Category: Local News

  • WANANCHI WAMETAKIWA KUTUMIA VYEMA MIUNDOMBINU YA NCHI IKIWEMO BARABARA

    WANANCHI WAMETAKIWA KUTUMIA VYEMA MIUNDOMBINU YA NCHI IKIWEMO BARABARA

    Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Rais JAKAYA KIKWETE wakati akifungua rasmi barabara ya Mwenge –Tegeta.

    Naye Balozi wa Japani nchini MASAKI OKADA amezungumzia juu ya ushirikiano uliopo kati ya Serikali yake na Tanzania

    kikwete3

     

    Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 imegharimu kiasi cha Sh. bilioni 77.85, fedha
    ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa
    la JICA. Serikali ya Tanzania imechangia asilimia 7.64 katika gharama za ujenzi
    wa Barabara hiyo.

    kikwete
    Mh.Rais akifungua barabara

    Katika ufunguzi wa barabara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam SAIDI MECK SADIKI amesema kuwa hali hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa magari.

    Naye Mhandisi Mkuu wa TANROAD PATRICK MFUGALE amesema ujenzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta imejengwa kwa kiwango chenye ubora

  • MKUTANO WA KIMATAIFA WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO WAANZA RASMI JIJINI DAR

    MKUTANO WA KIMATAIFA WA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO WAANZA RASMI JIJINI DAR

    chinaleo

    Mkurugenzi wa Kampuni ya Tekinologia ya Huawei Tanzania, Vincent

Wen(kushoto) akizungumza na washiriki katika mkutano huo.

    chinaleo2

    chinaleo3chinaleo3

    baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa

wa Tekinolojia ya Mawasiliano wakifatilia kwa makini mkutano huo ulioanza rasmi siku ya jana katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam kwa 

udhamini wa HUAWEI.

  • Wananchi Wasema Sauti Zao Hazisikiki

    Wananchi Wasema Sauti Zao Hazisikiki

    Twaweza

    Asilimia 70 ya wananchi sehemu mbalimbali nchini wameripoti kuwa sauti zao hazisikiki katika maamuzi ya serikali huku asilimia 71 wakiamini njia pekee ya kuleta ushawishi kwa serikali ni kupiga kula.
    Hayo yamebainishwajana jijini Dar es salaam kufuatia utafiti uliofanywa na Taasisi ya TWAWEZA uliohusisha mazungumzo ya wananchi juu ya hali zao na kupitia simu za mkononi uliopewa jina la Sauti za Wananchi.

     

  • Kamati Yapendekeza Mipaka Uhuru Wa Habari

    Kamati Yapendekeza Mipaka Uhuru Wa Habari

    Anna Abdalla

    Bunge maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma limependekeza kuwe na mipaka ya Uhuru wa Vyombo vya Habari badala ya kuwa na Uhuru usiokuwa na Mipaka.
    Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati Namba Kumi ya Bunge maalumu la Katiba Mheshimiwa ANNA ABDALLAH wakati akiwasilisha maoni ya Wajumbe walio wengi katika Kamati hiyo ambapo Kamati hiyo imevitaka vyombo vya Habari kulinda na kuheshimu Utu,Heshima,Uhuru na Staha ya Mtu

     

  • Tumieni Vizuri Tabiri Za Hali Ya Hewa

    Tumieni Vizuri Tabiri Za Hali Ya Hewa

    joel bendera

    Jamii imetakiwa kufuata na kutumia vema utabiri wa Hali ya Hewa unaotolewa kwa muda muafaka na mamlaka ya hali ya hewaTanzania -TMA ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuepuka madhara ikiwemo mafuriko.
    Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa wa Mkoa Morogoro JOEL BENDERA wakati akifungua Warsha juu ya umuhimu wa huduma za ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa Umma.
    Wakati huo huo Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dokta AGNES KIJAZI amewasisitiza wananchi kutopuuza taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa ili kujipatia manufaa katika sekta mbali mbali ikiwemo Kilimo na Afya katika jamii inayowazunguka.

