Tanzania, Yanga SC kinatarajiwa kuondoka leo Dar es Salaam kwenda Morogoro kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Singida Aprili 1, mwaka huu.
Robo Fainali za Azam Sports Federation Cup zitaanza Machi 30, Singida United wakiikaribisha Njombe Mji FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Machi 31 kutakuwa na mechi mbili, Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa JKT Tanzania Uwanja wa Namfua mjini Singida na Azam FC wakiikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

Wachazaji wote wa yanga wanapanda basi leo kwenda Morogoro, kasoro wanne waliopo katika kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars kipa Ramadhan Kabwili, mabeki Hassan Kessy, Gardiel Michael na Kelvin Yondan na kiungo Ibrahim Ajib pamoja na watatu waliopo timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, wote viungo Maka Edward, Said Mussa ‘Ronaldo’.
Taifa Stars itakuwa na mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na bila shaka mapema Jumatano Kabwili, Kessy, Yondan na Ajib watakwenda kuungana na wenzao kambini mjini Morogoro.
Ngorongoro nao watakuwa mechi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON –U20) Machi 31 Uwanja wa Taifa na baada ya mchezo huo Maka na Side Ronaldo nao watakwenda kambini.
Yanga inatarajiwa kugeuka Dar es Salaam mapema tu baada ya mechi yao ya ASFC mjini Singida ili kujiandaa na mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania tiketi ya hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia Aprili 7 Uwanja wa Taifa.

Comments are closed.