     

  • Ponda Aiomba Mahakama Morogoro Isimamishe Kesi Yake

    Ponda Aiomba Mahakama Morogoro Isimamishe Kesi Yake

     ponda

    Wakili Nassoro Juma anayemtetea Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda ameiomba Mahakama Kuu itumie busara kusimamisha kesi ya jinai inayomkabili mteja wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

    Ponda kupitia wakili huyo, aliwasilisha maombi akitaka mahakama iamuru kesi hiyo inayomkabili mkoani Morogoro isimame ili kusubiri kwanza uamuzi wa rufaa yake aliyokata mahakamani hapo.

    Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Ponda anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi katika maeneo mbalimbali mkoani humo, likiwamo la kukaidi amri ya Mahakama ya Kisutu.

    Mahakama ya Kisutu katika hukumu yake Mei 9, 2013, ilimtaka Sheikh Ponda awe mhubiri amani katika jamii likiwa ni sharti la kifungo cha mwaka mmoja nje baada ya kumtia hatiani katika kesi ya jinai mwaka 2012.

    Katika kesi hiyo, Ponda na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama, wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni na kuingia kijinai kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali eneo la ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd na uchochezi.

    Hata hivyo, Sheikh Ponda kupitia kwa mawakili wake alikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu.

    Kutokana na rufaa hiyo, ndipo walipowasilisha maombi ya kusimamisha kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

    Jaji Lawrence Kaduri anayesikiliza maombi hayo alikubaliana na maombi ya Jamhuri na kuahirisha shauri hilo hadi Septemba 10.

  • Ikulu Yakana Rais Kikwete Kuwaomba Ukawa

    Ikulu Yakana Rais Kikwete Kuwaomba Ukawa

     Salva-Rweyemamu

    Ikulu imesema Rais Jakaya Kikwete hakuwaomba wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), warejee kuendelea na vikao vya Bunge hilo.

    Ukawa ni umoja unaoundwa na wajumbe ambao ni wanachama wa vyama vya siasa vya Chadema, NCCR Mageuzi na CUF waliosusia Bunge la Katiba tangu Aprili 16, mwaka huu kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo.

    Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu alisema suala la Ukawa kurejea bungeni haikuwa ajenda kuu ya mkutano huo uliofanyika Ikulu ya Kilimani, mjini Dodoma juzi na badala yake kulikuwa na majadiliano ya jumla mchakato wa Katiba.

    Katika mkutano huo ulioratibiwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), viongozi wa Ukawa walikuwa sehemu ya ujumbe uliokutana na Rais Kikwete kwa ajili ya kuzungumzia mambo mawili; mchakato wa Katiba na jinsi ya kuwa na uchaguzi bora wa 2015.

    “Hilo suala halikuwa ajenda ya mkutano, hivyo kusema Ukawa wamemgomea Rais siyo kweli,” alisema Rweyemamu ambaye alikuwa akirejea habari iliyoandikwa na gazeti hili jana kuhusu yaliyojiri katika mkutano wa Rais Kikwete na viongozi hao.

    Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo alisema mkutano huo ulikuwa wa mafanikio makubwa na kwamba watakutana tena na Rais Kikwete Septemba 8, 2014 baada ya kamati ndogo iliyoundwa kukamilisha kazi yake. Kamati hiyo inawajumuisha viongozi wa vyama vya siasa ambavyo mbali na kwamba ni wanachama wa TCD, ndivyo vimekuwa vikivutana kuhusu mchakato wa Katiba.

    Viongozi hao ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ambaye ataongoza kamati hiyo na wajumbe wake ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

    Ukawa wamekuwa katika mvutano na CCM, ambayo katika kikao cha Kamati Kuu yake wiki mbili zilizopita, ilitoa taarifa kwamba inaridhika jinsi mchakato unavyokwenda ndani ya Bunge Maalumu na kuwataka wajumbe walitoka nje warejee bungeni.

  • Wafanyabiashara Kariakoo Wafunga Maduka Kukwepa Ukaguzi Wa Mashine Za EFD

    Wafanyabiashara Kariakoo Wafunga Maduka Kukwepa Ukaguzi Wa Mashine Za EFD

    DUKA 4

    Wafanyabiashara mbali mbali wenye maduka eneo la kariakoo wamefanya mgomo usio rasmi wa kufunga maduka yao ili kutokaguliwa na watendaji wa TRA ambao wanaendesha msako wa kuwakamata wale wote ambao wanatumia mashine za EFD kinyume na matumizi yake halisi.

    DUKA 3

    Kwa mujibu wa hali halisi ambayo imeonekana leo katika eneo hilo  maduka mengi yamefungwa katika kile kinachoonekana kukwepa kufanyiwa tathmini ya matumizi ya mashine za ki Electroniki za EFD zinazofanya kazi ya kutoa risiti na kutunza kumbukumbu za mahesabu za mwenye duka.

    Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi ambaye aliongea na ripota wa EFM Bwana  Sosthenes Shayo alisema wao hawapingi matumizi au kutumia mashine za EFD wanapinga mfumo mbaya uliowekwa kwa ajili ya matumizi ya mashine hizo.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Mamalaka ya Mapato -TRA -amesema kuwa kufuatia Uhakiki huo yapo mambo kadha wa kadha ambayo wameyabaini kufuatia zoezi hilo ikiwemo uhafifu wa matumizi ya  mashine hizo.

    Wafanyabiashara mara nyingi wanalalamika lakini tukiitisha vikao hawafiki. Na pia baadhi yao kwa maana ya wachache wenye hitilafu ndio wanachochea wengine kugoma ili waendelee na kutotumia mashine hizo. Efm itakuletea habari zaidi juu ya sakata hilo.

     

     

  • Christiano Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya

    Christiano Ronaldo Mchezaji Bora Ulaya

    Ronaldo

    Mchezaji wa kimataifa wa Portugal anayechezea timu ya Real Madrid Christiano Ronaldo Jana usiku alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa mwaka 2014/2015.

    Ronaldo alitwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji Arjen Robben wa Bayern Munich Emmanuel Neur wa Bayern Munich katika sherehew iliyofanyika jijini Monaco nchini Ufaransa.

  • Okwi Arudi Simba Asaini Mkataba Kama Mchezaji Huru Kulinda Kipaji Chake

    Okwi Arudi Simba Asaini Mkataba Kama Mchezaji Huru Kulinda Kipaji Chake

    Okwi

    Aliyekuwa msambuliaji wa Yanga Emmanuel Okwi jana jioni amesaini Simba SC kwa mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.
    Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.
    “Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.
    Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni.
    “Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.
    Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia.
    Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu.
    Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao.
    Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.
    Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo.
    Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe.
    Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo(Jana) baina ya mchezo huyo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi.
    Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema.

  • Mbowe Akabidhiwa Fomu Ataka Ushindani Na Anayeona Anaweza Kummudu

    Mbowe Akabidhiwa Fomu Ataka Ushindani Na Anayeona Anaweza Kummudu

    mbowe

    Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana alikabidhiwa fomu na makada wa chama hicho na kumtaka awanie tena kiti hicho, ombi ambalo alilikubali na kufungua milango kwa wanachama wengine ‘kupimana naye kifua’.
    “Nafasi bado ipo, anayetaka kupima kifua na mimi ajitokeze. Tena nawaomba viongozi wangu msizuie fomu kwa anayetaka,” alisema Mbowe ambaye ameongoza chama hicho kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
    Makada wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiongozwa na kada maarufu, Athuman Mzigo (Mapigo Saba) kutoka Kigoma, walikutana na Mbowe na kuwasilisha maombi yao ya kumtaka awanie tena nafasi hiyo.
    “Kutokana na sifa za mwenyekiti wetu, tumechangishana Sh200 kila mmoja hadi zikafika Sh50,000,” alisema Mapigo Saba huku akishangiliwa na makada wenzake alioambatana nao na kuongeza:
    “Tumemwomba mwenyekiti agombee nafasi hiyo kwa kuzingatia sifa; kwanza anaijua vizuri idadi ya Watanzania na matatizo yao, pili anaungwa mkono na watu wengi na amekisaidia chama kukua. Tulikuwa na madiwani 40 leo wamefika 500, wabunge watano leo 48. Halafu hana ubaguzi ndiyo maana ameunganisha vyama vya upinzani na kuunda Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”
    Huku akichomekea maneno ya lugha ya Kiha, Mapigo Saba alisema kuwa maombi ya kumtaka Mbowe agombee pia yametolewa katika mikoa ya Rukwa, Manyara, Iringa, Njombe, Jimbo la Same Magharibi, Zanzibar, Mwanza na Kilimanjaro.
    Hotuba ya Mapigo Saba ilifuatiwa na salamu kutoka kwa wazee wa wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke, Baraza la Wanawake (Bawacha) na Baraza la Vijana (Bavicha).
    Akitoa salamu za Bavicha, mwenyekiti wa baraza hilo Njombe, Emmanuel Masonga alisema Mbowe ni sawa na Joshua aliyemalizia kuwaongoza wana wa Israel kuingia nchi ya Kanaani:
    “Sisi Wakristo tunajua kuwa Mussa alianzisha safari ya Waisrael kwenda Kanaani, ila hakuwafikisha. Kina Mtei (Edwin), Kimesera (Victor), Bob Makani na wengineo walianzisha safari ya kwenda Ikulu, ila hawakutufikisha. Mbowe ni sawa na Joshua atakayetufikisha Ikulu,” alisema Masonga.
    Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Susan Lymo alimsifu Mbowe akisema ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa katika chama hicho.
    “Mwaka 2000, kulikuwa na mwanamke mmoja katika viti maalumu, mwaka 2005 waliongezeka na kufikia sita na mwaka 2010 wamefikia 26. Mwenyekiti pia ameufanya mwaka huu kuwa wa wanawake kitaifa na ameongeza hamasa ya wanawake kushiriki siasa,” alisema Lymo.
    Mbali na viongozi wa chama, alikuwapo pia Sheikh Rajab Katimba kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu ambaye alimsifu Mbowe na kuomba agombee tena nafasi hiyo.
    Baada ya Mratibu wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), Nickson Tugara kummwagia sifa Mbowe, Mapigo Saba alimkabidhi fomu, huku makada wakiimba, ‘Jembe, jembe, jembe…”
    Mbowe aliishukuru Kamati Kuu ya chama hicho kwa kupanga uchaguzi Septemba 14, mwaka huu ambayo ni siku yake ya kuzaliwa huku akiahidi kujenga chama imara.
    “Mtaiona Chadema mpya ifikapo Septemba 14. Hiki chama hakitakufa na hatutamvumilia mtu yeyote wa kabila lolote atakayekivuruga,” alisema.
    Mbowe alisema hajawahi kuomba kugombea uenyekiti wa chama hicho tangu aliponza mwaka 2000… “Napata wakati mgumu ninapofikia wakati huu.
    Chadema ina watu mbalimbali wenye taaluma na uzoefu, kwa nini mimi? Makundi haya yaliyojitokeza kunichukulia fomu yanaweza kutafsiriwa na wapenda majungu kuwa nimepanga mimi.
    “Leo ni mara ya tatu naombwa kugombea uenyekiti, sijawahi kuomba. Mwaka 2004, Mzee Makani aliniomba nikamkatalia, lakini akaunda kikundi cha wazee walionichukulia fomu.
    Mwaka 2005, chama hakikuwa na mgombea urais, awali alijitokeza Profesa Mwesiga Baregu lakini akajitoa, nikaambiwa nibebe mzigo. Mwaka 2009 nikaombwa tena kugombea.”
    Alisema amedhamiria kujenga chama kimtandao na kimfumo ili kuondokana na mfumo wa kienyeji… “Huko nyuma wakati wa uchaguzi watu walipeana tu nyadhifa kiundugu tukadhani chama kimeongezeka. Lakini wakati huu uchaguzi umefanyika kwa miezi tisa.
    Tulisema hatuwezi kufanya uchaguzi wa Taifa bila kupata viongozi wa mkoa, wilaya, kata, kijiji na mtaa, kitongoji na shina.
    Tumefanya uchaguzi, watu wamepima na kuona mambo magumu, mara unasikia wanakimbia wakisema wameacha uenyekiti, uache wakati chama kinakua?”